
Habari Mh Balozi na Mkuu wa wilaya ya kule nanihii karibu na wazo hill.
Kwa heshima na taazima kwa wadau wote nina swali la kizushi kama picha hapo juu inavyojieleza.
Katika pita pita zangu duniani nimegundua kwamba njia za reli/railways zote zilivyojengwa kuna kokoto kibao kuzunguka hizo Reli sasa nauliza ni kwa nini zisingewekewa mchanga ama rami na badala yake zimewekwa kokoto?? Natanguliza shukrani maana kuuliza si ujinga pia mimi physics yangu shuleni was not reachable.
Mdau College Park,
Maryland (USA)
Small area low pressure, ingekuwa mchanga/lami na uzito wa train wangekuwa na kazi ya kunyoosha kila siku baada ya kudidimia,
ReplyDeleteits all i got!
Wataalamu wanaweka Kokoto kwa sababu mbalimbali-(i)Kokoto ni bei nafuu kuliko zege (ii)Kokoto zinarahisisha maji ya mvua kupenya ardhini bila ya kudhuru njia za reli (iii)Wakati wa joto kali,vyuma hivyo huwa vinatanuka na vinaweza kusababisha zege kupasuka pasuka ambapo ghalamu ya metengenezo ni ya juu sana. (iv)Ukijenga kwenye mchanga, mvua ikinyesha utakuta reli yote imehamia upande mwingine ambapo gari moshi aliwezi pita.
ReplyDeleteKwa hayo na mengi zaidi ndio maana wataalamu wanatumia kokoto. Kumbuka rami inafaa lakini bei mbaya sana.
Nafikiri nimesaidia!
-ZERO-!!
Mdau kwa kifupi ni kwamba kokoto ndio zina nguvu ya kubeba treni.
ReplyDeletelami (sio "rami") itatitia.
Mchanga huna hata haja ya kuuliza.
Kokoto zinatumika kama shock absorberz. Zisipowepo, ardhi hutetemeka sana, na kama inapita karibu na nyumba, zinaweza kubomoka na kutengeneza nyufa kwenye kuta au ardhi yenyewe.
ReplyDeleteIngwe.
KAKA MI NAFIKIRI WAO WALIOGUNDUA HIYO RELI KUNA WALICHOFIKIRIA MPAKA WAKAAAMUA KUWEKA KOKOTO KULIKO KUWEKA HIYO LAMI UNAYOSEMA WEWE SASA MDAU WANGU HIYO RELI UNAYOIONA IMEWEKWA KOKOTO KWASABABU TU TRENI INAPOPITA ZILE KOKOTO ZINAKUWA KAMA ZINAZUWIA MTIKISIKO KWA ASILIMIA FULANI KULIKO KUWEKA MCHANGA AMBAO USINGEWEZA KUSTAMILI KWA KAZI HIYO SAWA KAKA ANGU........
ReplyDeletekuna jamaa yangu mmoja alifanya kazi kwa wazungu, akasema wazungu ni wachawi, so ile kokoto ni zindiko tu, kwani ndo reli haichimbiwi chini bali huegeshwa tu katika kokoto. na hivyo kokoto zinakuwa kama shock absober.
ReplyDeletesijui kama alinidang'anya.
Hilo swali inabidi mashaka & Co wajibu maana hapa mimi nilikuwa nashangaa why kwa nini??
ReplyDeleteMambo ya Physics ya O na A level nimesahau kidogo,nimeanza kuzeeka lakini ni masuala ya Expansion and contraction ya hayo mataruma.Yakichemka yana/expand,so kokoto ni nzuri kuliko lami.Lami itayabana yasitanuke Utajibiwa vizuri na wanaokumbuka,No cheating in science
ReplyDeleteNice question...
ReplyDeletehapa sasa mnatuchanganya kabisa sasa ile reli kama inaexpand wakati wa joto mbona treni huwa inafit kwenye hio reli iwe joto au baridi?
