msafara wa magari ya polisi ukiwasili mahakama ya hakimu mkazi kisutu muda mfupi uliopita
watuhumiwa chini ya ulinzi mkali wa askari maalum wa kupambana na ujambazi
hapa hatumwi mtoto
wakiwa kizimbani tayari kusomewa mashitaka yao

kwa kuwa washitakiwa ni wengi (jumla wako 38) na wamechukua nafasi yote mahakamani, paparazi wanakula nao sahani moja kupitia madirishani. kuna wengine wamebaki melini na huenda mahakama ikahamia melini kwani meli hiyo inasemekana haitakiwi kuzimwa na ni wao tu wanaoweza kuendesha mitambo,
-----------------------------------
PS: Kijana aliyempiga kofi Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi naye ameletwa mahakamani hapo asubuhi hii na kusimama mbele ya hakimu mkazi Mh. Neema Chusi.
Baada ya kusomewa shtaka, mtuhumiwa alikiri kumshambulia aliyekuwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwa kumpiga kofi shavu la kushoto Machi 10, 2009 katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar.
Mwendesha Mashtaka Monica Mboga (Wakili wa Serikali): Je Ni kweli ama si kweli?
Ibrahim Saidi a.k.a Sultan a.k.a Ustaadh: Ni kweli

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Je serikali haina uhakika na wanachokifanya? inakuwaje hao jamaa chini ya ulinzi waruhusiwe kukaa melini kwao? hata ikizimwa au ikiharibika ni kosa wao kuweko katika bahari yetu sasa hasara ni juu yao.

    ReplyDelete
  2. Hao jamaa wafungwe wanatupunguzia SAMAKI lol! Bado Meli za Wale wa Europe pia wazikamate. Ustaadh amekubali kama kafanya Kosa wamuweke Miezi Siat ndani. Wadau mnawaona kina Michuzi wanatowa Vioo vya Dirisha Ili wapige Picha nao si washtakiwe? mnalionaje hili? hahahhaa michuzi usiogope. From Pazi.

    ReplyDelete
  3. Ustaadh Jela hiyooooooooooo, umekiri na kumrahisishia kazi sana Hakimu na waendesha mashtaka

    ReplyDelete
  4. Ustaadh Sultan haongoüpi, anasema kweli daima.

    Alimpiga kweli Mzee Mwinyi, hivyo angebisha ningemshangaa Ustaadh Sultan.

    Umati mzima ulishuhudia, kuna picha na video.

    Hahahaha Ustaadh bwana. Pole sana, maisha ni kupanda na kushuka.

    Afadhali ungechikichia zako viwanja, haya yote yasingekukuta maskini, yaani hii frustration ya maisha ya bongo ndio imekuzamisha kwenye imani kali.

    ReplyDelete
  5. Ama kweli tanzania ni tanzania, sheria na uongozi wake tunaujuwa wenyewe. hivi inakuwaje mtuhumiwa anapigwa na watu wakati akiwa chin ya ulinzi? nimeona picha tele katika sites tafauti na unaona dhahiri kama askari wamemzunguka mtuhumiwa lakini watu wanafanikiwa kurusha makonde. Kisheria hakuna aneruhusiwa kuchukuwa sheria mikononi mwake, huyu kijana japo kuwa amefanya kosa na hao waliompiga yeye ni lazima washikwe, well kama nilivyosema ni KISHERIA lakini haya yametokea tanzania!!!!!

    ReplyDelete
  6. Mwenye Meli aitwe na atozwe bonge la faini,kisha wachukue ,meli yao.IKIJA kamatwa tena katika pwani yetu kwa uvuvi haramu basi Meli itaifishwe.Lakini ni vyema vilevile wakaelimishwa kwamba wanaweza kupata kibali cha kuvua katika Pwani yetu wakiomba KIBALI MAALUM TOKA SERIKALINI na kufuata masharti yote watakayo pewa,wao wapate na sisi pia tupate.Wavuvi waliokamatwa ndani ya meli hiyo waachiwe huru lakini kwa onyo na karipio kali,kwamba watakapo kamatwa tena katika pwani yetu kwa uvuvi haramu basi kifungo chao watakijutia!Nafikiri huo utakuwa ustaarabu tosha.Tuwape "element of doubt"kwamba pengine wavuvi hawakuzijua sheria za kimataifa kuhusu uvuvi baharini.Nina uhakika baada ya ujumbe wa meli hii kusambaa kwa wavuvi wengine wa kimataifa,basi matukio ya aina hiyo yatapungua zaidi na zaidi.

    ReplyDelete
  7. Jamani wanashangaa hivi wanajua hata kinachoendelea na hao wakalimani waliotafutwa wataawaaminije kama hawatasema uongo kuna mmoja anaweza akatetewa hapu either serikali au watuhumiwa.
    na hao samaki wanapelekwa kule vic fish anauziwa mwenye kiwanda au wanahifadhiwa kwa muda then watajua wafanyeje na mbona nasiki kuna meli nyingi tu kule ina maana serikali ilikuwa inaogopa kuwakamata au. du inaonyesha samamki wengi sana wameuzwa

    ReplyDelete
  8. ustaadh amedhirisha kwake dini imelala kusema uongo ni dhambi amekubali kosa, ahukumiwe awahi kutoka aendelee na mambo yake

    ReplyDelete
  9. Kwa mujibu wa waziri Pombe wakipatikana na hatia wanaweza kutakiwa kuacha meli. Taifa litapata hela zaidi likinadi meli kuliko kuuza skrepa. Wacha tuwalinde humo humo melini.

