JK akimlaki rais wa uturuki Mh. Abdullah Gul aliewasili leo dar JK na Mama Salma Kikwete wakiwa na wageni wa0 rais Abdullah Gul wa uturiki na mkewe Hayrunnisa Gul wakipozi baada ya kulakiwa uwanja wa ndege wa julius nyerere leo
Mama wa kwanza Salma Kikwete na Mama wa Kwanza wa Uturuki wakikata utepe kuzindua kwa pamoja shule ya wasichana ya FEZA sehemu za Kawe, Dar, leo




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Hivi nchi yetu imekuwa Ikulu ndogo Africa? Mbona tuna-host maraisi wengi hivyo tena wa nchi kubwa kubwa? Hivi nani anagharimia hizo party na gharama nyingine za kukaribisha hao wageni? Na ghafla kuna nini Maraisi hao wamekuwa na interest sana na nchi yetu? mimi nadhani kuna kitu cha maana si bure. Hawa wenzetu hawana rafiki. Kama hawana cha kufaidi wasingekuja bongo...ni mafuta nini? au gas au alimasi au dhahabu? Lazima kuna jambo siyo bure...!!

    ReplyDelete
  2. We anon wa 9:53PM hujui Tanzania ni nchi mmoja wapo duniani iliyobalikiwa kuwa na rasilimali nyingi. Tena ni nchi yenye eneo kubwa kwa upande wa Africa mashariki yenye ardhi ya kutosha na eneo kubwa lenye rutuba kwa kilimo. na khali ya khewa ya kitropic. rasilimali zimelala humo. usione ukubwa wa bure huo.mote humo mpaka wanakokaa wanyama poli zimejaa rasilimali.Wazungu wanasema huko Africa.ni bara la kesho, kwa tarifa yako kama hujui, tatizo sisi wafrica tumelala mno. kazi ufisadi, wizi, wizi tu ndio wanadhani dili, kumbe huko ni dalili ya kushidwa kujiongoza na kuendeleza, wenzetu wanasubiri mpaka tumeshidwa kabisa watanza kujipenyeza, na hapo ndio basi tena Itakua Africa ya wote.

    ReplyDelete
  3. Huyo anon namba moja Naona kaudini kanamnyelea sema tu kashindwa kusema, so kahamishia frustration zake kwenye blah blah. Ingewa huyo Rais Umetoka EU asingeandika kwa hasira.
    This is the Data from CIA Factbook.

    TANZANIA

    mainland - Christian 30%, Muslim 35%, indigenous beliefs 35%; Zanzibar - more than 99% Muslim

    That is the hard Truth my friend swallow it and leave happily dont let religious hatred consume you.

    ReplyDelete
  4. TUNA LAANA SISI,TULILAANIWA SIKU NYINGI TU,

    ReplyDelete
  5. WATANZANIA TUNAKUWA NA MAWAZO POTOFU SIKU ZOTE.SASA HAPO SUALA LA UDINI LINATOKA WAPI? ANON WA 9:53 AMEULIZA KUNA NINI INGAWA AMEKUWA SUSPICIOUS LAKINI HAKUJADILI UDINI ILA ANGEELEZWA HIVYO NDIO DUNIA INAVYOKWENDA KWA HIYO SI JAMBO LA AJABU KUTEMBELEWA NA RAIS WA NCHI NYINGINE.ANON WA 12:42 INAONEKANA HAJUI KITU ANACHOSEMA AU HAJAELEWA NDIO MAANA ANALETA DATA AMBAZO NADHANI HAPA SI MAHALI PAKE NA HAZIKUULIZWA NA MTU YEYOTE.INASHANGAZA LAKINI NDIYO TANZANIA HII YETU NA HAO NDIO WANANCHI WETU.

