
Safari hiyo itajumuisha wanamuziki wote 26 wa bendi hiyo pamoja na viongozi wawili, Mwenyekiti wa African Stars Entertainment Tanzania (ASET), Msiilwa Baraka, ameiambia globu ya jamii sasa hivi.

Alisema kuwa waandaaji wa tamasha hilo la Mfalme wanajua kile ambacho wamepenzi wa muziki wanataka katika kukata kiu ya burudani na kuifanya Twanga Pepeta kuwa bendi pekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kushiriki mara nyingi zaidi kwa upande wa muziki wa dansi.


Alisema kuwa tamasha hilo linashirikisha vikundi mbali mbali vya buridani kutoka barani Afrika, mashariki ya Mbali na Ulaya na moja ya shughuli au tukio kubwa la mwaka nchini Oman.


Mwenyekiti huyo alisema kuwa Twanga imeandaa nyimbo mbali mbali mpya na za zamani zikiongezewa na mirindimo ya ngoma asilia katika kutoa taswira halisi ya muziki wa Kitanzania na Afrika kwa ujumla.
Alisema kampuni yake ya ASET inauchukulia muziki kama KAZI nyingine zaidi ya burudani ya kawaida na ndiyo maana hutafuta masoko ya nje na kuwezesha vijana wengi kujipatia ajira ndani na nje.
ASET pia inamiliki bendi nyingine moto wa kuotea mbaliijukanayo kwa jina la Vibration Sound chini ya mwanamuziki nyota, Ellystone Angai ambayo imekamilisha album yao ya kwanza yenye nyimbo sita na itazinduliwa rasmi hivi karibuni.
Alisema kuwa tamasha hilo la Muscat linashirikisha vikundi mbali mbali vya buridani kutoka barani Afrika, mashariki ya Mbali na Ulaya ikiwa ni moja ya tukio kubwa la kuanzia mwaka mwaka nchini Oman.
Bendi hiyo itaondoka Jumatatu usiku kwa ndege ya KENYA AIRWAYS Tayari kufanya mambo makubwa katika tamasha hilo na itarejea nchini siku moja kabla ya Valentine day Februari 14 na kuendelea na maonyesho yake ya kawaida hapa nchini
Sherehe hii Inaitwa Muscat Festival sio muscat music festival na sio tamasha la mfalme. Mbona mnatoa data wrong wazee?
ReplyDeleteSawa mdau kalamu ya mwandishi iliteleza. Ni Muscat Festival pia tamasha huwa chini ya Mayor wa Muscat. ASET
ReplyDelete