Salaam kwako Issa Michuzi,
Naomba kuweka pole kwa mdogo wangu, Mahir R. Meghji (pichani) na kuwataarifu ndugu, jamaa na rafiki zetu kuhusu "Racial Attack" iliyomkumba huko Perth Australia.
Mahir aliondoka kwenda Perth kutokea Chuo Kikuu na amekuwa huko kwa miaka miwili huko akichukua PhD katika mambo ya mawasiliano. Majuzi usiku akiwa anatembea kuelekea alipokua amepaki gari. Vijana watatu wa kizungu walimnyemelea kutoka nyuma na kumpiga na baseball bat kichwani karibu na jicho.
Mahir ameumia sana na amelazwa huko Australia. Kijana mmoja alikamatwa lakini wawili walifanikiwa kukimbia.
Naomba sala na dua kutoka kwenu kwa ndugu yetu.
Natanguliza Shukrani.
Mdau Nyangu.

PS: Haya ndio mambo yanayotokea huko http://www.rediff.com/news/2009/jan

/27sikh-cabbie-among-victims-of-

race-attacks-on-aus-day.htm
Wao wakipata matatizo kwetu inakuwa big deal...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 39 mpaka sasa

  1. pole sana mahir...watu wengi wamesahau kwamba makaburu wengi waliochoshwa na situation ya sauzi waliamua kuamia Australia..sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la waafrika australia..racial tensions are bound to happen...pole sana mahir and get well soon.

    ReplyDelete
  2. pole sana ndugu yangu Racism bado ipo kabisa duniani hata kama waseme nini mimi naona imemalizika kimaandishi tu lakini practically watu weusi bado ni victim wa racism nimeshuhudia kwa macho yango hapa holland

    ReplyDelete
  3. NINI MAANA YA UBAGUZI WA RANGI??? Ni kitendo kifanywacho na Mzungu, mweupe dhidi ya mweusi au???Kama hicho kitendo cha kupigwa na Baseball bat kimetafsiriwa ni ubaguzi wa rangi, je kumnyofoa na kumuua zeruzeru kwanini kisiwe ubaguzi wa rangi??

    SOMA HAPA

    Nimekaa na kufanya tafakari ya kina kuhusiana na mauaji ya ndugu zetu Albino yanayoendelea kuisakama Tanzania. Dhana mbili zinajitokeza katika tafakari hiyo. Moja ni dhana nzima ya ubaguzi wa rangi na pili ni tathimini yangu kuhusu mikakati ya serikali ya Tanzania kuwahakikishia usalama ndugu zetu Albino.

    Ukiangalia ubaguzi wa rangi uliokuwepo Afrika Kusini enzi za Makaburu, watu walipangwa katika makundi kutokana na rangi zao; weupe ( Wazungu ), watu wa rangirangi (coloured ) na weusi ( Waafrika ). Huduma zote, ikiwa ni pamoja na elimu, zilitolewa kwa kuzingatia rangi ya mtu.

    Kulikuwa na kumbi za starehe kwa ajili ya watu weupe, ambapo mtu mweusi hakuruhusiwa kuingia. Kuna sehemu zingine ambazo mwafrika hakuruhusiwa hata kukanyaga kabisa. Akikamatwa, alipewa kipigo kikali na hata kutupwa lupango ( jela).

    Ubaguzi wa rangi, hususani dhidi ya Mwafrika, ulikuwepo hata katika nchi za Magharibi. Nakumbuka nimeona picha zilizoandika “only for blacks and dogs here.” Hii ilikuwa hatari sana, kwani mtu mweusi alinyimwa haki zake kutokana na rangi ya ngozi yake .

    Sasa tujiulize.Hivi Albinno ni mtu wa namna gani? Anaweza tambuliwaje kwa muonekano wake? Sintopenda kuingia ndani zaidi kuchimba sababu za kibaiolojia zinazo mfanya mtu azaliwe Albino. Hata hivyo mtu haitaji microscope ( darubini) wala elimu ya Chuo kikuu kumtambua Albino.

