Roonye akiona nyekundu leo

TEHE TEHE TEHE TEHE TEHE TEHEEE TEHE TEHE TEHE TEHE TEHE... 

NA BADO!

TODAY RESULTS
Blackburn 1-1 West Ham
Fulham 2-0 Man Utd
Stoke 1-0 Middlesbrough
Portsmouth 2-1 Everton
Tottenham 1-0 Chelsea
West Brom 1-1 Bolton

nenda BBC SPORT kuona mambo yalivyokuwa dakika kwa dakika

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. ha ha ha ha ha ha ha ha wamelewaaa magoli hao piga huwa.na bado villa wanakuja kuuuuua.

    ReplyDelete
  2. Safi sana, kabla ya taarifa hizi nilikuwa nasikia maumivu ya kichwa sasa yameisha naingia mtaani kifua mbele najua kuna akina nanihii huko taarifa hizi hawajapata!!!

    ReplyDelete
  3. hiyo rooney ilivyoandikwa sasa duh,!!!

    ReplyDelete
  4. Michuzi, USIMCHEKE MAMBA KABLA HUJAVUKA MTO ohhh,cku hizi mambo yamebadilika ndugu yangu.
    Matokeo ya leo ni mazuri kwa pande zote mbili,NI NGUMU kucheza na timu inayopigana kushuka daraja kuliko inayowania ubingwa,leo nadhani wengi watakubaliana na kauli yangu hii.
    Wakubwa leo wamekumbushwa tena maana wamelewa na ratiba ya UEFA.
    katika mpira BAHATI au ngekewa huwa ina nafasi kubwa mno so wadau msijeumiza vichwa kuwa kesho liver lazima ashinde,kama bahati iko kwao watashinda ila kama haipo hata wakicheza 12 hakuna kitu.Man U hawakuwa na bahati kwani 2nd half wamekosa magoli mengi mno,then Chelsea pia zali halikuwa kwao leo,Alex kagongesha mwamba dakika za mwishoni,Malouda nao kakosa nafasi za wazi,Drogba vichwa vyote na Terry vilikosa mwelekea,ila angalia timu ambazo zimewafunga mashambulizi yao yalikuwa kama ya hawa wakubwa??je wangekuwa wanashambulia sawa na wakubwa leo si ingekuwa aibu nyingine?Fulham 7 man u 1,Tottenham 5 chelsea 1.sasa mkapumzike mpishe international games then mjipange upya wakubwa

    ReplyDelete
  5. Ama kweli soccer buludani....yaani huwezi kuamini mende wanaangusha makabati week end hii.
    Ukubwa wa pua kweli sio wingi wa makamasi.Man u mganga wao kaenda fungate au ni vp?last week Best defender VIDIC aka VIDA alifanya madudu ya kufa mtu,week hii Mzazi Scholes nae anataka kuwa kipa wapili as if hakuna makamera,anadhani ni mwaka 902??One mistake one goal,sasa kwa mtaji huu hadi league iishe si ndio utasikia Everton bingwa?ama kweli ng'ombe wa masikini hazai na akizaa jua hasara tupu.Essien karudi lakini wapi majeba wamelazwa chaliiiiii

    ReplyDelete
  6. KUDADADADADADADADADDADADADADADADADADADADADADADADADDADADDADDADADADDDADADADADDADADDADDADADADADADDADADADADADADADADADADADDADDDADDADADADADDADADADAKI !!!

    MI NILIWATELL KUWA HAO MAN U NI KAMA DEMU MREMBO..ATABANAAA LAKINI AKIANZA KUACHIA VITU ATANOGEWA NA NDIO ITAKUWA KAZI YAKE...RAHAAA, UTAMU..RAHAA, UTAMU

    NA BADO!!

    MZEE WA LIVA

    ReplyDelete
  7. ONYO, USITUKANE MAMBA KABLA HUJAVUKA MTO.

    ReplyDelete
  8. wamefungwa wazomeeni oooooooooo,wachekeni haaaaaa.
    Tumetoka kuuwa GAMUTU 3-1 leo mbona raha ndani ya Dar

    ReplyDelete
  9. Nyie MAN YU hamna lolote na huyo baba yenu Sie Alex FOOLGUSON kichwa chake kimeishapoteza network sasa mtachezea vichapo hadi moke, nyama nyie

    ReplyDelete
  10. Nyie MAN YU hamna lolote na huyo baba yenu Sie Alex FOOLGUSON kichwa chake kimeishapoteza network sasa mtachezea vichapo hadi moke, nyama nyie

    ReplyDelete
  11. ahaha leo mendo kadondosha kabati ahaha kudadadeki nackia Scholes kumbe alikuwa Volleyball captain wa England team Olympic so alichanganya kidogo madawa pale ila yote tisa kumi ni lile goli la yule mtoto Gera mtoto nuksii lile goli Rooney miaka 10 afungi alaf nackia dogo kapata membership free anfield kuangalia mechi zilizosalia bureeee.
    Ni hayo 2.

