waziri wa nchi ofisi ya rais (muungano) muhammad seif khatibu (nyeupe mbele), naibu waziri wa habari, utamaduni na ichezo, joel maximo (shoto kwa mh. khatib) na kocha marcio maximo wakliwa na taifa stars baada ya kurejea majuzi toka ivory coast. hadi sasa mjadala umekuwa mkali ila wadau wengi wamekuwa wakitoa maoni kwa jazba badala ya hoja. swali ni rahisi sana. maximo anatufaa ama hatufai. toa sababu na pia wazo mbadala ili tuweze kusonga mbele

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Bro hii Link imekaaje, maana nikibofya hapo kwenye link ya msiba inanipeleka kwenye msiba wa mwaka jana;Saturday, July 5, 2008 uliotokea Uingereza

    ReplyDelete
  2. Huyu Mitchu leo kaua mtu nini?
    mbona kachomoa haraka?

    ReplyDelete
  3. Hapo alipotufikisha ndio mwisho wa uwezo wake kajitahidi sana na katufanyia makubwa na tunamshukuru. Tunahitaki kocha mwingine atutoe hapo na kuendelea mbele, mwalimu aliyefundisha vizuri shule ya msingi huwezi kuendelea naye sekondari kwa kuwa kafundisha vizuri msingi. Habari ndo hiyo!!

    ReplyDelete
  4. NAFIKIRI AENDELEE MPIRA WA TANZANIA BADO UPO CHINI,NA TATIZO KUBWA WACHEZAJI WA TANZANIA HAWANA NIDHAMU YA MPIRA NA HILI NDILO TATIZO KUBWA TANZANIA NZIMA NIDHAMU YA MPIRA HAKUNA NA TATIZO LA PILI NUI KUBWA AMBALO NI KUWA HAWAFUNDISHIKI SASA HAPA SIJUI NI UMRI AU ELIMU NI TATIZO KUBWA

    ReplyDelete
  5. NAFIKIRI AENDELEE MPIRA WA TANZANIA BADO UPO CHINI,NA TATIZO KUBWA WACHEZAJI WA TANZANIA HAWANA NIDHAMU YA MPIRA NA HILI NDILO TATIZO KUBWA TANZANIA NZIMA NIDHAMU YA MPIRA HAKUNA NA TATIZO LA PILI NUI KUBWA AMBALO NI KUWA HAWAFUNDISHIKI SASA HAPA SIJUI NI UMRI AU ELIMU NI TATIZO KUBWA

    ReplyDelete
  6. hafai,hana jipya kama waliopita tu,MAXMO analipwa vizuri anapewa sapoti kila kona lakini matokeo mabaya, Makocha wetu waliopita wakupewa sapoti kama anayopewa Maximo ,binafsi naamini wakipewa nafasi makocha wa nyumbani au kocha wa nje mwingine tunaweza kwenda mbali zaidi kutokana na sapoti kubwa kutoka kwa Rais, wadhamini,wachezaji na wananchi kwa ujumla.ni wakati sahihi kwa TZ kufanya mabadiliko.

    ReplyDelete
  7. MAONI YANGU - MAKULILO Jr,

    Kumekuwepo na hoja nyingi, na baadhi ya wadau waliongea redioni akina Mziray na mwenzake kuwa Maxiomo hatufai.Walitoa sababu zao, moja ya sababu kubwa ni kuwa kocha kutoka Brazil huwa hawana mafanikio nje ya Brazil.Alitolea mfano wa Pereila na Scolari.Na wengi wanataka kocha kutoka Ulaya.

