

Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hawa madiwani hawana cha kutusaidia kabisa,maana hata sijui kazi yao. Natamani bunge liwafute maana vyeo vimezidi hadi watu kutojua majukumu yao, na kuishia kukataza tu kila kitu.Kuma diwani mmoja wa maeneo ya kimara huku ye ndio balaa yaani katugeuza wakazi wa kimara rasilimali yake.Anakila dili na dawasco wasifungulie maji hata wiki tatu mfululizo ili diashara yake ya kuuza maji ichanue akishavuka lengo jamaa ndio wanaruhusu maji,huku wananchi wake wakiwa taabani kwa kukosa maji.Mwisho wa siku kila mwenye center kaamua amuige kubeba tanki la plastiki nao kupiga dili haramu,kila kona utakuta watu wanauza maji wakati kimara kuna tanki kuubwa tu la maji likihudumia maeneo ya sinza kijitonyama na daabhi ya sehemu za katikati ya jiji.Siku moja tukaona ni ujinga kumvumilia tukavamia nyumbani kwake baruti tukamrubuni mlinzitukamfunga kamba kina mama tukawafungulia geti tukafungua matanki yake raia wakachota maji yake buuuule kwa masaa takribani manne hadi raia wakatosheka yaliyobaki tukayamwaga yote tukaanza. Na tulifanya hivyo makusudi baada ya kuteswa sana na uhaba wa maji wakati kwake maji hayakauki.Makamba alifungua kisima ili wananchi wawe wanachota maji ,duh tulitumia siku 5 tu jamaa akaweka stopper akaunganisha bomba hadi kwake na kwake kaweka pampu kuvuta maji yote yaende kwake ili afanye biashara. Sasa hapo mtasema mnadiwani au mwizi tu type za EPAZ
ReplyDeletePresidaa angetembelea na huku ili tumchomee huyu diwani anaitwa M....o
NB:sijatoa jina najua utaibania tu maana ni diwani kwa tiketi ya CCM
Jamani wakati mwingine na sisi wananchi tunalea mambo ambayo hayafai. Sasa wananchi wa Kimara Diwani kama huyu anafanya mambo ya ambayo si ya kibi naadamu kama hivi, na nyie mna ushahidi wote kama hivi alivyoeleza mdau., kwanini msimuanike siku zote hizo mnasubiri mpaka mada juu ya madiwani itoke kwenye globu ndo mueleze, tena sio kwenye "front page" ni humu ndani ambapo pia inaweza isionekane vizuri. Kwani huo udiwani si kapewa na wananchi wa eneo la Kimara ?!Huyu hakuteuliwa na Raisi, hivyo wananchi wenyewe mnauwezo wa kudili naye, wala msisubiri mpaka Raisi atambelee huko.
ReplyDeleteSasa kama JK alicheza hapo na anaona hali halisi ilivyo sasa na anakaa kimya wengine wafanyeje?
ReplyDeleteKili
BG
CCM NAMBARI WANI OOH! NAMBARI WANI NI CCM. TUNAMLAUMU NANI? SISI WENYEWE NDIYO TULIOTAKA TUWE NA MADIWANI WA CHAMA KIMOJA, HAYA NDIYO MALIPO YAKE. WAO WANAVAA SUTI NA LUNCHI KWA RAISI HUKU SISI WAKITUACHA KWENYE UCHAFU ULIOKITHIRI.
ReplyDeleteALBINO ACHENI KUJIINGIZA KWENYE SIASA, TATIZO LENU SI LAKISIASA NA NYIE SI WATOTO WA WANACCM TUU. KAULI ILIYOTOLEWA NA WAZIRI MKUU HAIKUWAKERA WAPINZANI TU KAMA MNAVYOSHAWISHIWA NA WANA BAADHI YA WANACCM KWANI WATANZANIA WENGI HATUKUAMINI KAMA KWELI WAZIRI MKUU ANEWEZA KUTAMKA HILO AMBALO LINGEWEZA KUTUMIWA VIBAYA NA KUSABABISHA VURUGU. WAPINZANI PIA WANA WATOTO NA NDUGU AMBAO NI ALBINO, MJUE HILO. HAMTALINDWA NA WANACCM TU BALI NA WATANZANIA WOTE.
ReplyDeleteasante annon wa kwanza umesema kweli,,yan kimara hakufai jamani hakuna maji kabisaaaaa na ni mradi wa mtu pale,,,
ReplyDeleteuyu diwani awajibishwe shenzi zake sana,nyamafu sana (michuzi sijachafua lugha post hii0
job description za madiwani zikoje?
KIMARA JAMANI KUIANGALIWE
Mimi hapa nitawatetea madiwani hasa kuhusu sehemu kama hizi. Ninakumbuka miaka mwanzo ya 2000 bustani hizi zilikuwa wazi ila tatizo ni kwamba jamaa wengi walikuwa wanazitumia kama sehemu ya kujisaidia, haja kubwa kama uyoga vile. Wale ombaomba wote hapo ndiyo ilikuwa sehemu yao ya kulala na kupika na kujisaidia.
ReplyDeleteUshauri wangu mi kwamba: Hawa madiwani wazitengeneze sehemu hizi waweke vyoo na kuweka mwangalizi wa kudumu ambaye kazi yake ni kucharge kiingilio cha shs hata 50 kwa kichwa ili watu wenye kupenda kupumzika wapumzike, Ila suala kubwa na wale migambo wanapita wanatia minyororo magari baadhi wawekwe hapo kupambana na vibaka ili kuimarisha ulinzi na usalama wa watu, vinginevyo sehemu hizo zitakuwa KOSOVO yaani mtu akitia mguu tu anatoka kama alivyozaliwa vibaka wanamnyang'anya kila kitu mpaka nguo.