ReplyDeleteMkuu wa Wilaya ya Nanihii, hili sio swali la kizushi..ebo.
ReplyDeletehi jameni
ReplyDeletemashaka na huyo co wake wa huko London Dr Shayo siyo engineers. Hapa kwa kweli utakuwa umewaonea. Nafikiri ungerusha hiyo kombora kwa wataalamu wetu wa pale kitivu cha uhandisi mlimani dar.
Ingekuwa jambo la maana umwambie mashaka au huyo co wake Dr Shayo wajadili ile hotuba na mazungumzo ya IMF na mtizamo wa madhara ya mtikisiko wa uchumi wa dunia na madhara yake yaliyofanyika dar hapo ningekuelewa ndugu, ila hili la reli kwa kweli umekosea
Mbona kwenye underground trains au subway wasemavyo unyamwezini hakuna kokoto?
ReplyDeletemdau swali tamu sana hili! wanatumia kokoto kuweka kwenye reli ili mtu akigongwa na treni aumie sana then wamsingizie yeye ndio kaligonga treni si unajuwa wazungu wazushi? ni hiyo tu ndio sababu kwa sababu wangeweka rami au mchanga mtu akigongwa angekuwa haumii sana
ReplyDeletetunasema kiswahili lugha ya taifa halafu watu wanaandika kizushi kabisa
ReplyDeletetaazima badala ya taadhima
rami badala ya lami
ghalamu badala ya gharama
aliwezi badala ya haliwezi
jamani jamani mbona mnatuharibia lugha yetu?
ReplyDeleteSi kweli kuwa mchanga hautumiki kubeba reli. Kwa hakika ni kuwa kokoto ama mchanga vyote hutumika, huenda tu wewe umekuwa na bahati ya kuona kokoto pekee.Kazi ya kokoto au mchanga ni kuhamisha uzito wa treni kwenda katika msingi, kama wengine walivyosema "shock absorber".
ReplyDeleteKwa maelezo zaidi ya nini kinaendelea soma hapa:
http://science.howstuffworks.com/train2.htm
- Ballast
ReplyDelete- It helps in draining the rain water easily off the track.
- It prevents capillary rise of surface water to track due to large voids.
- It helps prevent weed growth on track.
- It gives some elasticity to track structure.
- Loose nature of ballast helps easy maintenance and adjustment of track levels.
- It protects the form of top surface of formation.
These are scientific reasons. Tanzanian Engineer, Texas
mbona kwenye reli za Tram ni lami tupo? Hamna kokoto.
ReplyDeletehttp://www.lightrailnow.org/images/or2-lrt-tram-strres-curve-20040327c_n-z-adam.jpg
[IMG]http://www.lightrailnow.org/images/or2-lrt-tram-strres-curve-20040327c_n-z-adam.jpg[/IMG]
Reli zote, iwe ya mizigo (heavy rail), ya mijini (light rail, transit, people movers, trolleys) zinafuata uhandisi unaofanana, bidhaa za ujenzi zinaweza kutofautiona kwa sababu zifuatazo.
ReplyDeleteKokoto zinatumika kama msingi unaunaowena kustahimili uzito bila kudidimia na usioathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa kwa kipindi kirefu.
Misingi ya reli, barabara, majengo, n.k. inaweza kujengwa kwa kokoto, zege, vyuma ama mbao (piles), nk. Chaguo la mjenzi litategemea upatikanaji wa bidhaa, gharama, ubora, lengo la ujenzi, na ufundi ama teknolojia itakayotumika.
Kwa mantiki hiyo, mchanga na lami sio chaguo bora kwa reli za maana. Mchanga hauwezi kuhimili upepo au maji. Lami ina uhai mfupi (miaka 15 mpaka 20). Kwa reli ndogo saaana zinazotumika kwa nadra na kwa matumizi ya kujifurahisha, kama ile ya pale Dar uwanja wa sabasaba, sio lazima viwango vyake vya ubora vilingane na vile vya reli za matumizi ya kutegemewa kama reli za mizigo ama usafiri.
