Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi, amedai amezushiwa juu ya habari kwamba ameoa tena na akadai kuwa uongo unaenezwa na watu aliowaita ni mafisadi wenye lengo la kutaka kumjengea chuki katika jamii.
Mengi anadaiwa kumwoa Lilian Kimaro na ndoa yao ilifungwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Kanali Fabian Massawe.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, Mengi alisema habari hiyo pamoja na nyingine kama vile ‘ana kashfa ya ufisadi na ndoa baina yake na Chadema yabainika’, ni za kutunga na zinasambazwa na magazeti aliyodai yameanzishwa na wale anaowaita mafisadi.
“Magazeti haya yanayofadhiliwa na watuhumiwa wa ufisadi yamekuwa yakiandika mambo mengi yaliyojaa fitina na uongo dhidi yangu na familia yangu,” alisema Mengi. Hata hivyo, hakuyataja magazeti hayo zaidi ya kueleza kuwa yapo 15.
Hata hivyo, Mengi aligoma kuulizwa maswali kuhusu hoja yake hiyo ya ndoa ili aweze kutoa ufafanuzi zaidi.
“Naomba msiniulize maswali, nyie wenyewe fanyeni utafiti ndio maana mnaitwa waandishi makini,” alisema.
Mengi alisema mafisadi hao wameanzisha magazeti hayo ambayo alidai yanasambaza fitina na uongo uliotungwa kwa madhumuni ya kuufanya umma uelekeze nguvu na mawazo yao katika fitina na uongo huo na kuacha kufikiria na kuzungumzia tatizo kubwa la ufisadi.
Alisema fitina na uongo wa mafisadi hao ni sumu inayosambazwa ndani ya jamii na inaweza kujenga chuki, kuwagawa wananchi na kuvuruga amani.
“Iwapo vurugu zitatokea, basi mafisadi hao wataanza hata biashara mpya ya kuuza silaha ili Watanzania wazitumie kuuana wenyewe kwa wenyewe.”
Mengi alisema wengi wa mafisadi wanaishi maisha machafu, lakini akagoma kuyaeleza kwa madai kuwa ni hadi pale Baraza la Habari Tanzania (MCT) litakapotoa msimamo wake juu ya uandishi wa mambo ya faragha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Mafisadi hawakumpiga picha Mengi ...ni yeye mwenyewe ndiye aliyepiga zile picha . Kusema nimechoka huu mtindo wa huyu Mheshimiwa kila mara potraying as a victim ! Kila kitu kuna mtu amesababisha ..

    ReplyDelete
  2. Sasa Bw. Mengi anakataa nini kuhusu kuoa. Mimi binafsi nilikuwa nimeona amefanya jambo la busara sana kuoa kwa sababu kuishi single kwa mtu mzima kama yeye sio busara.
    Na picha tumeziona za kwenye harusi, hongera sana Mangi kwa kupata jiko!Au mpaka tuweke kwa misupu

    ReplyDelete
  3. Mambo mengine sio ufisadi. Tatizo ni picha kuonekana kwenye mtandao wa kipuuzi. Kuwaambia waandishi wafanye utafiti juu ya ndoa yake ni dharau. Kuna mambo ya msingi ya kuandika,lakini sio ndoa ya Mwenyekiti wa makampuni ya IPP. Hayo ndio mambo ya TOILET NEWSPAPERS!

    ReplyDelete
  4. Jamani eeehhh!! Hivi zioe picha tulioona Mengi akiwa na kimwana tena kwa mapozi ya kiana ni za nini? Alikuwa kwenye maonesho ya mavazi au? Maana simuelewi huyu mzee wetu sasa. Yule dada kweli kwa muonekano wa nje katulia sasa mzee anaruka kimanga, hii imekaajekaaje sasa???

    ReplyDelete
  5. Nina hakika muda si mrefu ukweli utajulikana. Tatizo teknolojia ya habari hasa kwa kompyuta inatoa uhuru wa kubadili picha ya muhusika ndiye siye. Mwanya huo unaweza kuwa umetumika katika picha zilizosambazwa mtandaoni. Lakini kwa kutumia teknolojia hiyo hiyo tutajua ukweli.