    Hapo ndio hoja ya kocha sehemu atokayo inapoanza.Inabidi tuondokane na suala la kusema kocha bora lazima atoke ulaya na si Brazil.Brazil ni nchi moja, wakati Ulaya ni bara lenye nchi 45.Sasa jutakua punguani wa akili kulinganisha maendeleo ya nchi 45 zilizoendelea na nchi moja iliyo masikini kama nchi za Afrika. Kwa ambao hamfaham, Brazil ni nchi masikini kama nchi nyingine za Afrika tu, huwezi kufananisha na nchi nyingi za ulaya ambazo zimeshaendelea kiuchumi na mambo mengineyo.Hivyo usilete hoja hapa kuwa makocha toka Brazil hawawiki duniani.Swali la kujiuliza, je, ni maokocha wangapi wa Brazil wameshawahi kufundisha nje ya Brazil?Je, walifanikiwa kiasi gani?Na pia tuangalie upande wa pili, je ni makocha wangapi wa ulaya wameshawahi kufundisha Brazil?Je waliwika huko?Au ni timu ngapi za ulaya zilipokutana na klabu za Brazil ziliambulia vichapo?

    Hapa tusingumzie kocha anatoka nchi gani, tuangalie uwezo wake.Maana kama makocha ulaya tumeshafundishwa na makocha wengi tu, uwezo wao ulionekana.Tukianza kusema kocha wa Brazil hana rekodi, hivi tuje kwenye basketball, Tanzania ina rekodi gani kimataifa??Hakuna rekodi yoyote ile zaidi ya kuwa kichwa cha mwendawazimu.Lakini HASHEEM THABIT sasahivi anawika Marekani nzima kwa basketball, wakati hakuna matanzania mwingine ktk historia ya mpira wa kikapu kaisha cheza ktk level ya Thabit.Sasa tukiangalia rekodi hiyo, basi Hasheem hajui kucheza.Hapa ni uwezo binafsi wa mtu, na si katoka nchi gani.

    Suala la pili ni watu kuiga mpira wa kwenye TV na kutaka uwepo Tanzania ndani ya siku mbili.Usione timu kama Real Madrid, Chelsea nk zinafukuza kocha kama asipoleta mafanikio ktk klabu.Lazima uangalie uwezo wa wachezaji wa timu kama Chelsea, ni professional, na ile kazi ndio yao, wanalipwa mamilioni ya hela, we angalia hela kama ya Robinho, sio mchezo.Sasa tayari environment ni nzuri ya kuweza kufanya vizuri ktk mashindano...wana haki ya kumfukuza kocha kama asipofanya vizuri ktk mashindano.

    Tuje ktk soka letu, huwezi kamwe kuwafananisha hawa wastaafu wa soka, eti mchezaji kama Nsajigwa miaka 28 akacheze ulaya, timu gani itamchukua??Inatakiwa uwepo ktk soko la mpira kama akina Beckham ukiachilia umri wake, rekodi yake inajulikana hivyo umri sio tatizo ndkio maana AC Milan wanamng'ang'ania abaki nao.Sasa huyu Nsajigwa atachukuliwa na timu gani??

    Maximo kafanya kazi kubwa sana jamani.Tusiangalie kuchukua kombe la mataifa ya Afrika au kuingia kombe la dunia tu ndio mafanikio.Cha msingi ni kujenga timu imara ya miaka mingi ijayo.Na hicho ndio Maximo kakijenga, na anaendela kukijenga.Kaondoa ile imani kuwa mchezaji wa timu ya taifa lazima uwe simba au yanga, sasahivi hata timu ya vijana, huko jk ruvu, azam nk watu wanapiga soka.Kitu kikubwa sana hiki.Pia kubadilisha uchezaji, toka butua butua hadi gonga za maana.Kutoa sare na cameroon, senegal, ghana hapo bongo sio suala la kitoto jamani.Tulikua tunafungwa home hata na shelisheli, leo hii tumesahau hayo yote eti hajachukua kombe la mataifa ya afrika.

    Watu wengine wanakuja na suala la kusema kwamba kocha mzalendo sijui akipewa hizo support kama maximo lazima naye aifikishe mbali.Hapa hakuna vya kusema hoja za uzalendo au nini, tunaangalia uwezo wa mtu kikazi, na anafanya nini.Katika kuijenga timu ya muda mrefu, lazima gharama itumike...we angalia timu ya Man City inavyojenga, inachukua wachezaji wengi wazuri kwa gharama ya juu, na inajipanga kwanza, sio tu baada ya kumchua Robinho, then Bridge nk then uchukue kombe, la hasha ni muda unahitajika.Hata Chelsea leo hii ina kiburi cha kufukuza kocha baada ya kujijenga kwa muda, nhaijakurupuka tu.

