Chuo Kikuu cha University of Dodoma

Bwana Misupu,

naomba tujadili hii issue ni juzi tu hawa ndugu zetu (watani wa jadi) walikuwa wanalalamika eti wananyanyapaliwa kwenye kazi bongo sasa kama majigambo yao yote ya kusoma yanaishia kutoa vyeti feki hizo sifa wanazohitaji kupewa zi wapi? naomba wadau wachangie!

Mdau Ujerumani


mambo zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. sio chuo kikuu cha university of dodoma,umechapia,kama hujui ngeli andika kibongo tu,
    ulitakiwa uandike "chuo kikuu cha dodoma" au "dodoma university". kama lugha haipandi,andika tu hiyo lugha ya madafu yenu hiyo..

    ReplyDelete
  2. That right! nilitaka kusema hivyo hivyo amechapia, rekebisha kiswahili hicho!

    ReplyDelete
  3. We comment ya kwanza ndo mshamba umeingia lini hapa kijijini? naona huna hata siku tatu....anewei msalimie my wife wako....nahisi pia unaishi karibu na barabara ya bagamoyo road....Bye

    ReplyDelete
  4. 1.Ndugu yangu hajaelewa idiom na venacular ya blog yetu ya jamii.Humu tiunasema mai wife wangu tunaandika chuo kikuu cha university of Dodoma.Hii ndiyo lugha yetu katika blog hii, karibu!It is an essential part of what characterises the Michuzi Blog brand.
    2. Lakini kwa upande wa vyeti feki vya watani vilivyogunduliwa chuo kikuu cha University of Dodoma (sic)je tunajuaje na huko kwenye ajira zingine hatuna vihiyo wa kikenya? Je kweli watanzania kweli tuko macho katika ajira zingine nje ya sekta ya elimu ya juu? Hakika elimu ya sekondari na ya msingi tunaliwa. Kwenye mabenki je na kwingineko?
    3. Hawa watani zetu wana mantikim ya ajabu wanpo ng'ang'ania land sharing kwenye ushirikiano wa Afrika ya mashariki. Kukodolea macho kwao ardhi yetu kunatokana na ufisadi wa ardhi uliyofanyika enzi za ukoloni na ukaendelezwa na watawala baada ya uhuru nchini kwao- kuna wakubwa wana ardhi saizi ya wilaya nzima.Sasa wanataka eti land sharing ili wale waliokosa ardhi kwao kwa sababu ya ufisadi wao wawsukumie Tz au wanataka kuendeleza ufisadi huo kwenye ardhi ya Tanzania. Sera za makusudi ya kumiliksha dola ardhi zilituepusha na ufisadi huo hapa kwetu. Na wao wakifanya sera za makusudi wanaweza kuepukana na tatizo hilo. Hivi kweli inaingia akilini kwamba ufisadi wetu wa TZ wa EPA kwa mfano au Richmond ufidiwe na pesa kutoka Central Bank of Kenya? Kama haiingi akilini, basi vivyo hivyo haiingi akilini eti kuwe na land sharing ili kutatua taizo la ardhi la Kenya au nchi yoyote nyingine ya Afrika ya Mashariki ambalo linatokana na siasa hovyo na ufisadi.
    4.Mwisho hivi kuna nchi katika Afrika ya Mashariki inaweza kutufundisha Tanzania Land Sharing?? Hakuna. Tuna wakongo, warundi, wanayarwanda na wengineo kadhalika ambao tumewapa ardhi na uraia, hifadhi ya kisiasa na uwezo wa kupigania haki kutoka siku nyingi. Kenya au Rwanda zimewahi kufanya nini katika hili? Suluhisho ni nchi zote za Afrika mashariki kuondokana na siasa za ukabila na ufisadi ili ziondokane na matatizo ya ardhi na ziache kutamani, kuonea wivu na kukodolea macho ardhi ya majirani zake.Hata misahafu inakataza tabia hii jamani!
    Kaka Michuzi hii comment muhimu pandisha juu kabisa isomeke wadau wakiiingia tu kwenye blog. Sijui viongozi wetu wa siku hizi wanawaonea aibu watani wetu wa jadi. Ni muhimu kuewapasha laivu mara moja moja hawa watu.

