WADAU NAOMBA KUULIZA. HIVI RAISI MTEULE WA MAREKANI BARAK HUSSEIN OBAMA ANA WAKE WANGAPI?
NAULIZA HIVYO KWA SABABU KIJIWENI KWETU KUNA UBISHI KWAMBA JAMAA ANA WAKE WAWILI NA KWAMBA NI MMOJA TU NDIYE ANAKUWA FRONTI, NA MWINGINE ANAMINYA NYUMBANI.
NAOMBA MSAADA NIFAHAMISHWE TAFADHALI KUHUSU UKWELI WA MAMBO..
MDAU
MWANANYAMALA KOMAKOMA, DAR

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

  1. Mdau wa Mwananyamala,
    Fahamu kuwa Obama si Rais Mteule, ni Rais wa Marekani. Kabla ya kuapishwa alikua ni PRESIDENT ELECT, Lakini maana ya ELECT sio MTEULE, Mteule ni "appoint"., hivyo kabla ya kuapishwa alikuwa ni Rais Mchaguliwa..hicho ndio Kiswahili sanifu. Ningependa tuwekane sawa hapo kwanza maana waandishi wengi wa habari walikua wanaandika Mteule kila wakati, yule sio Kingunge aliyeteuliwa na Kikwete, Obama kakutana na wapiga kura na kashinda uchaguzi.

    Suala la mke: Ndoa za mitaala na za wake kibao za kiafrika usidhani kila sehemu zipo mdau.Obama ana mke mmoja tu, Michelle na watoto wawili tu. Kama mtu mwingine anajitangaza basi ni kushoboka kwake tu.

    Jamani, mfaham kuwa Obama ni typical American, kwahiyo usianze kuchukua mila za Kijaluo muanze kumpatia Obama.

    MDAUZ

    ReplyDelete
  2. acheni mijadara ya kijinga. mmeishakuwa watu wazima na mna mjukumu mengi yanayo wazunguka.badala ya kufikiria mjikwamue vipi na umasikini, mna concetrate katika midahalo ambayo haina faida kwenye maisha yenu. EBO

    ReplyDelete
  3. Huyo aliyekwambia Obama ana wake wawili mwambie akome kabisa kuongea vitu visivyo na ukweli.
    Barack Obama ana mke mmoja na ni rock of his family ambaye ni Michelle Obama,na watoto wawili tuu ambao ni Obama girls Sasha (7) na Malia (10). mwambie aache kumchafua Obama kwa kumbambika kuwa ana wake wawili anadhani ni Mbongo yule wa Kuoaoa kila mwanamke???

    Mfikishie huo ujumbe huyo mwenye kuosha kinywa.

    Mdada mwenye hasira.

    ReplyDelete
  4. Hivi wewe mdau wa Mwananyamala, shule umeenda kweli? Ni swali gani hili. Kwa wenzetu kule, sheria ni MM1.. (Mke, Mume 1) usifikiri kila mtu wana tamaa za wake zaidi ya mmoja. Nenda waambie hao wenzako wa kijiweni watafute shughuli zakuweza kuwa endeleza badala yakupiga umbea usie na maana. Mwenzenu Obama ndio anavuna matunda ya kazi yake kubwa, sasa nyie mnavuna nini?

    ReplyDelete
  5. President Obama ana mke mmoja tu huyo Michelle-kipenzi wake wa siku zote;na angekuwa na mwingine lazima tu wamarekani wangejua by now toka majournalists na mapaparazi especially during election time kwa jinsi walivyo kuwa wanamtafutia drama.

    ReplyDelete
  6. WEWE KWELI UPO KOMAKOMA,JITAHIDI KUJIELIMISHA NA KUWA MDADISI WA MAMBO,OTHERWISE UTAKUWA MBUMBUMBU WA MAMBO MADOGO KAMA HAYO,INTERNET UNAYO SI NDIO?HADI UKAWEZA KUTUMA HIYO MSG KWA MICHUZI SASA TUMIA HIYO ZANA KU-RESEARCH FACTS NA SIO KUROPOKA KAMA UMETOKA USINGIZINI.