    Nionavyo mimi, naamini bila pingamizi lolote kuwa mauaji ya Albino yanayoendelea kuitikisa Tanzania “Kisiwa cha Amani” ni mwendelezo wa dhambi ya ubaguzi wa rangi, lakini huu ni ubaguzi mkali zaidi katika historia ya mwanadamu kushinda hata dhambi ya biashara ya utumwa.

    Nasema nimkali zaidi kwani unalenga kuondoa maisha ya mwanadamu kwa ukatili wa kunyofoa viungo, tofauti na ule wa kumzuia mweusi kutembelea mitaa fulani au katika upandaji wa mabasi n.k !

    Ni kwa kuangalia rangi ya ngozi yake, unaweza kumtambua Albino. Kwa bahati mbaya, Albino anayezaliwa Afrika, ni tofauti na yule wa nchi za Ulaya na Marekani, kwani Albino wa nchi hizo, hatofautiani sana na mtu wa kawaida. Rangi yake inarandana na ya mzungu . Si ajabu kama naye angefanana na mwafrika, angebaguliwa na kuuawa.

    Kinachonishangaza mimi, ni kwanini Tanzania au Watanzania kwa ujumla hatusemi ukweli kuwa mauaji ya Albino yanayoendelea, ni ubaguzi wa rangi ili tuweze kupambana nao ipasavyo na Jumuiya ya Kimataifa iweze kutoa msaada sawawa na ambavyo jumuiya ya Kimataifa, hususani Tanzania, ilivyojitoa muhanga kung’oa mzizi wa ubaguzi wa rangi Afrika Kusini?

    Kwa mtazamo wangu, Watanzania tumeaminishwa kuwa Tanzania ni kisiwa cha Amani na hivyo sisi ni bora zaidi kuliko Taifa lolote kiutamaduni na kimaadili. Hii si kweli na huu ni mtazamo potofu ambao tusipokuwa makini, utatufikisha pabaya.

    Kwa uzoefu wangu, kitendo cha ubaguzi kikifanywa na Taifa jingine mfano Burundi, Kongo, Afrika Kusini, Ujerumani, M arekani ama Israeli, tunawanyooshea kidole kuwa wamepotoka huku tukitamka wazi kuwa nchi hizo zinafanya ubagauzi wa rangi. Je, kwa nini kitendo hicho kikitendeka Tanzania kama cha mauaji ya Albino, tunapata kigugumizi kutamka wazi kwamba ni kitendo cha ubaguzi wa rangi na tunaanza kutafuta majina mengine kama vile “unyanyasaji wa Albino” na k.n yasiyotoa picha halisi ya mambo yanayoendelea?

    Kwani ubaguzi wa rangi lazima kitendo kifanywe na mtu mweupe ( mzungu ) dhidi ya mweusi ( mwafrika ) ili kistahili kuitwa ubaguzi wa rangi? Vipi kama kitendo hichohicho kitafanywa na mtu mweusi dhidi ya mtu mweupe ( mzungu / albino ), hakiwezi kuitwa kitendo cha ubaguzi wa rangi?

    Au kama mtu mweusi atafanya kitendo cha kumbagua mweusi mwenzake kutokana na rangi yake kama vile mweusi sana , mweusi tiii! mweusi wa kati, nacho hakiwezi kuitwa ubaguzi wa rangi? Na vipi kama mtu mweupe ( mzungu ) akimbagua na kumnyanyasa mweupe mwingine kama vile Mchina , Mwarabu n.k, kitendo hicho kitaitwaje?

