Mama salma kikwete
Na Anna Nkinda wa Maelezo


Mama Salma Kikwete amewataka wanaume wa mkoa wa Mara kuacha tabia ya kuwapiga wake zao bali wawasaidie kufanya mambo ya maendeleo ambayo yatawasaidia kujikwamua kimaisha.

Mama Kikwete aliyasema hayo jana wakati akifungua semina ya siku mbili ya uwekezaji na ujasiriamali iliyofanyika katika ukumbi wa uwekezaji uliopo mjini Musoma.

“Nilikuwa nasikia kuwa eti wanawake wa mkoa huu wakipigwa na wanaume zao ndiyo wanaonekana kuwa wanapendwa sana sasa sijui kama ni kweli au la, lakini kwa kuwa leo niko na nyinyi wenyeji wa Mara nitajua kama ni kweli ”, alisema.
"Tatizo langu mie kwa watani zangu hawa ni hapo, je kinamama si wataona waume zao hawawapendi?
"Nasikia eti ikipita wiki bila kupigwa mama wa kikulya huanzisha zogo mwenyewe na asipopata kichapo basi atarusha jiwe juu ya bati afu atakinga mgongo iliaangukiwe nalo ndo amani inarejea ndani ya nyumba, kweli hayo watani???", alihoji.
Mama Kikwete pia aliwataka wakazi hao kuachana na imani za kishirikina za kuamini kuwa ukiwaua walemavu wa ngozi (albino) utapata utajiri na kuwataka kuwafichua wauaji wa albino.
“Kila mtu ana haki ya kuishi kama mwingine si vyema kuwafanya albino hawana haki ya kuishi na kuwaua pasipo sababu”.
“Acheni kuua albino kwani utajiri hauji kwa kuuza viungo vyao bali kwa kufanya kazi kwa bidii na kijituma kwa kufanya hivyo mtafanikiwa na kuondokana na umaskini”, alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Habari kaka Michuzi.
    Kuna swala lilitanda katika vyombo vya habari kuhusu kupigwa kwa rais Mstaafu. Utashi wa binadamu hauna nafasi katika imani za watu.
    Pitia mchomeko
    Pope Benedict XVI has said that handing out condoms is not the answer in the fight against HIV/Aids, as he makes his first visit to Africa as pontiff.
    Source; http://newsvote.bbc.co.uk/1/hi/world/africa/7947460.stm

    ReplyDelete
  2. We Mama namba 1, ni kweli wenzio bila kupata kipigo cha kutosha kila wiki huwa mambo hayaendi vizuri ndani ya nyumba, hata malavi=davi nayo huwa hayanogi. Mwanaume asiyejua kumpiga mkewe huhesabika kama ana kasoro na ndoa yake huwa haidumu hata miaka miwili. Mwenzetu una bahati ya kuolewa nyumba kubwa ambako hata ukipata kichapo cha JK inakuwa kimyakimya, sisi wenzio hujisifia.
    Nasikia wanawake wa mjini huwa mnawapiga waume zenu wanapowakosea na mfano ni wa kaka Ben na dada Anna, je ni kweli??

    ReplyDelete
  3. Nadhani huyu mama anavutia kumsikiliza akihutubia!!

    Point!

    "Utajiri huja kwa kufanya kazi kwa bidii na kijituma kwa kufanya hivyo mtafanikiwa na kuondokana na umaskini"

    Utani!

    "Nasikia eti ikipita wiki bila kupigwa mama wa kikulya huanzisha zogo mwenyewe na asipopata kichapo basi atarusha jiwe juu ya bati afu atakinga mgongo iliaangukiwe nalo ndo amani inarejea ndani ya nyumba"

    ReplyDelete
  4. sasa mama itakuwaje kwa wake zetu kwasababu bila kumpiga mwanamke hatajisikia kuwa anapendwa na mwanaume hujulikana kama ni mkali ukiwa unampa kipigo mtoto wa kikurya,inaonekana mama utaki kabisa malavidavi,mwambie mzee akiwa anakupa kichapo hata wewe utajiona kuwa unapendwa ila asipo kupa kichapo basi ujue hakupendi
    marwa tarime

    ReplyDelete
  5. mtende hata siku moja hana heshima kwa mwanamke. wanaume wa kitende nguvu zao zote huishia kupiga wake zao. hao watu ni washari sana. nilisoma habari wakati mmoja kuwa baba fulani alikwenda nyumbani kwa wazazi wa mke wa mtoto wake akaanzisha ugomvi halafu hao wakwe wa mtoto wake wakampiga. alirudi nyumbani kwake na kumkata masikio yule binti wa watu aliye olewa na mtoto wake. huu ni ukatili wa aina gani. huyo mtu anatakiwa apewe kifungo cha muda mrefu sana ili asirudie kitendo hicho.

    ReplyDelete
  6. Sidhani kama hadithi za zamani bado zipo mpaka leo. It is just a myth. Je ni kweli kuwa wamakonde wanakula watu? simply because of ndonya. Wapiga wanawake ni everywhere duniani si wakuyra tu!! notably hata wanaume hupigwa vilevile. as a first lady naona ni talalila tu kama muungwana wake.

    ReplyDelete
  7. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni......mama yetu wakwanza yupo juu.Huwezi kumfananisha na wengine walopita,she's a hard work first lady .I can now prove that ...behind any successfull man theres a woman.Mama Kikwete yuko vizuri.Big up mama....Congrats.
    Cha Chandu- Uk

    ReplyDelete
  8. Mama Mpendwa,

    Gwa niyaba ja Wakuriya wenzangu nasema asante sana gwa usia. Tutajitahidi kuacha kuwachapa kina Bhokhe.

    Rakini hii gampeni iziishie gwa Wakurya tu. Naguomba ienderee mpaka Moshi ukawausie na Wachaga na Wapare waache zijui kufanya nini? Uwaambie na Wamwera, Wamakua, Wayao, Wamalaba na Wamakonde waache yale mambo yao. Tena uwaambie Wamakonde waache kuchanja uso gwa sababu wanawatisha watoto na watalii gutoga Uraya hivyo kulisababishia taifa hasara ya fedha za kigeni. Na Wasukuma waache mambo yale gwa sababu mambo yao siyo mazuri yanaharibu sifa ya taifa. Ukifika Bukoba uwausie na Wahaya. Gwa ufupi tu naomba uendelee kutupa usia wanao wapendwa tunaokupenda sana Mama yetu.

    Chacha Matiko Mwita, Fort Ikoma, Musoma.

    ReplyDelete
  9. mama unapendeza sana kwa hijabu na ushungi.

    ReplyDelete
  10. mimi hapa simwelewi mama wa kwanza! si wanawake wanaolewa ili kupigwa au usasa umebadilisha mila!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...