Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya,
Hapa UK kama mjuavyo kuwa wiki hii wapenda kandanda watatupa macho na masikio kwenye michuano ya kikombe maarufu cha F.AKettering Town FC ni ngeni masikioni mwa wapenzi wengi, lakini ni klabu cha ajabu kidogo, kwani ndicho kilichopachika mabao mengi zaidi katika michuano hii mpaka sasa, na leo kipo dimbani kumenyana na Fulham FC.
Lakini si hivyo tu, bali hii ndio timu pekee, pengine duniani, iliyoonesha ubavu wa kutangaza hadharani kuwasaidia waathirika wa mateso ya njaa, umaskini, maradhi, uvamizi na unyanyaswaji wa nchi ya Palestina kupitia kwa shirika la Interpal.
Jezi ya wanandinga hawa watayoshuka nayo dimbani kesho ina tangazo kubwa la kushajiisha misaada kwa wapalestina.
Mambo si mambo, hivi karibuni mwanasoka wetu kutoka barani Afrika, Freddy Kanoute wa Mali anaecheza soka huko Hispania, alishtukia akipigwa faini na chama cha soka cha Uhispania kwa sababu alikwidua fulana yake kuonesha simanzi zake kwa wahanga hao wa kipalestina kupitia fulana aliyoivaa ndani, akishutumiwa eti kuchanganya kandanda na siasa!!
Jamaa wadau haya yamekaaje?Kwani mimi toka nilipokuwa mdogo nikijua kuwa soka na siasa ni chanda na pete, ndio hata tunapigiwa nyimbo za Taifa, tena wachezaji wakalazimishwa kuziimba, sababu huwezi kutenganisha siasa na mchezo wa kandanda.Nifunueni macho wadau maana mimi hapa sielewi sawa sawa.
Ni kweli kandanda halichanganywi na siasa? Mbona Kattering Uingereza linachanganywa? Au pana zile ajenda za siri za "ALL ANIMALS ARE EQUAL BUT SOME ARE MORE EQUAL THAN OTHERS"?
Tafadhali fuatilia ushahidi wa Kattering na wa Kanoute katika kurasa hizi:
Ahsanteni sana Mdau Leicester, Uk

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Mpira ni kazi na hakuna sheria ya kazi inayoruhusu kuleta hisia zako za kidini au siasa katika eneo la kazi.
    Kama unataka siasa nenda kwenye siasa, ukichanganya ni halali yako kufungiwa.Sioni point ya Kanoute au mtu yeyote kujifanya ana uchungu na wapalestina wakati historia inaonyesha wazi huo mgogoro unachangiwa na kodi ya nchi wanazoishi.Kwani hamjui kuwa Uingereza ndo ilifanya draft ya mkataba wa Israel kuwa taifa huru?
    Sasa hicho kitimu cha mchangani kwa nini kisitumie nguvu zake kuilaumu serikali badala ya kwenda kupiga longolongo kwenye mechi.
    Leave our beautiful game (football) out of politics stuff.
    Nawasilisha.

    ReplyDelete
  2. JIFUNZENI KISWAHILI KABLA HAMJAWEKA MAKALA YENU HUMU NDANI JAMANI! I HATE BROKEN SWAHILI! IT SUCKS!!!!

    ReplyDelete
  3. Mdau inawezekana una kumbukumbu ndogo ama unaamua kwa makusudi kukumbuka kitu kimoja na kusahau kingine; Unakumbuka jinsi mwaka 2006 kwenye fainali za kombe la dunia mchezaji wa Ghana alipigwa faini na FIFA baada ya kushangilia kwa kuonyesha fulana ya ndani iliyokuwa na bendera ya Israel (Star of David)?? Hiyo nayo imekaaje??

    Sitaki kusema kama vitendo vyote viwili ni vibaya ama vizuri lakini inaudhi kuona mtu unatoa hoja iliyolalia upande mmoja. Ungetoa mifano yote miwili, na ukahoji hiyo imekaaje ningeona kweli una hoja ya muhimu lakini sasa inaonekana unachofanya ni kupiga propaganda.

    ReplyDelete
  4. Watu wengine, bwana! Wewe mdau wa Leicester unatafuta kutukanwa kwa kuzua mada hafifu kama hii ya kujadiliwa. Mie yangu macho na masikio kwa wabeba maboksi wataporudi kujirusha mwisho wa wiki

    ReplyDelete
  5. Imekaaje! Kwani wewe ulitaka ikaeje? Wewe mtoa hoja hii una lako jambo, uwe wazi tu.

    ReplyDelete
  6. mtowa maoni wa mwanzo umezungumza utumbo kiasi kwamba hata kukujibu naona ni kupoteza wakati.

    Kwa wapenda mpira wote duniani wanajua sheria za kuvua jezi, kuvuta juu jezi na kuonyesha ujumbe kwenye jezi ya ndani.

    wachezaji wengi huvaa jezi ndani zenye ujumbe fulani. kuna wanaovaa ujumbe wa kidini kama akina kaka na wengine kina kanoute wanaonyesha support zao kwa jambo fulani. wote hupewa onyo au faini kutegemea na FA ya wanapocheza mpira wanavyoona uzito wa kosa hilo. ndio maana hivi karibuni timu nzima ya liverpool hawakuadhibiwa kwa kuvaa jezi za ujumbe wakati wa warm up kabla ya mechi.

    Kattering wao hawavai hiyo logo kwa support ya palestine, wanavaa kutangaza huduma za interpal ambazo husaidia palestine. Hiyo ni tafauti kubwa. Ni kama UNICEF wanavyotangaza huduma zao katika jezi barcelona.