    Kwa uzoefu wangu, hasa baada ya kuangalia matukio ya hivi karibuni ambapo Waafrika Kusini waliamua kuwavamia na kuwaua wahamiaji kutoka nchi nyingine za Afrika, Tanzania ilikuwa mstasri wa mbele kukemea vitendo hivyo. Tanzania ilitoa tamko kali na kwa uwazi kabisa ikisema, “ Dhambi ya ubaguzi bado inaitafuna Afrika kusini.”

    Nikaanza kuangalia mambo mengine ninayoyashuhudia kila kukicha huku Marekani. Mtu akifanyiwa kitendo fulani, kwa mfano, ikiwa ni mweupe kakifanya, hukimbilia kusema ni ubaguzi wa rangi.

    Sasa mimi najiuliza. Je endapo Mtanzania mweusi mmoja ataenda nchi yoyote ya Magharibi kama vile kusoma au kufanya kazi halafu akauliwa na kunyofolewa viungo kama wanavyofanyiwa Albino, Tanzania itasemaje? Haina ubishi , kila mtu atasema “amebaguliwa na kuuwawa kutokana na rangi yake.”

    Swali langu la msingi ni hili: Kitendo cha Albino kunyofolewa viungo vyake kinyama na hatimaye kuuawa na mtu mwenye rangi nyeusi kisa rangi yake ni tofauti na cha mtanzania mweusi aliyebaguliwa na kuuawa ugenini hususani katika nchi za magharibi? Kwa nini mauwaji ya Albino yasitajwe kama ubaguzi wa rangi? Maana Albino naye hutambuliwa kwa rangi yake!

    Kama tumefikia hatua ya kuuana kutokana na rangi zetu; moja nyeusi, nyingine ya rangirangi ( coloured ) na wote ni binadamu tena watanzania, tuanaelekea wapi ndungu zangu?

    Serikali ya Tanzaia inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kupambana na janga hili la mauaji ya albino. Uamuzi wa kugawa simu kwa albino wote, pengine waweza kusaidia kwa kuwawezesha kupiga simu polisi wanapovamiwa.

    Lakini Serikali inawasaidiaje albino waishio kijijini ambako hakuna umeme? Simu hiyo inachajiwa kwa teknolojia gani? Je simu hizo hizitakuwa kivutio kingine na hivyo kuwafanya wavamiwe zaidi?


    Kama imefikia hatua albino hawezi kutembea peke yake au kutembea baadhi ya masaa hususani jioni, kama imefikia hatua Mbunge maalum ambaye ni albino lazima apewe ulinzi maalum ili asinyofolewe viungo vyake, falsafa ya Tanzania kama kisiwa cha amani iko wapi?

    Ndugu zetu wa Marekani wanaelekea kuishinda dhambi ya ubaguzi wa rangi, kwani hatimaye wamefikia hatua ya kumchagua mtu mweusi kuwa Rais wao kwa kuangalia uwezo wake, hoja zake na si tena kigezo cha rangi kama Dr. Martin Luther King Jr aliposisitiza katika ndoto yake ( I HAVE A DREAM). Mwaka 2010 kama mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakuwa albino, tutakuwa tayari kumpigia kura endapo atakuwa na sifa za kutuongoza? Tafakari, Chukua hatua.

    Nawasilisha hoja!

    MAKULILO Jr
    www.makulilo.blogspot.com
    makulilo@marshall.edu
    West Virginia, US

    ReplyDelete
  4. I don't particularly hate white people per se lakini jamani mliooa na kuolewa na caucasians mtanisamehe. who in their right mind would want that skin? They just hating coz ours looks muuuuch better we need no layers of make up. We are cool, we are always in despite the trials and tribulations of our mother land

    ReplyDelete
  5. Pole sana mshikaji wangu Mahir...I wish you get well soon. Sasa Babu, wewe pamoja na kuwa una kijirangi angalau chepesi kuliko sisi wengine wenye rangi typical za kimatumbi wamekufanyia sasa si balaa hiyo?

    Anyway, ugua pole babu..nitajaribu kupata namba yako kutoka kwa Prince na nitakucheki baadaye.