    ReplyDelete
  12. Premier League raha sana namna hii, maana huyu naniino alikua anajua yeye ndo yeye, sasa atleast kaonja utamuuu rahaaa bado Villa, na raha Villa afungwe kesho ili aje akiwa amejeruhiwa against mashetani waliopoteza network..Arsenal Oyeeeeeeeee

    ReplyDelete
  13. Ukitazama fixture ilivyo kwa takribani mechi tisa zikizobaki ni wazi kwa matokeo haya ya leo,mechi ya Liverpool na Aston Villa ni fainali.Na kama Livapool akishinda hii mechi mkono mmoja unashika kombe,kwani kati ya Man,Chelsea na Liverpool angalau Liva ana mechi rahisi kiasi,japo wote itabidi wacheze na Arsenal.
    But Villa wapo kwenye wakati muhimu kuliko kwa sasa,hivyo kesho watajipanga vizuri ukitilia maanani last match walilala kwa Totenham tena wakiwa home.
    Kazi ipo

    ReplyDelete
  14. Vidic three match ban(now 2) Scholes three match ban, Rooney possible suspension with over reactions!
    United shughuli pevu!

    ReplyDelete
  15. uwezo wa Sir Alex F. umefikia mwisho. inawezekana vipi aingize washambuliaji wengi wakati wao ni pungufu.

    ReplyDelete
  16. kipigo tulichowapa hawa man utd bado kimewachanganya 4 nyingi bwana,kazi kweli kweli safari hii

    ReplyDelete
  17. i hope most wangekumbuka comment i made after Liverpool defeated Madrid.nilisema endapo Liverpool atamfunga Man United,kuna possibility Man United akawa na bad run kama ile ilioikumba Chelsea baada ya kupigwa na Liverpool(1-0)ktk game ya kwanza.now the same happened to Manure.

    game ya Liverpool na Aston Villa ni ngumu kwa wote kutokana na sababu tofauti.Liverpool wao wanamfukuza Manure while Villa wao wanawafukuza watengeneza Magobore.so game itakuwa na mshikemshike.
    but predictions, 2- 1.Liverpool pointi zote tatu.goli la ushindi huenda likafungwa na yule asiyetarajiwa(how abt Carragher)hahaha

    "LFC 4 LIFE"

    ReplyDelete
  18. kuhusu Sir MaBIG G,kuwa na washambuliaji wengi ni tactical change tu na wala has nothing to do with coach's ability.vi2 kama hivyo sometimes works na sometimes vinakataa.
    Fergie kashafanya hivyo mara nyingi tu na kushinda.last week kabla ya kupigwa bao la tatu na Liverpool pia aliwaingiza Barbatov na Giggs wakati still ndani kuna Ronaldo,Rooney na Tevez.lkn hali ndo ikazidi kuwa mbaya.
    so kuwa na washambuliaji wengi kunaweza kuwa na faida na hasara zake just like any other formation.u can get it right/wrong.
    Makocha wengi wanafanya hivyo but ONLY pale goli linapohitajika zaidi.

    "LFC 4 LIFE"

    ReplyDelete
  19. rooney angevunja kibendera mbele ya maximo angemfukuza timu.kuwa hana nidhamu ya ndani na nje.MAN U naona bado wanamkumbuka TORRES NA GERRARD NDIO MAANA WANAKUNYWA TU.
    MAXIMO ANADAI KUNA TIMU IKO SOUTH AFRICA IMEMTAKA ANAJUA ANGEKWENDA SOUTH AFRICA NA AKASHINDWA KUWAPA KOMBE ANAFUKUZWA BORA AKAE NA SISI WAJINGA TULIOMPA HADHI YA UWAZIRI.AMA KWELI WAJINGA NDIO WALIWAO.

