Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani (Tanzanite Society) inakuletea sherehe kabambe ya kuadhimisha siku ya wapendanao duniani itakayofanyika katika ukumbi wa Tropican Pub (zamani Taitec-Area51, simu: 0476-78-0560) ulio karibu na kituo cha train cha Sagamino (Sotetsu line) siku ya Jumamosi ya tarehe 14/2/2009.

Katika sherehe hiyo Dj mzoefu Pembe aka Dj Zee atawapatia Watanzania na wahudhuriaji wengine muziki safi wa aina mbali mbali.
Kingilio: 2000Yen, utapata kinywaji kimoja.

Kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa wapendanao watakaopendeza zaidi. Ukipata taarifa hii mtaarifu na mwenzio, asije akakosa fursa hii ya kuburudika na kukutana na watanzania wenzake. Taarifa hii imetolewa na Kamati ya Uhamasishaji na Starehe ya Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani.

Kwa maelezo zaidi kuhusu sherehe hii tafadhali wasiliana na wafuatao:

Bw. Kapinga(080-3097-5744),
Bw. Pembe (080-3458-8786),
na Bi. Mariam(090-4422-8555).

================================================


Uongozi wa Jumuiya
Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani (Tanzanite Society)

M/Kiti: 090-3899-0638
Makamu M/kiti: 080-30975744
Katibu Mkuu: 090-4130-4754
Katibu M/Msaidizi : 090-9801-4433
K/Mwenezi : 080-3532-4043 =======================================================

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Nyinyi Watanzania mnaoishi nchini Japan "You have Brighter Minds,atleast",kuliko hawa ma Dummies wanaoishi Uingereza,hasara tupu!Congratulations!Mkihitaji Dagaa wa Kigoma au Ngisi au Matoke ya Bukoba au Kivelege cha Iringa tutwagieni email tushughulike huku ili msherehekee kwa salama!Msisahau kucheza Sindimba na Lizombe huku Mkirusha Roho!"najuta kukufahamu"----mgosi wa ndima----

    ReplyDelete
  2. Itakuwa raha sana, nategemea kutakuwa na mishikaki, sijala siku nyingi.

    Ato de.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...