    Mzee wa nyufa hapa, G.(old Kibaha pal)

    ReplyDelete
  6. Ni kweli wadau pamoja na ubaguzi wao. Tension imeongezeka kutokana na wengi wa wazungu kupigwa chini makazini. Wao wakiona foreigner wanafikiria ni wafanyakazi waliochukua kazi zao.

    ReplyDelete
  7. mkuu wa wilaya, kunandugu zetu bongo wanatamani kuja kwa wazungu, lakini hali huku sio kabisa, maisha wanayoishi ndugu zetu huku na wanavyotazamwa ni ya kinyani, ndani ya mabasi, kumbi za starehe, hata njiani. unajiona tofauti kabisa, lakini waafrika bado wakifika huku wanajiona wamemaliza. ukisikia vijana wanavyoshindana kusema wapo ulaya, utafikiri wameyashinda maisha.
    pole sana MEGHJI, wewe ni mwafrika machoni mwa wazungu, japo nanyi mkiwa tanzania kama machotara wengine hujiona bora kuliko sie tulioweusi kama WASUDANI KUSINI. UBAGUZI KANISANI NA MISIKITINI. MUNGU YUPPO WAPI SASA.

    ReplyDelete
  8. mambo hayo yapo hata huku russia na ukraine cha muhimu ni kutembea kwa makundi hasa nyakati za usiku tusijisahau sana jamani unajua huwezi jua watakuotea lini!!!!pole man huku russia watu hao wanaitwa skin head!!!!

    ReplyDelete
  9. Sorry for the attach Mahir. May the Lord heal u and keep u well.
    Lisa!

    ReplyDelete
  10. mdogo wangu yuko finland na kila siku anasikitika kiasi gani ubaguzi ulivyokithiri kiasi kwamba amekuwa na mawazo tafauti kuhusu aina yeyote ya wazungu. kiasi haamini kiasi gani tunawathamini wazungu wakija tanzania, pia kuwa inakuwa big deal wakiibiwa au kupigwa nchini tanzania lakini sisi tukiwepo nchini mwao ni tafauti.

    Pole sana ndugu mahir

    ReplyDelete
  11. Man! what a shock! Pole sana Mahir and get well soon. Dua zetu zipo na wewe.

    ReplyDelete
  12. Pole sana ndugu, Matatizo hayo yapo sana kwa hawa watu weupe wanaoona waafrica hatuna haki ya kuwa katika ardhi zao na wasio na elimu ndio wabaguzi kwani waliosoma wote wanajua kwamba wao wenye ngozi nyeupe ndio walianza kuja kwenye ardhi zetu tena kimabavu na bila vibali, sasa siku hizi tunakuja nchi zao kuhalali na kwa kuwaomba tukifika wanaona tunawabana, cha msingi wadau ni kuendeleza libeneke bila kujali wabaguzi kwani ni asilimia chache sana ya wazungu wapuuzi na wasio na elimu ndio wabaguzi, we need to stay focused na kuface challenges zinazokukuta kila siku bila kukata tamaa kwani hiyo ndio misingi ya majasiri na wapenda maendeleo, Ukikaa ndani na kusema "wabaguzi hawa" hutafika kokote kwenye maisha haya kwani hata Africa wenyewe kwa wenyewe tunabaguana, wenye kajirangi kidogo wanatuona wamatumbi watwana, kisa wao ni vizazi vya mabeberu wa kiarabu waliotutawala.....Waafrica tunadharauliana wenyewe kwa wenyewe na hatupendani seuze wasio na rangi yetu.. angalia mfano tu uliotokea kwa watani wa jadi mwaka jana, na kwa jongwe....au Sauzi mwaka jana walivyowachoma watu moto... Jamani Dawa ni KUKOMAA NAO.... MPAKA KIELEWEKE.

