Haya tena, leo ndio mwanzo wa mashindano ya kitaifa ya kikapu - NCAA Basketball Tournament (March Madness) - huko marekani na mdau Hasheem Thabeet anaelezwa kuwa ni mmoja katika wale watakaotupiwa sana macho kutokana na kupanda kwa kiwango chake na kuitangaza vyema nchi yake.Pichani ni ukurasa wa mbele wa gazeti maarufu la marekani la 'new york post' la leo ambapo hasheem katawala ukurasa karibu wote. pia unaweza kuangalia video yake katika linki hiyo hapo chini uone anavyofagiliwa. Yaani hadi inatia raha unaambiwa. 

Mungu Mbariki Hasheem
Mungu Ibariki Uconn
Mungu Ibariki Tanzania

http://www.dailymotion.com/video/x7
hpim_hasheem-thabeet-goes-home_sport

Also click
Hashim Thabiti akifanya vitu vyake.  http://nbcsports.msnbc.com/id/29126211/displaymode/1247/
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Wabongo bwana kwa kutia chumvi !! Mimi nimeliona hilo gazeti la New York Post na hiyo stori iko ukurasa wa mwisho kabisa na siyo mbele kama mdau aliyeleta hii habari anavyodai, matter fact tunaomba ufafanuzi zaidi maana huo ukurasa unaweza kuwa mbele kama hilo gazeti lingekuwa la kiarabu kama al haram lakini unfortunately ni la kiingereza so get your fact right brother.
    Good luck hasheem will be watching you young N’
    Mdau DC

    ReplyDelete
  2. mimi nina kaushauri ka bureee kwa "MR THE BEAT"kama wenyewe wanavyomwita pale UCONN ongeza ka mwaka kamoja tu hapo UCONN maanake NBA siyo ya kitoto,na wewe game lako kwa NBA kwa mtazamo wangu bado changa.

    ReplyDelete
  3. jamaa naona anaingia kwa spotlight sasa nimeaona habari yake ccn sports leo

    ReplyDelete
  4. kama mtu anaishi UK anaweza kumtizama Hasheem Kwenye Sentanta huwa Timu yake inaoneshwa sana mwenyezimungu amjalie mazuri na amuepushe mabaya, Vijana na watoto wapate kuiga mfano wake.

    Ushauri wangu kwa Hasheem.

    1. Chunga sana Madaktari utaopewa
    2. Unapokwenda Out na Wenzako chunga unavyokunywa

    3. Tizama Ya Kobe yanaweza kuwakuta wengi.

    kama kuna mengine wadau naomba mpeni ushauri kama anasoma utamsaidia.

    Inshallah mwenyezimungu atazidi kukufungulia Amin. Mdau Pazi.

    ReplyDelete
  5. Hasheem anatisha..Huu ndo mwaka wake wa kuingia NBA ingwa baadhi ya wameraki wanasema ataliwa 'alive' maana hajakomaa kihivyo ila mi naamini anaweza..Dolla milioni 2 mpaka 4 si mchezo kwa kijana huyu ambae sidhani kama aliwahi kuota ndoto hii..Kila la keri brother..'We will be watching'
    Tunakupenda..
    Cheupe

    ReplyDelete
  6. Hasheem leo kaibuka na pointi ishirini na ribaundi 16 dhidi ya Chatanuga. Shughuli ndio inaanza lakini na wamecheza na heavy underdog. Kila la heri mechi zijazo, endelea kuiweka Tz kwenye ramani ya dunia.
    Naungana na mdau anayeshauri umalizie mwaka wako wa mwisho hapo UConn. Jim Calhoun ni miongoni mwa makocha bora wa kikapu atakuandaa vizuri kukabiliana na watemi wa kinyemela wa NBA. NBA wachezaji kibao wanazo za yule fala wa Pitt. Ukizidiwa mara mbili tatu basi ESPN watakutukania mpaka mama yako. Malizia mwaka uongeze msuli na uwezo wa kupachika vikapu ili ukiingia NBA watu wasikufananishe tu na Dikembe Mutombo bali wakuone kama hybrid ya wachezaji bora wote wanaowafahamu...difensi kama Mutombo, midanki kama Shaq enzi zake, mihook kama Kareem Abdul Jabar na kucheza na bodi kama Tim Duncan.
    Naamini nawasemea wabongo wote nikisema tunakutakia kila la heri na mafanikio.

    ReplyDelete
  7. WABONGO BWANA TABU TUPU,JAMAA ANAJUA ANACHO FANYA NDIO MAHANA YUPO HAPO .WASHAURINI WATOTO WENU NA NYIE WENYEWE KUACHA POMBE.

    ReplyDelete
  8. naishi n,y nikweli yuko jarida la mwisho kwenye new york post make ndio jalida la michezo kiukweli ka fagiliwa vilivyo mwaka huu naomba kwa ushauli wangu mdogo dogo ka shule mwaka mwingine mmoja NBA ni ngumu mshikaji benchi inaweza ika kuchania bukta zako zote waone wenzako kina KG ata kina kobe game lao lilikua kubwa lakini mwaka mzima walikaa benchi za nguvu ongeza mwaka dogo

    ReplyDelete
  9. Iwe mbele au nyuma kwa mtu anayejua advertising zote mbili ni prime spots, what ever it is ni kijana mzuri na akipata washauri wazuri atafika mbali sana. Vilevile akumbuke hadithi ya "sifa zilimuua mjaluo" asije akalewa sifa akawa hashauriki

    ReplyDelete
  10. Kwa wanao fatilia!!!