    ReplyDelete
  6. Wewe Anoy wa 12:42 hutumii akili kabisa. Mambo ya Udini unayatoa wapi? Mbona unapitwa na wakati? kwani Raisi wa China aliyekuja Juzi ana dini gani? Kwani George Bush aliyekuja mwaka jana si Mkristo tu? Ukweli ni kuwa haya mataifa yanajipendekeza na siyo bure. Acha akili fupi za kuingiza udini kwenye mijadala ya maana. Hiyo ni luck ya confidence. Kwahiyo kama nchi ni ya Kiislamu tusiseme kwavile Kikwete yuko madarakani tutakuwa tunaleta udini? Mbona hata Mkapa walimchanganua hivyo hivyo na hapakuwa na cha udini? tunafanya analysis kutokana na tunavyoona. We might be wrong but there is no problem questioning the system...so please acha mambo yako ya udini hapa...!!

    ReplyDelete
  7. ahha feza boys.nakumbuka mbali sana.sasa hivi feza girls safi hiyo.i give shout out to all wanafeza walipo,na waalimu wote.
    feza erker lises cok guzel.
    tesekur ederim-thank you.nakumbuka.

    ReplyDelete
  8. nadhani wote hamjaenda kwenye point,kipindi hiki viongozi wa nje wamekuwa wengi kutokana na juhudi za JK,KUMBUKA JAMAA ALIKAA wizara ya mambo ya nje kwa miaka 10,na ukiangalia kwenye historia ya african union utaona ni kiongozi aliyejiwekea history kwa international relation.JK anaushawishi mkubwa wa kuwavuta wawekezaji,sema kuna watu wanatumia kumchafua.big up JK wewe unaweza.tz na wewe tutafika.mwendo huo huo,na wakikusogelea ni lupango tu kama kawa.tanzania bila mafisadi inawezekana.

    ReplyDelete
  9. JAMANI KAMA KWELI TUNATAKA KUJIFUNZA BASI TUJIFUNZI KWA WATURUI NI WACHAPAKAZI SANAA NA NCHI AMBAYO IMEAMUA KUSONGA MBELE KIUCHUMI HAPA ULAYA TAZAMA MIAKA 10 ILIYOPITA WALIKUWA WAPI NA MPAKA SASA WAPO NO 13 KTK G20 YANI WANAIKARIBIA G8 KWA MIAKA MICHACHE HAPO BAADAE NA HUYU RAISI NA WAZIRI MKUU WAKE NDIO WALIYOIFIKISHA TURKEY HAPO ILIPO SO RAIS KIKWETE NA MZEE PINDA WANANAFASI NZURI YA KUKAA NA HAWA JAMAA KUWAULIZA NI VITU GANI WAFANYE.BRO MICHUZI HAPA TURKEY UKIFANYA UFISADI UMEKWISHA HAKUNA CHA MSALIE MTUME

    ReplyDelete
  10. Napenda kumjibu mdau kwamba Tanzania ni nchi ya "MAJUWA" na "BABWEGE". Tanzania ni nchi pekee duniani ambayo "Mgeni masikini" akitua Tanzania bila senti moja ataondoka tajiri mkubwa au atatajirika hapa hapa nchini. Ni nchi pekee duniani ambayo huwababaikia sana wageni na kuwakumbatia. Mimi nimetembea nchi kibao duniani sijaona nchi yeyote ambayo inambabaikia mgeni, kwanza "Mzawa" kinachobakia "labda atapata mgeni lakini hakuna uhakika. Dunia nzima washaambiana. Nchi nyingine mwekezaji lazima awe na ubia na Mzalendo au Mzawa lakini sio kweli kwamba ati Kikwete ndio anawaleta kwasababu amekuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka 10 ati anasafiri sana. Huwo ndio ukweli wenyewe.

    Mdau Stockholm

    ReplyDelete
  11. Naungana na anon aliyesema kuwa hapa kuna suala la udini, kwa kuwa kaja rais Muislamu wanapokuja wa Kikafiri na yoyote yule hata waje mara mia na wafanye wafanyavyo hakuna mjadala humo ndani akija wa kiislamu tu, joto juu. Kwa nini?? kweli ni udini? Nchi hii mwisho tutakijua tu kama nchi hii ilifanya mikataba ya kikanisa na kuuzwa kwa kanisa ma mchonga au la?? ikos siku mwishowe tutakuja jua tu!
    Waturuki Hoyee!

