

Msikilize anavyoongelea libeneke la ulimbwende:
bofya hapa
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
interview ni nzuri lakini swala la kutembea na vichupi ni vigezo mi naona ni huuni,uzuri wa mwanamke ni kujifunika sio kutembea uchi ndo mana malaya hawana hadhi kutokana na vinguo vyao sasa chupi ndo kabisa !
ReplyDeleteni umasikini ndo unafanya wazazi waruhusu watoto wao hama sidhani kama wangekubari watoto wakae vichupi hata kama ni kwa siri eti mbele ya majaji na wahandaaji tu! hiyo ndo siri kweli?
sasa ndo nini kufanya mbele ya majaji na wahandaaji tu wakati mtoto kasha sign mkataba wa kuingia kwa hiyo akishinda si ataenda miss world? sasa huko hatokaa kichupi mbele ya world?
bora vichupi viruhusiwe tu au vikataliwe kabisa.
tena mnakataa vichupi nchini (TZ) kwenye mashindano ya miss tz kisa utamaduni sasa wanao enda miss world wanatangaza utamaduni unao kataliwa na kupingwa na dini zote nchini alikotokea mlimbwende(TZ)
alafu anatangaza mbele ya ulimwengu
mbona nchi inaji contradict?
ni biyashara na shetani ndo anayetamba duniani hivi sasa. hii kazi ni haramu mkubari msi kubari.
Hoyce usiseme usingefika ulipofika kama isingekuwa miss TZ nielimu yako na usharp wako ndo umekufikisha ulipofika.(au wame kubrain wash)
cha muhimu usisitize wazazi wasomeshe watoto zao sio kuimiza waruhusu watoto zao waende kwenye mashindano ya uzuri. unataka kuniambia usingesoma ungepata kazi ya bank kisa wewe ni miss TZ 1999. please .
Anony wa kwanza unakasirika bila sababu! Hoyce hajasema mabinti wasisome! wala vichupi sio uhuni. Uhuni ni pale ambapo watu wanaweka mbali madhumuni na maana ya kuwa miss na kuhusudu ngono na hao waulimbwende. Baadhi ya watu wamekuwa wakifanya juu chini ili tu aweze kutembea na mlimbwende hususani vijana ambao hawajatulia hata mababa waliooa na familia zao. Pia mamiss wengine huwa tu wana tamaa ya kupata vitu dezodeo au kwa njia ya mkato kwa kujihusisha na tabia chafu. Nchi zilizoendelea wanavaa hivyo vichupi na hawajihusishi na mambo ya ulimbukeni kwa kiasi kikubwa kama Tz tunavyofanya.
ReplyDeleteMi nawashauri wanotaka kuingia kwenye mashindano ya urembo wasome na sio kuacha shule kisa urembo, mamiss wengi Tz wameacha shule na hawajarudi tena baada ya kushiriki urembo kitu ambacho ni tofauti na nchi nyingine hususani zilizoendelea. Sasa hilo sio bango la kumshikilia Hoyce, wengine wanaingia kichwa kichwa bila kuwa na mpangilio na kusudio lenye maana.
Majaji lazima waweke standards za kuingia kwenye umiss juu zaidi ili wenye sifa ndo wachaguliwe na watanzania pia wajiheshimu, mambo ya ngono lazima tujifunze kusema hapana na kuacha ngono za sifa la sivyo ukimwi utatumaliza. Kuendelea kulalama mambo ambayo hayahusiani na sii chanzo cha matatizo bado tunakwepa majukumu ambayo tunatakiwa kujitwisha na kuyatatua.
Huyu si ndiye yule shangingi aliyebubujikwa na machozi kisa Richa Adhia kashinda Umiss? So tangu wakati ule nimemtoa maanani kabisaaa... I hope amejirekebisha na kuacha imani za kibaguzi tena I hope amemtafuta huyo Richa na kumuomba radhi...Mbali na hayo sina kibaya cha kusema kuhusu huyu dada...
ReplyDeleteMdau, Boston, US
wewe Annoy. hapo juu ningekuona kwa sura ningekupa BUSU!
ReplyDeleteUmesema vyema.Elimu dada Hoyce, its your education that put you there, tena ningewashauri hiyo kamati ya Miss Tanzania waanze kutoa Scholarship za Kusomesha hao ma-miss instead of Magari!
Nawasilisha!
shukran
Melissa
Uzuri unao sema mimi naona cream imezidi. Na nimeshaona hivyo kwa wanawake wengi wazuri sana lakini bado watazidishia hiyo cream halafu mtu anakuwa kama sanamu na hata kwenye harusi pia. Nadhani ukijipodoa tu simple mtu unaweza kupendeza zaidi. Mfano wa karibu mtu kama Michael Jackson vipodozi vikizidi matokeo ndiyo hayo.
ReplyDeleteMtoto mzuri sana na nakuzimia, punguza vipodozi angalau ngozi ya mwili na uso vingeendana.
kama beyonce vile..kaolewa na nani,nani tena huyo kaniwahi..wengine wote mliocomment HATERS FALL BACK MAFAZ
ReplyDeletemdau wa Boston umenifurahisha sana. Ingawa sikubaliani na kumwita Hoyce shangingi, lakini kitendo alichofanya baada ya Miss Tz 2007 kilikuwa ni cha aibu sana. Kama ye kweli ana hasira na wadosi angeanza kulia na wabunge na mawaziri na vigogo wengine waliokamatia uchumi wa Tanzania. In her position as a former Miss Tz ilikuwa ni aibu kuonyesha ubaguzi wa wazi namna hiyo jwa Richa.
ReplyDeleteWhatever you may feel towards Richa (be it because she's of Indian origin; or be it because you thought she was not the deserved winner), you will have to agree that Hoyce should not have caused all that tantrum and shed pretentious tears in public after the judges announced Richa to be the new Miss Tanzania. Hoyce owes both Richa and the Miss Tz committee an apology