LIYUMBA AKIONEKANA KUWASUTA WALIOMZULIA KUWA KAINGIA MITINI ALIPOINGIA KATIKA CHUMBA CHA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI WA KISUTU LEO.


MSHTAKIWA KATIKA KESI YA MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA NA KUSABABISHIA SERIKALI HASARA YA MABILIONI YA FEDHA AMATUS LIYUMBA AMEFIKA KATIKA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU JIJINI DAR ASUBUHI HII TAYARI KUENDELEA NA KESI YAKE, KINYUME NA UVUMI KWAMBA AMEINGIA MITINI ULUIOSAMBAA KILA KONA KWA WIKI NZIMA SASA.

HIVI SASA NI HAFTAIMU NA KESI ITAENDELEA BAADA YA MAPUMZIKO YA MCHANA. WADAU MSIKONDE WALA NINI. MTAPATA KILA KITU KABLA YA SIKU KUMALIZIKA LEO.
KUSIKILIKZWA KWA KESI HIYO KUMEMALIZIKA MUDA MFUPI ULIOPITA AMBAPO HAKIMU AMEMFUTIA DHAMANA YAKE NA AMERUDISHWA RUMANDE HADI KESI YAKE ITAPOTAJWA TENA MACHI 10, 2009.
ZOGO KUBWA LILIIBUKA KATIA YA UPANDE WA MASHTAKA AMBAO WALITOA OMBI LA KUFUTWA DHAMANA KWA WALICHODAI UKOSEFU WA UAMINIFU, NA UPANDE WA DHAMANA ULIODAI KWAMBA MTEJA WAO HANA NOMA WALA NINI.
UBISHI WA KWANZA NI PALE UTETEZI ULIPOSEMA LIYUMBA ALITOA PASI YA KUSAFIRIA KIMAKOSA KWANI MTOTO ALIYETUMWA KUILETA WAKATI WA DHAMANA ALILETA ILIYOEKSPAYA, BADALA YA MPYA. HATA HIVYO UPANDE WA MASHTAKA UMEHOJI KWA NINI LIYUMBA ALIONGOPA WAKATI WA MAHOJIANO KWAMBA HANA HATI INGINE.
KIMBEMBE KINGINE KILICHOMRUDISHA LIYUMBA RUMANDE NI HATI ZA MALI ALIZOTOA AMBAZO ZIMESHINDWA KUIRIDHISHA MAHAKAMA KUWA NI KAMILIFU.
angalia video ya liyumba leo mahakamani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 43 mpaka sasa

  1. Watanzania tutafanyiwa usanii mpaka lini jamani? Du!

    ReplyDelete
  2. hahah hii ndo kuonyesha hatuna Askari makini mtu kama yupo hapo hapo Dar wameshindwaje kumpata askari wetu mazezeta kweli du haya yetu macho tutaona kipi kinaendelea leo mdau atellenbosch

    ReplyDelete
  3. HONGERA BABU LIYUMBA KWA KUIBUKA KUJA KUPAMBANA NA KESI YAKO ANA KWA ANA. NAUNGANA NAWE KUWA HADI SASA HUNA HATIA YOYOTE HADI HAPO MAHAKAMA ITAKAPOAMUA VINGINEVYO.
    NAJUA WAZI KUWA ULISAINI MIKATABA ILE KWA ROHO SAFI KABISA WAKATI UKIKAIMU NAFASI YA UGAVANA WAKATI SHEMEJI YAKO BALALI ALIPOKUWA AKIKUACHIA OFISI ANAPOKUWA NJE YA NCHI AU MAPUMZIKONI.
    BALALI HAKUMWACHIA NAIBU WAKE JUMA RELI OFISI KUTOKANA NA UWEZO MDOGO WA KUFANYA MAAMUZI MAKUBWA KAMA YALE YANAYOHUSU MASLAHI YA TAIFA.
    ITHIBITISHIE MAHAKAMA KUWA HUNA KOSA LOLOTE NA KWAMBA HIVI SASA MAJENGO HAYO YANATUMIKA KAMA KAWAIDA KWA ASILIMIA MIA MOJA.
    AIDHA UGAWAJI WA VIGARI VYEKUNDU USIHUSISHWE KABISA NA KESI HII KWANI HAYO HAYANA USHAHIDI NA MAMBO YA NDANI YAFAMILIA.