    ReplyDelete
  12. yeah..alkadashilar..oshuk bulduk..jamani feza boys imetoka mbali wamekuwa na feza girls hongera sana..yemek cok guzel...jamani tuache maneno mengi ikumbukwe mgeni njoo mwenyewe apone waache waje wengi tuu sasa ni sisi wenyewe wabongo tujipange tunawapokea vp..ila tukibaki kuchonga tutaendelea kuwa kalabagao..heshima kwa rais kikwete kazi yako nzuir ulipkuwa unaenda kuwatafuta wabongo walichonga safari za ulaya haiziishi wanakuja kwako wanaendela kuchonga unawa host vp? jamani wabongo mfanyie kipi kiwe kizuri kwenu.rais wetu kazi anafanya tena kubwa tuu/ikumbukwe rais wetu anahistoria nzuri tuu ya utumishi toka alipokuwa anasoma na ninahisi ni rais amabe anaijua vizuri bongo na wabongo mtaa kwa mtaa na anajua vizuri mahusiano ya kimataifa kwani amekuwa waziri wa mambo ya nje kwa muda mrefu ila anahitaji suport yetu/wabongo tunapenda starehe kuliko kazi mtu analia maisha bora wakati kila siku anashinda bar hakumbuki ata kuwekeza vicent vyake kwani kasahua cent moja ya leo na mbili za kesho kutwa mtondo goo siwakilisha shilingi ila yeye hiyo cent moja anataka aibamize lager leo akiwa na msemo ponda mali kufa kwanja/wachina wakitua bongo wakaa uswahilini mnawaponda/wajanja hao wanaijua pesa subiri mchina huyo huyo miaka 10 ijayo unamkuta tajiri...
    feza erlises cok guzel..alakashilar nakumbuka kituruki heheheh...
    kaka michuzi upooo/wakumbushe wabongo ulianza wapi kama si kupiga picha za mitaani sasa hv kila siku mafokeshi viwanja kula bata/wabongo tuamke tusiwe wazembe ndio maana ukimwi utatumaliza kwa kupenda vya urahis maisha kukomaa na kutake risk

    ReplyDelete
  13. jamani hawa sisi longolongo kama matifa mengine wameahidi kujenga chuo kıkuu bası watanjenga bandari na barazetu zitakua poa.jamaa wakıtoa project basi hufatilia mpaka mwisho.siunakumbuka kıle cha dodoma walıkuwa waarabu sasa waturik BG UP TURKEY

    ReplyDelete
  14. Woote mnaolalamika kuwa jamaa kasema udini inaonyesha udini mnaweza kuwa nao. Udini huwa hauko wazi bali utaona reaction za watu kwa kupitia mambo mengine mara waonapo alama ya dini. Hautasikia mtu anasema "mi nachukia waislamu/wakristo" bali "kwa nini hiyo nguo imezuia nywele tunataka tuzione uzuri wake kwa nini usivae kawaida" au "Abdalah jina refu saana au gumu kwa nini usitwe bahati" au "kwa nini unaenda kanisani nusu uchi" kumbe dini ndo tatizo.

    Mbona watu hawakulalamika alivokuja Juntao au banda?

    HAMNA SIRI WATANZANIA WOOTE (yaani dini zoote) WANA UDINI KISIRISIRI NA HUDHIHIRISHA INDIRECTLY. na unawanufaisha duniani au mbinguni wanaoufanya.

    KAZI KWAKO KU-INTERPRETE KAMA NI UDINI AU LAA.

    ReplyDelete
  15. UDINI NI MADA NGUMU MNO KWA WATANZANIA NA HAWAUELEWI NDO MAANA NI KAZI KUISHA. WENGI HUFIKIRI UDINI NI KUFUATA DINI KUMBE NI KUCHUKIA WATU WAFUATA DINI NYINGINE.

