No one has ever accused President Paul Kagame (pictured) or his administration of a lack of ambition.

This is a government that has made it a habit to undertake seemingly impossible tasks and more or less succeed in most of them.

Take the example of the almost quixotic goal of harnessing the methane gas in Lake Kivu for electricity.

The gas has been bubbling up from the bottom of the lake for thousands of years and no one ever thought to use it for anything.

Up to now, it actually has been something of a time bomb, given what happened in Cameroon in 1986, when Lake Nyos suddenly emitted a large cloud of carbon dioxide, killing 1,700 people.

Enter the administration of Kagame, which instead saw an opportunity in a problem...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Huyu ndio MWANAMUME

    Sio kina JK wanaleta upuuzi hapa wa kutupa Tshs. bilioni 300 kwa consultants wa kutoka nje eti kununua Smart Cards!!

    Nani kasema watalaamu wa Bongo wanashindwa kutengeneza Samrt Cards?

    Hebu kaa vizuri na wadau wote wa ICT kuanzia UDSM mpaka kwenye Makampuni ya umma na ya binafsi wakueleze vizuri kama kweli wanashindwa kutengeneza Smart Cards kwa ajili ya National Identity Cards Project.

    Wake UP JK... kuna credit crunch halafu wewe unataka kutupa pesa nje ya nchi???!!!

    ReplyDelete
  2. PAUL KAGAME NDIYE MWENYEWE BWANA,HATA GEOGRE BUSH NA WAZIMU WAKE ANAMKUBALI.NINGEPENDA KAMA ANGEKUJA KUWA RAIS WETU HAPA TANZANIA ILI ANGALAU TUTUMIE KILIMO CHA UMWAGILIAJI NA KUJITISHELEZA KWA CHAKULA.FEDHA INAYOOKOLEWA IJENGE HOSPITALI VIJIJI VYOTE TANZANIA.
    AU MUNASEMAJE WADAU,SI NAONGEA POINT HAPA??

    ReplyDelete
  3. Huku kwetu Tanzania yanakuja maisha bora kwa kila mtanzania. Kwa sasa wafugaji kufilisiwa baadaye wakulima. Ndipo tutakuwa na maisha yaliyo bora. Aise!

    ReplyDelete
  4. KAGAME NI RAIS MAKINI SANA...
    LICHA YA KUSIMAMIA UCHUMI YAKINIFU..AMEPUNGUZA GHARAMA KWA SERIKALI KWA KUFUTA MAGARI YA SERICALI KUTUMIKA WEEKEND NA SHUGHULLI ZISO NA MSINGI.. NI BORA HAWA MAWAZIRI WATUMIE MAGARI YAO BINAFSI NA KUDAI EXPENSE PALE INAPOHITAJIKA NA KUNA VIDHIBITI..

    ReplyDelete
  5. swadakta, very impress. hongera anony. 1 and 2

    ReplyDelete
  6. Wewe anon wa kwanza nakuunga mkono, kama kuna vichwa vimejaa maji basi nafikiri vyetu wabongo vimejaa na kufurika.
    Just imagine hata kutengeneza IDs, its just IDs, IDs tunaweka tender watu wa nje waje kutuonyesha. Hata mtoto wa darasa la saba anajiuliza why, why????

    Najua Mungu anasamehe kila kosa, ila viongozi wetu naona itabidi awepe exception waingie moja kwa moja motoni. Kwaninini hizo hela zisitumike kujenga hata barabara, tangu nizaliwe nasikia barabara ya kibiti lindi, kibiti lindi. kwanini wasitenge kwa ajili vitu muhimu kama hivi.

    ReplyDelete
  7. Huwezi kuwalinganisha Kagame na Kikwete. Acheni upuuzi nyie. Kubwa la Kagame ni uvamizi wa DRC na watu milioni sita kuuwawa bure.

    ReplyDelete
  8. Ripoti za UN zinaonyesha maangamizi aliyoyafanya Kagame ndani ya DRC. Huyu si wa kulinganisha na Kikwete. Michuzi acha censorship. Unapoweka kitu acha kijadiliwe kwa uhuru.

