WATANZANIA WOTE MUISHIO READING, BRACKNELL, WOKINGHAM MNAKARIBISHWA KWENYE KIKAO CHA MCHAKATO WA KUUNDA JUMUIYA YA WATANZANIA UTAKAOFANYIKA TAREHE 15/03/09
MAHALI:
READING 1A BAMBURGH CLOSE, RG2 7UD
- KUTAKUWA NA UGENI KUTOKA CHUO KIKUU CHA EDINBURGH KWA AJILI YA KUELEZEA JINSI YA KUPATA UDHAMINI KWA KUPITIA MFUKO WA MWALIMU NYERERE KUTOKA KWENYE CHUO KIKUU HICHO CHA SCOTLAND [NEW MWALIMU NYERERE SCHOLARSHIP FOR TANZANIANS]
- KUTAKUWA NA MGENI KUTOKEA CONCERN WORLD
- MWAKILISHI WA SHIRIKA LA KIMATAIFA LA KUSHUGHULIKIA WAHAMIAJI [IOM]
KWA MAELEZO ZAIDI TAFADHALI WASILIANA NA;
MAIRA BENJAMINE MIGIRE- +447799212095
WOTE MNAKARIBISHWA – KUTAKUWA NA CHAKULA (free of charge) VINYWAJI VITAKUWEPO KWA KUJINUNULIA
KIINGILIO BURE!!!!!!!!
Akhsante.
Uingereza kuna jumuiya ya Watanzania au Tanzania Uk Association iliyoanzishwa na balozi wetu mama mpendwa Mwanaidi Shariff Maajar.
ReplyDeletesasa watu wa Reading kuanza kufungua jumuiya zingine za watanzania wakati hii aliyoanzisha balozi ndio inaanza kuchukua kasi si jambo la busara.
kuweni kitu kimoja, kwanini msiwe na Tawi la TA huko READING? au mkiwa na tawi mtakosa fursa ya kuwa viongozi wa kitaifa wa jumuiya? subirini uchaguzi wa TA muwe viongozi kuliko kujigawa kiasi hiki.
kama ilivyo chama cha kina mama Tawa cha hapa UK.kinafanya kazi nzuri sana kama ile ya kumsaidia yule dada aliyekuwa mfanyakazi wa ndani akalipwa pounds elfu sitini kwa msaada wa TAWA chini ya mama kilumanga,
ghafla watu wengine huko Reading wameanzisha jumuiya ya kina mama inaitwa Diaspora kwanini wasiwe kitu kimoja na TAWA?
UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU.UNGANENI MUWE TAWA AU TANZANIA ASSOCIATION CHINI YA ULEZI WA BALOZI AMBAYE ANAPENDA WATANZANIA WAWE WAMOJA.
NI USHAURI TU,JUKUMU LA KUAMUA LIKO KWENU.
Annon hapo juu, fanya uchambuzi kwanza kabla ya kukurupuka na kushutumu watu. Aliyekuambia huu umoja unajitenga ni nani?? Waswahili kazi kukimbilia kulalamika bila ushahidi. Kaa chini tafuta ukweli kabla ya kuja kwenye mablog kulalama.
ReplyDeleteKwanza kuhusu umoja mbalimbali, hata huku UK na nchi zingine zina Association nyingi na inategemea kila moja inashughulika na nini. Haiwezekani Umoja flani ukajumuisha kila mtu. Nahisi kila Association inayofunguliwa ina malengo yake, na ndiyo maana hata Vyama vya siasa vipo vingi.
Ushauri wako mzuri lakini hauna ukweli kamili.
Huu umoja wa TA nani kakuambia umeanza kuchukua kasi?? Kasi ipi?? TA ina miaka miwili, sijaona lolote la maana walilofanya zaidi ya Mwenyekiti wake kufanya Biashara. Sijaona wakitembelea miji mbalimbali kujaribu kufungua hayo "Matawi". Tumejaribu sana kupiga simu na kutafuta majibu kwa Mwenyekiti wa TA na Katibu wake, lakini kila mara wako busy au wanafanya Biashara. Sasa sisi Watanzania tufanyaje?? Inaonekana Umoja huu ni wa LOndon kwa Mwenyekiti wa TA na kwa Balozi. Tunamuonea huruma huyu Mama Balozi maana anahangaika sana kuwaunganisha Watanzania. Lakini Abuu anaharibu sana.