    ReplyDelete
  7. mh mmeanza, hamkosi la kusema? au la kutunga? loo

    ReplyDelete
  8. Mshaanza kashfa zenu

    ReplyDelete
  9. Ana wake watu wengine ni Maria and Sasha.... what kind of stupid question. Marekani kuoa mke zaidi ya mmoja ni HARAMU au ILLEGAL, UA KOSA LA JINAI.... Next time jadilini maswala ya Tanzania.

    ReplyDelete
  10. Wabongo hamuachi....?!!!!any way Obama ana mke mmoja jina lake Michelle, na watoto wake ni wawili mmoja ni Sasha na mwingine ni Malia.Ni mkristu hivyo sidhani kama madhehebu yao yanaruhusu mke zaidi ya mmoja,umejibiwa?.

    ReplyDelete
  11. hahaaha, ebwana asante kwa kunifurahisha siku ya leo.. hizi ndio sensi of hyuma tunazotaka kila siku maishani...
    hahahahahaha

    ReplyDelete
  12. Obama hana mke wa pili na wala mapaparazi wenye uchu hawakupata ushahidi kama hata aliwahi kuwa na nyumba ndogo......Wadau tukumbuke Obama ni mzungu na wala sio mmatumbi. Haya mambo ya kimatumbi ya kukusanya magolikipa halafu unashindwa kutunza watoto hana...Inabidi sisi wamatumbi tujifunze kutoka kwa huyu bwana..

    ReplyDelete
  13. Unajua Marekani sio kama huku bongo ambapo mtu mkubwa anakuwa na nyumba ndogo tena kama kumi hivi lakini haigunduliki. Kama Obama angekuwa na kashfa kama hiyo ingegundulika mapema na asingeweza kugombea hata uraisi. Unajua watu wengi tena wakubwa wakubwa sana marekani na wenye influence kubwa sana katika siasa za marekani hasa die hard conservatives (wale wasiobadilika) hawampendi Obama na walitoa kashfa nyingi mpaka za kumuita kuwa yeye ni mpinga kristo yule aliyetabiriwa kwenye biblia, wengine wakamuita gaidi, wengine wakamuita kuwa anavaa nguo za kienyeji za afrika, wengine wakasema atalisilimisha taifa la marekani, lakini kwa kuchunguza kwao kote walishindwa kupata hata chembe ya uasherati (kutembea na mke asiye halali) wa Obama. Kwa hiyo hayo kama yanatajwa sidhani kuwa yatakuwa na ukweli wowote. Msimuzushie mtu wa watu.
    Wengine hata wamemzushia kuwa amewaandikia barua maraisi wa afrika mashariki. Ni uzushi au ushereheshaji tu.
    Obama is clean

    ReplyDelete
  14. hii habari ya obama na wake wawili inaonekana mtu amekwa bored na maisha kwahiyo ameandika ili watu wabishane. who in sane mind will come up with such a story. acheeni uzushi isiokua na maana. kama kuna watu kwenye vijiwe wanazungumzia hilo ninaona hawana la kufanya na fikira zao ni za kitoto. kama kwenye vijiwe vyenu hamna la kufanya jaribuni kujiunga na shule za watu wazima au mjitolee kwenye community services. mkifanya hivyo mtajisikia vizuri kwasababu mtakua mmefanya jambo la maana kwenu wenyewe na kwa watu wengine.

    ReplyDelete
  15. watanzania hamna dogo,wenzenu walishaachana na obama ,sas hivi wanafanya kazi ninyi ndo kwanza mnauliza anawanawake wangapi.sheria za marekani haziruhusu mtu kuoa wake wengi,ukiwa polygamy kule unaweza kufungwa,sawa na denmark na kwingine walikoendelea.
    achane ujinga,jaribuni hata kujadili matokeo ya uchaguzi mbeya na mtakabali wa nchi yenu isiyo na mwelekeo,kuliko kujadili umbea usio na tija.

