KIKWEKWEREKWE
Hodi hodi blogini kaka michuzi naingia
Mimi wako muhisani ujumbe nakuletea
Kufuga nimetamani kuku ninawatajia
kaka kwako kweli kiko kikuku kikwekwerekwe.
Kama hakipo nyumbani basi chukuwa hatua
Wasomi nipatieni kama mtajionea
Kokote kitafuteni kikuku nahitajia
kaka kwako kweli kiko kikuku kikwekwerekwe.
Nimeshinda vijijini kikuku naulizia
Kikokoriko jamani kisiwe chenye udhia
Manyanyu kwangu sifani msije kuniletea
kaka kwako kweli kiko kikuku kikwekwerekwe.
Kishingo pia sidhani kama kweli kitafaa
Sikutumwa ugangani kufuga nimeamua
Ukweli nimetamani nasina nyengine njia
kaka kwako kweli kiko kikuku kikwekwerekwe.
nilijaribu zamani boi nikajifugia
wakangia maradhini mafua kuwaumbua
wakafa wote kwanini nimebadilisha nia
kaka kwako kweli kiko kikuku kikwekwerekwe.


Ama kweli Michuzi wadau umepata !! Dada yetu si useme tuu unatafuta Rijali , na utowe picha yako sisi hatujui hicho cha kwanza kwa nini kiliumwa mafua. Sema nakusifu kwa Usanii shairi limetulia.
ReplyDeleteKikuku cha namna gani, bora Jongwe jifugia
ReplyDeleteAtawika mtaani, Kuchi mbegu maridhia
Kidume cha fani, na masubwi ayajua
kwani unashida gani, spring chicken kulilia?
Kuchi yuko makini, si rahisi kukimbia,
Aina ya bukini, ni wazuri kwa tabia,
bara na visiwani, waheshimika sawia
Atawika mtaani, mbegu maridhia.
Vikuku taabani, nguvu pumzi huwaishia,
Siha yao matatani, sote twawaharumia
Kuchi wa bukini, kama punda milia
Musuli imesheheni, hakika utafurahia.
Vumilia jamani, kuchi utajipatia
Subiri hata mwakani, ogopa kiruka njia
Kunguru sije tamani, mwanzo kuangamia
kikuku cha nini, Kuchi utajipatia?
KIKWEKWEREKWE ??!!!
ReplyDeleteKaribu blogini hadi barazani ingia
Sisi wako wahisani ujumbe tumepokea
Kufuga umetamani kuku umetutajia
Kama kweli kiko kikuku kikwekwerekwe?.
Utakipata bwawani, kama umedhamiria
Wasomi blogini, mada wameistukia
Imeingia akilini, kikuku wahitajia
kama kweli kiko, kikuku kikwekwerekwe?.
Umeshinda vijijini, kikuku kukiulizia
Kikuku makini, kisije leta udhia
Hutaki purukushani miwaya kukuletea
Kama kweli kiko kikuku kikwekwerekwe?.
Kwa sura usidhani, kama kweli maridhia
Si elimu au fani, huwezi kutambua
Ukweli kwa darubini,hakika utajua
Angaza kwa Salmini, Amrefu jipimia
Hapo ndo yakini, kikwekwerekwe kungamua
Usijaribu kizamani, sura kutangulia
Au tajiri mjini, jina zuri kuvutia
Taingia maradhini mafua kujiuumbua
Mauti harakani, hatari kukurubia
Yataka ndo yakini kikwekwerekwe kungamua.
'''Mdau Bonde la Mpunga'''
hayo maoni ma3, hujaridhia?
ReplyDelete