    ReplyDelete
  10. sasa jamani naomba kuuliza hao wanaochungulia hawana vitu vya maana vya kufanya yani umbea tu wanaume wazima go do some work or somethn

    ReplyDelete
  11. Hawa jamaa sura zinaonyesha hawajui wanachokifanya nadhani kuna tajiri mmoja kawadanganya na kuwaleta nao wakakubali kwa umaskini wao sasa sheria inawaangukia. Hii ninaiona ni sawa na wanaokamatwa kwa kubeba/kukutwa na unga wakati mabosi wao wako pembeni.

    ReplyDelete
  12. Aaaah naona vijana wa kifilipino wamejaa.

    Hawa jamaa kwa wale ambao hamjawahi "kuzamia" meli ndio hivi sasa wanatamba kwa kazi za melini.

    Makampuni mengi ya meli huwa yanaajiri Wafilipino maana inasemekana wanapiga kazi kinoma.

    Enzi zile ukiongelea meli ilikuwaga "Wagiriki", siku hizi ni "Wafilipino"

    ReplyDelete
  13. sisi tutaibiwa na kila mtu viongozi wanaiba watu wa nje wanaiba lol na hao jamaa kila siku wapo hapo wavuvi gharamu hivi hapo bongo hatuna hata meli ya polisi manake hio iliyo wakamata inatoka cape town na ni mali ya RSA kwahio meli hio next week ikiondoka wezi wanaendelea kama kawa na inakuja huko kwa mwaka mara moja nani anajali mali asili zetu hatuna chombo kinachoweza kulinda kwahio tutaibiwa mpaka tufe

    ReplyDelete
  14. Nyie mnashangaa alipigwaje kibao wakati kuna walindi...Kamuulize Bush huko TX alipigwaje kiatu wakati paparazi wote ni walinzi wake....tehetetetetetet


    Na hao wenye meli ....kweli bongo sheria easy...waache hiyo meli ife...kwani wao walifuata nini hapo....Ingawaje wanasema you are not guilty until proven so ...lakini kesi yao ni black and white kwani wameingia kuvua kwenye sehemu sio yao na ni haramu ....na wakiwekwa lupango watakaa kwenye meli mpaka muda wao uishe teh tehetehe ..Nani atrefill gas?????? bongo hiyooooo...tusije jikuta tunawajazia na mafuta tena

    ReplyDelete
  15. Leo ndiyo nimejua maana ya msemo wa Kiswahili " nimeamka vibaya ". Everything I see I see wrong. Damn it, ningekuwa Bongo na mimi nanyemelea AK 47 navaa jeans na t-shirt yangu najichanganya na maaskari napuliza mirisasi kwa wavuvi haramu. Halafu BBC wanatangaza wavuvi haramu wameuawa na askari wa Tanzania. Kudadeki,baada ya hapo hatoki mkuu, wasaidizi wake, wala wananchi wake kwenda popote si EU, US wala Asia-Pacific. Na Wabongo waliopo mabeach nyanya vita na Wafilipino. Wafilipino wanavyopenda ugomvi wa visu halafu wana makanjanja ya uboi na Wabongo hatuna makanjanja k...bake Michuzi kila siku atakuwa anabandika matangazo ya misiba na michango za kurudisha maiti.

    ReplyDelete
  16. Naomba serikali ibadilishe sheria askari anapokuwa na silaha lazima awe amevaa sare ya uaskari.

    ReplyDelete
  17. MWINYI (MZEE RUKSA) NDO KIPENZI CHA WENGI AKIFUATIWA NA KIKWETE (MLA FISADI).

    ILA ALITAKIWA KUSEMA KIPIRA AU SI BILA KIPIRA RUKSA, NATANIA.

    ReplyDelete
  18. meli haitakiwi kuzimwa?ni wao TUUU wanaojua kutumia iyo mitambo??

    bullshit,
    meli inatumia nuclear mitambo au nini??
    yan ata ukienda ubalozi wa marekani tu apo bongo utapata ma-engineers wa ilo dude!!

    afu lugha gani ao watu??

    meli ya sauzi ikiondoka wizi upo pale-pale

    ReplyDelete
  19. YOTE TISA - KUMI HAO ASKARI WENYE SILAHA - WANADHANIA WAKO KWENYE FILAMU YA KINIJERIA? AIBU GANI HII? KHA!

    ReplyDelete
  20. Mkuu,

    Nakuomba wasiliana na wakuu kuhusu hili suala la askari kuvalia nguo za kiraia na kubeba silaha kali kama AK 47. Hii ni hatari sana kwa usalama kwa sababu haimtambulishi kirahisi askari hivyo ni rahisi kwa wenye nia mbaya kughushi kama maaskari.

    Jambo jingine ni huu mtindo wa kuwabeba watuhumiwa kwenye magari ya wazi. Jambo hili ni hatari kwa askari na watuhumiwa hali kadhalika kwa sababu kuwa kwenye magari ya wazi kunawaanika askari na watuhumiwa hadharani. Inaweza kuwa hatari kwa askari kwa sababu m/watuhumiwa wakitaka kutoroka. Inaweza kuwa hatari kwa watuhumiwa ikiwa watashambuliwa na maadui zao au wenye visasi nao.

    Hii ni tahadhari kabla ya hatari. Asante.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...