Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. CHIBILITI ATATULETEA UMEME,TUSUBULI TU

    ReplyDelete
  2. Michuzi,
    Mi napenda kutoa dukuduku langu linalonikera sana na jinsi Watani wa Jadi(Kenya) wanavyojitangaza na MLIMA KILIMANJARO licha ya kwamba hawana haki ya kufanya hivyo.

    Siwezi kuwalaumu Wakenya wakati Wizara ya Utalii nchini inashindwa kuutangaza Mlima Kilimanjaro na kuonekana kama upo ndani ya Tanzania.

    Nasema hivyo kwa sababu kuna taarifa karibu mwezi mzima sasa imekuwa ikitolewa na vyombo mbalimbali vya habari ulimwenguni na hasa Uingereza kwamba kuna watu mashuhuri wanaenda kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia watoto masikini(RED NOSE).

    Moja kati ya taraifa hiyo imeandikwa kwenye mtandao wa YAHOO ikisema STARS SET OFF FOR KILIMANJARO CLIMB; Tena bila kuataja mlima huo kama upo Tanzania!

    Kati ya nyota hao yup mke wa beki wa kushoto wa CHELSEA na ENGLAND ASHLEY COLE, CHERYL COLE na mwenzake KIMBERLY WALSH na mwanamuziki nyota wa TAKE THAT, GARY BARLOW.

    Pia yupo Dj maarufu wa Radio 1, Chris Moyles, mwimbaji maarufu Ronan Keating na wengineo.

    Nyota hao waliondoka UK kwa ndege maalum ya shirika la ndege la KENYA(Kenya AIRWAYS)na ikiwa imepakwa rangi nyekundu kwenye pua yake kuambatana na sherehe hizo za kuchangisha fedha za kusaidia masikini. Walitua Nairobi kabla ya kwenda kupanda mlima Kilimanjaro Arusha Tanzania.

    Kwa kutumia Kilimanjaro na kujitokeza kuchangia sherehe hizo za Red Nose, celebrity hao hivi sasa wameshangisha zaidi ya paundi milioni moja katika kipi cha wiki moja tu kwa kudhaminiwa na wachangiaji.

    Hii inaonyesha ni jinsi gani wachangiaji walivyovutiwa na ujaisiri wa celebrity na jitihada zao kuhakikisha wanatimiza azma yao ya kupanda mlima Kilimanjaro ili kuchangisha fedha za kusaidia masikini.

    Ingawa habari zao zinatolewa kila siku kwenye vyombo vya habari huko Uk na mitandao mbalimbali ikiwemo Yahoo,MSN na mengine, lakini neno Tanzania limekuwa likitajwa kwa tabu sana licha ya kwamba wasomaji wa habari hizo walipaswa kuafahamishwa watu hao wapo nchi gani au Kilimanjaro ipo nchi gani huko Afrika.

    Na hata hivyo,sijui kama vyombo vya habari au mapaparazi wa bongo wanatumia nafasi hiyo kupata picha ambazo zingesaidia sana kutangaza Kilimanjaro hivi sana na siku zijazo.

    I wish waandishi au wahariri wa magazeti yetu wangejua umuhimu wa wa watu hao na hata kupata nafasi ya kuwahoji ili kupata maoni yao na kujua kama kweli walikuwa na taarifa zozote kwamba Kilimanjaro ipo ndani ya Tanzania!

    SWALI LANGU NI HAYA:-

    Hivi serikali yetu haikuwa na taarifa za ujio wa nyota hao wakashindwa kuandaa utaratibu ambao ungesaidia kuitangaza nchi kwa kupitia mlima Kilimanjaro?

    Je hakuna ndege itakayo Uk-Amsterdam-na kutua Kilimanjaro (KLM) ambako safari yao ingekuwa fupi zaidi badala ya kupitia nchi jirani ya Kenya?

    Mbona Uganda ambayo ipo karibu na Tanzania, haitumii ujanja kama watumiao Wakenya wa kuitangaza nchi kwa kutumia Mlima Kilimanjaro?

    Yapo maswali mengi kuhusu Kenya kuitangaza nchi yao kwa kutumia jina la Kilimanjaro kama vile upo ndani ya Kenya wakati hawana chembe ya ardhi zaidi ya kuuona kwa mbali tena mpakani?

    Viongozi gani wasiojua hata haki miliki ya mali za nchi yao. Hivi Wakenya wangefurahi kusikia Tanzania inajitangaza kwa kupitia moja ya rasilimali zao?

    Ubalozi wa Tanzania UK kwa kushirikiana na Mali Asili walitumia zaidi ya £50,000 kutangaza biahsara ya utalii ya Tanzania kwenye mabasi, taxi na vituo vya mabasi UK. Je matangazao hayo hayakusaidia kuwafungua wageni na kujua Kilimanjaro ipo Tanzania?

    Kama KILIMANJARO haupo Tanzania, bora serikali ikatangaza rasmi na kuweka jambo hili wazi badala ya kuwaachia watu wasio na haki miliki ya kitu fulani, kutumia jina la kitu au nchi fulani kujipatia fedha isivyo halali.

    Wote tunafahamu maana ya haki miliki. COKE hawawezi kutengeza soda yao kwa kutumia INGREDIENTS za PEPSI kwani kwa kufanya hivyo wanajua kitim kitim chake. Vipi Wakenya wajitangaze kwa kutumia mali ya nchi jirani bila kushutumiwa?

