konda ambaye alitaka kuleta za kuleta akiwa amezungukwa na abiria wasiotaka mchezo baada ya kutaka kuwatoza nauli ya zamani ya sh'ngi 300 badala ya sh'ng 250/- kwa madai hajapewa taarifa rasmi zaidi ya kusikia kwenye globu ya jamii... (ops! sore) ... vyombo vya habari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. mbona wanaleta mchezo mchafu hawa watu wa daladala,kila mafuta yakipanda wanakuwa wanapandisha bei,iweje leo bei za mafuta duniani zipo chini wao waongeze bei,ni kwakigezo gani waongeze bei,
    hawa jamaa na ni mafisadi pia

    ReplyDelete
  2. kumbe makonda wako blogguni pia!?

    Salaalleh!

    = = =
    Buffalo,
    New York

    ReplyDelete
  3. Watanzania tumieni akili zenu msikubali kugeuzwa Makenge na hawa "wanasiasa" wa Sumatra!Leo hii hapa nchini hebu nieleze shs.50/= au shs.100/= utanunulia nini?Ina thamani gani katika uchumi wetu? Basi dogo la HIACE lina uwezo wa kubeba abiria 30.Kwa nauli ya shs.300/=kwa kila abiria hizo ni shs.9,000/=kwa mwenye Basi.Chukulia Basi hilo litoke Ubungo kwenda Posta limejaza abiria hao 30,lazima litumie petroli au dizeli isiyopungua lita 3!Kwa bei ya shs.1,400/= kwa Lita moja ya petroli au dizeli,hizo ni shs.4,200/=.Bakaa kwa Kondakta kwa safari hiyo moja ni shs.4,800/=tu!Gari likiwa safarini litakunywa Oil,litahitaji mafuta ya breki,mbali na uchakavu wa matairi na gari lenyewe,hapo bado hujazungumzia ada za kwenye stendi na ushuru mbalimbali pamoja na kodi ya mapato.Wote tunajua msongamano wa magari Darisalama,dereva hata kama angetaka kwenda spidi ya kasi kiasi gani,katika kila masaa matatu,hawezi kufanya mizunguko zaidi ya mmoja,toka Posta hadi Ubungo nyakati za asubuhi abiria wakiwa wengi zaidi,nyakati zingine za mchana ni za kubahatisha.SUMATRA wanapo wadanganya abiria kwamba walipe "Nauli Halali"ya shs.250/=,hivi kweli wametumia akili au wanafanya mzaha?Wanataka kuziendesha hizi Daladala kisiasa ili kufurahisha wapiga kura,ili serikali ionekane inawajali watu wake?Badala ya kurekebisha kwanza mambo ya msingi zaidi?Nafikiri,uamuzi wa haki na wa busara,kwa kila abiria,ukitaka kupanda basi la Daladala,kwanza muulize Kondakta nauli ya kule unakotaka kwenda.Akikujibu ni shs.300/=na wewe umeridhika kwamba ni shs.250/=ya Sumatra,basi usipande basi lile,subiri lingine litakalo kubali kukuchukua wewe kwa nauli hiyo ya shs.250/=.Lakini,tusitake kulazimisha mambo ya biashara kisiasa.Kupunguza Nauli kuna Ukomo wake.Vinginevyo,mabasi yote baada ya muda mfupi yatakwama na huto ona basi la abiria likiranda mitaani.Hivi sasa wenye Daladala hawana chaguo la kufanya,daladal hizo wazipeleke wapi,vinginevyo usingeziona barabarani.Tusipitishe maamuzi kwa KUKOMOANA TU,madhali wapo wajnja wachache waliodhamiria kuiteka nyara biashara ya uchukuzi wa abiria katika jiji la Darisalama kwa kuleta Mabasi Makubwa zaidi ya abiria!Tumesha sahau kwamba ni mabasi hayo madogo ndiyo yaliyo wakomboa wakazi wa Darisalama kwa kipindi kirefu wakati pakiwepo uhaba mkubwa wa mabasi ya abiria!mimi sina hata basi moja la daladala na sijihusishi na biashara hiyo kwa sasa,kwasababu mtaji huo sina.Lakini nazungumza kama mchumi wa usafirishaji abiria na mizigo bila ya kupendelea upande wowote kwa maslahi ya nchi na watu wake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...