    UDINI HAUKO DHAHIRI BALI UMEJIFICHA KWENYE KAULI NA MATENDO NA KWENYE VIVULI VIINGI (LOOP HOLES). KWA SABABU HAKUNA MTU ANAPENDA KUITWA MDINI.

    ReplyDelete
  16. WATU WALIOACHA UDINI NI BAADA YA KUSAIDIWA NA WATU WA DINI NYENGINE.

    ReplyDelete
  17. KWE ANONO WA 12:54 UMESEMA SIO WENGINE KUROPOKA TU, KWELI VIONGOZI WETU WANITAJI, VIONGOZI KAMA HAWA ILI WAWAPE IDEA YA MAFANIKIO KATIKA NCHI ZAO, NCHI KAMA UTURUKI INA MAFANIKIO TU SANA, HAO WENGINE WAMEKALIA NA MAMBO YAO WENYEWE, SISI TUNATAKA MAENDELEO ILI WATANZANIA NAO WAESHIMIKE, TOKA KIZAZI MPAKA KIZAZI WAISHI VIZURI, KAMA NCHI YEYOTE YENYE MAENDELEO WANACHI WAKE WANAVYOISHI.KWANI KUNDI KUBWA LA VIJANA HAWANA KAZI. HUKU KWETU NA HAO WALIOKO MADARAKANI NDIO WIZI, WIZI, TU NA HUO UFISADI

    ReplyDelete
  18. HIVI MNATAKA NANI AJE KUWEKEZA?

    SAMAHANI, WATU WA ASIA WANAORUHUSIWA NI: JAPAN, CHINA, INDIA, NA ISRAEL.

    ReplyDelete
  19. mie nakaa uturuki , hawa watu niwashenzi kupita kiasi na hawapendi watu weusi, wanasesema sisi ni shetani, pia miskitini kwao huruhusiwi kuingia sasa nin wanataka tanzania. na diniyao ndo inawafundisha ushezi hou kazi kwenu watanznia matajiju siku ikifika. pia msaada gani wanatka kutoa woa wenyewe shida tupu, wankimbia kwao kwenda nchi nyingiene na hakuna anayewatka.
    ama kweli TZ nchi yamabwege

    ReplyDelete
  20. ANNON WA 3.18AM
    SAAAAAFI NA SAWA KABISA,WANAORUHUSIWA KUWEKEZA UMU NI JAPAN,CHINA,INDIA,ISRAEL,URUSI(kutoka asia)
    watu/mtu/kikundi/nchi yoyote yenye udini-udini hatuitaki kabisa ao mafisadi wa kidini kwani ndo utasikia mtu kakulupuka na vijisheria vya kishenzi ETI VAZI RASMI LA KUJISETIRI LA MAOFISINI,TANZANIA??au mwataka agenda zetu za siri?masenene wakubwa.
    ofkoz tunasubiri tuone kafata nini Tz mana ni nchi yetu so kuhoji ni kuzuri tu na sahihi mana awa watu hawaji bure umu,,,
    LAZIMA TUWACHUNGUZE ASWAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  21. MICHUZI MBONA HII PICHA YA ZIARA HII YA RAIS WA UTURUKI HAIJASEMA KAFATA NINI??
    JE NI ZIARA YA KIRAFIKI,KIKAZI,KIBIASHARA ZAIDI-UWEKEZAJI KTK SEKTA MBALIMBALI,KUTOA POLE,KUFUNGUA SHULE YA FEZZA AU NINI?
    ZIARA ZOOOteee UWA TWAAMBIWA MBONA HII HAIJAELEZWA?
    picha hazijakamilika toeni maelezo bwana sio kubandika sura apa!!
    ni hayo tu kwa uzuri!!

    ReplyDelete
  22. Shenzi sana, Israel wa nini chinja chinja hao, watatuibia ardhi zetu ili waasisi Israel Kuu! India nao wa nini hao? shida ziemwajaa sisi watanusaidia nini? Haya wenzenu kenya waoneni sasa rais wa Iran yuko huko akifanya ziara ya kibiashara. Njie watanzania udini utawabakiza nyuma!

