The late Musa Yohana Tuguta

The Tugutas family is sad to announce the death of of their beloved father Mwalimu Musa yohana Tuguta ( 2/26/1942- 2/8/2009) today 2/8/2009 in Dallas TX
Preparation for the transportation of his body back to Tanzania is underway.

MR Tuguta was a husband of Ellen Tuguta
He was father of
Emmanuel Tuguta- Swaziland
Suzana Tuguta-Rwanda
Fadhili Tuguta-Houston Tx
Rose Tuguta-Dallas TX
Yohana Tuguta- Orlando Florida

God has allowed him to rest


for contacts
Fadhili Tuguta 713-259-1211
ftuguta@yahoo.com
Yohana Tuguta
713-513-0611 ytuguta@yahoo.com
Rose Tuguta2149918224
Kwa mtu yeyote anaejisikia kutoa ubani na kuisaidia familia ya Mzee Tuguta katika mipango ya kusafirisha mwili wake Tanzania tumetayarisha account kwa ajili hiyo;
ROSE TUGUTA ( for Musa Tuguta)
route #111993776
account#3091714987
Washington Mutual Bank

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Huyo Marehemu mbona mwafanana??? au nakosea wadau??
    hebu angalia picha ya Marehemu na hiyo picha ya michuzi aliyoweka ktk globu ya Jamii

    Wafiwa poleni

    ReplyDelete
  2. Poleni sana wana familia ya Tuguta. Mwenyezi Mungu awape faraja katika kipindi hiki kigumu na ampokee marehemu katika ufalme wa milele. Amen.

    ReplyDelete
  3. poleni sana wafiwa, inaumiza sana, ila basi tu hakuna cha kufanya, naikumbuka sana hii familia nzima ya mwl.Tuguta zamani sana kule morogoro, watoto wakiwa bado wadogo,lakini leo hii naamini wamekuwa watu wazima pengine wengine na familia zao, poleni sana jamani, familia hii kweli imepoteza mtu wa muhimu kwao, nifamilia ambayo mtu yoyote angependa kuwa na familia kama hiyo
    baba na mama Tuguta waliweza kuiweka kwenye mwelekeo mzuri na wa maadili familia hii. inafuraahisha sana, basi muzidi kujikabidhi kwa Mungu katika kipindi hiki kigumu, Mungu atawasaidia na kuwabariki sana,twazidi kuwaombea sana. hata hivyo maisha yasiku hizi ninyi si wa kwanza wengi wamepita katika wakati mgumu kama huo.

    ReplyDelete
  4. R.I.P Mwalimu Tuguta, namkumbuka marehemu mwaka 1975 pale Mkwawa akiwa amekaimu nafasi ya Mwalimu Mkuu palitokea kasheshe ambapo virungu vya FFU vilitembea na wenzetu wa kidatu cha sita walirudishwa makwao kwa muda. Mungu aipumzishe pema roho ya marehemu na kuwapa nguvu na imani ndugu wa karibu katika wakati huu mgumu wa maombolezo

    ReplyDelete
  5. We anony wa kwanza, acha kuleta utani msibani.

    Wafiwa nawapa pole sana.

    ReplyDelete
  6. Wafiwa poleni sana. Miaka mingi imepita. Namkumbuka Mwalimu Musa Tuguta wakati nikiwa Azania Sekondari form 1 mwaka 1966 nilimkuta yeye akiwa Form Six. Alikuwa ni mwanafunzi aliekuwa akitetea haki za wanafunzi. I remember this particular incindent. We had a mzungu headmaster whose name was K.R Jones very fat and he was showing a scowling face every time ili kututisha. Alikuwa na mentality ya kikoloni kwa sababu alikuwa anawadharau sana waafrika weusi bila hata ya kuficha.Kila alilokuwa analizungumza lazima atoe tusi la kudharau akili ya mwafrika. Mind you that was 5 years baada ya kupata uhuru wa nchi yetu na tulikuwa tumeiva na misimamo ya Mwalimu Nyerere ya kutokubali mwafrika adharauliwe. Basi wanafunzi tukaamua kugoma. Jones alipokuja kutuona tukamfukuza na akakimbilia wizarani. Ndipo akaja na marehemu mwalimu Julius Mganga wakati ule alikuwa ni CHief Education Officer. Naye akawa upande wa headmaster. Wewe wacha Musa Tuguta atoe cheche za kumcharaza headmaster na pamoja na Chief Education Officer. Tulishangaa kwa sababu tulikuwa tunamuona kama ni mtu mpole. Cheche alizozitoa pale nafikiri kama sikosei zilisababisha we suspended. I think for two or so weeks. Kuanzia pale akawa hero wetu. Unajua tena sisi vifomu one na ushamba ushamba wa primary tunashangaa shangaa. Ndiyo maana wakati ule akina Samuel Sita chuo kikuu wanaongoza mgomo wa JKT usalama walikuja Azania kutufuatilia ili kuhakikisha hatujoin ule mgomo. Hizo ndiyo enzi za mwalimu.

    Namuomba Mwenyezi Mungu awape wanfamilia moyo wa subira Inshallah.

