Muammar Gaddaffi and Africa Union on United States of Africa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Mwanzo mzuri wa kumchukia raisi, kwa sababu ni mwarabu nini?

    ReplyDelete
  2. huyu mtu hata hajui demokrasia ipo vipi na ndotoyake ni kuwa raisi wa kwanza wa usa, kama alivyoalika wafalme wote wa kiafrika, akajipajika kuwa ni mfalme wa wafalme. majibu ya museveni na kikwete kwa mh.huyo yalikuwa matamu sana.

    ReplyDelete
  3. ni vitu vya kushangaza mtu kama huyu kupewa uenyekiti wa AU

    ReplyDelete
  4. mpira umekwisha sasa hivi na bwawa la maini wametandikwa bao 1 kwa bila. haya sasa tusikie michuzi na wadau wenzake wa bwawa la maini wanasemaje.

    ReplyDelete
  5. Bwawa la mananihii, zero toffeee 1

    ReplyDelete
  6. United States of Africa jina tu au functional body?What are the established parameters of such an august institution that affiliated african countries have to meet and qualify?Hivi viongozi wa Africa mmelishwa kitu gani?Dou you really have a Dream,A Vision in Life?Au mpo mpo tu?Are we talking about an african association or a functional political authority comprising of all african countries?Au mnataka kwanza ianzishwe serikali moja ya bara la africa ndipo baada ya hapo muanze kuulizana,je,tunataka serikali hii iwe na muundo gani na katiba gani? Is this what you african heads of states are trying to tell us into believing you,we the nincompoops and the chimpanzees of the equatorial forests!mbona mnatugeuza hatuna akili hivyo?kosa letu kuwapa madaraka mtutawale siyo?au madaraka mliachukua bila ya ruhusa yetu,ndiyo maana kuna communication "gap" baina yenu na wale mnaowaongoza?kweli,matako ya sufuria hayaogopi moto,ni kazi yake!

    ReplyDelete
  7. Ubaguzi upo kwenye damu!!!, Naona wengi wanaomchukia huyu jamaa sababu kubwa ni ubaguzi. Utaratibu wa kumchagua mwenyekiti upo wazi, leo huyu kesho yule, sasa tusubiri tuone atafanya nini, kwani na yeye ni rais na anahaki ya kuchaguliwa mweneyekiti kama wengine.
    M3

    ReplyDelete
  8. Nasikia huyu bwana ndie mmiliki wa Bahari Beach Hotel.

    ReplyDelete
  9. Hao United States of Afrika ni kisingizio cha kukuchukua ardhi yetu na maliasili nyingine tulizobarikiwa, kamwe tusiwaruhusu ....;-)

    ReplyDelete
  10. awe mwarabu, awe mkritu au mwisilamu ,haijarishi. lakini ni ukweli usiopingoka kuwa hana adabu, hajui demokrasia ninini, na wala hatki kukosolewa.hujasikia anavymwandaa mwanae al islamu ghadaf kuwa raisi wa libya. inasemekana japo alienda shule, lakini alishalewa madaraka na hana akili timamu tena. muulize yeye ni nani libya, utacheka.HATA HIVYO NDO AFRIKA, HATA IDD AMINI ALIWAHI KUWA RAIS WA BODY HIYO.

    ReplyDelete
  11. Maoni yanaashiria kuna racism, isije kuwa ni chuki zilizopandikizwa kwenye somo la siasa. Au basi mafunzo ya dini ndo tatizo.

    Watu tulimchukia gadafi eti tuliambiwa alimsaidia idi amini.

    Mimi siamini kuwa amini alivamia TZ, kwa sababu wakati huo obote alikuwa kapinduliwa na anaishi bongo na alikuwa rafiki mzuri wa nchi yetu. Inawezekana sababu ya siri ya vita ni kumrudisha obote madarakani, na sababu inayouzika ni kwamba tumevamiwa. Hakuna ushahidi zaidi ya masimulizi. Kwa wazalendo vipofu samahani.

    ReplyDelete
  12. Kwa kifupi AU haina uwezo wa kuleta maendeleo wala kusaidia wananchi wake. Vita vinaendelea Uganda, DR Kongo na kadhalika. Wanajeshi wanapindua serikali Afrika kila siku, sana sana AU wanawafukuza katika umoja huo. AU haina tofauti yoyote na OAU, wananchi sasa hatudanganyiki tena. Madikteta wa Afrika wanajulikana na hawawezi kutuongoza. Karibuni nusu ya Afrika inaongozwa na viongozi waliochukua madaraka kwa nguvu na wako miaka mingi tu.

    Huyo Gadhafi mwenyewe ni dikteta wa miaka mingi. Afrika hatuwezi kuwa na umoja wa nchi tano kamili kama Umoja wa Afrika mashariki, je hio USA yetu itawezekanaje?

    Bora pesa zinazotumika kufanya mikutano haya, itumike kuwanunulia watoto wetu madaftari na madawa. Tunapoteza muda wetu na viongozi wasiojua haki ya binadamu ni nini.

    Aluta Kontinua.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...