Kwa mara ya kwanza Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Japan inawaletea sherehe ya kukata na shoka huko CHIBA kwa ajili kuwakaribisha wanachama wapya wa Jumuiya kutoka Chiba na maeneo ya jirani. Jumuiya itatumia nafasi hiyo kujitangaza na kutoa maelezo na taarifa mbalimbali kwa watanzania ambao bado hawajajiunga. Dj wako Pembe al-maarufu DJ ZEE atawakilisha kama kawaida yake. Taarifa ya ukumbi na mambo mengine ni kama ifuatavyo:-
SIKU: Ijumaa ya terehe 13/3/ 2009
MUDA: Kuanzia saa tatu usiku mpaka majogoo
UKUMBI: Uptown 125, karibu na kituo cha treni cha Funabashi (JR soubu line)
KIINGILIO: Yen 2000 unapata na kinywaji kimoja
Jumuiya inapenda kuwakaribisha watanzania wote wa maeneo ya KANTO na Japan pamoja na marafiki zao, njoo tucheze lingala, bongo flavor na zilizopendwa.
Kwa taarifa zaidi na jinsi ya kufika ukumbini tafadhali wasiliana na wafuatao:-
1. Ukumbini : 047-425-0071
2. Mr. Hassan: 080-6548-7078
3. Mr. Yusuph : 080-2064-6573
4. Mr. Pembe: 080- 3458-8786
==================================================
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...