Marehemu Newaho Mbeye

Mazishi ya Marehemu Newaho Mbeye yatafanyika katika Makaburi ya Kinondoni kesho tarehe 9/1/2009 siku ya Ijumaa mchana.
Ratiba ni kama ifuatavyo:-

Saa 5.00 Asubuhi mpaka saa 6.00 mchana = Misa na Chakula nyumbani kwa Marehemu Tegeta karibu na Nyamachabesi. (Mabasi ya Mwenge -Bunju, kushuka ni Kituo cha Nyaishozi)

Saa 6.00 mchana hadi saa 7.00 mchana= Kutoa Heshima za Mwisho
Saa 8.00 kuelekea Makaburini= Makaburi ya Kinondoni.

Akiwa ni mtumishi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bibi Newaho Mbeye alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumanne katika Hospitali ya Misheni Mikocheni alikokimbizwa baada ya kuugua ghafla.

Kabla ya kukutwa na umauti, Hayati Newaho alikuwa kitengo cha Huduma za Wateja- sehemu ya mapokezi ambako aliendelea na kazi zake kama kawaida mpaka muda wa kufunga ofisi ulipofika hiyo jana huku akionekana kuwa na afya njema na huku akitekeleza majukumu yake ya kila siku.

Kwa wale waliofika makao makuu ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, tangu walipokuwa Sukari House hadi walipohamia Kurasini sura ya marehemu Newaho Mbeye sio ngeni kwao. Mipango na maandalizi mengine ikiwemo mazishi vinaendelea na taarifa kamili baada ya mawasiliano kati ya Uongozi wa Mfuko na Familia ya Marehemu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE MILELELE, MOLA AIWEKE PEMA ROHO YA MAREHEMU NEWAHO MBEYE
AMIN
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Oooh Masikini.
    niliiona hii post sikujua kama ni huyu mdada Mungu ailaze Roho yake mahali pema peponi Amen.
    Mikongoti Jr, KL

    ReplyDelete
  2. Newaho namkuombea kwa Mwenyezi Mungu aiweke roho yako peponi. Tulikupenda sana lakini Mungu amekupenda zaidi. kazi ya Mungu haina makosa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...