Lami inaweza kuwekwa juu ya kokoto pale reli inapokatisha barabara ama inapokwenda sambamba ndani ya barabara za magari.
Mwenye wazo tofauti, nikosoe ili nijifunze.
Siku njema wadau.
Hata kama sababu SI sahihi zinazotolewa humu, bado inaonyesha Mna Akili ndg zangu maana nyingi zinameki Sensi.
ReplyDeletehata kwenye subway kuna kokoto mkuu, ila kama kokoto zinasaidia kutanuka na kusinyaa kwa chuma mie naona kama kwenye reli ya chini ya aridhi(tube)hakuna joto la kusababisha chuma kutanuka, sababu hakuna jua la kuchoma ile reli kule chini.mie nadhani zinasaidia kuzuia nyasi zisiote na zikaziba njia ya tren. ndo maana hata reli ya kwenda kigoma na mwanza toka dar hakuna mtu wa kufyeka majani sababu kokoto zipo milele na milele.
ReplyDeleteKwa wale wanaosema reli za chini ya ardhi hazina kokoto (kama ni kweli) inawezekana, kwani kitaalamu tetemeko la ardhi hutoa madhara/mitikisiko mikubwa kwenye surface kuliko ndani ya ardhi,Japo tetemeko huanzia chini ya ardhi.
ReplyDeleteKwa maana hiyo, treni ya chini ya ardhi huwa haitoi mitikisiko ya ardhi mikubwa ukilinganisha na kama ingekua kwenye surface.Ardhi hu-absorb mitikisiko.
Ingwe.
1.mchanga - hautumiki kwa ajili kama ni upepo mkali mchanga unaweza kupeperusha, pila magugu na vitu vingine vinaweza kuota kwenye reli na kufanya gharama za kuyatoa kua kubwa.
ReplyDelete2. lami - inafaa, na inatumika kwa wale mliofika ng'ambo mtakua mmeona city train, ukiweka kokoto kwenye reli za mjini magari yakipita yatatapakaza kokoto zote.
3. lami ina tanuka na kusinyaa kama chuma lakini katika joto tofauti.
3. lami ni bei mbaya sana na inahitaji ukarabati wa mara kwa mara ndio maana kokoto zinafaa
wewe uliyesema subway hakuna kokoto kakuambia nani???
ReplyDeletekokote zipo sana tu.
Tram hakuna kokoto kwani wengi wetu tunajua zinapita mijini sasa kama wakiweka mikokoto mijini sijui itakuaje...
ila subway\metro kokoto sana tu.
Bwana naona mnanichanganya tuuuuuuuuuu. sielewi lipi jibu
ReplyDeletemdau netherlands
kokoto ni silaha kama abiria wakivamiwa na majambazi.. ndo hivyo tena. ni mawe tu!
ReplyDeleteHILI SI SWALI LA KIZUSHI,NAMI NIME ELIMIKA.
ReplyDeletewe acha ushamba hivi yiho pic ulipewa na mtu? Maana kama ni wewe ulichukua hiyo ungeweza jua kuwa hapo hakuna kokoto kuna mbao zilizokobolewa hapo mjinga sana wewe.