    ReplyDelete
  6. http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?id=15803

    Michuzi embu tuweekee hiyo data hapo kwenye link.. na nukuhu waziri wa nchi zenje.. ndio tumenunua prado 80 aidha tumenunua treka 12..mimi nadhani inabidi tuwapigie magoti wakoloni warudi tanzania asap...kama viongozi wetu wataendelea kua hivi.
    Mbona Rwanda waliweza kuwabadili mawaziri kuhusu magari ya serikali TZ vipi?????? michuzi usiniue weka hii hapari ni muhimu kwa wabongo kuelimika....

    ReplyDelete
  7. kuoa sio jambo la ajabu, in fact ni jambo la heshima. kwa hiyo mimi sidhani kama ingekuwa ni kweli basi angekataa. by the way, kwa mtu kama mengi kufanya sherehe ya kuoa na jinsi anavyofahamika, huenda taarifa za sherehe zingeweza kuwepo magazetini hata kabla ya harusi yenyewe na watu wangehudhuria. anaweza akawa hajaoa kama alivyosema. picha zile hazionyeshi kuwa ni harusi ile. zile ni picha tu unaweza ukapiga na mtu basi.

    ReplyDelete
  8. MSAADA TUTANI:-

    Huyu Mheshimiwa alikuwa akiishi na mke hapo awali au alizaa zaa tu watoto??
    Tusaidiane taarifa wadau, kwani wengi hatumjui sana huyu bwana kiundani.

    BAGAMOYO.

    ReplyDelete
  9. hahahah.....may be zile picha walizipiga kwenye new year's eve....

    ReplyDelete
  10. Mie naona ni changamoto imetolewa kwa waandishi wa habari. Watoe data kuwa ni lini na wapi ndoa ilifungwa. Watupe na photocopy ya cheti cha ndoa.

    Hapa tatizo si picha ila ni habari iliyoambatana na picha. Waandishi walishadadia kuwa kaoa,so lazima wawe na proof!

    Otherwise,weka habari za pembejeo za wakulima na tafsiri ya mitaala ya kilimo ili wananchi wafaidike kwa wingi ukizingatia kuwa kilimo ndiyo uti wa mgongo wa taifa letu

    ReplyDelete
  11. Anayedaiwa Kuoa amekataa kwamba si kweli Hajaoa!Iweje mumlazimishe? Kwani kuoa mke ni mbaya? Ukweli utakuja julikana tu.Maisha ya mke na mume kawme hayawezi kuwa siri ya muda mrefu.Kwa nini waandishi uchwara walishikie bango suala hilo? Kuna nini cha ajabu hata kama ni kweli Mengi ameamua kufunga ndoa tena? Kinawauma nini?Mwenyewe kakataa,si basi!Wapo wanaomtakia mabaya Mengi kwasababu zao binafsi.Nafikiri hawatafanikiwa kwa utaratibu huu.

    ReplyDelete
  12. Ndoa ya Mengi, Historia ya Mengi katika Ndoa yake ya Awali na mengine mengi hayatusaidii kujenga nchi. Naomba waandishi wa Habari ifikie wakati muwe mnatoa habari za kuwajenga watanzania na sio umbea umbea asante sana ulieandika toilet newspaper.

    Kuna sehemu nyingi sana huku nchini mazingira yanaharibiwa toeni habari kama hizo pamoja na namna ya kukabili hali hiyo. acheni umbea
    Mashaka akiandika makala yake hamna comments. Kigogo akipiga picha na familia yake au kidosho wake Front page Why?????????????????????????

    ReplyDelete
  13. Mbona Mengi amekazania sana kulaumu mafisadi, kulikoni? Maswala ya arusi na ufisadi yanaendana vipi?