    ReplyDelete
  13. Pole sana kijana Mahir.Kwa kweli mambo ya kibaguzi yanatisha sana katika hizo sehemu.

    Lakini pia Mahir ulitakiwa ukienda huko ueneze utamaduni wa kitanzania na sio kusuka rasta.Hao jamaa inawezekana wanaona kuwa watu ambao wana rasta ni wahuni na wavuta bangi wa Jamaica.

    lakini sikubaliani kabisa na kitendo cha hao wabaguzi kumpiga Mahir

    ReplyDelete
  14. pole sana kwa dhoruba iliokupata.

    ReplyDelete
  15. This is very sad. Nakupa pole sana Mahir. Bora fedhuli mmoja wa hao watatu amekamatwa. Nategemea utapona na kumaliza masomo yako. Peace!

    ReplyDelete
  16. Pole sana ndugu yetu.Mungu akupe nafuu na upone. Lakini je serikali zetu zinachulua hatua gani kwenye matukio kama haya. Should the Tanzanian government not at the very least give full publicity to this incident and warn Tanzanians to be watchful wherever such racial incidents occur. This might at least shame host governments in countries where such incidents happen to take more preventive and punitive action. I know we are small but we can certainly make a noise. We also need to engage Australians and others visiting/living in our country about such incidents and ask them why such things are happening in their country and ask them what their governments will be doing about it. Waandishi wa habari mpo? You can help a great deal in this by probing their diplomats and other nationals on these stories.

    ReplyDelete
  17. Incidents like these should be front page news in The Daily News, The Guardian, The Citizen and so on. It should be the first item on TV and radio news etcetera. We ca pressurise these countries if we want. I ask everyone reading this comment to ask every Australian you meet about this incident and others like it and express your concern. Mkinyamaza tu yataendelea mambo haya haya kila siku. You can be an agent for positive change.Tusinyamaze tu.

    ReplyDelete
  18. Mahir pole sana tunakuombea upone haraka na uje kujenga taifa. Mwana-Kibaha Secondary mwenzako

    ReplyDelete
  19. MAKULILO Jr
    Maneno mengi wakati hakuna lolote unalojua. Malbino hawauliwi kwa sababu ya rangi yao au ubaguzi...

    ReplyDelete
  20. Jambo hili lingefanyika huku kwetu Afrika nyie mlioko utumwani huko ughaibuni mngechonga sana

    ReplyDelete
  21. Du hata Australia? nchi yenye mafolena zaidi ya 95% na bado wanavutia mafolena waende kwao!
    Du anyway baguzi is just a baguzi hata akiwa nje ya nchi yake. Utakumbuka yule mjeshi wa Uingereza(aliyetoka Iraq) aliyemdedisha yule mwanamke wa kiTZ kule ufukweni,kesi yake ilivyopotea kimyakimya

    ReplyDelete
  22. kusuka rasta ni utamaduni wa kiafrika wa enzi. ubaguzi wa rangi unatokea gainst watu weusi, weupe wahindi na kila kikundi cha watu na hata ndani ya kikundi cha watu eg waafrika wa afr kuikasini agains waafrika wegine ila in this case umetokea from wazungu to au muafrika. hii ofcourse inaweza kutokea hata dar au nchi nyingine ya afrika na ni bahati mbaya imetokea huko na it doesn t matter mtu kaoa nani au anaishi wapi. mahir amesoma kule tokea degree ya kwanza na masters na alirudi tanzania kufundisha chuo kikuu miaka michache kisha akaenda tena kufanya phd. hivyo anakufahamu kule na si mgeni na miaka yote haikumtokea kitu kama hiki ni bahati mbaya imetokea sasa.

    ReplyDelete
  23. Nyangu, poleni sana aisee kwa hilo shambulio lililompata rafiki yetu Mahir. Tunamuombea Dua ili apone na kurudi katika hali ya afya njema!!