    ReplyDelete
  4. Tarehe February 24, 2009 10:29 AM
    Sio Askari tu, TAKURU aka taasisi ya Kuizia Rushwa pamoja na Usalama wa taifa wamesema walikuwa hawajui alipo. Sasa hapo ndio utaona ni usanii

    ReplyDelete
  5. Pole sana kaka Liyumba,mungu atakusaidia afya njema uendelee na kesi yako.

    ReplyDelete
  6. TAKUKURU mpeni zawadi Liyumba kwa kujitokeza mwenyewe na aendelee na kesi yake.
    Amedhihirisha ujasiri mkubwa na kuonyesha kuwa Nahodha hatapiki baharini hata bahari ikichafuka sana kutokana na mawimbi makali.
    Sasa anazo nyaraka zote za kumuweka nje kihalali zinazofikia kiasi cha BILIONI 55.

    ReplyDelete
  7. Duh, PCCB ivunjiliwe mbali, haiwezekani kutangaza dau nono kwa mtu ambaye hata hajaingia mitini. ina maana wanausalama uwa PCCB hawana mbinu za kutress wahaliofu zaidi ya kuwakamata matrafiki.

    ReplyDelete
  8. Ni magazeti ya kijinga tu yaliyo sambaza uvumi huo kwamba katoweka. Mtuhumiwa tangia mwanzo alitakiwa kufika mahakamani tarehe 24 na hakutakiwa kufika popote pale kabla ya tarehe tajwa. Sasa iweje ikaripotiwa kuwa kaingia mitini! Hakuna gazeti hata moja iliyokwenda kumhoji wakili wake anayejulikana kujua ukweli au kumuuliza kama ni kweli hajui aliko mteja wake! Watanzania tuache uvumi na uzushi usio kuwa na maana. Jamani!

    ReplyDelete
  9. Huyu mtu kalisababishia Taifa hasara ya mabilioni ya fedha za wavuja jasho. Hivi kweli anaweza kuichezea serikali namna hii? Polisi wanasema hawakuwa na hati ya kumtafuta wala kumkamata, Takukuru wanasema walikuwa wanamtafuta kila pembe. Hapana huu ni mchanga wa macho, hivi vyombo vya dola vilikuwa vinajua kabisa Liyumba yuko wapi na vilichangia kumficha. haya yetu macho na masikio - Michuzi endelea kutupasha.

    ReplyDelete
  10. Wakili wake alisema ukweli kuwa jamaa aliamua kupumzika. Sasa swali ni kwamba vyomba vya habari tuviamini kwa kiasi gani? Mithupu nawe ni mdau wa vyombo vya habari, so hapo samahani kidogo. Vyombo vyenu ndivyo vilikuza sana swala hilo.
    Watanzania tuwe makini maana hapo akili zetu zinachezewa...
    Lakini pia jamaa anahoji uwajibikaji wa vyombo vya dola ikiwa ni polisi walishindwa kweli kubaini alipokuwa? Basi Liyumba ni zaidi ya Zombe kwa utaalam.. au ndo kusema alikuwa na pesa nyingi za kuwafumba midomo kila askari aliyekutana naye...

    Mdau Mbeya.

    ReplyDelete
  11. Liumba ana soo harafu anajitafutia umaarufu kimtindo...wabongo visa, teheheeeee

    ReplyDelete
  12. ukiwa na hela bwana yote yawezekana!!!!!!!!!!!!!!wizi mtupuuuuuuuuuuu.

    ReplyDelete
  13. Dont be Fooled Danganyikans!Liyumba and Kweka are not the Culprits who should really be brought to court!Taken for a Ride!Hii kesi upelelezi wake utaendelea hadi 2010!How many of you will have died of AIDS? sticky itchy!