    ReplyDelete
  14. Nimesikitika sana kuona Mengi ameweza kuongea hayo maneno yasio na busara. Alitegemea nini mtu kama yeye ambaye ni public figure( or celebrity) ni kama kioo cha watu wnengi hapa nyumbani. Kama anataka kufanya mambo yake kisiri either hafiche kwa maana hasingeruhusu camera impige or aseme ukweli kuhusu kilichoandikwa kama ameoa or hajaoa, badala ya kusingizia watu. Yeye mwenye magazeti yake huwa yanaandika stories za watu je yeye kwanini hasiaandikwe?. Halafu kajibu mwenyewe kwa kusema nyie ni waandishi wa habari fanyeni kazi yenu so hayo magazeti yamefanya kazi yao sasa ni wajibu wake yeye kutuambia ukweli kuhusu maisha yake. Yeye ni one of the succesful citizens and people will always reflect on him and his work. He need to be a good example and act up as an idol. Angekuwa marekani kwa kujibu hivyo angeshaumbuka hasa kwenye taarifa za habari.

    ReplyDelete
  15. Jamani binadamu nyie...mmezidi looh!! kwa nini mnaingilia uhuru wa mtu??? Kaoa, kaolewa wote hao ni binadamu wanahaki ya kuishi maisha wanayoyataka ukizingatia wanajua wafanyalo na hawamdhuru mtu mwingine...

    ReplyDelete
  16. Sure anon wa 11 feb. 9:26. Mzee kama huyo angeonesha busara na kutunza heshma yake kwa kunyamaza asipende kujibu jibu au kulumbana lumbana tuuu kila kukicha, yeye kama kaoa ni jambo la kheri wala hawakulazimishana kwa mtazamo wangu wa zile stailo za picha wako happyyyyy ni hiyari yao wenyewe wawili, na ni busara kuoa kuliko kuvunja vunja amri ya sita kila kukicha.
    Kwa upande wangu ingawa sijui kama ndoa yake ya awali ikoje au matatizo gani nisikiavyo yeye yuko peke yake, saa kuliko kuazirika na upweke heri kuoa sasa kikubwa ni nini? napenda hekma ya uislam kuwa waweza oa au olewa kama umetaliki au talikiwa unakuwa huru hamna kuficha ficha na kwenu hugombwiiiii

    ReplyDelete
  17. mzee Mengi,
    sio busara kila kitu uwe unasingizia mafisadi, mafisadi this mafisadi that !! be driven by your conditions and your values, only that way you will be proactive, to be driven by your emotions and your feelings you will be reactive,that is why you react to any mention of your name and go an extra mile to cleanse your act by playing victimization ! half the people who read about your marriage online will forget it when they sleep why?? because they have so many problems of their own to worry about who you married and why you married !!!but because you are reactive you will worry and loose sleep over this, and given your age, i bet you will go downhill quickly such that you new bride wont handle it!!
    if i were you.., i would never comment on such a personal matter, also i would exercise caution in my personal affairs and be extremely guarded because as a public figure, media both negative and positive will be interested in you.. by the way you should know.. you own both print media and radio, tv etc....MY TAKE.

    ReplyDelete
  18. Michuzi nilitarajia utatoa issue yangu ya prado watu wachangie... sikua nachangia ndoa ya mengi...

    ReplyDelete
  19. Mzee mengi kila kukicha wewe ni kukanusha hili na kukataa kile hivi ni kwa nini? mbona umefanya jambo jema tu, kuoa katika umri wako japo umechelewa lakini ni jambo jema sasa tatizo ni nini?

    Unataka kila siku tuzungumzie mafisadi? aiwezekani tunaitaji kupumzisha akili na kuongea mambo mengine. na kwa nini ulikataa kuulizwa maswali na waandishi wa habari? si ulijua kuwa watakubana?
    Jua kuwa dunia ya sasa aina siri watu ni wajanja sana na dunia ni kama kijiji hivyo si rahisi kujificha.
    nakupa hongera kwa kupata jiko.

    ReplyDelete
  20. mmmmhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  21. Kudo's bibi umeme!

    ReplyDelete
  22. Habari kama hizi ni kwa magazeti kama ya hello magazine uk na sio kitu cha journalists kufanyia kazi maana ni umbeya tu wa celebrities wa kusomwa na mama wa nyumbani ni sio kitu chenye umaana wowote kwenye jamii. mengi alioa na kuzaa watoto watatu na mke wa kwanza kisha akaoa mwanamke mwengine ambaye nasikia kaachana nae. nadhani hakumuacha mke wake wa kwanza yani hamna divorce ingawa hawako pamoja

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...