Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na Viongozi wa Chama cha Maalbino Tanzania, kwenye Jengo la Utawala la Bunge Mjini Dodoma walipokwenda kunmshukuru na kumpongeza kwa kuongoza juhudi za serikali kutatua tatizo sugu la ukatili dhidi ya maalbino. Mwenye kilemba chekundu ni Mbunge wa Kuteuliwa Al- Shaimaa Qwegyir

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hello Bwana Michuzi,
    Tunashukuru kutuletea habari hii lakini kwa mtazamo wangu kutumia neno maalbino sio sahahi. Mimi sio albino lakini linaniuma sana. Naona kama vile tunawadhalilisha vile. Ukitaka kujua kama ukiwaaita hivyo ni vibaya, jaribu kulirudia neno "maalbino" mara tano hivi utasikia.
    Albino ni kwa kiingereza, kwa kiswahili sanifu wanaitwa zeruzeru. Hata wakiwa wengi wanaitwa zeruzeru kwa sababu haina wingi. i.e sio mazeruzeru.
    Tuwajali hawa watu wanapata shida sana wadau wangu.
    Prince Gonasha.

    ReplyDelete
  2. huna point ulikosa cha kuchangia ukaona bora usikae bure tu ukaamua kuandika chochote funga bakuli lako nexttime mdau wa kwanza.

    ReplyDelete
  3. kunasiku nilisoma news kuwa mr. pinda na mkewe wamemchukua mtoto zeruzeru huko chato alikotembelea, na kuwa wataenda kuishi nae kwake wadau wenzangu mwili ulinisisimuka jinsi mr.pinda alivyoonyesha upendo nilifurahi sana anaroho safi sana waziri huyu. tena katoa mfano mzuri sana ameonyesha kuwa alilelewa ktk malezi ya hali ya juu na anamaadili mema.
    UKIONA UNAPENDWA KUNAJAMBO UNATENDA TAZAMA UTABAINI NA KUBISHA UTASHINDWA
    KUANZIA HAPO MIMI NAMPENDA SANA MR. PINDA NA MOLA AMJALIE SANA

    ReplyDelete
  4. wewe mdau hapo juu koma kabisa kama hauna cha kukifukiria!!!!!!!!!!!!!!

    mdau tanahimba.

    ReplyDelete
  5. WW MUDAU NAMBARI WANI, YAANI INGEKUWA NI MASHINDANO YA MBUZI DUNIANI UNGEKUWA NAMBA WANI KWA AKILI FINYU NA POINTI PUMBA

    HIVI ULIANDIKA HIYO POINTI AKILI IKIWA KWENYE SUFURIA MLIYOPIKIA UJI AU VIPI?

    WW BWEGE SANA, NAONA ULITULIA KWELI KWELI UKIDHANIA UNAMWAMBA POINTI ZA KISOMI HAUJUI UNAMWAGA UHARO WA KUKIMBIA MTU, KAMA ZA MCHUMI WA TEXAS??

    SIKU NYINGINE NIPIGIE TIGO KABLA HAUJAWEKA COMMENT, KWA SABABU COMMENT YAKO INATIA KICHEFUCHEFU

    MKEREKETWA YOMBO VITUKA
    DAKIKA 30 ZIMEKWISHA

    ReplyDelete
  6. WACHAFUA HALI YA HEWA HUA HAWAKOSEKANI HATA KAMA JAMBO NI ZURI KIASI GANI!!!......
    KILA MTU ANA UHURU WA KUTOA MAONI YAKE KULINGANA NA VILE ANAVYOLIONA JAMBO.

    ReplyDelete
  7. MIMI NAWAFAHAMU BAADHI YA ZERUZERU, WANAPAKA DAWA FULANI HIVI KWENYE NGOZI, INAWASAIDIA KWENYE JUA. JE INA MADHARA? MBONA SISIKII IKIPIGIWA DEBE IINGIE KWENYE DAWA ZA BURE? AU MBUNGE WAO HAJUI HILO?
    MI NAONA UDHAIFU WA ALBINO NI MDOGO SANA KAMA HAKUNA UNYANYAPAA, WANAHITAJI TU SUPORT NDOGO WAENELEE KUPAMBANA NA MAISHA KAMA WENGINE, SI WALEMAVU WA KIUNGO CHOCHOTE, KWANINI WASISAPOTIWE WAKATI NI NGUVU KAZI KUBWA SANA YA TAIFA?
    MIMI NIKIWAONA WANAPATA KANSA, NASIKITIKA SANA, NA GHARAMA KUBWA ZAIDI KWA SERIKALI KUITIBU, MBUNGE NILIDHANI ANGEANZA NA HILO, LAKINI NAONA BADO (LADBA KUNA TATIZO NIFAHAMISHWE) WAPEWE MGAO WA SUNSCREEN ZAO BURE KAMA WENYE UKIMWI NA ARV ZAO, MARA MOJA KILA MWEZI!!!

    ReplyDelete
  8. Mimi nakubaliana kabisa na mdau wa kwanza huko juu na wote waliomshambulia hawakumshambulia kwa hoja bali kwa "u-nazi".
    Albino siyo neno la kiswahili, na ma-albino sijui ni lugha gani. Kwa kiswahili hawa wenzetu wanaitwa zeruzeru kama alivyosema mdau huko juu kabisa.
    Mimi binafsi niliwahi kusoma shule iliyokuwa na wanafunzi vipofu. Baadaye wakaanzusha "crusade" kuwa wasiitwe vipofu na wanataka kuitwa wasioona. Sawa, jee wapi utachorwa mstari? bubu aitwe asiyesema?, kiziwi aitwe asiyesikia?, mgumba aitwe asiyezaa?,
    Jaribuni kuongea kwa hoja humu siyo mnakurupuka tuu na maneno yenu ya kibwegebwege kama tigo, uharo, nk.

    ReplyDelete
  9. NINAWASHAURI MAALBINO MSIKUBALI KUYAFANYA MATATIZO YENU YAWE YA KISIASA, NYIE HAMKUJIUNGA KWENYE UALBINO HIVYO MUAMINI KUWA MATATIZO YENU YATAMALIZWA NA WATANZANIA WOTE BILA KUJALI ITIKADI ZA KISIASA NA KIDINI KWANI JAMII ZOTE ZINAO ALBINO KATIKA FAMILIA ZAO. VIONGOZI WENU WANAPOWASHAWISHI KUWA MATATIZO YENU YATAMALIZWA NA CCM TU MSIWAAMINI. WAO WANAWEZA KUWA NA MALENGO YA KISIASA TU, LAZIMA MUAMINI KUWA WATANZANIA WOTE NDIO WATAKAOYAMALIZA MATATIZO YENU.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...