    ReplyDelete
  14. come on brother michuzi!!! utasemaje ni uvumi? jamaa hakufika mahakamani siku alotakiwa kufika na hadi wadhamini wake hawakujuwa aliko na matokeo yake wakasukumwa mahabusu, sasa unataka kusema kuwa hayo yote ni uvumi tu? muda wote huo alikuwa msalani hapo hapo mahakamani ila mlango ulikuwa haufunguki? huyu jamaa kajaribu kutoroka nchini na ameshindwa plain and simple. Na kwa masharti ya dhamana yake huyu anatakiwa kurudi rumande kwani alishindwa kufika mahakamani siku alotakiwa bila ya udhuru wowote na mawakili wake walishindwa kueleza sababu za kutokufika kwake. Pia kama mie ndie mmoja wa wadhamini wake nadhani kwa sasa ningelijitowa kwani jamaa haamiki na hajali mtu yeyote ila nafsi yake tu.

    ReplyDelete
  15. HUYU MTU ANA KESI MBILI HIYO YA MABILIONI NDOGO KUBWA NI ILE WA NYEKUNDU!!!

    ReplyDelete
  16. Duuuuuuhhhhh!!!! Guy can play with everybody's brains!! Yani anotweka na kuibika atakavyo. Hiyo si kali kweli. Manake mtu wa system huyu, sio kingine, na kaibuka tu baada ya kuhakikishiwa mambo yatakua shwari. Corruption is like one-hundred headed snake, ukikata kichwa upande huu kichwa kingine kinaibukia upande mwingine. In short, hapa watu wanacheza mduara tu.

    ReplyDelete
  17. huyo jamaa inabidi apigwe kama six month behind the bars kwa violation ya bond yake then baada ya kifungo ndo kesi iendelee manake akiachwa hivi tu mwisho anaweza kuja toroka kwa helcopta kama kule mijamaa ya ugiriki

    ReplyDelete
  18. Ahsanteni sana manake kwa kisa hiki tumeuza magazeti kama njugu!

    ReplyDelete
  19. Mhuu!watu wa bongo kwa usanii hawawezekani. Haya usikute hata hata hiyo kesi feki!

    ReplyDelete
  20. Uzushi umezidi,magazeti mmeuza, majungu ndio jadi yetu. Tafuteni story nyingine.

    ReplyDelete
  21. liumba lazima kuna watu wengi wakubwa wameusika hata gavana wa sasa hivi alikua bot na amekula panga...
    ndiyo yale ya richmond wapambe ndio wanafikishwa mahakamani king pin haguswi.....
    kuna watu wengi sana wako nyuma yake lakini hawatajwi

    ReplyDelete
  22. Kazi kwenu Liumba kanyimwa dhamana. How on earth could he give an expired passport and yet hakimu akaikubali? Inaingia akilini kweli hii. Wakati hiyo sio official document tena. Jamani nakubaliana na SPika Sita kuwa mahakimu wengine mm mm mm non non. Aibu na fedheha tupu. Jaji Mkuu kazi unayo

    ReplyDelete
  23. Kazi kwenu Liumba kanyimwa dhamana. How on earth could he give an expired passport and yet hakimu akaikubali? Inaingia akilini kweli hii. Wakati hiyo sio official document tena. Jamani nakubaliana na SPika Sita kuwa mahakimu wengine mm mm mm non non. Aibu na fedheha tupu. Jaji Mkuu kazi unayo

    ReplyDelete
  24. Usije ukashangaa stori nyingine ikakuhusu wewe mwenyewe, kumbukeni yale mliyoyafanya kisiri, wewe wakati upo kwenye ile kampuni ambayo sasa imefilisiwa ulifanya nini? Pekenyu pekenyu utakutwa na wewe, ili tuuze magazeti!
    M3