    ReplyDelete
  7. hizi stoey zinaonyesha huhy mtu alikuwa safi sana. poleni wafiwa , na Mungu ailaze mahala pema peponi.
    Anaonekana alichukia ubaguzi na kuipenda nchi yake sana, lakini wanae wote wapo nje ya nchi kimaisha, nini siri ya hii nayoweza kuiita kasoro, kwani sasa wanaeudi tanzania msibani kama wageni.
    poleni sana, wenye habari zake zaidi leteni,zinajenga uzalendo.

    ReplyDelete
  8. Familia ya Tuguta...POLENI SANA!

    Tulisoma na Musa Tuguta pale Bwasi Primary School (Majita). Yeye alikuwa ametokea sehemu za Ukerewe (shauri wa uhaba wa nafasi za shule katika medhehebu ya wa-Sabato) kujiunga na Darasa la Tano. Mimi nikiwa darasa la Sita.

    Baadaye tukaenda Ikizu Middle School (Musoma). Tulikutana tena hapo Chuo Kikuu Mlimani!

    Yego omura wa Tuguta, wachisiga! Mbenawe,ejao joone echijo'kujichuka
    kajanende na kajanende! (Ewe bin Tuguta, umetuacha! Lakini yote yako tutayakumbuka milele na milele!)

    Born Again Pagan

    ReplyDelete
  9. Poleni familia ya marehemu, na Uweza wa Mwenyenzi Mungu uwajalie nguvu na uvumilivu mwingi katika hiki kipindi kigumu. Namkumbuka Mr Tuguta toka Baraton University Eldoret Kenya, one of my favourite Lectures. RIP mwalimu!!
    Mage-Canada.

    ReplyDelete
  10. ina lilahi wa ina ilah rajiuni.mungu amrehemu.

    ReplyDelete
  11. Kwa hizi comment za leo, naona Mwl. Tuguta hakika alikuwa mtu wa watu!

    Mungu awafariji wafiwa.

    Mdau- Amsterdam

    ReplyDelete
  12. Ina lirahi wa ina hirai rajuuni, poleni sana familia ya Mwl, Tuguta mungu awape moyo na nguvu kwenye kipindi hiki kigumu.

    ReplyDelete
  13. Poleni sana, familia ya Mwalimu Tuguta. Mimi ni mmoja wa wanafunzi wa Mwalimu Tuguta, Mkwawa High School, 1971-72, katika somo la Jiografia. Alikuwa mwalimu wa kiwango cha juu kabisa, kwa kila hali. Katika ufundishaji wake wa mazingira ya huko hewani (taaluma ambayo Kiingereza huitwa "climatology") nakumbuka hadi leo jinsi Mwalimu Tuguta alivyokuwa anasisitiza nadharia za Trewatha, ambaye alikuwa bingwa duniani. Alivyotufundisha masuala ya muundo wa dunia, mabonde na milima, miamba na udongo, na jinsi yanavyoathiriwa na upepo, maji, barafu, matetemeko ya ardhi na volcano (taaluma inayoitwa "geomorphology" kwa KIingereza) sijasahau, ingawa leo mimi ni mtafiti na mwalimu wa masomo tofauti kabisa. Ninaposafiri kwa gari sehemu mbali mbali, iwe ni Tanzania au sehemu nyingine, huwa naangalia mawe, miamba, mabonde, milima, na mito na kadhalika, na kukumbuka yale aliyotufundisha Mwalimu Tuguta, kujua hiyo miamba ilitokeaje, au mto umekaaje, na kwa nini. Ningeweza kuandika kirefu zaidi. Cha msingi ni kuwa mwalimu mwenye kuweza kumjenga mwanafunzi maishani namna hiyo ni baraka ya pekee.

    Alikuwa mtaratibu na aliyeheshimiwa sana. Ametuachia mfano wa pekee, na njia bora ya kumwenzi ni kufuata nyayo zake.

    Kwenu watoto wake, ndugu na jamaa, namwomba Mungu awapeni nguvu ya kustahimili kipindi hiki, na amweke mwalimu wetu mahali pema Peponi. Amina.

    ReplyDelete
  14. Familia, marifiki na chuo cha Baraton Poleni sana. Kwa kumpoteza mmoja wenu. Mwalimu Tuguta sifa zake ni nyingi sana na alikuwa Mwalimu aliyejitolea katika kazi yake. Jipye Moyo wenzangu Mwalimu ameenda kupumzika

    ReplyDelete
  15. aliipenda sana kazi ya ualimu ingawa TZ sasa uwalimu ni kama kushindwa kufanya mambo mengine. Mzee Tuguta alikuwa kati ya wanafuzi waliomaliza on top of his class ,high school na university (mlimani)miaka ya 60`s na kuwa mwalimu badala ya kufanya mambo mengine kwa sababu alihieshimu sana taaluma hiyo, ndio maana alikuwa kati ya waanzilishi wa chama cha walimu Tanzania(Chakiwata) na baadae kuwa Rais kwa miaka kadhaa mpaka walipokiandika katiba mpya kama kilivyo sasa hivi pamoja na Prof Godfrey Mmaali miaka ya 90`s

    ReplyDelete
  16. God Rest his soul in Eternal peace....He was my Teacher, a Mentor, and a very good friend....May God give his family strength as they go through this trying moments.

    ReplyDelete
  17. Mwalimu alikuwa mtu mcheshi aliyependwa na wengi.
    Wanafunzi wa Baraton tulikupenda lakini Mungu alikupenda zaidi.

    Poleni famila ya Mwalimu Musa Yohana Tuguta.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...