    Mengi ninayo naweza kujaza BLOG yako kuhusu Wakenya na MLIMA KILIMANJARO. Nina imani wapo watakaounga mkono na kuwaamsha viongozi wenye BONGOLALA.

    MDAU, MACAU

    ReplyDelete
  3. HAPA TUJADILI UMEME KWANZA NDIYO MADA YA KIPANYA,MIMI BINAFSI NAMSHANGAA MD WA TANESCO,YEYE ANAJUA KUWA DOWANS WAMESHAISHITAKI SERIKALI KWENYE BARAZA LA USULUHISHI LA KIMATAIFA,PARIS LEO TENA UNATAKA KUILAZIMISHA SERIKALI INUNUE MITAMBO ILIYOTUMIKA,KWA NINI KAMA ALIJUA INATAKIWA KUANDALIWA MAADNDALIZI YA KUNUNUA MITAMBO MINGINE HAWAKUJIANDAA???? NI JAMBO LA KUSIKITISHA SANA TANZANIA SIJUI TUNAENDA WAPI???? NAMSHANGAA ZITO KUSHABIKIA KUNUNUA MITAMBO ILIYOTUMIKA.LAKINI UKWELI NI HUUU MIMI NINAVYOJUA MITAMBO HII NI AKINA ROSTAM NA KAMA MNAVYOJUA ROSTAM AZIZ NI SHAREHOLDER WA VODACOM NA WAZIRI WA NISHATI WA SASA NGEREJA KABLA YA KUWA WAZIRI ALIKUWA MWANASHERIA (COMPANY SECRETARY) WA VODACOM,NDIYO MAANA UNATEGEMEA NINI????? ACHA NCHI IWE GIZANI KAMA MLIJUA HILO KWA NINI??? HAIKUANDALIWA MITAMBO MINGINE.MD WA TANESCO AMECHEMSHA HII NDIYO MAMBO YA KULINDANA KUMCHAGUA FULANI HUYU HAKUFAA KABISA KUWA MD-WA TANESCO

    ReplyDelete
  4. Nilisikia sikia kuwa ubalozi wa Tanzania nchini uingereza (kusaidiana na wizara husika ya tanzania-utalii.....) kama wakisema wamejaribu kujitangaza kwa kuweka matangazo kwenye mabasi ya nchini humo kuhusu mlima kilimanjaro, na mengineyo ya utalii wa kitanzania. sijui kama ni habari ya kweli au matangazo hayo hayakuwa na effect yoyote labda. Bado sidhani kama kuna jitihada zimefanywa za makususdi kuwezesha kujitangaza na kujilikana kuwa Tanzania ina mlima huu mlima.Cha kushangaza kuna wamarekani nilibashana nao saana kuhusu kuwa eti huu mlima uko kenya,mie nikiwaambia uko Tz.Imagine! Na si mtu mmoja, hata kuna baadhi ya wajapan pia ilikuwa the same thing. Kwakweli Tanzania kama asemavyo mchangiaji wa pili hapo juu, tumelala na hili linatokana na wizara husika kutofanya kazi yake huku wakiendelea kupata mishahara kila mwezi. Mabadiliko makubwa na ya makususdi yanahitajika haraka la sivyo wenzetu wataendelea kula kupitia mgongo wetu,Tanzania.

    Mdauz jp

    ReplyDelete
  5. Michuzi mbona unaruhusu comment ambazo hazihusiki na TOPIC!!!

    Sasa Kenya imetoka wapi wakati swala ni umeme hapa?!! KERO TUPU!!

    Ndo blog zinavokufa hivo!!

    ReplyDelete
  6. Michuzi, asante sana kwa kutuwezesha kubadilishana maoni juu ya masuala mbalimbali ya kijamii, na pia sina budi nimshukuru bw kp kwa kazi nzuri sana anayofanya ya kuibua masuala muhimu bila kupoteza vionjo vya burudani. Ninashauri, mchangiaji anapokwenda nje ya mada (kama hawa walioleta mambo ya k'njaro na utalii), basi unaweza kubandika maoni yake kama mada mpya ya kujadiliwa. hii itasaidia kuwa na mwendelezo wa mada moja kwa wale wanaotaka kuchangia.

    ReplyDelete
  7. kilimanjaro na umeme,wapi na wapi!!

    kama una uchungu sana go and match

    ReplyDelete
  8. Tani 70 Elfu au 70,000 maana yake ni kilo 70,000,000 wadau mpo hapo?

    Sasa tuchukulie kilo moja ya samaki iwe mathalani TZS 3,000 (ndivyo ninavyo nunua mimi pale Mbezi Tangi bovu barabarani!). Tathmini ya HASARA KWA HII MELI MOJA NI TZS 70,000,000 * 3,000 au Kwa maneno mengine TZS 210,000,000,000 kwa kifupi TZS 210 Billioni!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.

    EPA iwekwe kando. Hivi tuna matatizo gani hapa Tanzania?????????????????????????????????????????????

    Kwa nini hawa mabaharia wasitunikiwe nishani ya rais ya Kilimanjaro???????????

    Magufuli kazi yako tunaiona. Tunaomba hesabu hizi zisomeke hivi ili watu waelewe mambo in 'perspectives' vinginevyo itakuwa inaonekana ni habari nyepesi nyepesi.

    Au mtuambie walikama tani 70 na sio 70,000!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...