    Timu zinalipwa kuvaa majina ya kampuni na mashirika kwa hivyo kattering hawana kosa.

    ReplyDelete
  7. mchangiaji wa mwanzo ulianza vizuri points zako lakini umejikanyaga vibaya mwishoni.

    ReplyDelete
  8. Nakubaliana na mchangiaji wa pili, watanzania tunajisifu kila siku kuwa sisi ndio tunaosema kiswahili fasaha, tunajidai kuwa kiswahili asili yake ni kwetu tanzania, lakini jinsi watu wanavyoondika kiswahili kibovu sio kwenye blog hii tu ila kila blog pamoja na magazeti nyumbani mtu unaona kinyaa kabisa.

    ReplyDelete
  9. Siasa zinazokataliwa ni za kuwasaidia wanyonge hasa wale ambao waliposhambuliwa baraza la usalama lilishindwa kupitisha azimio ma kusimamisha mapigano mpaka wakafa maelfu. Hizo ndo siasa za upande mmoja, za ukoloni mamboleo wa watu kufukuzwa katika ardhi yao, wakaletwa wengine makundi kwa makundi na kupewa uraia wa hapo, na wanapodai haki yao hukandamizwa na kuitwa magaidi.
    Hiyo ndiyo siasa ya sasa baba!

    ReplyDelete
  10. naungana na watoa maoni hapo juu kuhusu kiswahili kilichoandikwa kwenye makala,yaani ni kibovu mno.kiswahili ni lugha ya taifa lakini watu hawajui kukitumia.

    ReplyDelete
  11. Nyie yule jamaa kuonesha bendera ya Israel wakati anachezea Ghana kiasi apigwe Fine sababu hawaitangazii Israel, Kuhusu Kettering wao wanaitangazia Palestina Aid ambayo ni tangazo lililokubaliwa kama Barcelona na Unicef hapo ndio mtaelewa nakila pesa wanaonunulia jez\i ya Kettering ya UK kama ni ya palestina pesa zinaenda kwa palestina sababu wanatangazia na Telegraph pia sawa na Man U kutangazia AIG kila Kodi ya mmarekani inaenda kwa Man United. ni mikataba tu iliyokubaliwa sio. sio kutangazia kitu ambacho hakipo kwenye mkataba na nchi yako.

    ReplyDelete
  12. Oya yule mchezaji wa Ghana kafanya kosa kama kosa alilolifanya Kanoute Kuhusu kettering Town Hawana kosa sababu wapo kwenye mkataba huo wa kutangazia ambao umekubaliwa na Chama cha michezo.

    Ghana Mchezaji wake alionesha Bendera ya Israel yeye haimuhusu kufanya vile sababu ipo nje ya mikataba na nchi yake wakati ni kombe la dunia ni kuhusu nchi yako tu.

    Kanoute naye kafanya kosa kubwa kama kusaidia Palestina una muda wa kusadia kwa njia yako au kufanya maandamano peke yako nje ya timu yako alionesha flana yake ni kama kutangazia ambayo haifai kabisa sababu timu yake haitangazii kitu hicho.

    Kettering Town wana kila haki ya kufanya hivyo kutangazia hilo tangazo kama Aid. Kettering Town hawakuanza juzi kutangazia Hilo tangazo toka Msimu ulivyoanza inavyoonesha. GAza aliwahi kufundisha hiyo timu kama sikosei akafukuzwa kwa ulevi wake. From JAmes Ndosi.

    ReplyDelete
  13. Hako katimu kako ka Uswazi kanatafuta umaarufu tu. Kakishukiwa dhahama kadadai kameonewa ili mradi tu watu wakaoneone.

    ReplyDelete
  14. http://www.inminds.co.uk/boycott-arsenal.html Si Kosa hata Arsenal Football Club wanasaidia Israel si kosa kwayoyote ambaye anaona atamsaidia mwenzake bwana.

    ReplyDelete
  15. Wote mpo sahihi kwa mtazamo wenu,lakini tujaribu kutofautisha siasa hasa za kimataifa ambazo zinaweza kugawa kundi fulani la watu kutokana na uhalisia wa siasa wenyewe,mfano mwaka jana wakati kosovo wanajitenga toka serbia,mkimbiaji wa serbia alishinda akavua fulana yake iliyoandikwa "kosovo is serbia" alinyang'anywa ushindi na kurudishwa nyumbani kwao serbia,kwani uhalisia wa siasa ulikuwa uhasama sana hadi leo japo jamaa washajitenga,kumtangaza mungu kunaruhusiwa kama kaka kwa mfano,ila si kukashifu imani ya mtu,kuhusu palestine kule kuna siasa ya kimataifa ambayo wadau mnaifahamu,hivyo kushabikia michezoni ni kuwagawa watu makundi kutokana na siasa ile,wenye masikio na wasikie.

    ReplyDelete
  16. MAHALI GANI KWENYE T-SHIRT INAONYESHA HIYO TIMU INASHANGILI AU KUUNGA MKONO WAPALESTINE? MIMI NINAVYOFAHAMU HIYO KAMPUNI NI MFADHILI WA HIYO TIMU NA INAMAKAO MAKUU YAKE PALESTINE.

    ReplyDelete
  17. fullish,,,
    imekaaje kivipi,elezea kama wewe ni rijali tuone umu ndani
    wee kama stress zinakusumbua nenda kajipembue uko
    usilete habari za kijinga ivi
    afu weee michu???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...