Wasalaam Bro. Misupu.
Leo nimekutana na ishu ya umri wa kuishi wa watanzania wa bara na visiwani ambao ni utata mtupu. Kwa heshima na taadhima naomba niwasilishe kama nilivyoikuta kule jamii forum na wa wadau wachangie. *****************************************************
Tofauti kubwa hivi nchi moja- je ni sawa?
Tofauti kubwa hivi nchi moja- je ni sawa?
Wandugu nimeenda BBC country profiles nikaangalia Life Expectancy (LE) Tanzania (51 years men: 54 years women) na Visiwani (42 years men: 44 years women) tofauti miaka zaidi ya 10 yaani Tanzania wanaishi miaka 10 zaidi kwa wastani ukilinganisha na Zanzibar!
Hii inawezekana ktk nchi moja??
Nilidhani LE visiwani ingekuwa juu zaidi kwa vile ukimwi kule kidogo!
Waungwana mnasemaje?
Wenzetu Visiwani mnasemaje?
*****************
Mdau Sevedo


Mtu wangu, du, sijui nisemeje. Nadhani wakati unaangalia hiyo habari na miimi nilikuwa naangalia. Kwa sababu hata mimi ilinishtua leo nilipoangalia, ila sikuwa na sababu ya kuandika hapa kwa ajili ya mjadala kwa sababu najua wanachemsha saana aisee. Nikicomplecate issue, ukiangalia BBC, utaona kuwa Uganda na Ethiopia ni masikini kuliko Tanzania lakini ukifungua hapa, http://www.aneki.com/poorest.html, kati ya nchi masikini, hizo nilizozitaja hazipo lakini Tanzania ipo. Mimi uzuri nimetembelea hizo nchi zote Ethiopia na Uganda, wale bwana wamechoka. Ethiopia ni Addis Ababa tu, kama ilivyo Uganda, ukitoka pale kampala, utashangaa. Kwa sababu sio kama tz ukienda mbeya, kuko shwari, ukienda moshi, kuko juu, ukienda mwanza, Bukoba, ndio usiseme. Tanga pia nni jiji siku hizi na mambo yako shwari. Pale watu wanatesa saana kuliko hata daa.
ReplyDeleteKuhusu Zanzibar na Tanzania, inawezekana ni kweli kwa sababu ngoma Zanzibar ipo tena kwa sana, chapaneni kavu huko Zanzibar ndio mtajua maharage ni mboga. Tena kuna biashara chafu kuliko sehemu yoyote ile Tanzania. shauri yenu mnaodhani kuwa kule ngoma hakuna. Pile, health care sio nzuri sana Zanzibar. Mimi naishi Zanzibar, lakini nikiumwa naamini sana kwenda dare s salaama kuliko kutibiwa kule. Hata private hospitals zinachemsha. Nilishawahi kugombana na waganga wa hospital ya Marie soppers baada ya kumlaza mgonjwa wangu na kumpa dawa za taiphoid bila hata kumpima. Nilipomchukua na kumpelea kwingine akapimwe, nikagundua kuwa hana typhoid. Wanasiasa Zanzibar wanasema wameondosha malaria, sasa shauri yenu kama mnawaamini wanasiasa, na ukienda hospital Zanzibar ukipimwa malaria utaambiwa negative kwa sababu wanasiasa wamesema kuwa malaria imeondoshwa Zanzibar. Alafu, bearing in mind that Zanzibar’s population is very small, one incidence can have a large impact in statistics. Hivi wewe, umeshaenda Pemba? Ubaya wa Zanzibar ni kuwa wataalamu wengi wazanzibari wanafanyakazi Daa. Huenda mishahara sio mizuri sana serekalini.
inawezekana hii yote ni kwa sab abu ya umasikini, ebu angalia uchafu uliojaa darajani manzese ndo unategemea mtu afikishe miaka 100 ng'o athubutu wengine tutakufa chini ya miaka 30, wenye bahati ndo watafika hiyo 50 mungu akiwapendelea, ni umasikini ndo unasababisha tufe mapema. nikisema umasikini nina maana lishe duni, huduma za afya duni, huduma za elimu mbovu, kilimo kibovu cha kizamani maisha duni in general
ReplyDeleteVery simple logic my friend. Hata ukichukua mikoa ya Tanzania bara bado LE zinatofautiana. LE ya Dar es Salaam ni tofauti na LE ya Kagera.
