Rais Jakaya Mrisho Kikwete amerejea Dar Es Salaam mchana wa leo, Jumapili, Februari 8, 2009, kutoka Mkoani Shinyanga ambako jana alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za miaka 32 ya kuzaliwa Chama cha Mapinduzi (CCM), katika nafasi yake kama mwenyekiti wa taifa wa chama hicho.
Rais Kikwete ameondoka mjini Shinyanga leo asubuhi kwa gari kwenda mjini Mwanza, ambako amepanda ndege kurudi Dar.
Rais Kikwete alitumia sherehe za jana kukiandaa chama chake tayari kwa Uchaguzi Mkuu wa mwakani, akisisitiza kuwa maandalizi tayari yanaendelea kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Akizungumza na maelfu ya wananchi kwenye Uwanja wa Kambarage, Rais Kikwete pia alisisitiza kuwa nia kuu ya CCM, kama ilivyo kwa chama chochote cha siasa duniani, inabakia kukamata na kudumisha madaraka ya kuongoza dola. “Chetu siyo chama cha mpira kama Yanga na Simba…”
Rais pia alitumia nafasi hiyo kukemea kwa mara nyingine tena mauaji ya vikongwe na maalbino kwa sababu za kiushirikina, akisisitiza kuwa ukatili huo kamwe hauwezi kuvumilika. Mkoa wa Shinyanga unaongoza katika mauaji ya makundi yote hayo mawili ya wananchi.
Aidha, Rais alitangaza hatua za Serikali kupunguza kiwango cha gharama ya kuunganisha maji kwa wananchi wa Kahama na Shinyanga, ambao watanufaika na maji kutoka mradi mkubwa wa maji kutoka Ziwa Victoria.
Vile vile, aliondoa sharti ya watu kulipia kwanza gharama za kuunganishiwa maji, akisema kuwa watu waunganishiwe maji na walipe gharama hizo hatua kwa hatua.
Mradi huo unaonufaisha watu nusu milioni kwa sasa, utanufaisha watu 1,000,000 ifikapo mwaka 2025, na umekamilika kujengwa kwa fedha ya Serikali ya Tanzania. Mpaka sasa kiasi cha sh bilioni 227 zimetumika kwa ajili ya mradi huo ambao sasa umefikia hatua ya kutawanya maji kwa wananchi.


32 years of CCM,we have had 4 presidents interchangeably,and we have come this far!One would have expected tremendous reformations towards increased Democratisation!Hata vumbi halijatulia la uchaguzi wa 2005 tayari watu wanazungumzia uchaguzi wa 2010!I think we need to change!Hatuwezi kwenda namna hiyo.Hatutafika.Hii dhana ya kupokezana "Vijiti"sidhani kama sisi watanzania itatufaa.Kila awamu ya uongozi ipewe majukumu yake na ibanwe kivyake kwa utekelezaji wa majukumu hayo na si vinginevyo.Kiongozi aliopo madarakani akishindwa kutimiza ahadi zake asisingizie mapungufu ya viongozi wenzake waliomtangulia.Lazima yeye abanwe na apimwe yeye kama yeye.This country has been led by Dogmatic Utopia ever since,from the word go in 1976 when some of us began our first employment in the govt after graduating from the University of Dar es salaam.So much Damage has already been done to this economy that went on unchallenged!Because such was the system!But now we would expect Kikwete to see things differently!Alas,but to no avail!The same menu of leadership style and momento!Protecting the status quo and political greed!No need for change.The Party Credo is there to stay,no matter what!The economic Rot notwithstanding!We now have more mouths to feed than ever before.We can not remain complacent.We can not afford decadent ideology of the "Five Wisemen!".Time to hatch out.You can fail in so many things,but you can't afford to fail "EVEN TO LISTEN"!-close to you-
ReplyDeleteJK muombe Obama akupe mazoezi yake, au vaa mashati makubwa mzee, viongozi ywa vitambi ni zamani ya kina Kawawa na wengine!!!
ReplyDeleteNafahamu mzee wakati utakuwa mdogo wa mazoezi lakini usijiachie kabisa. Wote tunaona fahari kwa uongozi wako, Tanzania ni moja ya nchi chache sana kwenye Bara hili la Afrika ambayo tuna amani na usalama, of course tunayo matatizo yetu amabo ni vigumu kuwepuka. Vile vile CCM ni chama cha siasa, tufasifanye na kuabudu kama dini, unaweza kuwa raia mzuri bila ya kuwa mwanachama wa chama cha siasa, ukweli na kuchagua chama au kiongozi inatokea siku ya kupiga kura kukubali chama kipi kitasaidia nchi au vipi. Sioni lazima ya watu kuwa na kadi ya chama, hiyo ni karatasi tu amabo wengi wanaichukua kwa sababu nyingine zaidi kuliko kusapoti chama.
mganga wa kienyeji/mchawi uyo au?si ndo waziri mkuu kawapiga marufuku kumbe ktk chama "letu" bado wamo tu?sasa tunafuta leseni za nini if wanatambulika??!!!
ReplyDeletenashangaa rais na waziri tofauti
kaaaaaazi kweliii