ReplyDeleteKwanza miaka miwili si imeshapita?? Kweli uchaguzi Mkuu wa TA si unatakiwa kufanyika?????
KUNA MTU ANAJUA NI LINI UCHAGUZI MKUU WA TA???
Au ndo mambo ya chini chini?? Hebu waachie watu wanaojua kufanya kazi waifanye kazi ya kutuunganisha Watanzania.
UCHAGUZI WA TA NI TAREHE 25/03/09 .TENA NIMESIKIA KUNA MTU KAANDALIWA ILI ACHUKUE KITI HICHO ,UONGOZI UENDELEE KUBAKIA LONDON.WATAANZANIA AMKENI.TUKATAENI UCHAGUZI WATANZANIA WENZANGU
ReplyDeleteTatizo watu wa READING ukabila mmeweka mbele kama hakuna kiongozi wa musoma basi mnaona jumuia sio yenu.hakuna sababu ya kuwa na jumuiya ya watanzania READING inayojitegemea, wakati tunayo TA.
ReplyDeleteABUBAKAR FARAJI ni bomba sana.
Tanzania Association inafanya mavitu kama mkutano wa diaspora nani kafanya?
KWANI MNACHUKIA TANZANIA ASSOCIATION KUWA LONDON?
ReplyDeleteNYINYI MKO READING LAKINI BADO MNAJIITA CCM LONDON.
LONDON NDIO JIJI NA UBALOZI UKO LONDON,HEATHROW MLIPOSHUKA IKO LONDON, JEE READING NI JIJI AU KIJIJI?HAMUWEZI KUSHINDANA NA LONDON,READING NI KULEA WAZEE TU HAKUNA ISSUE NYINGINE AU KUBEBA MABOKSI-TESCO.
wewe anon unaesema TA inafanya mavitu halafu unatupa mfano mmoja tu? ni miaka miwili tangu TA kuanzishwa kwa hivyo hebu tupe mifano mitano basi! hint usichanganye TA na majukumu ya Ubalozi katika kuitangaza tanzania.
ReplyDeleteNani kaandaliwa kuongoza kuwa mwenyekiti TA?
ReplyDeletejee nyinyi mnafungua jumuiya hii ya reading ndio majibu kwa TA? ina maana mmefungua huko reading kwa vile TA imejikita London?
ccm ilikuwa London lakini mmeipeleka Reading nani analalamika?katibu na mwenyekiti na wajumbe wote wa ccm wanatoka Reading,
lakini Tanzania Association ina wajumbe na viongozi toka mikoa yote.mwenyekiti Abubakar Faraji anatoka London wakati katibu mkuu wa jumuiya ambaye ndio mtendaji mkuu wa jumuiya Bwana Lusingu anatoka Reading, mnataka usawa gani zaidi ya huo? katibu wa TA anatoka reading badala ya kumuunga mkono mnaanzisha jumuiya nyingine au kwa vile yeye si mkurya ni mjita.
WATANGANYIKA BWANA OVYOO KAZI USHAMBA TU !
ReplyDeleteTA imefanya mambo mengi chini ya Faraji kama mna chuki nae kivyenu.mnasema mfanyabiashara mlitaka afanye CARE kama nyinyi watu wa reading?hivi unaweza kufanannisha Reading na London?London ina boroughs 33 yaani reading ni sawa na borough moja tu.cha ajabu hata kusoma mnakuja london huko kuna college moja tu ya ujanja ujanja.mnamuita mtu wa IOM hao kazi yao kuwasaidia overstayers jee hapo reading kuna overstayers ndio maana mnamuita huyu mtalaam?
ReplyDeletenyinyi watu wa reading kila dakika mko London mara mje home Office mara mje kwa solicitors etc mnataka makao makuu ya TA yawe reading,hiyo ccm imelilia iwe huko lakini shughuli zenu mnakimbizia london. hata mkitoka musoma mnapokuja UK ndugu zenu huwa mnawaaga kuwa mnakwenda LONDON hamsemi mnakaa READING kwani ni kijijini.
kwa wasioijua reading ni mji wenye magodown ya maduka yaani watu wa hapo kazi yako kupakia mizigo kwenye malori ya mizigo kwenye hayo magodown. na kina dada kazi yao kubwa ni care kulea wazee wa kizungu.
maofisi yote makubwa yako LONDON yaani serikali ya uingereza ni LONDON.
LONDON ni sawa na Dar-es-salaam na Reading ni nusu ya sumbawanga kwani hata hadhi ya sumbawanga ni kubwa.