    ReplyDelete


  9. Grrrrrrrrr....Yake Yale ya JK Kiboko, JK shujaa, JK aunguruma, JK safi n.k

    Wengi wenu humu mnamsifia Kagame peke yake...yeye ni President amefanya mazuri yake (hasa kwenye kupiga vita rushwa)...lakini pia ana kesi ya kujibu kuhusu kifo cha Raisi wa zamani wa Rwanda na mauwaji ya kule Congo kupitia Gen Nkunda.

    Mnasahau pia historia ndogo tu ya Rwanda ya 1957-1959 na 1994.

    Hawa wanaojenga Rwanda sasa hivi ni watoto wa Warwanda waliokimbilia Ulaya na Marekani n.k tangu 1957.

    Kizazi hiki pamoja na kile kilichokimbia 1994 ndio waolirudi na kufanya maajabu haya yanayoonekana.

    Bila ya hawa Kagame asingeweza kufanya kitu kwa sababu 2 kubwa:

    1. Nguvu kazi kubwa sana (watu milioni 1) waliuwawa 1994.

    2. Ingechukua miaka mingi sana kwa jumuiya ya kimataifa kuiamini Rwanda kama nchi iliyosimama, na kuanza kwenda kuwekeza.

    Hivyo, wa kuwapongeza ni hawa Warwanda walioamua kurudi kutoka Ulaya na America n.k na kwenda kuijenga nchi yao Rwanda. Hawa ndio wameweka chachu ya maendeleo Rwanda. Na hatimaye kuirudisha nchi yao kwenye ramani ya Africa na Dunia kimaendeleo. Hawa ndio wenye vision ya Rwanda iliyoendelea.

    Rais Kagame amekulia kwenye kambi ya wakimbizi na kupigana msituni maisha yake yote mpaka alipokuwa Rais. Warwanda wakiamua kesho Kagame hawafai wala hatachukua round, watamtoa.!!

    NI WANANCHI NDIO WANAOJENGA NCHI JAMANI SIO RAIS.

    Tukibadili fikra hizi za kuona Rais ndiye anayefanya kila kitu na kustahili sifa zaidi, nchi yetu Tanzania nayo itaendelea.

    ReplyDelete
  10. Hivi ni nani aliuwa wanyarwanda wengi zaidi 1994 ni RPF au INTERAHAMWE? Na kama waliuwawa watu milioni moja wengi wao invyodaiwa ikiwa ni watusi, je ni kiasi gani hao watusi waliouwawa? Na wahutu ni wangapi? Tuangalie Idadi ya watu wa Rwanda mwaka 94 ilukuwa milioni saba hivi na 84% wahutu, 14% watusi na hao wengineo. Kwa idadi hiyo ya milioni saba ina maana Rwanda ilikuwa na watusi 980000 tuseme milioni basi. Kwa mantiki hiyo kama waliokufa wengi wao ni watusi Rwanda kungebaki watusi wachache sana na ukweli ni kwamba si hivyo. Lakini kwa kuwa RPF wako madarakani, wameitumia propaganda ya mauwaji hayo ya kimbari kwa manufaa yao ili waonekane wao ndio waliuwawa zaidi.
    Tujiulize kama Habyalimana asingeuwawa je mauwaji haya yangetokea? Jibu ni Hapana. Na sasa ni nani aliyemua Habyalimana kama si Kagame na RPF? Kwa mantiki hiyo Kagame ndiye kiini cha Mauwaji ya Kimbari ya 1994 na ulimwengu sana unafahamu hilo. Bila shaka atakuwa na mwisho kama akina Taylor na Bemba. Ni mengi maovu amefanya huyu Kagame.
    Anasema kamkamata Nkunda. Hiyo danganya toto. Mbona hajapelekwa DRC akajibu mashtaka. Au basi ampeleke Nkunda The Hague au Arusha tuseme kweli Kagame Mwanaume. Huwezi kumlinganisha Kikwete na muuwaji. Tena mkome kabisaaaaaaaaa. Mlinganishe Kagame na akina Mobutu, Savimbi, Sanko, Taylor, Eyadema, Mengistu, Bokassa, Amini na Doe.
    Huu ni wakati wa demokrasia. Kagame kajenga demokrasia ipi? Kutembelewa na akina Bush na Clinton ni sababu ya Genocide tu kwa nchi hizo kubwa kutokuingilia kati. ni 'Sympathy' tu. Ila sasa wameishamjua undani wake.

    ReplyDelete
  11. ni sawa kabisa annon wa 1 na 2!!
    we need something to b done in Tanzania,,,jamani jamani jamani?

