
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar, Profesa Adedeji amemweleza Rais Kikwete kuhusu hatua zilizofikiwa katika mchakato huo unaoelekea kukamilishwa katika Tanzania.
Profesa Adedeji amemwomba Rais Kikwete kuendelea kuunga mkono jitihada za kukamilisha mchakato wa kuundwa kwa Baraza la Utawala la Taifa (NGC) katika Tanzania.Pia Profesa Adedeji amemshukuru Rais Kikwete kwa kuliunga mkono baraza hilo kifedha na kumwomba aendelee kufanya hivyo.
Rais Kikwete ameuambia ujumbe huo wa watu 27 kuwa angependa kuona mchakato huo unakamilishwa katika Tanzania, ili nchi iweze kufanyiwa tathmini yake ya kwanza Januari, mwakani, 2010.Pia Rais Kikwete ameahidi kusaidia kuongeza uhalali wa NGC, na pia kuangalia jinsi gani mchakato mzima unavyoweza kusaidia haraka zaidi kifedha.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
afadhali tuwe na chombo chetu sie watawala(executives,admins,directors,managers etc)
ReplyDeletesie wenye "TAALUMA" hii apa ndo tunaofanya sehemu yoyote ile iende,sio wale wadandiaji!!
pitisha JK
Kidogo niseme Emmanuel kaja bongo kufanya nini wakati ligi haijaisha.
ReplyDeleteJamani msaada kwenye tuta. Mimi sielewi wala hainipi maana kwanini TZ hatuungi mkono kukamatwa kwa raisi wa Sudani Omar al - Bashir na mahama ya kimataifa? Sipati maana kabisa maana huyu jamaa ni muuaji kabisa anafaa hata kukatwa kichwa chake kikatwe kabisa, sasa TZ wanapasema itakwamisha suala la amani sielewi. Amani itakujaje wakati yeye haonyeshi ushirikiano hata na international peace keepers.Sioni ni kwanini tuaungana na china, mchina anaona raha sababu anafanya biashara, anuza silaha zake. Siimpendi mchina hata kidogo. Naomba kuelimishwa zaidi juu ya msimamo wa TZ.
ReplyDeletesio Abedayo na wewe!!!!!! ni ADEBAYO
ReplyDelete