Mfano London kuna timu kama chelsea,Fulham,west HAM,ARSENAL,CHALTON ETC HUKO READING KUNA TIMU MOJA NA IKO DARAJA LA KWANZA SIO BARCLAYS.
MICHAEL JACKSON ANAKUJA KUPIGA LONDON 02 MWEZI UJAO.READING HAJAWAHI KWENDA MWANA MUZIKI YEYOTE MAARUFU WALA HATA PAMBANO LA NGUMI HALIJAWAHI KUPELEKWA HUKO KWA VILE HAKUNA KUMBI ZA MAANA,
BORA WATU WANAOISHI MAJIJI KAMA BIRMINGHAM,MANCHESTER N.K
Hizi jumuiya ni upuuzi mtupu, inatosha tu watu kukutana kwa ajili ya misiba na furaha, bila ya kuwekeana majisheria ya majumuiya. Nyinyi mmekwenda nchi ya watu kutafuta maisha sio kuonyeshana nani kiongozi.
ReplyDeleteKila mtu atafute maisha yake kwanza na masuala ya majumuiya hapo mtapokuwa mko sawa kimaisha sio kupotezeana muda sasa.
Mdau.
Former Reading resident.
Habari wote.
ReplyDeleteWatanzania wanakuwa wengi uingereza muda unavyokwenda. Wazo la kuwa na jumuia kubwa ni zuri, lakini wakati huo huo sio mbaya kuwa na nyingine ndogo ndogo kuweza kukidhi mahitaji ya members wa magroup hayo na labda maeneo yao. TAWA wakiwa na mambo yao wanakaa wanaongea wanasaidiana. Reading nao wakiwa na mambo yao local, watakaa wataongea watayamaliza, it is much more effective kuliko kusubiri TA, ambayo inaoonekana watu wanaargue haifanyi kazi in the first place. Katika hali halisi hata London vilevile ni kubwa, watanzania waliopo walijaribu kushiriki (nilienda kikao cha kwanza about two yrs ago) the number of attendees was impressive- a hundred-twu hundred or more, vikao vilivyofata- number ilishuka mno. Kuna mahitaji ya msingi (primary) - Watu wanapenda kujua watapata nini- individually wakiwa member wa jumuia, kwa mfano Nikifiwa nitapata members wengine kuniona, kunichangia na vitu kama hivyo- Sidhani kama TA inakupa uhakika wowote kwa vitu kama hivi. Suala la kujumuika na kupati (sijui siku ya uhuru) ni kitu kizuri lakini hili ni hitaji la nyongeza- secondary, its leisure actually- nafikili TA inakupa hakika ya vitu kama hivi. Waache watu waanzishe local jumuia, after all kama hatujashikaman kwa maana aya TA, basi sio mbaya kuimarisha local and regional jumuias ili tuweze kujenga TA baadae.
Joune- Aristotle.
kama READING wanafanya CARE na TESCO na wa London wanafanya nini?
ReplyDeleteMake naona Mzee mzima kataja O2, Hathrow, Michael Jackson, hajasema hilo linamnufaisha vipi?
kwa Anon aliyesema Kongozi mpaka awe mkuria ndipo wa Reading waridhike, ni upupu mtupu. Huyo aliyeitisha mkutano(Mgirire) na mwenyekiti wa CCM kabila moja na Lusingu,ina maana watanzania ndio muhimu. story za Mkuria, Mjita, au Mzenj Pure ni upupu. TA hata hawasemi unakuwa mwanachama kivipi hata website yao.
zaidi kuwa na jumuia nyingi kama Lewsham, Barking, Hammersmith, Islington, Edgeware hapana tatizo, si watanzania? TA ingejumuisha hizo jumuia ndogo za nje ya London(vijini) na hizo za London.
TA ina fanya mambo mengi ya misiba na wagonjwa sema watu wanachuki binafsi na Abuu Faraji.Abuu anatumia www.tzuk.com yake kuwaunganisha watanzania na hata kutangaza habari zenu watu wa reading.lakini bado mnampiga majungu.hakuna anayewazuia kuanzisha kila siku jumuiya mpya ila msemo unabaki pale pale umoja ni nguvu.