    ReplyDelete
  25. Bro mithupu! mi nashangaa kuna baadhi ya wadau Wanaonesha kwa wazi kabisa kumtetea huyu Bwana mkubwa LIYUMBA, Inawezekana ndo ndugu zake au ndo wale anaotafuna nao yale mabilion? Wakati sie akina KAYUMBA tuna kula kwa kubangaiza? Ni kweli kabisa mahakama ndo itabaini kama ana hatia ama la, but walio mfungulia mashitaka sio wabumbavu,kumpeleka kortin mtu asie husika.Hata kama hakuhusika moja kwa moja. basi kwa njia moja ankesi ya kujibu.
    bro mithupu ninamachungu sana na watu kama hawa,nshafikia hatua mbaya ya hata kujilipua angarau watu kama hawa wapungue ili ndugu zetu mtakao baki muishi in peace and I can rest in peace.

    mdau GEITA

    ReplyDelete
  26. Du,Kaaaaaaaaaaaaaaaaaazi kwelikweli! hatimaye singo ya liumba kutoroka imexpire, kama kawaida wabongo tuanzishe nyingine ya kusukumia siku ziende! wazungu wakizungumzia masuala ya ubunifu na maendeleo sie tumekalia uzandiki na majungu

    ReplyDelete
  27. NewsUpdate:The Daressalaam Rumour Mill is believed to be the biggest employer in TZ,employing about 95% of the DSM active workforce whose pa capita income is pegged at US Dollars 0.005!How do people survive under those circumstances!Jeeez!Beat that record East Africans if you can!

    ReplyDelete
  28. POLE MPENZI WANGU UTASHINDA TU

    ReplyDelete
  29. Duh jamaa NI bongE la msanii wa kweli kaanzisha movie na watu wote macho kwa Liyumba kumbe yupo tuu kapozii na mambo yake anaweka sawa kweli nimeamini kuwa hizi ni kesi za wasanii wa kundi la uchaguzi wa mwaka 2010 tusubiri ile ya EPA nayo ita kufa kifo kidogo kidogo mpaka tunatahalalisha wenyewe MWISHO KUWA HAWANA KESI YA KUJIBU
    MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  30. hii kesi ni laini sana ndiyo maana hata yeye amerudi hawawezi kumfunga eti amesababishia hasara serikali. Hawana ushahidi kama alichukua panga na serikali ikisema alichukua panga hapo kesi itakuwa ngumu zaidi kwao kwani watatakiwa wadhibitishe kitu ambacho hawawezi. Adhabu ya kusababishia hasara serikali ni kufukuzwa kazi...hahaha

    ReplyDelete
  31. hii kesi ni laini sana ndiyo maana hata yeye amerudi hawawezi kumfunga eti amesababishia hasara serikali. Hawana ushahidi kama alichukua panga na serikali ikisema alichukua panga hapo kesi itakuwa ngumu zaidi kwao kwani watatakiwa wadhibitishe kitu ambacho hawawezi. Adhabu ya kusababishia hasara serikali ni kufukuzwa kazi...hahaha

    ReplyDelete
  32. hii kali........sasa ofisi zetu za uma uwajibikaji uko wapi namaanisha polisi na takuru. sioni sababu kama mtu yuko tanzania mshidwe kumpata

    mdau neth

    ReplyDelete
  33. Hivi huyu KAYUMBA ni nani, maana kila kona ni KAYUMBA! KAYUMBA!

    ReplyDelete
  34. that's TZ people, ndo hali halisi. Get your money and you can do anything, play with/against anyone, and be goddamn sure you'll win. It's a comedy, and everyone is watching it and laughing. How a man can make fun of the whole system and live to talk about it is beyond me. But it happens. In tanzania. Brace yourselves up for more comedy, and just accept it as it is becoming part and baggage (not parcel) of tanzanianism.

    mungu tusaidie, tuokoe........

    ReplyDelete
  35. HIVI MNAOLAUMU MAGAZETI MNA AKILI TIMAMU KWELI?

    NDIYO MAANA WABONGO TUNABAKI MALOFA, WAKENYA WANATUPELEKA MBIO, NYUMBA ZA SERIKALI ZINAPORWA NA TAIFA STARS INAFUNGWA.