    Ndio maana wachezaji wadogo kama akina Athman Iddi, Haruna Moshi nao wanajiona eti ni wa kimataifa.Bado sana, ongeza juhudi, nidhamu iwepo, na ondoa majigambo..ondokana na sifa za kijinga za mtaani na redioni zinazoweza kukupotosha.Wewe mtangazaji unamlinganisha Haruna Moshi mfano tuchukulie na Seedolf, hiyo kweli akili..inamfanya naye huyo Haruna Moshi avimbe kichwa, matokeo yake akitoka hapo simba ni kwenda Tukuyu United huko, mwisho wa soka, inabaki enzi zetu

    Maximo abaki,
    Mbona kwenye siasa Kikwete anazidi kupewa muda wa kujipanga?Tuwe wavumilivu ndugu

    MAKULILO Jr,

    ReplyDelete
  8. MAXIMO ANA PROGRAM NZURI AMBAYO TAYARI IMESHAANZA KUNYANYUA SOKA LA TANZANIA.TATIZO LETU KUBWA NI WACHEZAJI WETU WAPO VERY INCONSISTENCY LEO WANACHEZA VIZURI KESHO WANAVURUNDA HALAFU KINACHOENDELEA NI MAJUNGU MATUPU KAMA KAWAIDA YETU WASWAHILI.NASHINDWA KUELEWA KUWA WADAU JE HAWALIONI JINSI AMBAVYO SOKA LETU LILIVYOPANDA NA JINSI AMBAVYO KOCHA MAXIMO ANAVYOPIGANIA NIDHAMU KATIKA TIMU KITU AMBACHO NI MSINGI KATIKA MICHEZO YOYOTE ILE..NIDHAMU UWANJANI NA NJE.ACHENI MAJUNGU JAMANI KWANI HAMJALIONA SOKA LETU LILIVYOPANDA HADI LEO..JE HAIKUWA NDOTO KWETU KUWAKWAMISHA CAMEROON,SENEGAL,COTE D'VOIRE NA BURKINABE LAKINI LEO TUNAWEZA.SIELEWI KWA NINI WADAU WANAJENGA CHUKI NA MAXIMO WAKATI TUNAONA MATOKEO YA KURIDHISHA KITU AMBACHO HATUJAWAHI ONA KABLA.NDIO ANAWEZA KUWA MKALI LAKINI HIYO NI KAZI YAKE NA YEYE PIA KAMA BINADAMU ANAPENDA KUONA TUNASHINDA ILI AJENGE CV YAKE.WATANZANIA TUTULIE TUMWACHIE KOCHA KAZI YAKE..YEYE AMETUFIKISHA HAPO ATATUFIKISHA MBALI ZAIDI KAMA ATAPEWA USHIRIKIANO ZAIDI NA WADAU NA WACHEZAJI.

    ReplyDelete
  9. Tatizo lenu watanzania katika mpira mnataka kwenda mwezini hata kabla ya kujua kutengeneza chombo sembuse kujua urubani!
    Maximo katutoa mbali sana tulikuwa tuna kula magoli ya fedheha hata kwa ndugu zetu wa jirani.
    Leo kila mtu anajua mprira lakini ni kwa kuona tu katika runinga.
    Mkiambiwa wachezaji fulani ni walevi na hawanana nidhamu imekuwa nongwa.
    Miaka ya zamani waulizeni kina Tenga chini ya Mkorea Pak Yung Yang na professa Victor. Wachezaji walikuwa mpaka wanabeba vyuma ili kujenga mwili. Hii yote inawezekana kwa kuwa na nidhamu.Vinginevyo tuanzishe ligi ya maneno tu!