    ReplyDelete
  20. Ndugu yangu Ayaz (Manyu damu) pale rock city wiki hii presha itamuua, dogo acha kuzima zima simu maana utakosa madili. Oyaaa Nyemo nyemo hamna hilo ni jinamizi la bwawa la maini!
    Mshkaji wangu Efraim wa Oman (Ze Blues) nae haonekani siku hizi, Si mje gunners tu wajameni!!

    ReplyDelete
  21. Kuna kajamaa flani kalikua kanajiitaga "Mdau Willy - UK",

    Najaribu kutafuta Comment yake siioni,

    Kwa anamjua amwambie aweke comment bwana kwenye hii issue,

    Naisubiria kwa Hamu.

    MUOSHA KINYWA ORIJINO

    ReplyDelete
  22. AMA KWELI SASA NIMETHIBITISHA MAN U NI TIMU YENYE WACHEZAJI WENYE VIPAJI KIBAOOOO!q!!
    1. VIDIC A. FOOTBALL B. RUGBY
    2.RIO A.FOOTBALL B.TAARAB (HE COMPLAINS ALOT)
    3.SCHOLES A. FOOTBALL B. HANDBALL
    4.RONALDO A.FOOTBALL B. DIVINGC. ATHLETICS
    5.ROONEY A. FOOTBALL B. KURUSHA TUFE C. BOXING

    MAN U MDEBWEDO WATU WANAJIPIGIA WANAONDOKA..RAHAAA, UTAMU, RAHAA, UTAMU!!!

    ReplyDelete
  23. NOW WE BELIEVE PREMIER LEAGUE IS ALL ABOUT MAN U>>> hahahahahahaaa

    DUH Kweli ant-man u ni wengi duniani.Chelsea nae kachapwa,hakuna comment,Everton kachapwa,no comment,Arsenal kashinda few comments,Tottenham kashinda no comment,LiverFools hajacheza ALOT of comments.Nawaombea ushindi mnono maana mkifungwa nadhani blog nayo maoni yatafungiwa kwa muda.
    Tottenham tumeshinda hakuna anayetufagilia au hamkuona game??
    Jamani KIZURI sifia KIBAYA kandia.....!!

