alhaj muhidin ndolanga (kulia) na ndugu, jamaa na marafiki wakipokea mwili wa mkewe, mama ndolanga, aliefariki jana huko India alikokuwa amelazwa kwa matibabu. hii ni leo mchana. kwa mujibu wa alhaj ndolanga, mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho huko Kibaha, na mwili utaondoka nyumbani kwake mikocheni baada ya salat adhuhuri (saba na nusu)
balozi wetu nchini malawi, meja jenerali makame rashid (kati) na amin bahkressa wakimfariji alhaj muhidin ndolanga ambaye amefiwa na mkewe
makamu wa kwanza wa rais wa shirikisho la soka nchini mh. nyamlani (pili shoto) akimsikiliza alhaj muhidin ndolanga wakati yeye na wadau wengine wa soka walipokwenda kumsindikiza kupokea mwili wa marehemu mke wake mama ndolanga uliowasili leo mchana toka India.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Pole sana bwana Ndolonga kwa kufiwa na mkeo. MUNGU ailaze roho ya mama yetu mpendwa mahali pema peponi AMIN.
    Mungu awajalie nguvu na ujasiri wewe pamoja na ndugu wote wa marehemu katika kipindi hiki kigumu

    ReplyDelete
  2. jamani auntie yangu. kweli unarudi kwenye boksi? uchungu tulio nao haulezeki. Poleni kaka zangu na wadogo zangu

    ReplyDelete
  3. RIP Mama Ndolanga, we will miss you terribly. Mungu awape nguvu na amani watoto wa marehemu, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu. Amin.

    ReplyDelete
  4. Poleni sana nduguzangu.Kazi ya MUNGU inshaalah.

    ReplyDelete
  5. Poleni sana familia ya ndolanga, mama ndolanga nilipata kumuona mara moja pale katika ukumbi wa diamond jubelee, hakunifahamu sikumfahamu ila tuliketi jirani nae na alizungumza nami kama vile alinijua siku nyingi, kwangu mimi alikuwa mama mwenye upendo na bila majivuno. Mungu ilaze roho ya marehemu pema peponi, Amen.

    ReplyDelete
  6. picha ya marehemu ipo wapi? huyu ni mama yake na salum au

    ReplyDelete
  7. R.I.P Mamake Alhaj Ndolanga.
    Inna Lilah waina Ilaihi Rajiuun.

    ReplyDelete
  8. Poleni sana jamani. Mungu aipumzishe roho yake mahali pema peponi. Mama ulikuwa mcheshi sana huna majivuno, mvumilivu, jasiri,na uliyejua kupambana na maisha. Kwa kweli ni huzuni sana. Poleni sana watoto, Baba Sofia pole sana kwa kuondokewa na dada yako.

    ReplyDelete
  9. Pole sana fammilia ya Ndolanda na Marehemu alazwe mahali pema peponi.
    Nilitaka kujua huyu aliye fariki ni mama yake Salum? tulikaa nao Oysterbay zamani sasa sijui ni yeye au maana hapo picha haionekani .

    ReplyDelete
  10. Pole sana wafiwa. Mwenyezi Mungu ailaze mahali pema peponi. Naomba simu ya Mariamu (Mama Mdogo). Anapatikana wapi??

    ReplyDelete
  11. Kaka Michuzi, naamini kabisa mama Ndolanga alikuwa na jina lake na la ubini kabla hajawa mama Ndolanga. Ni vizuri ukatuandikia majina kamili ya individuals hata kama waliolewa miaka 100 iliyopita. Please!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...