JK akiongea na Bw. Aaron Regent Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick Gold corporation leo ikulu, dar. Kulia ni Meneja Mkuu Mtendaji wa Barrick Gold Tanzania Bw. Deo Mwanyika na wa pili shoto ni BW. Kelvin Dushnisky, Makamu wa rais wa Barrick' Gold Corporation.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Enzi za Mzee Ruksa Ikulu walikuwa wanaenda wadosi. Sasa hivi tumeendelea wanaenda wazungu. Nikitaka mweusi mbongo kwenda Ikulu inakuwa mtafutano.

    ReplyDelete
  2. Naomba kujua nasikia share za barrick zinauzwa sana UK bila wabongo wenye uwezo kujua na kununua

    ReplyDelete
  3. Shea za Barrick zinauzwa Toronto na New York kwa tiketi ya ABX. Nadhani sheria ya nchi yetu inayozuia kuwa na pesa za kigeni ughaibuni inaweza kuzuia usiweze kuzinunua kwa mujibu wa sheria lakini masoko hayo hayana noma. We pitia tu kwa dalali na hela yako jamaa wanakuuzia share kama njugu.

    ReplyDelete
  4. hao jamaa huwa hawaruhusu wabongo kununua hisa zao nchini tanzania. hisa zao huuziwa watu wanaoishi nchi za west. hii yote imeletwa na uzembe wetu. waheshimiwa wetu wanajali nini wakati wao wanazinunua hizo hisa nje ya nchi.

    ReplyDelete
  5. Commenting on comment posted at 9:19pm - Perhaps wadosi were allowed to go to Ikulu during mzee ruksa but at least these wadosis were born and raised in Tanzania - now Tanzania is replacing wadosi with wazungu and chinese...and still wazawas are left behind...why?

    ReplyDelete
  6. ni wezi tu hao, wanatuachia mashimo tu.

    ReplyDelete
  7. i dont get it at all!!
    anyway,lets see JK

    ReplyDelete
  8. naskia jamaa hawa migodini,wanataka kufunga na wengine weshaanza na staff wamepunguzwa kinoma!!

    mtikisiko wa uchumi duniani
    ni kweli???

    staff zaidi ya 200 instantly hawako kazini/wameachishwa/wameacha??

    ReplyDelete
  9. Naomba wadau mnaojua suala la Barrick shares nje ya nchi muandike wadau tujue na tuchangie inaweza kufungua macho wengi

    ReplyDelete
  10. Welcome to Tanzania Barrick Gold Corporation President and CEO Aaron Regent. Huyu Rais wa Barrick ni mara yake ya kwanza kutembelea Barrick Africa. Ameanza kazi hivi juzi tu na miezi miwili bado hajamaliza. Amechukua nafasi ya Rais wa Barrick wa zamani Gregory Wilkins aliyestaafu hivi karibuni. Najivunia kuwa mwana Barrick. As usual our Barrick Safety Vision is
    " EVERY PERSON GOING HOME SAFE AND HEALTHY EVERY".

    ReplyDelete
  11. Hiyo barrick inabana ajira Tanzania.Wamekamata migodi minne Tanzania(BUZWAGI,NORTH MARA,TULAWAKA,NA BULYANHULU(BULLY).Ukitimuliwa kazi Buzwagi migodi mingine huwezi ku-apply unaambiwa Bariick ni moja!!!Unabakiza Geita gold(GGM).Sounds awkward??
    Suala la shares inabidi serikali iingilie kati.

    ReplyDelete
  12. ''Reading Between the Lines"

    Huyo annon wa kwanza anaweza akanieleza kwanini kawachangua maraisi wawili kati ya wanne wa tanzania?

    Let me guess by finding the similarity of the two. OOH they are both from coast region and unfortunately Muslims. wait a minute.......!!!!!

    please balance your comment by telling us the dear guests of the first and third president of this republic or you have just left it of us to gues.

    ReplyDelete
  13. "Naomba wadau mnaojua suala la Barrick shares nje ya nchi muandike wadau tujue na tuchangie inaweza kufungua macho wengi"

    Ambao wangeweza kuwafungua macho waliachishwa. Waliobaki wote ni mbumbumbu katika masuala ya finance

    ReplyDelete
  14. Usishangae kuona jamaa wa Barrick ikulu yetu. George bush alikaa TZ siku nne kwa sababu ya business zake binafsi tu(eti analeta misaada! Kwa nini tupokee msaalda wa milioni moja wakati madini yanaweza yakatuletea bilioni?), yeye na baba yake wanashiriki katika hii kampuni. Research online utaona. Barrick imehusika na mauaji ya watu wakati wakilinda maslahi yao. My hope ni kwamba rais mpya, Obama hata deal na marais corrupt wa Africa. asimamishe misaada(inatuletea rushwa tu) na kuruhusu fair trade!

