A statement on the club's website revealed the move had been made "to maintain a challenge for the trophies we are still competing for".
Scolari, who led Brazil to their 2002 World Cup triumph, was appointed in June as the Avram Grant's replacement.
Chelsea, fourth in the Premier League and seven points behind Manchester United, will be led by assistant Ray Wilkins on an interim basis.
--------------------------------------------------------------
Natoa pole kwa wana wa darajani kwa kadhia hii. Nawaomba msikonde kwani kwa vile pochi mnalo basi ataletwa mwingine baabkubwa ila sidhani kuna atayemfikia 'nambari wani' Mourinho ambaye huko Inter Milan hadi leo hajawahi kufungwa. Ezza, Scolari wa Helsinki, upo hapo????
Ila uwongo mbaya, jamani. Penye ukweli usemwe. Na sie Bwawa la Maini tunampa onyo kali Benitez. Yaani tukikosa ubingwa mwaka huu atafute pa kwenda maana tushaanza kumchoka. We unauza ng'ombe kwa kesi ya kuku? We ngoja tu...
-Michuzi



Michuzi nakupongeza sana kwa kuwa muwazi leo,nimefurahishwa saaaana tena sana maana huwa unajifanyaga Benitez wako ni babkubwa kumbe anabahatisha sometimes.
ReplyDeleteKuuza ng'ombe kwa kesi ya kuku hiyo ni kweli kuwa Ben anacheza cheusi chekundu tena gizani.Anabeep naona siku hizi,we ngoja watu ka hawajamfukuzia mbali maana ubingwa mmh asali sana Man u aharibu mwishoni.
Atauza SIMU sasa ili anunue Credit za kuwapigia Anfield.
Chelsea Poleni sana kwa habari mbaya tena kipindi hiki.
ReplyDeleteNext game na Aston Villa tena kwao,itakuwaje jamani??
Michuzi Chelsea hawana hela tena kama zamani ndio maana hata wameshindwa kununua mchezaji january wameuza ili kupunguza madeni na mishahara coz walipunguza wafanyakazi miezi michache iliyobaki.
Tony Adams wa Portsmouth nae KAFUKUZWA michuzi au huna habariii??
Hongereni wana darajani kwa kuepukana na yule babu, amewakosti sana mwaka, bora mutafute kocha mwengine.
ReplyDeleteMICHUZI NAKUOMBA USIINGIE KWENYE MTEGO HUO WA MAJUNGU YA RAFA.JE USHAFANYA UTAFITI SASA NI KOCHA GANI YUKO MWENYE UWEZO HATA WA KUMKARIBIA RAFA AMBAYE YUKO AVAILABLE?AU UNATAKA KUWA KAMA CHELSEA KUMFUKUZA MOURINHO NA MPAKA SASA HAWAJAUNGA KUMPATA KOCHA MZURI?SIKILIZENI NYIE TIMU ZA HUKU HAZIUNDWI KAMA ZIMAMOTO,FERGI ALIAPPOINTIWA MANU 1986 NA KOMBE LAKE LA KWANZA NI CARLING 1991(MIAKA 5)SASA RAFA KAIKUTA TIMU MBOVU(MPAKA SASA WACHEZAJI WALIOBAKIA NI CARRA,GERRARD NA HYPPIA)ALIYORITHI,AMEJITAHIDI KUUNDA TIMU AMBAYO INACHALLENGE MUNATAKA AONDOLEWE,MNAJUA MADHARA YAKE,TUTARUDI NYUM 5 YEARS,KAMA CHELSEA SASA,KWA HIYO NAOMBA MWACHENI RAFA ALONE.WE SUFFERED ALOT WE DONT WANT TO GO BACK WHEN WE CANT EVEN QUALIFIED FOR CHAMPION LGE.
ReplyDeleteOCD
Mimi ni Blues damu, afadhali Scolari ameondoka maana ameshusha hadhi ya klabu yetu Chelsea.
ReplyDeleteBaada ya the special one kuondoa Avram kocha asiye na cheti alitutoa aibu kwa kwenda mguu kwa mguu na ManUtd ktk ligi Uingereza na champions League Moscow.
Sasa huyu Scholari alikuwa anataka 'beautiful game' kama la Brazil na la Arsenal, wakati wachezaji walizoea cha muhimu pointi hata ikiwa ushindi wa moja moja mechi kibao kwa kutumia goti na ugoko.
Amepafanya Stamford Bridge pasiwe uwanja wa kutuletea raha wala kuwatia hofu wageni.
Ila kweli tunahitaji mawinga kama walivyokuwa Duff na Robben, pia Bosingwa hafai tutafute mwingine.
Inshallah tutaibuka maana Wilkins ni mwingereza na anajua nini gemu la premier league na kabla ya Mei 2009 tutakuwa tumerudisha hadhi yetu
Mdau
West London
Ukerewe.
