mwanamuziki wa kongo anayeishi washington dc, samba mapangala (shoto) na wenzie wakimshangilia malkia wa taarabu bi. kidude aliyepanda jukwaani na kughani mistari kadhaa jumapili usiku ambayo ndiyo ilikuwa siku ya mwisho ya shoo za muziki ya sauti za busara katika ngome kongwe huko zenji. samba mapangala na bendi yake ya virunga walifunga pazia kwa kuvunja wadau mifupa hadi usiku wa manane.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. jamani nadhani wakati umefika tumpate panya anaeweza kumfunga paka kengele. Jamani ndugu zetu mliopo zanzibar tafuteni mtu wa kumuasa bi kidude awache haya mambo kwa umri alo nao.

    ReplyDelete
  2. bi kidude kwa umri wako na music wako ni nyota ya walioendelea. mungu akubariki uzidi kuishi na kutuburudisha. asiyekupenda aende na meli mpaka katikati ya bahari ya hindi akajitupe baharini akiweza aogelee. hata siku moja bi kidude usiwasikilize loosers. ninakueshimu sana kwa mungu kukupa maisha marefu na kuweza kuburudisha watu. usiache music kwani utachoka haraka sana. endelea kufanya what pleases you. hao wenye wivu na wewe ni wale wakifika miaka 50 wanakua vikongwe. BI KIDUDE GO GIRL

    ReplyDelete
  3. Anony wa 1:27am Naungana na wewe kumpongeza Bi Kidude..nashangaa watu wenye negative thoughts. Kwanza ni faraja kuona mzee kama yule bado anajitahidi kuendeleza kazi yake katika umri ule.Na kwa kujishughulisha namna hiyo kunapunguza athari nyingi zinazotokana na(umri)uzee. Na ntashangaa kama kuna mtu anamuona Bibi yule ni threat kwake kimuziki, basi huyo atakuwa ameishiwa kweli. Yule kwa sasa hivi anafanya kutumbuiza na kufurahisha watu hashindani na mtu sasa wivu wa nini?! Mwatakiwa kumpa heshima yake..Jamani!!

    ReplyDelete
  4. jameniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

    huyu bibi vipi?

    hebu apumzike.

    kwani hana watoto wamkalishe chini?

    mwenzie kafia kwenye daladala sasa

    yeye atafia stagini

    ReplyDelete
  5. Mnajua hashuo limemzidi na anahashuliwa huko kwao(maneno ya kizanzibari hayo jamani)
    kweli hata mimi naupenda mziki wake bt ukweli alitakiwa aache coz huyu anafika 100 nakitu miaka yake bt ndio hivo ''udongo upati uli maji'' ukizingatia mpk leo moshi anapuliza hiv kuna kumkumbuka mungu hapo,
    Niliwahi kupata story ya huyu bibi alivorudi toka germany miaka ya nyuma nlipokua mdogo,alipewa msala na mas'haf,sasa wadau wenzangu mlio upande wa kutaka astaafu mnajua alijibu nini mh!! ni hivi...anhelikua akisali angefika ulaya..n.k..(cjui imani hiyo aliipata wapi duh) so naamini ashakalishwa na kuambiwa kwa sana tu mpk leo but ndo hivo sikio la kufa haliskii dawa.. may be one day atajua km kuna kufa na mungu hupaswa kuabudiwa.

    mdau wa ughaibuni

    ReplyDelete
  6. sasa kaka mbona unabania comment yangu jamani!

    ReplyDelete
  7. Safi sana Bi Kidude. Endelea kutupa burudani bibi yetu. Maana taarabu ya sasa imekuwa kuchambuana tu. Tunahitaji kusikia taarabu ya asili.
    Ni jambo la kujivunia kuona bi Mkubwa kama wewe bado uko ngangari na hata mgongo haujakupinda. Vizee vya kizungu miaka hiyo vishapinda migongo na vingi havijiwezi na vishachanganyikiwa. Mimi kama mtanzania najivunia kukuona Ngangari.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...