    ReplyDelete
  15. Kila muwekezakaji anakaribishwa ikulu na wawekezaji wote ni sawa. Mi nataka kuja kuvua dagaa na kambale. Je nnakaribishwa ikulu?
    ameenda ikulu kufanya nini na kuzungumzia nini ?
    hayo ndio tunatakiwa kufahamishwa. Kuona watu wanachekeana tu na kuandika utumbo sio good news kwa watu walio makini na uchumi na biashara na nchi yao. Tunataka kujua mkutano wao na rais ulihusu nini? more favor?more ass kissing?

    ReplyDelete
  16. Anony wa kwanza nakusifu kwa summary yako.Umemamliza kila kitu.

    ReplyDelete
  17. Michuzi: Tundika, usibane! Hii ni mara ya pili kuandika.

    Katika sheria za madini na gesi kunakitu cha "production sharing agreement". Mwekezaji anakubaliwa kushirikiana na mwingine na kugawana shares. Serikali ni lazima ikubali psa hiyo na kutia sahihi.

    Barrick imekuwishapatana na wawekezaji wengine lukuku. Hata ya Buzwangi, nadhani, ni moja ya psa hizo. Na ndiosababu Karamag, pengine, alikimbia huko Ulaya na kutia saini hotelini, kuridhia kwa upande wa serikali.

    Cha kushangaza ni kwamba psa hizo hazipewi wazawa! Na kama zina wazawa ni wale tu waliomo katika serikali au chama tawala wenye kununua shares na hatuwajui!

    Hawa ndio CIT (Choma Iangamie Tanzania)!

    ReplyDelete
  18. Barrick shares trade under ABX ticker symbol, in New york stock exchange and Paris Bourse etc, also they are an equal employers, the largest mine has a union that represent miners, there is no redundancy of the 200 workers, na as rule of a thumb ukiharibu mgodi mmoja you cant just cross over to the rest of the mines, but if you resign on your own accord, you are welcome in any of their mines worldwide
    I have worked for barrick for 7 years and my current position ( somewhere else ) is a result of my dedication and hard work for them
    Barrick is regulated and applies SOX ( Sarbanes Oxley Act ) because it trades in USA, there is no foul play and if you have no facts, dont just speak or write out of blue, all cases and everything is openly and transparently explained in their quarterly reports that are not hidden.
    Some Tanzanians have shares in the company by the virtue of their position which they can claim when tehir employment conclude or continue with them... but shares trade where tanzanians can buy, currently the shares ziko juu because they are number one gold producers in the world.

    ReplyDelete
  19. Hi,
    I am quoting the comments of David Villa who says if you are terminated from one Barrick Site, you cannot get job in the other site, thats very true , Sikiliza David, mimi nafanya kazi kwenye mgodi wa Barrick kama Mine Safety & Training Officer (Afisa Usalama na Mafunzo wa Mgodi". Kazi zangu ni za kiusalama kama vile to make sure that people are not working under the influence of alcohol, they are not over speeding, wearing all Personal Protective Equipment, to test alcohol and drugs etc.. Sasa David nikikupima nikakukuta na mipombe huku unafanya kazi hiyo haina mjadala ni termination. Utakuwa terminated ikiwa umekutwa na alcohol zaidi ya 0.05 lakini chini ya hapo utapewa final written warning, na kwa taarifa yako hii ni Policy ya Barrick dunia nzima...kwahiyo mimi siwezi kukukuta na pombe au madawa ya kulevya tukufukuze kazi then uende Barrick Lagunas huko South America au Barrick Sedibelo Johannesburg ukaombe kazi, Barrick Gold Corporation tuna policy moja ya kilevi sawa?? Ukitimuliwa kwisha sawa mkuu?? Kwahiyo fuata sheria na kanuni usifukuzwe. Kwa taarifa tu ni kwamba Barrick is the biggest gold mining company in Tanzania and the world as a whole. Hapa Bongo tunamiliki migodi na Projects zifuatazo, Bulyanhulu Gold Mine, Tulawaka Gold Mine, North Mara Gold Mine, Buzwagi Project, Kabanga Nickel Project tunaendelea kufanya exploration tupate migodi mingine. Pia tunaongoza kwa kutoa ajira kwa wazalendo, kwa mfano tuna wafanyazi karibia 5,000 wa Tanzania hapa Bongo. Unaona sasa?? Na sasa hivi tuna mpango kwamba ndani ya miaka miwili ijayo nafasi zote za juu zitakua za wabongo, hadi sasa tuna ma meneja, ma superintendants wa bongo sio wa zungu tena, sawa David Fila?? Kwahiyo sisi Barrick ni kampuni bora na ya kuigwa!! Wengine mlisema ohh wanaiba mchanga wanapeleka nje, sio kweli, unajua gram moja ya dhahabu ni mchanga tani ngapi? kwa taarifa yenu gram moja ya dhahabu ni sawa na tani 12 za mchanga, kwahiyo wataiba tani ngapi za mchanga ili wapate hata gram 1000 za dhahabu??Mchanga wanaochukua ni ule wenye mchanganyiko na copper, hapa Bongo hatuna kiwanda cha ku process copper, sawa?? kuweni na mawazo au ulizeni kwanza kabla ya kuandika hovyo, hii blog inaheshimika sio kuleta mambo ya ze utamu hapa...
    mupozile@yahoo.com

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...