    ReplyDelete
  16. NINASHANGAA HII STORY TULIONGEA SIKU NYINGI PALE KIJIWENI JAMAA ANA WAKE WAWILI MMOJA YUKO KENYA NA MWINGI AMERICA. HUYU WA AMERIKA NDIYO ANAJULIKANA NASIKIA HUKO NA HUYU WA HUKU AFRIKA NI WAKUPOZEA TU. LAKINI NASIKIA SERIKALI INAMPA FEDHA NA KILA KITU.

    ReplyDelete
  17. Baraka Obama ana mke mmoja tu Michelle Obama na Marekani ndoa zaidi ya moja hairuhusiwi; mtu unaenda jela kwa hilo.
    Hizo tabia za wake wengi ni huko huko Bongo na nchi za kiarabu na zingine za dunia ya tatu na msidhani kwa vile wengi wanafanya hivyo basi ni jambo la kawaida.

    JK - TO

    ReplyDelete
  18. obama ana mke moja tuu. siyo kama huko watu wanaoa wake wengine. mungu alimteua mume na mke ni kitu kimoja siyo wake wengi.

    ReplyDelete
  19. Kwa kweli nitashangaa sana kama Watanzania mnashindwa kuelewa kuwa nchini Marekani hakuna siri. Ingekuwa ni hivyo mbona mngeshasikia, hilo jambo mnalolijadili kwamba huyu Rais Obama ana wake wawili sidhani kama ni kweli.Kwa kweli tafuteni kingine cha kujadili hususani mafisadi wa nchi yetu na mchango wenu kwa nchi yetu, kwani dunia ndiyo hiyo imeyumba Obama naongoza taifa kubwa ambalo dola yake inaongoza na amekiri kuwa hali ya uchumi ni mbaya. Badala ya nyie kujadili uzushi ni bora mkajadili namna ya kufanikisha hali ya uchumi wa nchi yetu, kwa sababu kuna taarifa ambo hazijatolewa rasmi kuwa nchi ya Tanzania itakumbwa na ethiopia(njaa) tufanye nini?

    ReplyDelete
  20. Muulizaji wa swali alisahau akataja jimna la Obama, lakini alitaka kujua KIKWETE ana wake wangapi na nyumba ndogo ngapi? Huyu mzee wetu ni kicheche sana. Najua Mithupu hii utaibania ili usikose safari za JK anaposafiri na nyumba zake ndogo.

    ReplyDelete
  21. Obama ana wake wawili.Michelle aliyeko marekani na mke wa pili ni mama yako wewe mdau wa Mwananyamala Komakoma ambaye kamtelekeza Mwananyamala komakoma kwa kuwa ni mumbeya kawa wewe ulivyo mumbeya.Huishi majungu kenge wewe.

    ReplyDelete
  22. nimeangalia documentary yake bbc jamaa kuna kitabu kaandika kuna kurasa ya bangi basketball, ngono na raggea ulirukwa kwenye hiyo documentary yawezekana ana wake wawili tusubiri credit crunch iishe yatajulikana tuu.

    ReplyDelete
  23. 100% Pure Rubbish
    what is that has to do with anybody???

    ReplyDelete
  24. Ni kweli kwa marekani ni illegal kuoa zaidi ya mke mmoja, lakjini kuna exceptionals za wale wahafidhina wa vijijini wanaoa mke zaid ya mmoja.

    Kwa wale wanafuatila vipindi vya CNN na Oprah Winfrey wanujua Ukweli huu.

    By RAF

    ReplyDelete
  25. Wewe Komakoma kabisa. Obama wake wawili? Hivi wewe unafikiri marekani ni uswazi kwa sababu ya tamaa zenu na ulafi wenu badala ya kumpenda mke mmoja mnahalalisha uzinzi. Acha hizo

    ReplyDelete
  26. Ni kweli kwa Wamerekani ni kosa kuwa mke zaidi ya mmoja, lakini kutembea na zaidi ya mke mmoja sio kosa? mmmh, hili lina hitaji hekima kufikiri
    m3

    ReplyDelete
  27. wewe uliye uliza hili swali na jamaa zako wa kijiweni please tafuteni kazi za kufanya achaneni kushabikia mambo ambayo hayata wasaidia kitu au peleka hilo swali kwenye utamu blog.