ReplyDeletemtake msitake Abuu kafnaya mengi akiwa na TA yake.
mlikuwa wapi nyinyi wana Reading kufungua majumuiya mengine kama sio mwanzo mzuri wa Abubakar Faraji na timu yake ya TA.
ni tabia ya binadamu kila mwenzako akiwa kiongozi wako unaona hafai hadi uwe wewe.
kama TA haifanyi chochite kwenye misiba nyinyi Diaspora na reading yote mmemsaidiaje kijana Elyas ALIYEFARIKI NORTHAMPTON?
sikilizeni wimbo wa twanga pepeta unaosema chuki binafsi haifai.
Jumatatu ujumbe wa Rais Karume unakuja London sio Reading.
ReplyDeleteutakuwa kwa siku nne zote watakuwa London. last week waziri mkuu alikuwa London hakuwa reading.
naona kazi za Care na kubeba box zimewapagawisha.Abubakar faraji anawapa nafasi kwenye website yake mjitangaze bado mnamchukia?basi tangazeni kwenye website yenu www.nifahamishe.
kwahiyo Maina ni chairman ccm,migire unaanzisha jumuiya hii uwe chairman na lusingu ni katibu wa TA nyie wote musoma lakini bado mnanung'unika na ABUBAKAR FARAJ?
ndio maana CCM UK imekuwa na mambo ya ajabu ajabu kwani maina hana ujuzi wowote zaidi ya kimbelembele.
London ni kama nchi ya mtakuja hakuna njia lazima mje tu.basi fanyeni mpango balozi auhamishe ubalozi aulete reading ili mfurahi zaidi, inaonekana mnaumia na vinauli vyenu mnavyotumia kwenda london kwenye mikutano.mnajikaza kisabuni.
WATANZANIA WENZANGU, HII NI HABARI NJEMA.
ReplyDeleteMNAKARIBISHWA KWENYE MKUTANO ILI MUELEZWE PAMOJA NA MAMBO MENGINE, UTARATIBU WA KUOMBA JKN SCHOLASHIP EDINGBURG UNIVERSITY.
TOENI KASHFA MTAKAVYO (SABABU NYIE NI MA-EXPERTS), LAKINI HUO UJUMBE MUHIMU WA MKUTANO USIWAPITE..!!
BY THE WAY: JOHN LUSINGU (KATIBU WA TA) HAJATOKEA MARA.
Watanzania Taarifa kuhusu scholarship ya Mwalimu Nyerere pitieni www.scholarships.ed.ac.uk au simu yao ni 00441316514070.
ReplyDeleteunatakuwa uwe na first class au upper second.
uwe unaishi Tanzania sio reading.
utalipiwa tuition fees,pamoja na tiketi ya kutoka Tanzania na kurudi na pounds elfu kumi za matumizi kwa mwaka mmoja ni kwa watakaosoma masters tu.
mwisho wa maombi ni tarehe moja april lakini uwe tayari una admission.
au pitieni website ya chuo cha Edinburgh ambayo ni www.ed.ac.uk hakuna haja ya kupoteza muda wa kwenda kwenye vikao wakati chuo hakijasema kama watu wapitie kwa agent yeyote.tena wale walipo UK hawatakiwi kuomba anatakiwa mtu aliye Tanzania.
Tunashukuru kwa msaada wa website nimepata taarifa zote za scholarship ya Mwalimu Nyerere nimempa taarifa mdogo wangu ajaribu bahati yake.
ReplyDeletemichuzi tunakushukuru kwani bila blog yako na mdau aliyeweka wazi website ya chuo sisi tulio mbali na reading tusingejua.
pia michuzi weka tangazo kubwa jipya likisema scholarship ya mwalimu Nyerere edinburgh university.
halafu unaweka link ya webiste yao ili wengi wajue www.ed.ac.uk
Watu wa reading waliwahi kumwambia balozi aende kwenye kampuni ya computer walipopewa computers zaidi ya miaka mbili kwa kusema wanazipeleka Tanzania matokeo yake wakazipeleka Musoma zote.
ReplyDeleteyaani balozi hakujua kama jamaa wanatumia mgongo wa nchi kwa maslahi ya mkoa wao tena kabila moja tu.
taasisi hiyo walikuwa wakijiita wafumbuzi charity.
kitendo cha watu hawa kuikataa TANZANIA ASSOCIATION maana yake wanamkataaa balozi kwani ndiye aliyefanya juhudi kuanzisha umoja huu wa watanzania.
sasa na wao kujianzishia jumuiya nyingine badala ya kumuunga mkono balozi sio uungwana.
hatumtendei haki balozi wetu.
tulikuwa wapi kuanzisha hizi jumuiya za kupingana nae huko nyuma?