Chelsea ni sawa na Kajumulo. Ina mashabiki wa msimu. Itashuka kama Leeds! Bado Wenger, wamemlea sana na Yosso wake, ambao hawana lolote. Draw wanashangilia. Benitez ndio season yake ya mwisho. Mchezaji mmoja tu Gerrard. Akiumia, wanaumiza kichwa. Man U, Ferguson ni Master wa mind games. Premier League anaifahamu kama mke wake.
ReplyDeleteInter milan Kafungwa na Fiorentina 3-0 wiki iliyopita. ila Morinho wanawe walikuwa Drogba na Lampard sio Terry, Yule kaondoshwa sababu ya terry. Scolari lugha imemuangushak uelewana na wachezaji ila ni manager mzuri mie naomba benitez afukuzwe hata mie nishachoka awekwe Hiddink, Benitez hata akifukuzwa nitampa heshima yake ya Kutupatia Champion L na FA. Nawapa Hongera Arsenal kwakuweza kumvumilia Wanger kama timu kubwa kufukuza basi ilikuwa ni Arsenal mara ya mwisho Arsenal kombe 2004 tena FA cup, Champion L Arsenal hawajawahi kuchukuwa Ila safarihii wanaweza kujakuchukuwa. Poleni Chelsea ndio Mpira tu huo. Maximo mchukueni ana Records nzuri Maximo hahaha. Arsenal na Chelsea mnagombania nafasi na Aston Villa? Mie Liverpoolfc Ila Kudadeki MAn U wanatesa tukubali tu. Man U ilichukuwa 23 yrs kushinda Ligi Liverpoolfc tusiwe nan jaa sana miaka ni 19 tu jamani Tena hapo kati FA Champion Lg tumebeba najuwa Ligi tunauchu nao Ila baada ya miaka 2 ndio tutabeba bado sana sie.
ReplyDeleteBado Wenger!
ReplyDeleteMWACHE AONDOKE BORA HATA YA GRANT ALIKUWA ANAJITAHIDI TIMU IMEPOTEZA REKODI YA UWANJA WA NYUMBANI NAJUA ANAFUATA BENITEZ,UBINGWA ASAHAU KABISA
ReplyDeleteMichuzi, si kweli kwamba Inter Milan ya Mourinho bado haijafungwa. Katika ligi kuu ya Italia, 'Seria A', imeshapoteza mechi mbili hadi sasa. Mechi ya kwanza ilifungwa na AC Milani, kwa goli moja la Ronaldinho. Pia Januari 18, ilifungwa na Atalanta goli 3-1!Upo hapo, mkuu?
ReplyDeleteMichuzi nakuunga mikono na miguu kabisa huyu Benitez Bwawa la maini lisipo chukua ubingwa mwaka huu atafute pa kwenda. Haiwezekani ato sare na vitimu vinavyochungulia kaburi. Na wana darajani aliwafunga kwa kubahatisha sasa kocha kama huyu wa wa kazi gani? Atasababisha bwawa la maini litembee pekee wakati inajulikana duniani kote na hata huko Mars ambako inasadikika kuna viumbe wa ajabu. LIVERPOOL YOU WILL NEVER WALK ALONE.
ReplyDeleteaje kufundisha taifa stars basi...naskia mkataba wa maximo inaiasha baada ya miezi michache. JK atamlipia salary yake ambayo ni labda asilimia 3 ya uchumi wetu hahaha
ReplyDeleteila ingekua freshi tungeweza kumleta tanzania kwa ghrama ndogo.
Ndugu zangu wa darajani nendeni kumwomba radhi Avram Grant arudi kuwaendelezea timu. Chelsea ilikuwa inacheza soka zuri chini ya Avram kuliko chini ya Mourinho na wangechukua ubingwa isingekuwa mwaka jana isingekuwa kuanza vibaya msimu kulikotokea chini ya Mourinho.
ReplyDeleteNdugu zangu wa bwawa mwacheni Rafa. Ile timu iliyobeba ubingwa wa mabingwa wa Ulaya...yaani ukichukua mabingwa wote wa Ulaya, wao ndio walikuwa bingwa wao, ilikuwa na wachezaji gani wa kusema watacheza festi ileveni ya dunia? Kina Luis Sans Gracia? Jamaa ni mtaalamu. Ukiangalia kwa pointi timu imekuwa ikipata pointi nyingi zaidi kadri misimu inavyozidi kusogea sema tu bingwa naye anapatikana kwa kuwa na pointi nyingi zaidi. Rafa mwacheni, mpeni hela akomelee kwenye kiungo kupunguza kumtegemea Gerrard.
Kuna nafasi huko Portsmouth, Tony naye karushiwa virago. Labda Big Phil atajitosa huko. Sasa hivi wasiwasi hauko kwa Arsene na Rafa. Mwenye shaka sasa hivi ni Gareth Southgate na Boro.