    ReplyDelete
  12. Lets all stop this silly debate about who killed what and what killed who?The PAST should not obscure our FUTURE!there is so much at stake ways ahead.Kagame anastahili pongezi zetu sana.Siyo kwasababu yeye peke yake ndiye aliyeibadilisha Rwanda hadi kufikia mafanikio ya sasa.Na siyo kwamba Bila ya yeye Rwanda isinge endelea zaidi kufikia pengine zaidi hata ya hapo ilipo sasa.At least Kagame has tried,has shown the way,he is a leader other african heads of state should find time to emulate!Simfagilii for nothing!Rwanda ya sasa imetulia,iko focussed.Ina Malengo na inajua wapi inataka kwenda.Imebainisha vizuri kabisa Priorities zake huku tunaita Vipaumbele vya Kitaifa.Wanyarwanda sasa wana umoja wa kitaifa tofauti kabisa na huko nyuma ambako tofauti za kikabila zilikuwa kikwazo kikubwa katika kuleta amani na utulivu cnhini.Except for those few disgruntled trouble shooters,atleast for now every Rwandese feels the atmosphere of freedom and boundless opportunities for self advancement!Rwanda ni nchi ndogo sana na ina watu wengi (overpopulated/high density).Wamenivutia sana jinsi walivyo makini katika kutunza mazingira yao,makini katika kuchapa kazi kwa akili na maarifa,makini katika kujiendeleza na watu wazuri sana!Yote hayo yamewezekana kwa hivi sasa kutokana na jitihada zake Kagame mwenyewe katika kuleta maelewano ya kitaifa na kumfanya kila mnyarwanda ajione ana haki sawa mbele ya sheria na ni sehemu ya Rwanda!Baada ya matatizo ya muda mrefu sana sasa wanyarwanda hawataki tena vita vya wenyewe kwa wenyewe,sasa wanataka maendeleo na kusonga mbele!Watanzania tunayo mengi sana ya kujifunza na kuiga kutoka kwa ndugu zetu wanyarwanda!Beautifull and Hardworking Honest God-Fearing People!God Bless You Kagame.----papperazi antonnio---

    ReplyDelete
  13. Wewe anon Soames,

    Kwa nini unakimbilia kulinganisha mahindi na mchele?

    (Au kuweka msisitizo kwa Kiinglish why compare apples to mangoes?)

    Tunaongelea mtu mwenye mikakati ya kiuchumi, wewe unaleta habari za mauaji.

    Those are tow different issues, na hata ukitaka watu wajenge hoja kwamba JK ni muuaji point hazitakosekana.

    Kwani unajua ni watu wangapi wamekufa kwa kukosa huduma muhimu ambazo zingeweza kutolewa kwa kutumia mabilioni ya EPA? na kwa kutumia fedha wanazonunulia mashangingi?

    Kwa hiyo acha hizo bwana. Kagame ameonesha uzalendo wa hali ya juu kwa kutoa fursa wataalamu wa Kinyarwanda wafanye kazi.

    Sasa kwa taarifa yako hao wataalamu hapo ndio watapatia uzoefu na kesho watakuja Tanzania au nchi nyingine za Afrika kuuza huduma zao.

    Wakati JK angeacha wataalamu wa Bongo watengeneze National ID wangepata uzoefu na kesho wangeenda kubid tender za namna hiyo hata kwenye nchi nyinginezo.

    Na unaposema eti "Wananchi ndio wanajenga nchi" sasa ulidhani ni kina nani wanaojenga nchi???!!!

    Ila hapa JK hataki hata kuruhusu wananchi wajenge nchi yao... si ndio vioja hivyo.

    Habari ndio hiyo.

    JK acha kubana... wataalam wa ICT wapo... vitambulisho sio rocket science wewe itisha kikao na wadau... anzia pale UDSM then ita na wataalam walioko makazini uone kama kazi haiendi.

    Naomba kutoa hoja.

