MWENYEKITI MPYA WA UWT MAMA SOFIA SIMBA

MH. SOFIA SIMBA AMEJIZOLEA JUMLA YA KURA 470 KUWA MWENYEKITI MPYA WA UMOJA WA WANAWAKE.
MH. SIMBA AMEWEZA KUMSHINDA MPINZANI WAKE WA KARIBU MH. JANET KAHAMA ALIYEPATA KURA 383, WAKATI MH. JOYCE MASUNGA KAAMBULIA KURA 10 KATIKA MCHUANO MKALI WA KUGOMBEA KITI HICHO KWENYE UCHAGUZI MKUU WA UWT ULIOFANYIKA DODOMA.


MH. SIMBA PIA NI WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS ANAYESHUGHULIKIA UTAWALA BORA

HABARI KAMILI





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. Hongera sana aunty Sofia. Tunakuamini utakuwa mstari wa mbele kuwahamasisha akina mama wa Tanzania mwakani wampigie kura nyingi JK na CCM. Wewe umesoma hakikisha unakuwa tofauti na Anna ABdallah kwa kuiongoza UWT kisomi na kileo. Kidumu CCM

    ReplyDelete
  2. Congratulations mama!!! Im so proud of you!!!! Mungu atakulinda na maadui wote...

    ReplyDelete
  3. Hongera kwa kushinda. Ila wasiwasi wangu ni kuwa utavimudu vyeo vyote sawasawa? Kama utaweza hongera sana. Ukishindwa utaonekana mroho wa madaraka.

    ReplyDelete
  4. Hivi hawa viongozi wana muda wa saa ngapi kwa siku kuweza kufanyakazi ya u-Waziri na u-Mwenyekiti na "biashara" nyinginezo pembeni?

    Kiongozi mmoja; wadhifa mmoja!

    Achieni na wa-Tanzania wengine nao wapate "maisha bora"!

    Circulation of the elite iko wapi?

    ReplyDelete
  5. Hongera sana mama Simba kwa nafasi hiyo ya kuwa mwenyekiti,kumbe wewe ndiyo msomi katika wagombea mimi sikujua hilo,jamani tunapogombea nafasi yoyote ni vizuri ukafahamu kwanza sifa zinazohitajika kwa mgombea katika nafasi hiyo.nawapa pole sana mama Janeti Kahama na mama Masunga hawakujua hilo.

    ReplyDelete
  6. congratulations Sofia,
    i am only worried tht after such hefty campaigns that saw you even campaigning in the guest houses on a sunday if it will make any difference to UWT or it will just be another of those paper pushing jobs, and words which we are really tired of hearing but can really rouse a huge audience in a frenzy of clapping and shouting,..yeah sasa kampeni zimeisha tuungane hakuna kusemanasema tena...hurrah hurrah.. hii inaonyesha wanawake tunaweza... hear hear hurrah hurrah.. tusibweteke blah blah.. hurrah !!
    please !! i hope overtime someone will come and tell us what we dont want to hear, and in this case, i will give a standing ovation lets not be copy paste sort of individuals especially when we hold high chairs such as these.. my thoughts

    ReplyDelete
  7. Ina maana watu wenye ujuzi wameisha au ni kwa nini mtu mmoja awe na kazi mbili? Ataweza kuwakilisha wanawake vizuri na bado kufanya kazi hiyo nyingine??

    mnamwona Hillary anaachia usenate tuige mifano. Two pension funds

    ReplyDelete
  8. Hongera mama Sofi ila vyeo mbona vingi utamudu dia? kwa nini jamani tusiwajaribu watanzania wengine nao pia tukaona utendaji wao pia kuliko kumbebesha huyu mama wa watu nyazifa nyingi namna hiyo? Waziri mbunge. Neki na uwenyekiti jamani vitampalia jamani hee.

    ReplyDelete
  9. Hongera mama,ulitoa speech nzuri baada ya kutangazwa mshindi.Nina swali jana nilibishana na rafiki yangu mmoja bar hadi glass zikapasuka.Eti huyu 'mmama'ni mke au ana uhusiano wowote na Idd Simba,mwenye jibu atuamulie ugomvi wajameni

    ReplyDelete
  10. David Villa, huyu mama hana uhusiano wowote na Iddi Simba, ni jina tuu kwani kama last name yako ni Mushi basi wachaga wote ni wanaoitwa Mushi ni ndugu???

    ReplyDelete
  11. Asante sana blogger uliyenijibu hapo juu.

    ReplyDelete
  12. Hongera sana Auntie So....

    Reena

    ReplyDelete
  13. Hongera mama. Well done na tunakutakia all the best katika kazi yako nzuri. Bravo mama Simba,
    Mdau

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...