Mtoto Ummi Mbega(3) anayesoma shule ya awali Highlands mjini Iringa akimkaribisha kwa maua Mama Salma Kikwete muda mfupi baada yakuwasili katika uwanja wa ndege wa Nduli Iringa kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili.Pamoja na mambo mengine Mama Kikwete alifungua Kongamano la Wanawake Viuongozi kuhusu ukimwi na jinsia na kufungua mkutano mkuu wa SaCOOS ya Wanawake Iringa.Mama kikwete alitumia fursa hiyo kuchnagia saccos za wanawake wa Iringa mjini na Vijijini Jumla ya Sh.Milioni nne kila moja ikipata milioni mbili.
Mbunge wa viti maalumu Iringa Bi.Lediana Mng'ong'o ambaye pia ni makamu mwenyekiti TACAIDS, akimkabidhi Mama Salma Kikwete Tuzo maalumu Iringa Women Leadership Award Kwa kutambua mchango wake katika mapambano dhidi ya gonjwa la Ukimwi nchini.Hafla hiyo ilifanyika wakati Mama Salma ambaye ni mwenyekiti wa taasisi ya Wanawake na Maendeleo WAMA alipofungua kongamano la Wanawake Viongozi wa mkoa wa Iringa katika ukumbi wa St.Dominic Mjini Iringa leo asubuhi

Mama Salma Kikwete na Mbunge wa Iringa viti maalum Lediana Mung'ongo wakiwasha mishumaa kuwakumbuka waathirika waliofariki kwa gonjwa la ukimwi wakati wa ufunguzi wa kongamano la ukimwi na jinsia la viongozi wanawake mkoa wa Iringa lililofanyika katika ukumbi wa St.Dominic mjini Iringas le asubuhi. Picha na mdau Freddy Maro wa Ikulu.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Jamani ni mimi tu au huyu first lady ananoga haswa...yaani ngozi laini lol....big up mama keep it up
    mdau DC

    ReplyDelete
  2. Hata mie namadmire saana anazidi kuwa mayai tuu kila siku. Ndio faida ya kuwa mnene maana uso unajaa unakuwa mnono na baby face kila siku. Actual hiyo ni study iliyofanyika US, unapozeeka unatakiwa ugain weight kidogo ili uso ung'ale.

    ReplyDelete
  3. UKIMWI umegeuzwa kuwa Biashara, NGO, watumishi wa Umma na camission wanafaidika kwa matatizo ya wengine

    ReplyDelete
  4. NDULI AIRPORT OYEEEEEEEEEEEEEEEEEE
    dah im so happy to here that nduli,naamini wameutengeneza sasa baada ya ujio wa bibie,,,

    jaman mamlaka husika tengenezeni airport iyo kwani iringa kuna vivutio vya kitalii kufa mtu,,RUAHA,MAPANGO YA KALE,DABAGA-matunda,nk nk ni sehemu tu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...