    ReplyDelete
  23. nani anasema safari ya raisi wa uturuki haijulikani lengo lake? kwa akili zako fupi unafikiri rais wa nchi anaweza kwenda nchi nyingine bila lengo lake kujulikana? au kanila bado halikupewa taarifa?
    mtabakia hivyo hivyo eti mpewe taarifa kwani nyie ni ikulu! lo!

    ReplyDelete
  24. ALAA, KUMBE NEGATIVITIES NA DALILI ZA UDINI ZINAKUJA KWA SABABU anafungua shule ya feza ambayo ni ya wasilamu. ok nimeelewa sasa, kumbe kweli kuna udini katika komenti.

    ReplyDelete
  25. KUNA MTU HAPO JUU HAJUI ANACHO KIELEZA KWANZA HAPA TURKEY ANAFANYA NINI AU KAZI GANI?maana sısı hapa kuna madentı ambao tunasaka nondo za uhandisi na udaktari hatujaona mtu kafukuzwa msikitini hata sıku mmoja.ACHENI MAJUNGU WABONGO MTU YUPO BONGO ANAJIFANYA YUPO TURKEY.MBONA HAZUNGUMZI CHUO KIKUU CHA DODOMA HAMSEMI NI PESA YA WAARABU İLE MBONA HAO MITUMEYENU NA YA ULAYA MASHARİKI HAJAWAJENGEA KITIVO CHA ELIMU KAZI KUTUKOPESHA NA KUTUBAMBIKIZIA MARIBA ACHENI MAJUNGU WABONGOO JAMANI.TURKEY WATAJENGA CHUOKIKUU ALAFUTUWAONE MKIGOMAA KWA MIKOPO NA BODI YENU MPAKA LEO HAIJAWATUMIA PESA WANAFUNZI WALIOENDA RASIA NA ALGERİA WANATESEKA TU WATOTO WAWATU

    ReplyDelete
  26. İSEE KUNA MPUMBAVU FLANİ HAPO JUU,SİJAPENDA KUMTUKANA LAKİNİ KWA JİNSİ ALİVYO ANDİKA İNASTAHİLİ,UTURUKİ NAİSHİ MİMİ BWANA,Nİ MWANAFUNZİ HAPA MİAKA MİNGİ TU, NDİO İNAKASORO ZAKE LAKİNİ HATA SİKU MOJA SİJAWAHİİ KUONA HALİ YA WATU WEUSİ KUCHİKİWA, NA HAMNA MSİKİTİ UTURUKİ MBAO İNAFUKUZA WATU WEUSİ,LABDA ANGENİTAJİA ALİİSHİ AU ANAİSHİ WAPİ NA MSİKİTİ ALİYEFUKUZWA İPO WAPE NİONE,YANİ NDA SHTUKA SANA,NA BADO NASEMA HUYO MTU Nİ MPUMBAVU,UTURKU Nİ İNCHİ İNAYOJİTAHİDİ SAN KİUCHUMİ,NA TANZANİA İKİWA NA UHUSİANO NA İNAWEZA KUPATA FAİDA KAMA SOKO,CHUO WATAYO FUNGU NAUHAKİKA NAO İTAKUA NA FAİDA KWA WOTE KWASABABU WANAFUNZİ WAPO WENGİ VYUO VİCHACHE,İNAİTAKUA KWENYE ZİLE UNİVERSİTİ NZURİ EAST AFRİCA