    ReplyDelete
  10. ACHENI KUPOTEZA MDA KUBISHAN BISHANA KAMA MAXIMO ANAFAA AU HAFAI,KASHAWAAMBIA HATAKI MKATABA MPYA SASA KWANINI MNA ENDELEA KUTAKA KUBISHANA KUHUSU MTU ANAYEONDOKA BADALA YA KUANZA KUJADILI MAKOCHA AMBAO MTAWEZA KUMPA NAFASI BAADA MAXIMO? HAMUONI KWAMBA MKIANZA KUJADILI KOCHA AMBAYE ATAFAA KUIFUNDISHA TAIFA STARS MAPEMA SASA HIVI ITAWEZA KUWASAIDIA KUMCHAMBUA VIZURI KOCHA HUYO? WATANZANIA TUNAPENDA KUBISHANA MNO BADALA YA KUTAFUTA SOLUTION.
    MIMI NAOMBA HUU MJADALA WA MAXIMO UFUNGWE KWANI HATA MAXIMO MWENYEWE KATWAMBIA ANATAKA KOCHA MWINGINE AJE ATUONGEZEE ZAIDI YA YEYE ALIPOFIKA.
    MDAU WA SOKA LA KISASA.

    ReplyDelete
  11. Maximo na hana uwezo.

    alisema mwenyewe kaja kujenga msingi hivyo hana uwezo wa kuleta kombe.

    pia amekuwa na chuki za kijinga na wachezaji.huwezi kumuacha chuji kijana ambaye kawapa wakati mgumu Cameroon.

    chuji angecheza chan tungeshinda mechi zile.kwanza ni kiungo mkabaji na anasaidia kufunga.

    nidhamu ndani ya nje sio kweli Stephen Gerrard ana kesi ya kumpiga mtu mahakamani lakini timu yake haijamfukuza.
    Ashley Cole anasakata jipya na mpenzi wake kama angekuwa maximo angemfukuza kwa kusema hana nidhamu asilimia mia moja anayoitaka.

    Maradona ni mchezaji ambaye amekutwa mara kadhaa na madawa ya kulevya lakini timu yake ya taifa kaifanyia mambo mengi pia ni maradona aliyeipa NAPOLI ubingwa italy.

    wachezaji kama George best na Gazza NI mfano wa wachezaji waliokuwa na nidhamu mbovu lakini makocha watalaam walijua jinsi ya kuwatumia.

    BOBAN ni mchezaji anayetengeneza vyumba vingi lakini unapomuweka nje unatukosesha magoli.

    Steven Gerrard na paul scholes waliwahi kuhitilafiana na kocha Ericson wa England kiasi cha Scholes kuamua kujiuzulu.

    Gerrard alikuwa akicheza chini ya kiwango na kuna mechi na ufaransa alifungisha hiyo ilitokana na kucheza role ambayo yeye alikuwa hawezi na alibishana sana na kocha.

    mchezaji kama ROONEY angepewa maximo angempoteza kwani alikuwa hana nidhamu na mbabe lakini walimu kwa vile wanajua saikolojia wamemchukulia anavyotaka na sasa ni mchezaji mzuri.
    kazi ya kutengeneza nidhamu ni ya mwalimu kina BOBAN NA CHUJI hawajafikia kiasi cha kushindikana.

    hakuna taasisi isiyo na cheki and balance.yaani maximo anawajibika kwa nani kama akikosea?

    inachoonekana TFF wana nidhamu ya uoga kwani wanaogopa kutofautiana na maximo wakiamini watatofautiana na JK.

    lakini nje ya ofisi zao wananung'unika sana juu ya ubabe wa maximo.

    mimi narudia kauli yangu kuwa kwa support wanayopata timu ya taifa hivi sasa hata timu akipewa mbaraka wa Ashanti basi stars watakuja na kombe la duniani.

    maximo ni failure mkubwa.

    kocha wa chelsea mwaka jana grant kapoteza mechi moja tu ile wiki na manchester alipopewa timu na kaipeleka hadi fainali kombe la ulaya kitu ambacho hakikuwahi kutokea lakini kaondolewa kwa vile hakuleta kombe.

    au maurinho asingeondolewa kwa vikombe alivyoleta.

    ukocha ni kuleta vikombe sio blaa blaa kama maximo.

