JK na Mama Salma kikwete wakipokewa mchana huu katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar mara baada ya kurejea toka London ambako JK alihudhuria mkutano katika mkutano wa awali wa  majadiliano wa G-20 ambao alikuwa amealikwa pamoja na viongozi kadhaa wa Afrika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Msaada tutani maana globuni panafundisha. Kwa nini kila rais akirejea kutoka nje ya nchi lazima akapokelewe na kiongozi mkuu mwingine uwanja wa ndege?

    ReplyDelete
  2. hawa jamaa wote wana matege fulani hivi, lakini inaonyesha MP angecheza soka angekuwa mkali kuliko JK.Au mnasemaje? Acheni hizo toeni jibu....

    ReplyDelete
  3. Hivi viongozi wetu hawana cha kufanya mpaka kila raisi anaposafiri wanamsindikiza na kumpokea? Kwanini tunapoteza muda na mambo ambayo hayana msingi. Unataka kuniambia kuwa lazima Waziri Mkuu au Makamu wa Rais lazima awe Airport kumpokea Rais wetu? Mbona nchi nyingi maraisi wao wanasafiri na wakirudi siyo big deal hapa mnataka kufanya kuwa mtu akisafiri kwenda nje akirudi ni mgeni maalumu? Hebu acheni kutumia rasilimali za nchi vibaya.

    ReplyDelete
  4. Mkwele huyu hata sijui anayemchagulia nguo anafanya kazi gani?!jamani hii kachumbali ni ya mapapai,matango,maembe,maparachichi.Me mkwere mwenzio lakini najua kujipangilia.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa March 19, 2009 8:55 PM umeona mbali. Pinda amekaakaa kucheza kwenye wing na kumimina mikrosi. JK angekuwa kama Mwaikimba.

    ReplyDelete
  6. Wadrobe Manager wake ndio yule yule wa fulanzz za Mkuu wa walaya ya Tegeta, usijali maana bei poa. Kajafikia bado viwango vya akina Mustafa Hassanali

    ReplyDelete
  7. hiyo inaitwa chuzi mix au supu ya bamia na kisamvu

    ReplyDelete
  8. Hata mimi ninajiuliza jambo hilo hilo yani lazima Rais apokewe na PM? ni kwa sababu za heshima /protokali au ndo njia nzuri ya kupeana briefing za haraka haraka?
    kuhusu pamba za JK nafikiri kakosea kidogo tu kuvaa tai ya bluu otherwise mbona kapendeza? kilasiku kuvaa suti inaboa kwa mvaaji na hadhira.
    Koku

    ReplyDelete
  9. Unacheki wapambe walivyojipanga aisee!

    Kati ya wote namfagili Mama JK kwa sana. Ni mfano mzuri kwa kina mama.

    A Wife must be the Husband's head cheer leader and his Number One die-hard Fan.

    ReplyDelete
  10. Mambo ya Protokali hayoo!!!!!! Nemburis

    ReplyDelete
  11. jk kwa sanaa bwana ..wameandika hapo akipokewa kutoka uk yeye na mkewe...wakati kila mtu anajuwa kuwa jk alikuwa uk hapa single...akila na yuele muimbaji wa BOT.....

    Mama alikuwa tanzania anaendelea na ziara zisizokuwa na kichwa waala miguuuu.....

    ReplyDelete
  12. kulikuwa kunaulazima gani wa first lady kwenda airport,maana ana onekana kama anakwenda sokoni hivi,huyu mama uswahiri umemzidi sana inabidi apate darasa maana kuvaa kumemshindwa.afate mfano wa mama mkapa bwana na mfagilia sana alikuwa first lady haswa mambo yake kizungu kizungu tu.

    ReplyDelete
  13. anony hapo juu umepatia mkuu wa kaya kakosea mavazi hata sarawili ya kahawia ingekuwa afadhali.

    ReplyDelete
  14. We anon uliyesema mama jk uswahili umemjaa hajui kuvaa, ni chuki zako tu, mama anapendeza sana na mavazi yake anajuwa kuwakilisha nchi yake haswa...toeni credits pale ambapo panafaa, kama mmetumwa tafuteni vigenge mfikishe ujumbe, mama anajituma mama presentable, usituletee mambo ya western wakati sisi ni wabantu, hakuna wa kuku support. Shame on you.

    ReplyDelete
  15. bongo watu hawana kazi!!Ndio maana hatuendelei!!

    ReplyDelete
  16. kweli bana suti kila siku inaboa! kusafiri na suti pia haipendezi! kuhusu mama yetu kwa kweli hilo vazi ni la heshima lakini sio la hadhi yake halinogi kwenye pozi laki first lady inabidi awe smart sio cultural

    ReplyDelete
  17. WANA-COPY CUT, HII ILIKUWA EZI ZA MWALIMU BASI WAO WANAENDELEZA TU, HATA KAMA WAKATI UMEBADILIKA NA KUPITA, WANAOOGOPA WASIPOENDA KUMPOKEA BASI UGALI UNAWEZA KUMWAGIKA, LAKINI NI KITU YA KIZAMANI SANA. ILA KAMA MKUU MGENI ANAKWENDA NCHI FULANI AKIPOKEWA NI SAWA KAMA VILE SISI TUNAVYOPOKEA WAGENI WETU STAND YA BUS, AU KAMA ANAEND NEWALA NI VIZURI MKUU WA WILAYA KUMPOEA KWA VILE MGENI WAKE, LAKINI SI SAHIHI KUPOKEWA ANAPORUDI NYUMBANI KWAKE ZAIDI YA DEREVA WAKE NA WANA USALAMA.

    ReplyDelete
  18. Vazi la JK liko poa na anakwenda na wakati! Ila huu utaratibu wa kupokelewa na kiongozi mwenzake kama PM au VP kila anapotoka nje ya nchi umepitwa na wakati na pia ni gharama.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...