ReplyDeleteUsidanganyike na hizo takwimu.Kawaida inatakiwa pawepo na takwimu moja tu ya Life Expectancy kwa Tanzania nzima,itakayo tilia maanani hali halisi ya Visiwani na Bara.Lakini ukitaka hali halisi ya kimkoa au kimaeneo basi patakuwepo tofauti chache kutoka sehemu moja hadi nyingine kulingana na sababu mbalimbali.Muhimu hapa kwa mazingira ya Tanzania ni kwamba kwa wastani Wanawake wameonyesha uwezo wa kuishi zaidi kuliko Wanaume.Mtanzania aliyetihadi kufikisha umri wa miaka 77 basi wakati wowote ataweza kututoka!Labda awe anaishi katika matunzo ya hali bora sana.Na kwa ujumla hivi sasa Vijana ndio wanaokufa kwa wingi zaidi kuliko watu wenye umri mkubwa zaidi!Umaskini wa Kipato na Huduma Duni za Afya zimechangia sana katika kupunguza uwezo wa watanzania kuishi umri mrefu zaidi.Wapo waliokadiria kwamba ukitilia maanani factor ya Ukimwi,basi Life Expectancy ya Mtanzania inaweza kushuka hadi miaka 37 hadi 45 kwa wastani!Lakini kwa makadirio yangu kwa hivi sasa,naamini Life Expectancy ya Mtanzania ni wastani wa miaka 52!Na ni kubwa kidogo kwa Wanawake.Hii ni kwa pande zote mbili, Bara na Zanzibar!Bado hatujachakaa kiasi hizo.Lishe Duni na Ukimwi vimechangia sana kupunguza uwezo wa watanzania kuishi miaka mingi kama hapo zamani.Vijana wetu wanazeeka mapema sana kuliko wakubwa zao!Life stlyles and Poor Incomes pia zimechangia sana.
ReplyDelete"There are three types of lies - lies, damn lies, and statistics."- Mark Twai
ReplyDeletemusiwe wajinga nyinyi kila linalosemwa magazetini kuliamini,
ReplyDeletehawa jamaa ndio western ndio wanaopotosha watu, hata wale watoto zetu wanaozaliwa ulaya na kupata elimu kule wanakuwa wanapewa maazo machafu, etu binadamu mwanzo alikuwa ni ngedere,na watoto wanakuwa wanachukulia kuwa ni kweli, mbona hivi sasa ngedere hawageuki watu tena? ni hewa gani ilikuwepo zamani ngedere walikuwa wakivuta na kupumua ambayo hivi sasa haipo ya kuwafanya wageuke tena binadamu,
je mtanzania akienda zanzibar umri wake utapunga miaka kumi nyuma? au mzanzibar akija mainland umri wake utaongezeka miaka kumi mbele,
musiamini kila lililopo kwenye gazeti, hawa wetern sometimes wanaokot jiwe tu, mara yule muokotaji anaanza kutangaza kwenye vyomb vya habari umri wa jiwe ni miaka elfu 10, kua tarehe pale kwenye jiwe la kumfanya aseme miaka elfu 10?
thanks
sometimes munawacha kuamni mambo ya kweli, munaamini zaidi magazeti.
ANON WA 12:13AM,nakuunga mkono ni umasikini lkn umesahau kuongeza na uvivu,ubwanyenye,ufisadi,uongozi mbaya.........
ReplyDeleteSisi ni "BEST USED BEFORE FORTY FIVE"
ReplyDelete