Mama Bishanga


Michuzi habari za bongo au Coted'lvoire, bado nakumbuka mambo ya mambo hayo nayamiss pia.
Leo sina zaidi ya kuwatakia mwaka mpya mwema uwe wa heri furaha na mafanikio kwetu sote wa-Tanzania wote.
Na kwa wasanii wenzangu nawapongeza kwa kazi nzuri mnazofanya hata tulio nje ya TZ tunafurahia juhudi zenu hasa kwenye sherehe ambapo ndio tunapata fursa ya kukutana na kulisakata rumba kama tuko bongo, hongera sana.

Kila la heri kwenu wote pamoja na Raisi wetu na viongozi wa jamuhuri yetu ya Muungano ya Tanzania.

MAMA BISHANGA

OHIO

USA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mama ulikuwa unajua kuigiza. Nakumbuka ulikuwa unatumia lafudhi ya kihaya. Ok Kila la kheri.

    ReplyDelete
  2. Hakika huyu Mama ni mzao wangu kabisa bila kusitasita. Yuko sehemu gani hapa Ohio maana nami nipo hapa lakini sijawahi kukutana nae. Wadau wa Columbus nisaidieni mawasiliano na Mama Bishanga kupitia kwenye mtandao wetu wa Wabongo. Mama Bishanga, kujuana ndio hukuhuku hebu jitokeze ujinyakulie riziki zako kiulaiiiini na kimyakimya kiutuuzima.

    ReplyDelete
  3. Watu kwa uroho???? mdau tarehe January 26, 2009 9:55 AM, umeona juu ya kichwa cha mama kuna picha yuko na na MZee i think?? halaf bado tu unauliza uliza... hebu kaa kimya...
    Mtu mzima oooovyyoooooo.

    ReplyDelete
  4. Umenoga mama yangu!!!!! mwanao Columbus

    ReplyDelete
  5. Hi Michuzi
    Nilikuwa naomba kama una e-mail address ya mama Bishanga. Nimejaribu kuweka comment hapa kwenye blog yako naona nimeshindwa. Nataka contact za mama Bishanga, niliwahi kukaa nae kipindi huko South Africa (Johanesburg) nataka nimsalimie.
    Mtanzania

    ReplyDelete
  6. nilikuwa najiuliza huyu mama yuwapi jamani kumbe ohio lool na mtoto wake naye alikuwa anaigiza yuko wapi jamani ningependa muona pia

    mhh nimefurahi huyu mama alikuwa kiboko hasa ile episode ya dili la kuuza nyumba na kugawana hela mama bishanga seki na aisha ile bwana ndio iliyofunga kazi aisha kiboko seki huyu mama kweli mama jua pale ndio mliigiza na ulivyoondoka kinyemela wapenzi tuliuuzunika sana but maisha popote nimefurahi kukuona bado una afya nzuri kabisa.

    ReplyDelete
  7. michu una roho ya kwanini wewe?ndo nini wabana meseji?
    nimesema ivi,,mama asante tushaona picha yako ya majuu kama kawaida ya wabeba box uko na asa iyo "kijitabia cha kithungu"kutundika picha ukutani,sio tabia ya kibongo basi tu tumerithi toka kwa mkoloni wetu,
    ingawa sikukumbuki,wee annon unaesema ati ana mume,,,mume ndo nini???watu wakuu wa dini washindwa sembuse ivi
    hahahahaaaaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...