toka vibajaji, vibeba-mishkaki na injini kiuno kuruhusiwa kutanua kama teksi, taratibu mitaa ya katikati ya jiji la dar limeanza kuona taswira kama hizi ambazo kufumba na kufumbua mambo yatakuwa kama mumbai. nimebishana kidogo na mwenye kibajaji hiki kuhusu rangi za bendera zilivyokaa. yeye kasema bluu kuwa chini ni sahihi. wadau msaada tafadhali

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Haa haaa, haya mambo mengine unaweza ukadharau lakini siku unapewa bendera yako nje ya nchi unaambiwa uishike hukawii mtu ukaigeuza. Sawa michuzi, huyo jamaa yupo right katika suala la kwamba bluu inakiuwa chini, kwa vile ni mito bahari na maziwa. Lakini amekosea jinsi ya kuifunga, ilitakiwa kijani ndiyo iguse mlingoti siyo bluu. Hilo ndilo kosa lake. Teh teh teh

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi sijui hiyo Picha ni yako? maana siwezi amini kuwa hata wewe hujui mpangilio wa rangi za bendera ya taifa, hata kama hujui si ungeenda karibu na mlingoti wa bendera uone zimekaaje? Rangi ya bluu huwa chini daima jamani Tuseme Mara ngapi mtuelewe?

    ReplyDelete
  3. Hiyo blue ikikaa chini au ikikaa juu itasaidia nini katika kuondoa umaskini wa Tanzania.
    Lete mada ya maana watu wajadili, sasa tukishakwambia inaka juu au chini ndo iweje? Hivi hunakazi yakufanya? Una muda mchafu sana eeh?

    ReplyDelete
  4. kilichobaki sasa ni ngombe kuanza kurandaranda mitaa ya city, hapo tutakuwa tumekamilika sasa kuwa kama mumbai

    ReplyDelete
  5. Kaka Michu,

    Huyo jamaa kachemsha kidogo tu, kwamba bendera imekaa sawa ila amekosea upande wa kunin'gnizia! - I hope that makes sense! Kiswahili kigumu duh!!!

    Mdau,

    Geneva

    ReplyDelete
  6. hapo mlipo mbona kuan bendera kibao jirani,kwa nini mbishane wakati ukweli upo wazi, rangi ya blue inakuwa juu, ndo inavyokuwa ,na itabaki hivyo.

    ReplyDelete
  7. HILI SUALA LA RANGI NAONA KAMA TUNGEMWACHIA KAKA LAWRANCE MASHA ALISHUGHULIKIE MAANA TUKILIZUNGUMZIA HUMU LINAKUWA KAMA KULETA UDINI. MICHUZI UNAONAJE? MIMI NI MPENDA HAKI NA SINA ISSUE NA MTU YEYOTE, MWENYE UWAMUZI WA MWISHO NI MASHA PEKE YAKE YEYE NDIYO WAZIRI WA MAMBO/MASHAURI YA KIGENI.

    ReplyDelete
  8. michuzi please natakiwa kwenda kazini kesho,,, mbavu zangu jamani,wouuuuu injini kiuno, kasoro za rangi ya bendera,

    ReplyDelete
  9. Kwani wewe ulitaka rangi ya blue ikae katikati?. Kwani hapo ulipo hakuna hata alama ya bendera ya taifa ukaangalia. Kwa wenzetu bendera ya Taifa ni kitu cha kujivuia, lakini kwetu sisi inashangaza kuona hata hatujui jinsi rangi za bendera yetu zilivyopangiliwa.Basi kwa kuwa uko kwenye mtandao angalia kwenye website ya selikali utapata jibu mara moja lenye uhakika wa bila kubishana kuliko kupoteza muda kwa kitu kama hicho ambacho kiko wazi

    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  10. Kwa habari nilizozipata ndani ya wiki hii, kuhusu hivyo vipikipiki vya muundo huo, na siyo vibajaji-kwani (vi)bajaji ni jina la kampuni inayotengeneza hivyo vijigari vya miguu mitatu(vijigari vya kiaina,-nilipomuuliza muhindi mwenyewe hakuweza kuvifafanua vizuri km ni vigari au vipikipiki)
    imeacha kuvizalisha/kuvitengeneza kutokana na kupitwa kwa wakati na sasa inatengeneza pikipiki za kawaida, na miaka ya baadae pengine vinaweza visionekane India tena, au vikaonekana sehemu zisizokuwa miji huko india.