    hatufai aondoke.
    mara aseme kuwa anataka vijana kwa asilimia sabini swali unaweza kumuweka nje DROGBA na kumpanga shaun wright kwa kigezo cha umri?

    au Lampard akae nje kwa vile ana miaka 30?Barrack ana 33.robert Carlos na Caf wamecheza hadi wakiwa na miaka 35 timu zao.

    shilton hadi miaka 40.david James ana 39.jee boban ni mkubwa kiasi hicho?mara aseme umri mara aseme nidhamu mara aseme kaja kujenga msingi yaani ni mr.visingizio.

    kama anataka vijana Nsajingwa ana miaka 34 kwanini kampa ukaptain?angempa kiggi makassy.

    mdau kisiju.

    ReplyDelete
  12. Alichosema mdau hapo juu nadhani ni sahihi kabisa. Mimi pia naona Maximo ameshaishiwa! Hatuwezi kulazimisha mtu wakati hata yeye mwenyewe anaona kuwa hawezi kuendeleza hii timu. Wakati umefika kwa Maximo kutafuta vilabu afundishe au kama anataka akafundishe timu zingine za dunia hii ya tatu ambazo zinahitaji msaada wake wa kuzitoa "kutoka katika vichwa vya wendawazimu hadi kuzifikisha hapa pa kuweza kutoa droo"". Sote tunaona uwezo wa Maximo ni kulazimisha droo na sio ushindi sasa mnategemea tutafika katika fainali na hizo droo. Timu haifungi, timu haina mbinu za kufunga sasa tufanyeje? Aondoke na tunamshukuru sana kama hataki basi tumpe timu ya Vijana kwani Tinoco si kakimbia. Timu ya Wakubwa apewe kocha mwingine toka nchi za Ulaya na sio Ulaya Mashariki. Mimi kwa mawazo yangu nilichokiona Stars sio kiwango cha mpira bali ni ukomavu wa kisaikolojia ambao Maximo amewajenga wachezaji. Sawa hilo ni kubwa lakini bila vibaji halisi na mbinu za kiuchezaji tutaishia hapa hapa kila siku. Inabidi tuwe agressive Watanzania kama tunataka maendeleo angalieni Wenzetu Waafrika Magharibi wanavyowatoa baruti makocha wao wakishindwa kazi. Basi nasi wakati umefika wa kuambiana ukweli kwani wakati wa kubebana umekwisha. Ni haya tu wajameni!

    ReplyDelete
  13. MAXIMO na msaidizi wake El-BASHIR
    wapewe muda wa kutosha kuendelea
    kukijenga kikosi cha "TAIFA STARS" kitakacholeta matokeo mazuri ya kimataifa.

    Tunavyo vipaji vya kuzaliwa nchini kinachotakiwa kucheza pamoja kwa maelewano,kiwango kama hicho kwa kawaida hupatikana katika mtazamo wa kupanga na kupangua.

    Mabadiliko ya walimu yataturudisha nyuma kimaendeleo kufuatana na kiwango tulichofikia sasa.

    mickey@mail-online.dk
    DENMARK

    ReplyDelete
  14. Kama Maximo akifunga virago vipi Profesa Victor Stancilescu akirithi mikoba?

    ReplyDelete
  15. MAXIMO HAONDOI TAYARI KAJIFANYA ANA PROGRAM YA MIAKA MITATU KAIANDAA ILI AWAPE TFF NA KOPI KWA JK.HUO NDIO MKWARA ANAOKUJA NAO.
    SWALI ALISEMA ANAKUJA KUJENGA MSINGI SASA ANANG'ANG'ANIA NINI?
    AONDOKE MARA MOJA.

    ReplyDelete
  16. Wadau wa soka,

    Maximo ametusaidia kwa kiwango chake. Pia mazingira aliyoyakuta wenzake wa nyuma wala hawakubahatika kuyapata. Tunakumbuka Mkwasa, Mshindo Msola, Kibadeni nk walivyokopwa hata posho ya kutunza familia zao wakiwa makocha Stars. Kambi ilikuwa inakopwa Jeshi la Wokovu. Ubora wa TFF umeweka mazingira ya kukuza soka. Ila ni muhimu wadau kujua kuwa Maximo hakuwa chaguo la TFF. Alichaguliwa na Kikwete (kama anavyochaguliwa mkuu wa wilaya) na hata TFF hawakujua katokea wapi?