    SI WOTE TULIONA PICHA ZA WALIOMUWEKEA DHAMANA WAKIWA MAHAKAMANI BAADA YA LIYUMBA KUTOFIKA MAHAKAMANI KAMA ALIVYOTAKIWA.

    SASA MNASHANGAA NINI NA KULAUMU MAGAZETI?

    KWELI UMASKINI WA AKILI NI MBAYA KULIKO UMASKINI WA MALI!

    ReplyDelete
  36. HAKI YA MAMA
    nimechoka kabisaaaaaaaaaaAAAAA,,,dah chekundu?

    ReplyDelete
  37. Eti ana kishimo (handaki) nyumbani kwake mithili ya kile cha Hussein wa Iraki?

    ReplyDelete
  38. Hapana ana kiorofa ndani ya orofa!

    ReplyDelete
  39. Wewe anon wa February 24, 2009 11:27 AM, jaribu kufanya home work kidogo kabla ya kuanza kuwatuhumu waandishi na wadanganyika wengine. Unaposema Liyumba a.k.a wa kuliboma hakutakiwa kufika mahakamani kabla ya 24/2 una maana gani? Ina maana hata TAKUKURU waliotoa ofa ya donge nono kwa mtu mwenye taarifa za mtuhumiwa hawakuwa na kumbukumbu hiyo kwenye nyaraka zao? au yule hakimu aliyetoa amri wadhamini wa Mtuhumiwa wakamatwe kwa kuwa mtuhumiwa hakufika mahakamani alichanganyikiwa? au kulikuwa na sababu gani nyingine ya wao kukamatwa?. Vyombo vya habari vimeripoti kile walichoambiwa kwa hiyo mimi sioni kosa lao

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  40. We mdau wa cardiff, fuatilia sakata lote kabla ya ku-comment! Wadhamini walifika mahakamani baada ya madai kwamba Liyumba katoweka au hajulikani aliko. Kwa kawaida, mdhamini hutoa guarantee kwamba mtuhumiwa atafika mahakamani siku iliyowekwa sio vinginevyo - na hii ndio maana waliachiliwa huru kwa sababu siku waliyo guarantee ulikuwa haujafika. Isitoshe, kwa kawaida, anayefika kortini sio mdhamini bali ni mtuhumiwa pekee ambaye asipotokea ndipo hakimu atatoa warrant ya kuwataka wadhamini waeleze kwa nini wasiswekwe ndani. Papara za Takukuru tu - mchanga wa macho tu hii

    Tunasikia kwa watani wetu kenya, bodi nzima ya Uchumi supermaket wana kesi mahakamani kwa maamuzu waliofanya kuuza jengo hasara. Kwa nini hapa hatuoni bodi nzima ya BOT wakiwajibishwa kwa maamuzi yao katika ujenzi wa twin towers. Kweka na Liyumba ni watu wadogo sana hata ngazi ya unaibu gavana hawafikii.

    ReplyDelete
  41. hapa naona ligi ndo kwaanza imeshaanza na mshindi wa ligi hii ya ubishi tutamtangaza soon msikonde wadau wangu bye

    ReplyDelete
  42. Liyumba ataidhinishaje ujenzi wa yale maghorofa mawili ya benki kuu?Yeye ni Karani tu (desk officer) pale benki kuu!Eti kwa kuidhinisha ujenzi "akaisaba-bishia serikali hasara(hasira) ya bilioni 221!Serikali ilikuwa wapi?Kwanini Bodi ya Wakurugenzi isikatae?Kwanini Gavana wa Benki Kuu asikatae?Kwanini Waziri wa Fedha naye pia asikatae? Cummon Danganyikans!

    ReplyDelete
  43. khaa kuna watu wana sura za confidence yani kwa msisitizo sura za ujasiri,,,kama uyu bwana!
    adi kesi itaisha tu kiaina-aina kwa sura hili

    mbona jamaa anajiamini ivo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...