    Tukivishabikia Watanzania SOKO lake kuu litakuwa nchini mwetu, Kwani vimeonekana vinakasoro au jamaa wameshabuni njinsi gani ya kuvitokomeza India na wanafikiria wapi, wapo kama walivyokuwa wao mwanzo wawarithishe

    Wabongo wake-up!

    ReplyDelete
  11. huyo aliyefunga hiyo bendera kapatia mpangilio wa rangi lakini ufungaji kakosea bwana hifungwi kwenye bluu ni kwenye kijani!!!!

    ReplyDelete
  12. kakosea ufungaji tu mpangilio wa rangi kaotea

    ReplyDelete
  13. ivi nyie mkoje??
    ndo nini ichi,aaaagh

    ReplyDelete
  14. Nadhani hii mada ilizungumziwa kipindi. Kaka Michu mi naomba kama kuna unauwezekano uwasilishe hili swali kwa wahusika ili jamii ipatiwe elimu juu ya hili - maybe kupitia luninga kila mwezi kwa miezi 6 ama zaidi.

    ReplyDelete
  15. Nadhani hii mada ilizungumziwa kipindi. Kaka Michu mi naomba kama kuna unauwezekano uwasilishe hili swali kwa wahusika ili jamii ipatiwe elimu juu ya hili - maybe kupitia luninga kila mwezi kwa miezi 6 ama zaidi.

    ReplyDelete
  16. Jamaa amepatia jinsi alivyoipangilia rangi zake ila naungana na Mdau wa Geneva na dada yangu Patricia kuwa amekosea kuivika kwenye nguzo...ilitakiwa mlingoti au niseme kile chuma alichotumia kuipeperushia kiwe ule upande wenye rangi ya kijani na nyeusi na sio huko alikotumia yeye kwenye rangi nyeusi na bluu. Lakini Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Nanihii, Mtoa maoni J wa February 06, 2009 10:18 amedokeza kitu muhimu sana. Kweli kuna haja ya wahusika kutoa elimu hiyo kwa umma. Ukweli watu wengi hawajui na hao wahusika wameziachia shule zifanye kazi hiyo kwa kuwaelimisha/kuwafundisha wanafunzi. Hapo ndipo kuna hatari; baadhi ya shule au sijui niseme walimu nao hawako makini katika suala hilo la bendera. Kwa mfano kwenye lango kuu (gate) la Shule ya Sekondari ya Uhuru Mchanganyiko iliyopo hapa Dar lango ambalo linatizamana na magorofa ya Shirika la Nyumba(NHC)yaliyopakana kabisa na kiwanda cha bia... au niseme hivi ukifuata barabara ya Uhuru kutokea Msimbazi Keep Left kuelekea Uwanja wa Karume au Ilala Boma, upande wako wa kushoto baada ya msururu mrefu wa maduka yaliyojengwa kwenye ukuta wa shule ya sekondari ya Benjamin Mkapa, utakutana na lango (gate) la shule hiyo ya Sekondari ya Uhuru Mchanganyiko ambapo, kulia na kushoto mwa lango hilo uongozi wa shule umechora bendera kubwa mbili za taifa nadhani ni kwa ajili ya kuwakumbusha wanafunzi jinsi bendera ya taifa lao ilivyo. Ni wazo zuri lakini cha ajabu bendera hiyo imechorwa juu chini!! yaani rangi ya kijani chini na ya bluu juu. Sasa mtoto/mwanafunzi tangu anaanza form one hadi atakapomaliza form four yeye ndivyo anavyoijua hiyo bendera, akishamaliza shule halafu mtu amwambie eti hivyo bendera imepinduliwa hatakuelewa kabisa, inasikitisha sana. Cha kushangaza zaidi ni kuwa hakuna hata mtu mmoja shuleni hapo anayejali hilo; si mwalimu mkuu wala hata hao walimu wa somo la uraia (civics)!! Sina data zaidi ila nadhani kosa hilo huenda limefanywa na shule nyingine nyingi tu...mikoani ndo usiseme kama hapa barazani watu hawaoni itakuwa nyuma ya nyumba! Hivyo uelewa wa suala zima la bendera na hata wimbo wa taifa kwa wengi ni mdogo, nadhani wahusika wachukue hatua za maksudi za kuelimishe Umma. Wakatabahu. Mdau Ben Ben

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...