    Kwa nini ni muhimu kuwa na kocha aliyechaguliwa na TFF?



    According to TFF, kocha waliyekuwa wanamhitaji ni atakayeendana na mikakati ya TFF ya kuinua kiwango cha soka Tanzania nzima (hapa ieleweke kuwa si Timu ya Taifa tu). Kama mnavyoshuhudia TFF inaleta mabadiliko mengi kwa kutumia sheria, kanuni na taratibu za kisoka incl. vilabu kuwa na timu za vijana na wanawake, Copa Coca cola, Taifa Cup, viongozi watendaji wa kuajiriwa na mikataba kwa wachezaji, TFF iwe institution (si ya mtu 1) nk. Lengo ni kuinua soka NCHI nzima. Sifa za kocha ambaye TFF walimhitaji ni pamoja na

    1. kufundisha soka,

    2. kufundisha makocha wa hapa kwetu na

    3. kuisaidia Tanzania kutekeleza mikakati yake ya muda mfupi, wa kati na mrefu kuendeleza soka.



    Hivyo, sifa za kocha waliyemtaka TFF ilikuwa awe pia ni MKUFUNZI (instructor) anayetambulika na FIFA.



    Nakumbuka TFF waliomba FIFA iwasaidie kutafuta kocha wa sifa hizo ili aje kujenga soka, kukuza na kulea vipaji vya vijana wetu. FIFA ilitoa ushirikiano na TFF waliongea na:

    a. kocha wa zamani wa Cameroon akawa very expensive. Pesa za kusaini mkataba tu (acha mshahara ilikuwa mara 2 ya mshahara wa Maximo kwa miaka 2).

    b. kocha wa Kongo DCR akawa anataka TFF isubiri hadi Juni amalize mkataba na Kongo wakati sisi tukikabiliwa na Africa/World Cup qualifiers July.



    Hapa alikuwa anatafutwa kocha mwenye uzoefu na mazingira ya Afrika ambaye kazi yake inakuwa kubwa (kufundisha timu, kusimamia kocha wa vijana, wanawake, kufundisha makocha wa vilabu, kutoa technical support kwa TFF ku-implement Strategy yake, etc). Bahati FIFA wakatuunganisha kwa Leal ambaye FIFA wanamkubali kwa hali ya kisoka ya Tanzania. Na kwenye mechi ya Community Shield kati ya Man U na Liverpool (kama sikosei), commentator alimwonesha akiwa jukwaani na kusema kabisa kuwa yuko kwenye mazungumzo na Tanzania. Ni kocha na mkufunzi wa muda mrefu anayetambuliwa na FIFA. Pia ni M-Brazili kama Maximo.



    Kufumba na kufumbua serikali ikaja na jina la Maximo na haikujulikana anatokea wapi {ingawa aliwahi kufundisha timu ya Livingstone (nirekebishwe km nimekosea) ya Scotland kwa muda}. TFF wakaduwaa na hawakuwa na cha kufanya. Kwa hiyo haya yanayotokea hatushangai kwani Maximo hana uzoefu na timu za taifa, si mkufunzi (hivyo suala la saikolojia ni doubtful) na hata kufundisha makocha wa ndani hajafanya. Hivyo, lengo la TFF bado liko mbali kufikiwa. Hizo zifa zinazotajwa tumshukuru lakini kwa kweli TFF walidhamiria kukuza soka kwa mapana yake. Tunachokiona ni kuchukua wachezaji Yanga (10), Simba (6), Mtibwa (3), na wawili watatu wa hapa na pale. Na kuwabadilisha kila siku.



