katibu mwenezi wa yanga, francis lucas, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya amana akikokuwa amelazwa.
kwa mujibu wa mmoja wa wajumbe wa kamati ya utendaji wa yanga, hashim lundenga, marehemu ataagwa rasmi kesho jumamosi katika hospitali ya amana kabla ya maiti yake kuhamishiwa chango'ombe kwa mazishi jioni yake.
francis atakumbukwa kama mmoja wa waandishi wapiga picha waandamizi nchini akiwa ametumikua vyombo kadhaa ikiwa ni pamoja na mfanyakazi na mtanzania.
MOLA AIWEKE ROHO YA MAREHEMU PEPONI
AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mpaka sasa kila nikiangalia website za nchi zingine zinazoshiriki CHAN naona profile za kila mchezaji wa kikosi chao. Lakini sie aaaah! Hivi Watanzania tunanini?? Mbona tuko hivi? Hebu michuzi posti profile achana na TFF hawana akili. Pole wafiwa mungu ambariki marehemu!

    ReplyDelete
  2. Poleni sana familia ya marehemu; ndugu, jamaa, marafiki na wanayanga wote.

    Astarehe katika amani!

    ReplyDelete
  3. poleni sana familia ya marehe.mwenzetu ndo kesha maliza kazi. iliyobaki kwetu sisi tulio hai kuishi maisha yanayompendeza Mungu kwani tusihuzunike sana tusije tukamkosea Mungu sisi tulimpenda lakini Bwana alimpeda zaidi.

    ReplyDelete
  4. MWENYEZI MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI - AMINA. YEYE AMETANGULIA, SISI TUTAFUATA.

    ReplyDelete
  5. Mungu amlaze mahala pema peponi.

    Habari nilizozipata asubui hii zinasema kuwa Yanga imempoteza mchezaji wake wa zamani Leonard Chitete aliyefariki alfajiri ya leo. Mungu amlaze mahala pema peponi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...