    ReplyDelete
  27. Maoni yote hapo juu ni reflection ya samples za Ubongo wa watu wa aina mbalimbali!Very interesting,when you go through an array of conflicting views!Ukiona popote mtu katika kujieleza anakimbilia Dini au Kabila au Rangi ya Ngozi au Maumbile ya Mwili (all these factors are God-given)au Ubora wa Elimu yake kama kigezo cha kuonyesha ubora wa hoja zake kwa lengo la kuwadhalilisha wengine ambao hawakuipata bahati alioipata yeye,basi TAMBUA WAZI KWAMBA mtu huyo ana mapungufu akilini mwake Na hayuko kamilifu!Kuhusu Ujio wa Viongozi wa nchi zingine duniani:Kikwete alipofululiza sana kwenda nje wapo watanzania waliomjia juu Kikwete na kulalamika kwamba kazidisha mno safari za nje na kwamba ni za gharama kubwa na hapati muda wa kutosha kuyafanyia kazi matatizo ya hapa nchini!Sasa Rais Kikwete kapunguza safari za nje.Badala yake Marais wa nje sasa wao ndio wanaokuja kwa wingi zaidi hapa kwetu.Cha ajabu badala ya kushukuru sana kwa kupata Wageni kama ilivyo jadi yetu watanzania,bado watu walewale wamebakia kulalamika kwamba uwingi wa safari hizo za maRais wa nje kuja nchini Tanzania sio wa bure,kuna jambo!Eti,pengine wananyemelea Rasilimali zetu!Kwa kweli Watanzania wenzetu "hawa wachache"mnatutia aibu tena sana!Hizo ni kauli zinazotoka kwa mtu ambaye hatumii akili zake kufikiri mara mbili kabla ya kutamka jambo!MaRais wa nchi mbalimbali kutembeleana ni jambo la heri kubwa sana.Ni jukumu la kila nchi kujitahidi kunufaika na safari hizo za maRais katika nchi zao.Watako lala na watakao kosa umoja na ushirikiano ndio watakao poteza.Wajanja na walioshikamana kitaifa ndio watakao nufaika.Uturuki au TURKEY ni "one of the oldest civilisations in the world".Wenzetu wa Uturuki wameendelea sana katika nyanja mbalimbali.Tena sana.Na tishio kwa nchi za ulaya ya magharibi.Ni watu ambao tunaweza kufanya nao biashara katika maeneo mengi.Hawana Makuu japo wametupita katika mengi.Watanzani wengi hawaitambui Uturuki kwa mapana yake na marefu yake.Nchi ya Uturuki na Dini zote NA Madhehebu mbalimbali.Tatizo letu hapa Tanzania ni kwamba sekta yetu binafsi bado ni dhaifu sana kimtaji na kielimu.Imekuwa hivyo kutokana na sababu za kihistoria.Tulirithi utawala ulioruhusu Serikali tu ndio iwe Mwajiri Mkuu,iwe inasimamia na kuendesha uzalishaji na biashara,iwe ndio inayokusanya kodi zaote na kuyatumia mapato yote,serikali ikawa ndio kila kitu katika maisha ya watanzania.Ukweli ni kwamba katika maisha ya kila siku HALI HALISI HAIKO HIVYO KATIKA NCHI ZOTE ZILIZO ENDELEA DUNIANI!Hadi hivi sasa bado kasumba na fikra mgando kuhusu serikali kufanya kila kitu katika maisha yetu ya kila siku BADO NI DONDA NDUGU (its a cancerous self-realisation)!Watanzania lazima tubadilike kifikra na kimatendo.Dunia haimsubiri mtu asiyetaka kwenda nayo,itakuacha!Watanzania tusikubali kuachwa na wenzetu,twende nao pamoja na ikibidi tuwapite twende haraka zaidi lakini kwa makini na salama zaidi! ---tonnie---

    ReplyDelete
  28. Huyo anayeleta mambo ya udini, anataka kuniambia waliompigia kura Kikwete na kumfanya Raisi walikuwa waislamu peke yao? Na unadhani kuwa hakuna wakristo ambao hawakumpigia huyo kikwete Kura? mbona unakuwa na akili fupi hivyo? Hivi elimu yako ni kiasi gani? Sometimes inabidi tu-question your education level maana mambo mengine yanataka (kashule kidogo).."SUTI BILA VIATU NI SAWA NA KIPARA BILA ELIMU"....!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...