MIE YANGA DAMU,NA ADUI NO ONE WA SIMBA. SASA MICHUZI KAMA SIO USHABIKI WA KITZ, WEWE HAO LV POOL WANKUFAHAMU,AU HADI KUSEMA SISI BWAWA LA MAINI,UMO LAKINI. SEMA MIE MSHABIKI WA LIVAPOOL ,TOA MAONI YAKO ,NA SIO UTOE MAONI NA YA WENZAKO WAKATI WEWE SHABIKI WA KITANZANIA,UNAYEFAHAMIKA HAPAHAPA MTANDAONI KWAKO,SIJAONA HATA MAONI YAKO KTK WEBU YA LV. POLE LAKINI.LIVAPULI HAIWEZI CHUKUA UBINGWA WA HUKO UKOLONI KWETU.
ReplyDeleteSi kweli ukiwa mtz na unashabikia Yanga au Simba ndio unajulikana kwa kuwa wewe mtanzania,Inawezekana kabisa hujulikani,lakini hakuna mtu analazimishwa kushabikia kitu asichikipenda.Michuzi anaipenda Liverpool,mwingine anaipenda Chelsea,mwingine Arsenal,wengine Man u,pia hata washabiki wa newcastle bongo wapo,Madrid,Barcelona,Ac Millan,Inter Millan,sasa msitake tuwe mashabiki wa labda Ashanti wakati hawatujui pia na wala soka lao haliburudishi kutazama.
ReplyDeleteELEWENI SOKA NI STAREHE KAMA STAREHE NYINGINE NA SIO KARAHA.kama wewe unapenda kuangalia soka la kishirikina wengine wanapenda soka la maana na ukweli.
Pia wanaoshabikia timu za ulaya wengi wao wanazo timu zao wanazoshabikia Bongo,hujanyimwa na usinyime wenzio.
Jamani mnapozungumza kuhusu bingwa wa champs league sio lazima awe na kikosi hatari duniani,ingekuwa hivyo basi madrid ile ya kina Ronaldo,Zidane,Figo,Raul,wangechuku kila msimu kabla hawajapanguka.Garcia ni mchezaji kama wengine,mbona Porto walichuku ubingwa na wakati ule timu haikuwa na majina makubwa??mbona chelsea anamajina makubwa na hajachukua ubingwa??
ReplyDeleteubingwa sio majina bali ni mfumo wa uchezaji na umakini wenu tuu kitimu.
Benitez analelewa na wasamaria wema ndio maana hajatimuliwa.
Huwezi kuuza Ng'ombe kwa kesi ya Kuku jamani ooh.
mteteeni weee lakini mwishoe yatamkumba tuu maana soka haiangalii sana historia ulifanya nini bali unafanya nn kwa wakati husika.mpooooooooooooo
KIDEDEA CHA UK AU MARY GOES ROUND HII HAPA TONY ADAM CHELSII SCOLARI INTER MWISHO WA MSIMU MORINYO UNITED GUS HIDINK PORTMOUTH AU MNABISHA?
ReplyDeleteChelsea walichemka kumchukua Scolari kwa kigezo cha WC winner. Jamaa hata record yake ya kombe la dunia mechi ngumu alizokutana nazo ni mechi yake dhidi ya England tu ambao kama si makosa ya David Seaman hali ingekua ngumu. Nusu fainali walikutana na Turkey ambao walikua hawana cha kupoteza. Ni mechi dhidi ya Germany angalau. Lakini kwenye Club level Scolari pengine angekua ni kocha wa kwanza Mbrazil kuwa na mafanikio,nakumbuka Luxemburgo alikuja kwa mbwembwe Real Madrid lakini akaishia kutupiwa virago tu hamna kitu.
ReplyDeleteJamaa alishindwa kabisa kucheza mechi ngumu ndio maana kuna kipindi aliweza kushinda mechi nyingi ugenini kuliko nyumbani sababu ya aina moja tu ya uchezaji wa passion build up kitu kilichokua kikiwachelewesha kufika kwenye 18 yards wakati wanapocheza na timu ngumu au derby matches na hii ndio sababu wameweza kupata point moja tu kati ya mechi zake dhidi ya the big four.Ni heri ya Grant japo nae alikua hana vyeti vya kutosha ila alikua na msaada wa Henk Ten Kate na Steve Clarke
Timu gani ya mwisho kuifunga Chelsea? Liverpool
ReplyDeleteTimu gani ya mwisho kuifunga Portsmouth? Liverpool
Next match
Manchester City v Liverpool.....
please taxi for Mr.Mark Hughes!!!!!!
Wadau mnajuwa mpira au mnalopoka tu???Mpira mmejulia wapi??Maana naona mtu kapoteza mda mwingi lakini hajaandika point yoyote ya maana........
ReplyDeletebenitez next au tu pinge?
ReplyDelete