Agnes Kitunga presses akibonyeza kitufe kumpata Mr. Khamis Abdallah Ramadhani
aliyekuwa mshindi wa mwezi huu wa Milioni 40 Tuzo Draw. Wanaoshuhudia ni Elihuruma Ngowi, Meneja Huduma na Bidhaa wa Vodacom (kushoto) na Abdallah Hemedi kutoka Bodi ya Michezo ya kubahatisha Tanzania.


MSHINDI WA MILIONI 40 WA MWEZI
HUU APATIKANA KWENYE DROO YA TUZO
Vodacom Tanzania imempata mshindi wa mwezi huu aliyejishindia shilingi Milioni 40 kwenye Droo ya Tuzo iliyochezeshwa leo hapa Dar es Salaam. Bw. Khamis Abdallah Ramadhan, fundi seremala na mkazi wa Buguruni DSM, ndiye aliyebahatika kunyakuwa kitita hicho. Akichezesha Tuzo Droo hiyo, Meneja Huduma na Bidhaa wa Vodacom, Bw. Elihuruma Ngowi amesema kuwa Tuzo Droo ni promosheni ya miezi 12 iliyozinduliwa rasmi mwezi Aprili mwaka 2008 kwa wateja zaidi ya milioni 4 kuwashukuru kwa mchango na uaminifu wao kwa Vodacom kwa kipindi chote cha miaka 8 Vodacom iliyoendesha shughuli za mawasiliano hapa nchini Tanzania.




Ukiwa na Tuzo Droo kutoka Vodacom Tanzania, kwa kila Tuzo Pointi MOJA mteja anayoipata, Vodacom inampatia NAFASI MOJA ya BURE ya kuingia kwenye bahati nasibu ya Tuzo Droo. Droo za wiki na mwezi zinamfanya mteja wa Vodacom aweze kubahatika kushinda zawadi za PESA TASLIMU au MUDA WA MAONGEZI.

KUMBUKA: Kumbuka zaidi ya Bilioni MOJA zinashindaniwa!!

Wateja wanawezaje kujikusanyia Nafasi zao za Tuzo Droo?
Kwa kila Tsh 100 (Bila Kodi - VAT & Excise) unayotumia kwenye mtandao wa Vodacom (Kuperuzi Internet, SMS, calls, MMS n.k.), unapata nafasi 1
Kwa kila dakika MOJA ya simu unayopokea kutoka kwenye mtandao wowote wa simu za Kitaifa, unapata nafasi 1
Kwa kila wiki MOJA unayoendelea kuunganishwa na mtandao wa Vodacom, unapata nafasi 1

KUMBUKA: Hakuna haja ya kujisajili.

Wateja wanawezaje kuangalia nafasi zao Tuzo Droo?
Kujua nafasi zako za Tuzo Droo, tuma SMS ya BURE isemayo au TUZO DROO au TUZO DRAW kwenda 123.

Ni lini Droo za Tuzo zinachezeshwa?
Droo za Kila Wiki
~ Washindi 100 wanapata Tsh 50,000 MUDA WA MAONGEZI KILA MMOJA!
~ Washindi 7 wanapata Tsh 1 MILIONI PESA TASLIMU KILA MMOJA!
· Droo za Kila Mwezi
~ Mshinidi 1 anapata Tsh 40 MILIONI PESA TASLIMU!

*Vigezo & Masharti kuzingatiwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. I always find it funny kwamba washindi na wasimamizi (Gaming Board) wa kamari aka bahati nasibu hizi mara nyingi huwa waislamu,

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...