    ReplyDelete
  5. WEWE UNATULETEA MJADALA FEKI, HIVI NI KWELI KENYA WANA VYETI FEKI? AU UNATAKA KUTUONESHA KUWA WEWE NI MZALENDO? HEBU TUELEZE WALE WALOKUWA WAKIJIBU MASWALI TOKA KENYA WAKATI WA MASHINDANO YA VYUO VIKUU VYA AFRIKA MASHARIKI NA KATI WALIKODISHWA TOKA BONGO? IWEJE WENYE VYETI FEKI WAMEKUWA NI KATI YA WASHINDI NASI TUKISHINDWA MIAKA YOTE. MBONA MAMBO YAO YA UCHUMI YAKO JUU, HIVI KWA UJINGA WAKO UNAONA PESA YETU IKO JUU YA YAO. UNAJUA VINGI VYA VIWANDA VYAO VILIVYANZA KABLA HAUJAZALIWA MPAKA KESHO BADO VIPO, VYETU VIKO WAPI? ACHA MAJADALA USIO NA TIJA.

    ReplyDelete
  6. annon 10.55pm we mgeni nini humu jamvini?

    ReplyDelete
  7. 7:33 Una matatizo ya kufikiri.Nyie Ndo Mzee Mkapa alisema wavivu wa kufikiri.Umekwisha ambiwa kuna vyeti fekikutoka Kenya (a fact) kwa wale walioomba kazi ya Ulecturer pale UDOM, sasa una chopinga ni nini ? hiyo fact au mawazo yako ya mgando?

    ReplyDelete
  8. Ni vema basi tuwe pamoja. Naomba ambao hawajapata habari ya vyeti feki wasome basi The East African ya tarehe 9-15 February 2009. Nadhani inapatikana mitaani Dsm tangu jana na vile vile iko www.theeastafrican.co.ke. Gazeti hili la Kenya linachapishwa na The Nation Media Group ya Kenya na wiki hii edition inmayosambazwa Tz inaongoza na taarifa yenye kichwa cha habari 'Fake Kenyan teachers rushing for plum jobs in Tanzania', ukurasa wa mbele kabisa.Mimi nina hakika tatizo letu kubwa kuhusudu tu vitu vya kigeni mradi cha kigeni.Sisemi hakuna vya kigeni vizuri lakini kuna kasumba imetuzidi ya kutukuza cha kigeni klwamba bora, na huo ndiyo mwanzo wa kutapeliwa kwetu. Kama wanadiriki kujaribu kututapeli ngazi ya chuo kikuu basi primary na sekondari ndiyo wametumaliza kabisa- tukisikia tu kiingereza na anatoka Kenya au Uganda basi tunajua mwalimu bomba.Hapana lazima tuamke na tuchunguze na kuchanganua zaidi- shule haziwi bora kwa kuitwa jina la kizungu (kama Green Acres, au St Kitugani wakati iko kwenye vumbi) na kuwa na waalimu wenye kuzungumza kiingereza cha kubahatisha na wenye uraia wa kigeni.Tunatapeliwa na tukubali tunatapeliwa tuamke.

    ReplyDelete
  9. Mnajua nyinyi msiwe wajinga na upeo duni wa kufikilia kwa kutumia criteria ambazo hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kufikilia,mtu na akili zako unaweza kusema eti yale mashindano ya celtel ndo kigezo cha kenya kuwa juu kielimu kweli?au sarafu ya shilingi ndo kigezo cha uchumi bora?au unataka niambia shilingi ya kenya ambayo ina thamani kuliko Yen ya japan basi Kenya ipo juu zaidi ya japani si ndio?jamani tuwe tunafikili kwa kutumia vichwa na sio nyayo za miguu wakati mwingine,Kiingereza sio kigezo kabisa ndugu zangu na iyo celtel nijui ni mashinddano kama ya imla tu ambapo watu wanafanya Publicity ukiniambia kenya wameshinda kwa kutoa Research bora katika vyuo vya Afrika hapo nitakubaliana na wewe

    ReplyDelete
  10. 1.Nyie mnaoleta habari za kukosoa lugha ya kiblogu nadhani ni wageni, hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa ku-comment then asifahamu kwamba mtu chuo kikuu cha university of dodoma si lugha sahihi, anafahamu bali hiyo ni lugha iliyozoeleka ki blogublogu.
    2.Na wewe unayeleta habari za celtel (Zain) university challenge huelewi kinachozungumzwa kwenye hii mada, fact ni kwamba kuna vyeti feki kutoka Kenya vimekamatwa na c kwamba wapi ni bora kielimu!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...