    Connecticut Surpasses Chattanooga 103-47 in First Round of NCAA Tournament

    http://www.uconnhuskies.com/AllStories/MBasketball/2009/03/19/20090319a.html

    ReplyDelete
  11. Jamani mambo bado kabisa, starehe ndio kwanza imeanza... Kama wewe ni mpenzi wa March Madness basi utakubaliana kabisa na mimi kwamba mambo ndio yanaanza.... Jumamosi Uconn anapiga na Texas A&M akimchapa A&M anakutana na Mephins ambao nadhani wengi tunawajua kwamba wana kiwango na experience kubwa... Na akimchampa Mephins then kuna Lousiville hapo ndio kwenye balaa...

    Bado chati yangu inaonyesha Bingwa ni Pitts.... Jumamosi Texas and Duke good game kuangalia maana A.J Abraham leo kanipa starehe.

    Mchumi wa Texas

    ReplyDelete
  12. ""Tarehe March 19, 2009 6:56 PM, Mtoa Maoni: Anonymous Dmoney

    Wabongo bwana kwa kutia chumvi !! Mimi nimeliona hilo gazeti la New York Post na hiyo stori iko ukurasa wa mwisho kabisa na siyo mbele kama mdau aliyeleta hii habari anavyodai, matter fact tunaomba ufafanuzi zaidi maana huo ukurasa unaweza kuwa mbele kama hilo gazeti lingekuwa la kiarabu kama al haram lakini unfortunately ni la kiingereza so get your fact right brother.
    Good luck hasheem will be watching you young N’
    Mdau DC""


    NANI KWA KUAMBIA IMEANDIKWA UKURASA WA KWANZA! UMEAMBIWA HABARI IMECHUKUA PAGE NZIMA. ACHA HIZO WEWE.

    ReplyDelete
  13. anon 8:24

    'Achunge madaktari, chakula, vinywaji'

    We unafikiri yuko bongo huyo, unahofu atalogwa?

    Acha mentallity za kishamba, tuendelee hata kimawazo basi na tuache kufikiria upuuzi.

    ReplyDelete
  14. wewe mdau hapo juu unaeponda kuhusu ushauri kwa Hasheem kuhusu kuchunga vyakula anavyokula, madaktari atakaopewa na vinywaji anatakavyokunywa, hiyo sio issue ya kurogwa ujue wenzetu wanaweza kumuwekea slow poison. wewe bado kichwa chako kinawaza wanga tu, lol! kuna mambo ya kuwekewa sumu.
    Huyu mchangiaji aliyetoa ushauri huo ni muelewa na anajua anachokisema.

    baby.

    ReplyDelete
  15. Kijana tunakukubali. Endelea kupeperusha bendera ya Tanzania

    ReplyDelete
  16. hakuna aliyesema maswala ya kulogwa au wanga kwenye ushauri zaidi ya nyie mie nimetowa ushauri tu sasa hayo ya mawazo mengine ni nyie poleni lakini.

    ReplyDelete
  17. Baby,

    Let me clarify.
    He's playing for THEM!, right? why should they do that. Hata kama ni slow poison, they get physical check up every now and then, even those doctors are smart enough and know BETTER not do something like that, if they do, in the next 10,20, years watajajulikana tu. It's not Bongo. Mnanishangaza!

    ReplyDelete
  18. Eti Slow poison.
    Hawajawawekea slow poison waafrika wengine waliowahi kucheza basketball(college or NBA) waje wamwekee THABITI?
    Thabiti ana nini cha ajabu kuliko kina MUTOMBO,IGOUDALA nk, kitakachowafanya watu wamfanyie upumbavu?
    Kama hatoweza kuwika katika huu mchezo itakuwa due to himself wala si kwa madaktari,makocha au wapishi.Marekani ya sasa si kama marekani ya 1920.Acheni fikra zenu za kiswahili bana.

    ReplyDelete
  19. Huyo mbeba boksi aliyemponda yule mdau aliyetoa ushauri wa Hashim kuwa mwangalifu kwenye vyakula na vinywaji ana mawazo "mgando".Yaani yeye anafikiri kuwa huko ughaibuni ndo hakuna mambo hayo badala yake anatuletea mambo ya uchawi hapa.Pumbavu!!

    Huyu jamaa kama sio mtoto basi atakuwa hajasikia na wala hajui mambo yalivyo(mshamba).Eti uchawi,WTF?.Uliza uambiwe,Unajua athletics BEN JONSON kilimtuta nini mwaka 1986?Mume wa Jones je?Yeye mwenyewe Jones?na walio wengi wakigundulika huwa wanadai kwamba ni vinywaji ambavyo wamekunywa vinakuwa vimewekwa hiyo kitu intentionally.Pumbavu kama wewe mnaobeba boksi bora muendelee kukaa hukohuko ili mpate akili.

    Michuzi kaka,usiache ku-upload hii.

    Mkulima-kijijini Gezaulole.

    ReplyDelete
  20. anon wa mwisho.

    We ndo unashangaza kabisaaaaa!

    Wakina Jones waliweka wenyewe hawakuwekewa na yeyotee.

    Sio Bongo ya kufanyiana ubaya kama mlivozoea ndo maana hata akili zenu zimekaa ki hivo tu, kufikiria utafanyiwa ubaya all the time.

    Nyie ndo mnafikiria ubaya na kutokupenda maendeleo ya wenzenu.

    Amkeni kifikra!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...