    ReplyDelete
  14. wewe anon wa Feb 24 1:24PM kuongelea genocide na chanzo chake is not a silly debate. Tunataka kujua ukweli wa mambo. Nani alifanya na alhusika vipi? Hivi unaona ni vyepesi sana kuacha roho za watu zaidi ya milioni zife bure? Mpa sasa Ulaya huwa inawasaka waliwauwa wayahudi milioni 6 na kuwafikisha kwenye mkono wa sheria, Cambodia vilevile. Uhuru upi unaouongelea Rwanda. Wapinzani wanafungwa bure, hakuna uhuru wa kujieleza wala uhuru wa vyombo vya habari.Ole wako umuandike vibaya Kagame, utakiona cha moto. Sasa ni uhuru gani unaosema? Tanzania iko katika mwelekeo mzuri. Walikuwepo waliokuwa wanalinganisha Tanzania na Kenya. Baada ya mauwaji ya juzi wameona ni nini thamani ya uhuru, amani na ustawi wa Tanzania. Utulivu wa Rwanda sio kwamba unatokana raia kama Tanzani, unatokana na mabavu ya jeshi.

    ReplyDelete
  15. Tarehe February 24, 2009 3:14 PM


    Umejaribu kusoma hoja yangu lakini hukunielewa...naona una fikra zile zile ninazozizungumzia hapo juu.

    Unaposema Kagame "AMERUHUSU" unarudi kule kule kwenye kumuona Rais wa nchi ni kama “Malaika wa Mungu”. Rais wa Rwanda aliyekwa madarakani na Warwanda. Hayo yanayotokea Rwanda ni Warwanda wameruhusu yatokee, na sio Kagame aliyeruhusu.

    Unachoshindwa kuelewa ni kuwa, kinachoifanya Rwanda iendelee leo ni mabadiliko ya "FIKRA" yaliyotokea kwa Warwanda. Imefika mahali wameamua kuwa tunaweza sisi kama Warwanda kuendeleza nchi yetu, hawaendelei kwa sababu Kagame ni Rais. Kesho na miaka mingi ijayo watazidi kuendelea hata kama Kagame hatokuwa Rais tena. Rais Kagame hatokuwepo milele, ila Warwanda watakuwepo milele. Ni hawa ndio walioamua kujiletea maendeleo kwa vitendo.

    Bila kuangalia Historia ya Rwanda huwezi kujua kwa nini leo Rwanda ipo hapo ilipo. Hakuna historia nyingine iliyoizamisha na kuinua Rwanda kama mauaji yaliyotokea 1957-1959 na 1994 ukiamua kuukwepa ukweli huu ni hiari yako.

    Tanzania tunalia na JK, JK. Rais wetu JK ni mtu mmoja tuliyemchagu wenyewe. Wewe unataka JK huyo huyo “AKULETEE” mabadiliko mpaka kwenye fani yako ya ICT. Yaani unataka Rais aende UDSM aitishe kikao na wadau wa ICT. Huoni kama hilo ndio tatizo tulilo nalo Watanzania. Tunaweka matumaini ya maendeleo yetu kwa mtu mmoja "Rais" badala ya sisi wenyewe Wananchi? Nani anayejua pengine JK hatokuwa Rais baada ya uchaguzi wa 2010…ina maana tuanza kumlaumu Rais mpya..!!??

    Ukibadilisha fikra zako, utaona JK hafanyi tofauti na lile aliloahidi kwenye uchaguzi wa 2000 au ambalo wananchi (walio wengi) walitarajia (nakupa pole kama ulitarajia mambo tofauti na yanayotekelezwa na Serikali ya JK). Na ndivyo Kagame anavyofanya, Warwanda walitarajia hayo kutoka kwake na wakamchagua kwa sababu waliona anaweza.

    Sasa pengine na sisi kama “Taifa” tukibadilisha matarajio yetu ifikapo 2010 Rais mpya awe JK au mwingine atatekeleza, matarajio hayo mapya…iwapo hatotekeleza basi ukiangalia Katiba yetu utaona inavyotuelekeza cha kufanya..!!

    Tukiendelea kusubiri Viongozi wenye nguvu kama “Malaika”, tunasubiri milele.

    ReplyDelete
  16. TULE WAPiiiiii
    so tender ni nje tuuu,kama twin towers za BoT,RICHMOND,EPA nk nk
    UNAKULA KWA UREFU WA KAMBA YAKO
    mjijuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  17. SOAMES,

    You better shut up my friend... You don't know squat about how this country is run.

    ReplyDelete
  18. Annoy of February 24, 2009 9:32 PM.

    MAY BE YOU ARE RIGHT... I WILL TAKE YOUR ADVICE. THANKS


    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...