ReplyDeletemuosha kinywa anon wa March 22, 5:54 ni kiboko!..Sijui ndo jazba yenyewe, hizo mbao ziko wapi? na zikikobolewa zafanya pumba, ama dona, au?..matusi meeengii, mbele kiza!!!- UZENG
ReplyDeleteMhashimiwa Muuliza Swali,
ReplyDeleteJibu alilolitoa mhandisi kutoka Texas lina karibia sana na ukweli .. kokoto kwa jina la kitaalamu ballast linafanya kazi kama godoro kwenye kitanda cha mwanadamu. zile kokoto zinawekwa kwa vipimo maalumu kama sijasahau ni za inchi 2 mpaka 3. Zinawekwa kwenye tuta kwa uwiano wa 1 kwa 1.5 kwa uwiano huo mtawanyiko wa nguvu zitokanazo na garimoshi inapopita juu ya reli ni mzuri kiasi kwamba ile sehemu ambapo kokoto inakutana na mchanga mgandamizo si mkubwa sana .. na kwa uwiano ule ni kwamba garimoshi ikikanyaga sehemu zile kokoto zinabonyea kama unavyoweza kubonyeza godoro. Naomba nitoe mfano wa treni, kichwa kinaweza kuwa na uzito wa tani 120 (88 Class Diesel Hydraulic system from Kruppe) uzito huo unatawanywa kwenye matairi ya 16 ya chuma ni uzito mkubwa sana. hivyo kokoto inautawanya uzito huko kama dogoro linavyotawanya uzito wa mlalaji. hata hivyo basi adui mkubwa wa kokoto ni mchana na vumbi. vumbi linafanya kokoto ziteleze na hivyo kufanya treni kugonga gonga kama gari lililoingia kwenye mashimo. Kutatua tatizo kama hilo kuna mitambo inaitwa ballast cleaners ambayo kazi yake ni kutoa kokoto kwenye reli kuzisafisha na kuzirudishia upya. Kutitia kwa tuta la reli (settlement) ni jambo ambalo haliepukiki nayo inaweza kusababisha treni kugonga ikiwa inapita. kuhakikisha kuwa kokoto zimekaa vizuri huwa zinashindiliwa kwa mashine za mkono (mfano wa mashine hiyo Pionjar, ambayo nimebahatika kuitumia) au kwa kutumia mashine kubwa zitembeazo kwenye reli (Tamping Machine, ambayo nimebahatika kuitumia katika reli ya TAZARA nilipofanya kazi kati ya stesheni ya kidunda, fuga, kisaki mpaka lumango).
wasalaam,
Mdau Tandale kwa Mtogole
Nakubaliana na wale waliosema kokoto zinasaidia 'ku absorb' uzito na kulinda reli na mazingira yake.
ReplyDeleteKuhusu 'tube' na 'tram' na 'DLR' kwa wale walioko UK.. ni kuwa hizo zote ziko kwenye category ya 'light railways' na zinatumika kwa kubeba abiria tu na kwamba uzito zinaobeba sio mkubwa kiasi kile.. ingawa nazo huwa na kokote baadhi ya sehemu.
Hizi reli zingine ni kwa ajili ya uzito mzito kwani treni za mizigo mizito huwa zinapita. Nadhani hii nyongeza imesaidia
mimi napita kila siku toka greenbelt to dc by train lakini sijaona kokoto kabisa hizo zote mbao hata hapo zinaonekana. Reli za bongo ndo zina kokoto siyo huku MD
ReplyDeleteWakandarasi wameiga umbo la binadamu kama vile JUU YA MDOMO KUNA MUSTACHI ndio maana wanaweka KOKOTO,
ReplyDeleteKokoto,zege,rami,mchanga yote kitu kimoja sawa na wali,mchele,mpunga,pilau,rice ni majina tu yanabadilika lakini yote ni kitu kimoja sijui nini kinachowachanganya.
kuna jamaa kasema Chuma kinatanuka wakati wa joto, Mwingine akauliza mbona treni linafit [hahah) JIBU na tren UTANUKA ndio maana linafit maana vyote ni VYUMA. vinatanuka vyote na vinasinyaa vyote.
Nywele,ndevu,mustachi,gaden,nyusi,kope na.........
Kwa wote mliochangia, mmejitahidi.
ReplyDeleteWee Mhandisi wa Texas, asante kwa kunikumbusha. Mzee wa Tandale pia nasema asante kwa majibu yako mazuri. Ila kwenye swali la baadhi ya reli hazina kokoto naona wengi mmepotea.
Kwanza nianze na kusema, nchi kama German, wana line za Trams ambazo ukiwa mbali huzioni kwani wamepanda nyasi na kuacha vimistari vya reli tu kwani reli huharibu taswira ya mji. Hivyo, mhandisi wa Texas, nyasi wakati mwingine zahitajika karibu na reli.