    Nilisukumwa kutoa mada kutokana na inconsistency za Maximo (of course na "ufungwa" wa TFF). Kwa upande wa Maximo

    1. Alitamba CHAN Ivory Coast kuwa anajivunia kikosi chake kwani ni vijana tupu, average age ni 22 years (refer to www.cafonline.com). Leo kaja nyumbani kasema timu ina,anataka 70% vijana.

    2. Kila siku husema huchagua wachezaji kuzingatia rekodi yao ya NIDHAMU,nk. Sasa hao wooooote aliyewahi kuwachagua hakujua rekodi zao????????

    3. Kwa kipindi chote alichokuwa nao NIDHAMU imeshuka wiki moja ya kuwa Ivory Coast???

    4. Yeye kama mwalimu alifanya jitihada gani kuwaweka kwenye mstari????

    5. Je anatoa motisha gani kwa wachezaji wazoefu ili kuwajenga wale wadogo kisaikolojia? Au anawa-treat wale wakubwa sawa na wadogo? Yaani Ferguson am-treat van Der Sar,Rio Ferdinand,Giggs sawa na Luis Nani,Anderson,Welbeck????? Saikolojia inakuja hapo.

    6. Ana ushirikiano wa namna gani na makocha wa ndani??

    7. Hukaa na makocha wa vilabu anakotoa wachezaji kujua wachezaji anaodhamiria kuwachagua?

    8. Akiwaambia wanahabari kuhusu nidhamu mbaya za wachezaji, je huwa wazi ili hata wachezaji wengine (na wadau) wajue na kujifunza???



    Nafikiri jibu analo Maximo mwenyewe.



    Kwa upande wa TFF, wala wasirudi nyuma. Lengo libaki pale pale kuendeleza mpira wa Tanzania kwa ujumla...si Stars pekee. Hivyo TFF imwache Maximo amalize muda wake. Kikwete kawaambia TFF wajiandae kumlipa kocha wa Taifa,hatamlipa tena. Nafikiri wakati umefika wa kutafuta kocha mwenye sifa ziiiiiiiiiiiiile mlizozitaka (coach, Instructor na mwenye kulea wachezaji na mpira kwa ujumla). Yeye amalize muda wake lakini kwa sasa ni kumtafuta mrithi wake mapema na kutafuta wadhamini/mipango ya kumlipa. La sivyo, tutaendelea ku-implement hiyo Strategy nusu nusu.



    Ieleweke kuwa TFF ililazimika kumkubali Maximo kwa kuwa aliletwa na Kikwete. {Mnakumbuka Kikwete kwenye Press Conference aliwashutumu wazi wazi TFF kuwa yeye katoa ofa ya kumlipa kocha wa Stars na TFF wamelala tu. Of course, hii kauli iliwachoma TFF kwa kuwa walikuwa wanahangaika usiku na mchana kutafuta kwa kutumia msaada wa FIFA ila wengi walikuwa ghali mno kwa serikali kumudu kwani Tanzania si soka tu. Michezo mingine na uchumi vinadai. TFF walikuwa very considerate kwa wa-TZ}. Kwenye hili, kauli ya Kikwete ilitusononesha wadau tuliokuwa tunajua harakati za TFF.



    TFF iache tabia za kizamani. TFF inasema inamsubiri Maximo aseme chochote kile juu ya wachezaji wasio na NIDHAMU ili wachukue hatua. Yaani hata kama Maximo ndiye mwenye makosa? TFF wawaweke chini na kuyamaliza. TFF haifikirii hilo. Badala take wanasubiri Maximo aseme anataka TFF ifanye nini kwa watovu wa nidhamu. Nafikiri hii ni uzamani. Namna nzuri ya kuboresha management ya soka ni kuwa pro-active si reactive. Pia, hata bila ya Maximo kusema, itumike ripoti ya meneja wa Timu na TFF iwaite wachezaji wale waandike maelezo yao na kamati ya nidhamu iwahoji na wamsikilize Maximo na mwisho (mara nyingi mtoto ndiye mwenye kosa) uamuzi wa busara na wa kujenga utolewe.



    I stand to learn more from you all.



    Mdau mwenzenu



    Geoff I. Mwambe

    Mannheim

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...