Home
Unlabelled
vibajaji oye!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Haa haaa, haya mambo mengine unaweza ukadharau lakini siku unapewa bendera yako nje ya nchi unaambiwa uishike hukawii mtu ukaigeuza. Sawa michuzi, huyo jamaa yupo right katika suala la kwamba bluu inakiuwa chini, kwa vile ni mito bahari na maziwa. Lakini amekosea jinsi ya kuifunga, ilitakiwa kijani ndiyo iguse mlingoti siyo bluu. Hilo ndilo kosa lake. Teh teh teh
ReplyDeleteKaka Michuzi sijui hiyo Picha ni yako? maana siwezi amini kuwa hata wewe hujui mpangilio wa rangi za bendera ya taifa, hata kama hujui si ungeenda karibu na mlingoti wa bendera uone zimekaaje? Rangi ya bluu huwa chini daima jamani Tuseme Mara ngapi mtuelewe?
ReplyDeleteHiyo blue ikikaa chini au ikikaa juu itasaidia nini katika kuondoa umaskini wa Tanzania.
ReplyDeleteLete mada ya maana watu wajadili, sasa tukishakwambia inaka juu au chini ndo iweje? Hivi hunakazi yakufanya? Una muda mchafu sana eeh?
kilichobaki sasa ni ngombe kuanza kurandaranda mitaa ya city, hapo tutakuwa tumekamilika sasa kuwa kama mumbai
ReplyDeleteKaka Michu,
ReplyDeleteHuyo jamaa kachemsha kidogo tu, kwamba bendera imekaa sawa ila amekosea upande wa kunin'gnizia! - I hope that makes sense! Kiswahili kigumu duh!!!
Mdau,
Geneva
hapo mlipo mbona kuan bendera kibao jirani,kwa nini mbishane wakati ukweli upo wazi, rangi ya blue inakuwa juu, ndo inavyokuwa ,na itabaki hivyo.
ReplyDeleteHILI SUALA LA RANGI NAONA KAMA TUNGEMWACHIA KAKA LAWRANCE MASHA ALISHUGHULIKIE MAANA TUKILIZUNGUMZIA HUMU LINAKUWA KAMA KULETA UDINI. MICHUZI UNAONAJE? MIMI NI MPENDA HAKI NA SINA ISSUE NA MTU YEYOTE, MWENYE UWAMUZI WA MWISHO NI MASHA PEKE YAKE YEYE NDIYO WAZIRI WA MAMBO/MASHAURI YA KIGENI.
ReplyDeletemichuzi please natakiwa kwenda kazini kesho,,, mbavu zangu jamani,wouuuuu injini kiuno, kasoro za rangi ya bendera,
ReplyDeleteKwani wewe ulitaka rangi ya blue ikae katikati?. Kwani hapo ulipo hakuna hata alama ya bendera ya taifa ukaangalia. Kwa wenzetu bendera ya Taifa ni kitu cha kujivuia, lakini kwetu sisi inashangaza kuona hata hatujui jinsi rangi za bendera yetu zilivyopangiliwa.Basi kwa kuwa uko kwenye mtandao angalia kwenye website ya selikali utapata jibu mara moja lenye uhakika wa bila kubishana kuliko kupoteza muda kwa kitu kama hicho ambacho kiko wazi
ReplyDeleteMdau
Cardiff
Kwa habari nilizozipata ndani ya wiki hii, kuhusu hivyo vipikipiki vya muundo huo, na siyo vibajaji-kwani (vi)bajaji ni jina la kampuni inayotengeneza hivyo vijigari vya miguu mitatu(vijigari vya kiaina,-nilipomuuliza muhindi mwenyewe hakuweza kuvifafanua vizuri km ni vigari au vipikipiki)
ReplyDeleteimeacha kuvizalisha/kuvitengeneza kutokana na kupitwa kwa wakati na sasa inatengeneza pikipiki za kawaida, na miaka ya baadae pengine vinaweza visionekane India tena, au vikaonekana sehemu zisizokuwa miji huko india.