Pili nije kwenye reli isiyo na kokoto. Kama walivyosea wakali wengine huko juu kuwa kokoto ni kama GODORO, basi kila reli inahitaji GODORO. Hata hizi zina magodoro yake. Kuna kitu kama MIPIRA/SPONGE ambazo huwekwa chini ya reli, chini ya mataluma na chini ya barabara nzima. Na pia huweka pembeni mwa reli. Mliopo mijini basi angalieni sehemu reli inakwenda pamoja na barabara, unaweza kuiona mipira hiyo kwenye tundu ilipo reli. Hii husaidia kwa mfano wakati wa msongamano wa magari, mabasi, zima moto na ambulance zinaweza kupita juu.
Kuhusu eti Metro/tubes kutokuweka kokoto kwa kuwa ziko chini-si kweli. Hata huko chini mtikisiko na kelele ni kubwa kama hawatatumia hii mipira/sponge.
Sponge/mipira ni aghali sana ndiyo maana nje ya mji hawaziweki. Miji mingi ni mpaka watu wapige kelele wee na kupeleka kesi mahakamani ndipo huwa zinanunuliwa na kuwekwa. Wasipopiga, basi sisi twasema hewala. Mwenye swali zaidi aulize ntampa more datas.
Mdau, Sikonge wa Sikonge.
CQ,
ReplyDeleteSasa mzee unamwaga Kifaransa hapa tutakuelewa? Wengine tukiweka Kinyamwezi hapa patakuwa hapatoshi. Tanzania ni Kiswahili na Kisukuma, ahh English.
Juu ya hivi vitu, ulitakiwa kujua maana huko France ndiyo wenyewe. Train lao linalotamba la TGV (soma TE-ZE-VE) ndilo linashikilia speed kubwa duniani na linauzwa sana dunia hii. Ili kufikia hiyo speed, ilibidi wajenge kipande cha reli maalumu, kuweka walinzi na kutafuta siku hali ya hewa nzuri na ndipo wakalispeed hilo TGV. Hivyo reli nzuri ni kitu muhimu kwa ili train liwe na speed kubwa.
Labda mambo yakabadilika kwa hili train linalotumia sumaku. Hili train huwa hata HALIKANYAGI RELI.
Nafikiri ukipitia kwenye YUOTUBE, waweza kupata more datas and videos. Sometimes check in DISCOVERY PROGRAMS.
Mdau Sikonge (Fundi Mchundo).
Its me again,
ReplyDeleteKwa watakaotaka kuona basi ingieni hapa kwenye hizi WWW.
http://www.roadstothefuture.com/Balt_Light_Rail.html
http://www.maximizingprogress.org/2009/01/greenways-grass-lined-metro-rail.html
Technician, Sikonge of Sikonge.
hili hi jibu la kutoka kwa mwanafunzi wa shule ya msingi:zinawekwa kokoto ili kuzuia ule udongo au mchanga chini yake kwanza usipeperushwe na upepo na hivyo kusababisha mashimo au mabondebonde;pili,kuruhusu maji ya mvua yapenye kirahisi kwenda ardhini bila kutuwama na kusababisha tope;tatu,kuzuia mmong'onyoko wa ardhi;nne,hata kama vyuma vya reli vitatanuka kidogo kwa joto la jua kokoto ni rahisi kumeza mtikisiko huo bila kusababisha mpasuko wa nyufa katika ardhi;tano,kokoto zinapatikana kirahisi zaidi huko maporini reli inakopita kuliko Lami au mbadala wake;kokoto zinasaidia kuongeza msuguano au kupunguza utelezi hata kwa abiria na hivyo kupunguza ajali za abiria kuanguka au kuteleza waingiapo na washukapo toka relini;sita,matumizi ya kokoto yanapunguza sana gharama za matengenezo ya njia ya reli;sababu nyingine mia mbili wiki ijayo......
ReplyDelete