    ReplyDelete
  24. yani uyo ni mwalimu wa "chuo kikuu gani Tz?"mawasiliano gani anasomea?
    jamani!!
    ubaguzi upo saaana tu hauishi,suala ni kukaza buti basi.
    aya pole

    ReplyDelete
  25. so how do you know its racism and not just thugs, hooligans or robbers? i hope its not just cause whites attacked a black

    ReplyDelete
  26. Namuunga mkoni mdau aliyesema issues kama hizi zinatakiwa kusimamiwa kidete. Lazima hawa wajinga wajue raia wetu wana thamani. Tukikaa kimya hawatajali wala kufuatilia wahusika ipasavyo. Angalia Israel au Marekani raia wao wakiguswa. Na sisi lazima tuonyeshe hiki kitu kimetuudhi sana.

    ReplyDelete
  27. pole sana mkuu sisi hapa south africa ndo tunaipata kweli kweli ukikaa kwa wazungu full wabaguzi ukikaa kwa weusi xenophobia basi tupo tupo tu nyumbani kutamu we acha tu

    ReplyDelete
  28. Haya ni yakawaida tu,ktk nchi za watu!kila siku yanatokea.

    ReplyDelete
  29. Mimi ninavyojua ni kua Mahir Meghji ni MWALIMU wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia ni baba wa watoto wawili. Yeye ni mtu katika watu. Mambo kama haya yanaweza kumtokea yeypte popote. Tabu iliyokuwepo ni kua credit crunch inawafanya hawa 'white trash' kua na hasira kupita kiasi, haswa kwa wale watu wenye rangi ambao wanaokekana kuwa wamefanikiwa katika maisha. Mungu atamsaidia Mahir atapona na kuendelea na maisha mazuri.

    ReplyDelete
  30. Jibu: Mahir ni Mwalimu wa chuo kikuu cha dar es salaam - Mlimani. Amesomea Degree na Masters zake Australia na hivi sasa anafanya PhD kuhusu mambo ya IT na Communication. Pia anafundisha chuo kikuu hapo Perth ambapo anafanyia PhD. Mimi nadhani ukweli ni kua hii attack ni economical... credit crunch imewabana wazungu kupita kiasi. Watakua wamemuona ana gari nzuri, labda confident wakaamua kumvamia... Pole sana Mahir. Nilimiss kukuona ulipokuja Dar hivi juzi but tutaonana karibuni. Ugua pole Prof.

    ReplyDelete
  31. Pole bwana mahir,Regarding the incidence.To Mr. MKULILO JR,What you are saying about Tanzania and albino I don't agree with you at all. What I know is that the albino are not being discriminated because of their color but rather is because of the witchcraft and Superstition that is going on in our country.Most of the people who are committing such Heinous crime are un educated people who think by doing so will become rich or it will benefit them in somekind of way.But we all know the truth... most of these called witch doctors are uneduacted so even if you will try to educate them about what they are doing,it will be imposible for them to understand. For me I think before you try to criticise Tanzanians for being racist you better check your facts first and then bring that point. Otherwise I think you are being hateful of other Tanzanians without any good reason.That's all I had to share.

    ReplyDelete
  32. nakubaliana na wadua juu kuwa inaweza kutokea popte hii. hata bongo mahir aliwahi kuvamiwa na majambazi wa gari na hata hii usikute ni majambazi au majunkie wametaka kumuibia. bongo kwenyewe ukatili umezidi huu angalia albinos wanavyouwawa au majambazi wanavyoua watu na hata ajali zikitokea wananchi wanavyokalia kuiba badili ya kusaidia majeruhi.nchi zingine ukatili na ubaguzi ndo ndo kabisa za kiafrika angalia afrika kusini, hutus na tutsis etc tusijidai eti ukiwa kwa watu ndo hatari kweli nyani haoni... . mahir kweli ni mwalimu chuo kikuu na cha dar na ana watoto wawili australia na mkewe ambaye ni mtu wa huko ila wote walikua dar wakati mahir anafundisha dar. hivyo mahir mji anaoishi anaujua na ni ajali ambayo inaweza kutokea popote.namtakia kuugua pole mahir kwani ni mtu poa sana mwenye huruma kwa kweli.

