JK amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Mfumo wa Kujitathmini Wenyewe katika Masuala ya Utawala Bora katika Afrika (APRM), ukiongozwa na mjumbe wa Jopo la Watu Maarufu wa Mfumo huo, Profesa Abedayo Adedeji.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar, Profesa Adedeji amemweleza Rais Kikwete kuhusu hatua zilizofikiwa katika mchakato huo unaoelekea kukamilishwa katika Tanzania.
Profesa Adedeji amemwomba Rais Kikwete kuendelea kuunga mkono jitihada za kukamilisha mchakato wa kuundwa kwa Baraza la Utawala la Taifa (NGC) katika Tanzania.Pia Profesa Adedeji amemshukuru Rais Kikwete kwa kuliunga mkono baraza hilo kifedha na kumwomba aendelee kufanya hivyo.
Rais Kikwete ameuambia ujumbe huo wa watu 27 kuwa angependa kuona mchakato huo unakamilishwa katika Tanzania, ili nchi iweze kufanyiwa tathmini yake ya kwanza Januari, mwakani, 2010.Pia Rais Kikwete ameahidi kusaidia kuongeza uhalali wa NGC, na pia kuangalia jinsi gani mchakato mzima unavyoweza kusaidia haraka zaidi kifedha.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. afadhali tuwe na chombo chetu sie watawala(executives,admins,directors,managers etc)
    sie wenye "TAALUMA" hii apa ndo tunaofanya sehemu yoyote ile iende,sio wale wadandiaji!!

    pitisha JK

    ReplyDelete
  2. Kidogo niseme Emmanuel kaja bongo kufanya nini wakati ligi haijaisha.

    ReplyDelete
  3. Jamani msaada kwenye tuta. Mimi sielewi wala hainipi maana kwanini TZ hatuungi mkono kukamatwa kwa raisi wa Sudani Omar al - Bashir na mahama ya kimataifa? Sipati maana kabisa maana huyu jamaa ni muuaji kabisa anafaa hata kukatwa kichwa chake kikatwe kabisa, sasa TZ wanapasema itakwamisha suala la amani sielewi. Amani itakujaje wakati yeye haonyeshi ushirikiano hata na international peace keepers.Sioni ni kwanini tuaungana na china, mchina anaona raha sababu anafanya biashara, anuza silaha zake. Siimpendi mchina hata kidogo. Naomba kuelimishwa zaidi juu ya msimamo wa TZ.

    ReplyDelete
  4. sio Abedayo na wewe!!!!!! ni ADEBAYO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...