    ReplyDelete
  28. Wewe Mdau ckia Baraka Hussein Obama ana MKE MMOJA TU. Na tangu akutane na Mkewe huyo hajawahi hata siku moja kubwenga mwanamke mwingine na hata hajawahi kufikiria kulala na mwanamke mwingine zaidi ya mkewe.....Umenisoma?

    ReplyDelete
  29. wewe ndo maana ungeacha kukaa kijiweni ambapo kuna pumba nyingi zisizo na kichwa wala miguu zinaongelwa na kuanza kufanya research mwenyewe kwa vitu vya kijinga kama hivi kabla hujauliza na kuonekana mvivu kusearch online.

    ReplyDelete
  30. nyie mnaosema "nyie wa huko bongo au africa,Tz" nyie wa wapi??yani kwenu wapi aswaa ebu mtueleze tujue humu katika blogu ya michuzi kuna wazungu-ngozi nyeupe wanaochonga kiswahili hiki chetu cha kibantu kama nyie,,,
    ovyooooooooo
    na wewe wa obama shut-up!

    ReplyDelete
  31. Sio mbaya kujua kama ana mmoja au zaidi bali mambo mengine ni kutumia akili. Angekuwa nae, hata kama ni 'nyumba ndogo' lazima wakati wa kampeni ingejulikana.

    Labda ungeuliza kama amewahi kutembea na mwingine zaidi ya huyo mke wake, tungekujuza kuwa alitembea na dada yako.

    ReplyDelete
  32. OBAMA ANA MKE MMOJA WA NDOA NA HANA KIMADA KAMA MARAISI WA AFRICA. MUME MMOJA MKE MMOJA NDIO AMERICA. KUWA NA NYUMBA NDOGO SIO CRIME IN AMERICA NA HAUWEZI KWENDA JELA KWA HILO. LAKINI IKITHIBITIKA YOU GONNA LOOSE A LOT IN DIVORCE.ABOMA ANGEKUA NA MKE WA PILI ASINGEPATA URAISI PERIOD.

    IT IS WHAT IT IS.

    ReplyDelete
  33. Obama angekuwa na mke mwingine, au hata angetembea njeya ndoa yake, REPUBLICANS na paparazzi wangemwumbua zamani!

    ReplyDelete
  34. Taarifa ya uhakika kabisa kutoka White House: Obama ana wake wawili na robo!

    ReplyDelete
  35. jamani huyo mwenye kijiwe na wengine wanaokubaliana naye ni watu wasio na akili. i am sure wanajua fika kuwa obama ana mke mmoja lakini wanataka kuona tutabishana nao mpaka lini. jamani do not argue with fools otherwise you will become one of them. tuwaache wakae vijiweni vyao wakijadili mambo ya upuzi. i am sure some of them wana watoto wadogo kwanini wasitumie huo muda kuwasaidia watoto wao kufanya homework zao. wanaweza kutumia huo muda wa kijiweni kuwasomea watoto wao vitabu au kuwapigia hadithi. watoto waliozoweshwa kusoma vitabu wakiwa wadogo hupenda kusoma wakiwa wakubwa. mkifanya hivyo at least mtakua mmesaidia jamii zenu na taifa letu la baadae.

    ReplyDelete
  36. michuzi utaniudhi sasa hivi you need to be biased na mahoja ya ajaajabu tuna mambo mengi ya kujadiri, hivi hata ikifahamika kwamba obama ana wake kadhaa itaisaidia vipi jamii yetu? au ikajulikana kwamba kiongozi fulani ana kimada itasaidia nini? ni lazima tujue kwamba viongozi kama watu wengine nao wa madhaifu ya kihisia kama ya mtu yeyote hivyo basi chochote atakachokifanya kuhusiana na maswala ya mahusiano ya kimapenzi ni suala lake personally na familia yake tusubiri mpaka tuombwe na muhusika ili tulijadiri. NIMEKASIRIKA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...