Tukivishabikia Watanzania SOKO lake kuu litakuwa nchini mwetu, Kwani vimeonekana vinakasoro au jamaa wameshabuni njinsi gani ya kuvitokomeza India na wanafikiria wapi, wapo kama walivyokuwa wao mwanzo wawarithishe
Wabongo wake-up!
huyo aliyefunga hiyo bendera kapatia mpangilio wa rangi lakini ufungaji kakosea bwana hifungwi kwenye bluu ni kwenye kijani!!!!
ReplyDeletekakosea ufungaji tu mpangilio wa rangi kaotea
ReplyDeleteivi nyie mkoje??
ReplyDeletendo nini ichi,aaaagh
Nadhani hii mada ilizungumziwa kipindi. Kaka Michu mi naomba kama kuna unauwezekano uwasilishe hili swali kwa wahusika ili jamii ipatiwe elimu juu ya hili - maybe kupitia luninga kila mwezi kwa miezi 6 ama zaidi.
ReplyDeleteNadhani hii mada ilizungumziwa kipindi. Kaka Michu mi naomba kama kuna unauwezekano uwasilishe hili swali kwa wahusika ili jamii ipatiwe elimu juu ya hili - maybe kupitia luninga kila mwezi kwa miezi 6 ama zaidi.
ReplyDeleteJamaa amepatia jinsi alivyoipangilia rangi zake ila naungana na Mdau wa Geneva na dada yangu Patricia kuwa amekosea kuivika kwenye nguzo...ilitakiwa mlingoti au niseme kile chuma alichotumia kuipeperushia kiwe ule upande wenye rangi ya kijani na nyeusi na sio huko alikotumia yeye kwenye rangi nyeusi na bluu. Lakini Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Nanihii, Mtoa maoni J wa February 06, 2009 10:18 amedokeza kitu muhimu sana. Kweli kuna haja ya wahusika kutoa elimu hiyo kwa umma. Ukweli watu wengi hawajui na hao wahusika wameziachia shule zifanye kazi hiyo kwa kuwaelimisha/kuwafundisha wanafunzi. Hapo ndipo kuna hatari; baadhi ya shule au sijui niseme walimu nao hawako makini katika suala hilo la bendera. Kwa mfano kwenye lango kuu (gate) la Shule ya Sekondari ya Uhuru Mchanganyiko iliyopo hapa Dar lango ambalo linatizamana na magorofa ya Shirika la Nyumba(NHC)yaliyopakana kabisa na kiwanda cha bia... au niseme hivi ukifuata barabara ya Uhuru kutokea Msimbazi Keep Left kuelekea Uwanja wa Karume au Ilala Boma, upande wako wa kushoto baada ya msururu mrefu wa maduka yaliyojengwa kwenye ukuta wa shule ya sekondari ya Benjamin Mkapa, utakutana na lango (gate) la shule hiyo ya Sekondari ya Uhuru Mchanganyiko ambapo, kulia na kushoto mwa lango hilo uongozi wa shule umechora bendera kubwa mbili za taifa nadhani ni kwa ajili ya kuwakumbusha wanafunzi jinsi bendera ya taifa lao ilivyo. Ni wazo zuri lakini cha ajabu bendera hiyo imechorwa juu chini!! yaani rangi ya kijani chini na ya bluu juu. Sasa mtoto/mwanafunzi tangu anaanza form one hadi atakapomaliza form four yeye ndivyo anavyoijua hiyo bendera, akishamaliza shule halafu mtu amwambie eti hivyo bendera imepinduliwa hatakuelewa kabisa, inasikitisha sana. Cha kushangaza zaidi ni kuwa hakuna hata mtu mmoja shuleni hapo anayejali hilo; si mwalimu mkuu wala hata hao walimu wa somo la uraia (civics)!! Sina data zaidi ila nadhani kosa hilo huenda limefanywa na shule nyingine nyingi tu...mikoani ndo usiseme kama hapa barazani watu hawaoni itakuwa nyuma ya nyumba! Hivyo uelewa wa suala zima la bendera na hata wimbo wa taifa kwa wengi ni mdogo, nadhani wahusika wachukue hatua za maksudi za kuelimishe Umma. Wakatabahu. Mdau Ben Ben
ReplyDelete