    ReplyDelete
  24. Mdau March 22, 5.55, jamani, Maximo ameshasaini mkataba wa mwaka mmoja..Tumechoooka!! Na mtunusuru masikio na macho yetu kwa masuala ya Maximo kwa sasa..unapozungumzia Rooney, wajua lolote kuhusu kandanda na jinsi Sir Alex achukiavyo utovu wa nidhamu na kujikweza? (ka Marcio Maximo)?
    *Yeyote mwenye uelewa mpevu wa soka anaona uhusiano wazi baina ya kumvumilia kocha, kumpa ushirikiano na muda wa kutosha kutimiza maazimio yake..Alex Ferguson, leo hii kocha mwenye mafanikio zaidi kwenye historia ya premiership ama hata ya kabumbu zima la kiingereza, aliponea mechi moja ya mwisho kufukuzwa..na wakati huo tayari aliishakaa United miaka 3 !..
    *Msimu wa 89/90, baada ya Sir Alex kufanya ‘shopping ya kuua mtu', United 'wakatuonea' Gunners 4-1 lakini baada ya hapo wakafululiza kupoteza mechi 6 na kutoa sare 2 (Mahasimu wao City wakiwatundika 5-1!). Manazi Manure na wanahabari wakaanza kulia ‘Fergia aende’!..Gemu iliyofata ikawa ni FA dhidi ya Forest, kila mmoja akijua kuwa Shetani wameelekea kibla na Fergie kibarua chaota majani!..Maajabu, Manure wakashinda 1-0 na baada ya hapo kama isemekanavyo imekuwa ni 'historia iliyotukuka'...
    *Sir Alex alisubiri misimu 6 kushinda taji la kwanza la ligi na Manure (1992)..kwa miaka yake 22, Fergie ni meneja wa pili kudumu kitini akimfuatia Sir Matt Busby (pia wa Manure, ambaye aliondolewa kitini na kifo, si kufukuzwa!)- halafu mtu ashangae kwa nini Utd ni moja ya klabu zenye mafanikio makubwa duniani?..
    *Pamoja na kijimfano chako cha Roonye, Sir Alex anajali sana nidhamu na hapendi hata chembe kujikweza kwa wachezaji! Chukua mfano wa magalacha kama Gordon Strachan, Paul McGrath, Paul Ince, Jaap Stam, Dwight Yorke, David Beckham, Ruud van Nistelrooy, Roy Keane na Gabriel Heinze wote wameondoka Manure baada ya kugonga mkenge ( wa Fergie) !..Hii pia yaweza kukuonyesha nguvu ya Meneja kwa timu na wachezaji.
    *Majuzi, Benitez kasaini mkataba, najua wengi mmeona pesa tu alizopata, ukweli ni kuwa Benitez amefanikiwa pia kusimikwa wazi kama mtu mwenye kauli ya mwisho kwa masuala yoote ya kiufundi hapo bwawani mainini. Kabla ya Benitez alodumu takriban miaka 5, Liverfools walikua nyikani na akina Phil na Monsieur Houllier, sijui- labda mwaka huu Kaanani inakonyeza !.. Monsieur Wenger, mmeona amedumu muda gani ?..Njoo basi ulinganishe na akina Spuds na Chelski wanavyofukuza ma-meneja na wanavowayawaya !..
    *katika medani ya kimataifa, Ujerumani (FRG na baadaye Germany), moja ya mataifa yenye mafanikio makubwa ya soka duniani, imewahi kuajiri takriban makocha 10 tu tangia 1908, ajabu iliyoje ! Si ajabu, ni busara za kijerumani ambazo hazipingiki kuwa mdau akishapitishwa kwenye tanuru na mchakato sahihi wa kupata kazi nyeti kama ukocha wa taifa, basi hayo siyo matipwi, ukichoka wachomolewa aingia mwingine ! Angalia Ufaransa jinsi ambavyo hawana matokeo ya kuridhisha, japo bado mustakbala wao wameukabidhi kwa Domenech, ingekuwa siye hawa wanazi wetu wangeshatimba hadi ikulu !. Katika kubadilibadili mitindo, wenzetu wa Afrika Kusini walimfukuza Carlos Queiroz mnamo 2002, hadi leo bado wana jinamizi la kubadili-badili na hawajashinda chochote. Taifa kubwa kama lao, sembuse sisi mpapasingo, kwangu pakavu tia mchuzi !..Linganisha na Ureno na Uingereza kwa kubadili makocha na mafanikio yao duni !
    *Me nafikiri twahitaji uvumulivu na kumpa ushirikiano Maximo na timu yake..Huu u-Yanga na u-Simba ukome hukohuko, ukomandoo Stars, mwiko. Wadau, kama mwapenda Chandimu ni vizuri kuwa na ufahamu..Asiye na data, na asifungue lake domo (asiingie malumbano), ila kama anataka kutuburudisha wadau wenzake !
    *Mwishoni, twajua kama soka yaweza kuwa si muhimu kulinganisha na mada za akina Mashaka. Hata hivyo tukumbuke kuwa michezo na sanaa hujenga sana uzalendo na utamaduni wa jamii husika. Zamani watu walipigana vita, siku hizi kwa kiasi kikubwa zimepitwa na wakati. Sasa twafungana magoli ama twachukuliana point na medali. Soka pia ni ajira ya nguvu ambayo sijui hata kama itaathirika sana na kwikwi za uchumi wa dunia. Me siachi kufikiri jinsi wa-nigeria takriban 100 na ushee wanaocheza Ulaya na kusaidia jamaa zao nigeria ama wale wa-brazil takriban 1,176… - UZENG (GUNNER/KANDAMBILI/STARS)

    ReplyDelete
  25. yaani we cheka tu lakini si unajua kuwa watu walikipiga UEFA mimi nafikiri sir anatakiwa kuchezesha kikosi cha pili ili jamaa wapumzike na msilikatae hili ushabiki tu... hata hamwangalii mambo yalivyo

    ReplyDelete
  26. Jamani inakuwaje mnalinganisha Rooney na wachezaji wetu wa bongo? Mnajua anauza fulana ngapi kwa mwaka? Mnajua anapachika wavuni na kutoa pasi za mwisho mara ngapi kwa mwaka? Mchezaji gani wa bongo analinganishika naye kwa hayo?
    Mnaomlaumu Maximo kwa kujali mambo ya nidhamu mkumbuke kwamba Maximo hajawahi kumtupia daluga mchezaji wake. Beckham ashawahi kutandikwa daluga la pua na Fergie. Angekuwa Maximo amefanya hivyo wabongo mngefanyeje hapo?
    Taifa Stars kiwango chake kinapanda. Sasa hivi tunaambiwa tutapata mechi ya kirafiki na New Zealand. Kwenye ranking za FIFA New Zealand iko kwenye 80 bora. Miaka ya nyuma wasingecheza na wachovu waitwao Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...