    ReplyDelete
  33. Mahir mwenyewe mtu poa sana, very focused na anaipenda nchi yake.

    Ugua pole Mahir. Mungu akusaidie Ukamate Phd yako uje kutufundishia vijana wetu. TAIFA LINAKUHITAJI.

    ReplyDelete
  34. Kwa kweli huyu MAKALIO WA VIRGIN ...IA du uelewa wake unatia huruma kabisa.

    Hawa ndio wale walio uchi kiakili na hawajjijui. Sasa sijui tumuelimisheje kwamba Albino si Rangi tu.

    Na kusema kwamba hao wachawi na waganga na wateja wao wanaowinda viungo vya Albino ni wabaguzi warangi sasa sijui ni shule gani utawapeleka watu kama hawa akina Mkulilo wa makalio waweze kuelewa tofauti.
    Tumuombee na kumuonea huruma, hawezi kuelimika kabisa.

    EWE MWENYEZI MUNGU UMSAMEHE MKULILO MAANA HALIJUI ALINENALO!

    mzawa

    ReplyDelete
  35. yaani hiyo habari imenisikitisha sana pole sana mshikaji wangu mahir, inabidi uwe muangalifu sana hawa watu hawaaminiki saa nyingine. pole sana mungu atakusaidia washkaji zako tunakuombea.
    nyam

    ReplyDelete
  36. Pole sana na mwenyezi mungu akulinde

    Lakini kwanini mara nyingi mtu akipigwa na Wazungu tunakimbilia kwamba sababu ni Racism.Ndugu zangu maswala mengine inahitaji tupate habari kamili na sio kwamba kila mtu akipigwa basi ni rasicm.Mimi naishi nje na nafahamu vijana wa kizungu wanavyofanya maamuzi yao ya kipuuzi na wanaweza kumpiga mtu yoyote bila sababu ya maana na sio kweli kila mweusi anayepigwa na wazungu basi ni rasicm.

    kenge

    ReplyDelete
  37. Nimeona watanzania walivyokuwa na uchungu pale Mwenzetu anapopata na maswahiba lakini bado tunakazi kubwa nchini kwetu na watu wengi pamoja na viongozi wanaogopa kulisema hilo kwamba ndani ya Tanzania kuna ubaguzi wa hali ya juu kati ya jamii ya kiindi na wazawa.sitaki kuplay politics hapa lakini huo ndio ukweli kwani nimebaguliwa sana ndani ya nchi yangu na wahindi.

    mfano mzuri ukienda oysterbay beach hautaona mhiindi hata mmoja anaoga palipo mweusi (mzawa) utakuta wanajitenga mbali na watanzania wazao.

    Je huo sio ubaguzi au ndio mnaita community? hapana ni ubaguzi huo na viongozi wetu wanaogopa kulisema wazi hilo.

    Mdau Halihalisi

    ReplyDelete
  38. Hao wahindi sijawaona wakipiga watu wengine lakini hawa wazungu "waliomshambulia" wako violent.

    Na wazungu wote sio wabaya. Kinachokera ni pale mmoja wao akishambuliwa hata na kibaka huku kwetu wanavyopayuka. Mpaka travel advisory zinawekwa nk. Sisi tuko wapole watu wetu wakishambuliwa na ndio maana wanatuona ni carpet la kukanyagwa.

    ReplyDelete
  39. Ndugu na marafiki, nashukhuru sana kwa upendo wenu na dua zenu. Kwa kweli hii imenigusa na kunifariji sana. Ninaendelea vizuri sasa na nina watakia kila la kheri katika maisha...tuko pamoja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...