Alternative vijengwe vituo vya polisi katikati ya bustani kwa ajili hiyo tu waweke na Camera za kucheki usalama eneo lote, hayo ndiyo matumizi ya kodi zetu sio kulipana posho tu.
Hii system yetu Mzozo tupu.
ReplyDeleteDAR jiji(Mkoa mdogo)kuliko yote Tanzania nzima,lakini kuna
1-MEYA
2-MKOA WA MKOA
3-WABUNGE
4-MADIWANI
5-WAKUU WA WILAYA
6-MKUU WA POLISI
7-WAKUU WA POLISI(MANISPAA)
Hao wote wanashughulika kulitumikia jiji.Matokeo hayaonekani.
Tunahitaji mtaro mkubwa saizi ya mto kupeleka maji ya mvua (na maji taka) yatokayo Hananasif, kukusanyika Bonde la Mpunga, Maandazi Road na Babeque village, Shule ya Msingi Msasani ili yaende baharini.
ReplyDeleteMadiwani, Meya na Mbunge wa maeneo haya wanahitaji msukumo kutoka kwa JK. Wananchi tuko tayari kuchangia. tunahitaji mtaalamu kusimamia na ramani tu.
Hatutaki kusubiri mafuriko.
Mdau Mkazi
Mimi jamani wadau naomba msamaha mapema kama nakosea.
ReplyDeleteNinachokiona na ambacho kinanisikitisha ni kuwa Bwana JMK anatafuta umaarufu rahisi (cheap popularity) na kuandikwa vizuri kwenye vyombo vya habari.
Hivyo anawaita watu na kuwasema ili sisi wenyenchi tuone anafanya kazi.
Lakini kiukweli hii si maana ya uongozi na si tulichomtuma kufanya.
Kazi yake kama kinara mkuu tuliyemkabidhi nchi ni kuweka sera safi, bora na zenye kueleweka na kuzisimamia vyema na kwa ushupavu.
Itakapofika wakati wa uchaguzi au wakati wa kuandika historia hatutajiuliza au kupima aliwasema sana wazembe bali ameweza kufanikisha nini na ameweza kuweka msimamo na muongozo gani.
Maana ukiwasema madiwani, au TRL, TRA, Bandari, nk basi utuambie kabisa pia kuwa mawaziri husika kazi imewashinda maana wewe ndie uliewateua.
Huwezi kuamka ukaanza kuzungumzia ufukwe, kesho bustani keshokutwa barabara za juu bila kuitizama kwa ujumla sera ya mipango miji, Makazi mijini na pia mfumo mzima wa serikali za mitaa na majukumu yake.
Hii ndio kazi ya Rais na timu yake ya Serikali kuu na sio kukaripia watu.
Na kwa jiji la Dar Es Salaam Master Plan yake, Makazi ya watu, sehemu za biashara na viwanda, bustani, Parks, huduma za jamii, ulinzi na usalama, nk.
Kwa mfano mpaka leo (miaka karibu hamsini ya uhuru) serikali yetu haijaweza kuainisha ni nini maana ya nyumba ya kuishi katika miji yetu. Lazima iweke standards na pia uwepo utaratibu maalum wa ujenzi. Na pia ni nini nafasi ya serikali katika kuhakikisha kila mtanzania anakuwa na makazi bora.
Kuna tatizo kubwa pia la uwiano wa makazi. Na hili linachangia sana katika swala zima la usafiri, huduma za jamii, na shughuli za kiuchumi.
Kwa mfano sehemu kubwa ya wenyenazo Dar wanaishi upande mmoja wa jiji na wale wasionazo wanaishi upande mwingine na hii linaathiri sana mzunguko wa hela na pia unadidimiza ukuaji wa shughuli ndogo ndogo za kiuchumi. Kwa maana wenyenazo hawaendi manzese, tandale, kigogo, tandika, n.k, kutumia hela zao. Matokeo yake ni kuwa haya maeneo yanazidi kudumaa wakati wenye nazo wanazidi kujenga kuelekea, bagamoyo na Mtwara huku maeneo yaliyopo karibu kabisa na jiji yanakimbilia kuwa kama Kibera, Nairobi.
Kwa upande wa usafiri kwa kuwa hakuna utaratibu katika ukuaji wa jiji basi hadi leo wote inabidi tuelekee Posta mpya au Kariakoo asubuhi na jioni tunarudi.
Serikali yetu sidhani kama watu wanakaa wakafanya debate ya sera ila inaonekana mpaka watu wa nje
( UNDP,IMF, EU, nk) waseme fanyeni hivi basi kwa kuwa wanatoa posho za vikao basi watu hao tunakurupuka tunafanya.
Jamani viongozi wetu wafanye kazi zao na sio watake tu kuonekana wanafanya kazi.
Pamoja na yote napenda kumpongeza sana bwana JMK kwa kiasi fulani kuiacha Sheria ichukue mkondo katika kesi mbalimbali hasa za UFISADI. Kinachotakiwa aingilie ni kuimarisha maslahi ya watu wa mahakama yanaimarishwa ili kupunguza angalau kidogo hamu ya UFISADI kwenye makesi hayo.
Maana si chakula wamepelekewa??!!
Mungu Ibariki Tanzania,
Mungu iokoe Tanzania.
Mzawa