Michuzi habari kazi,
Naomba kwa hisani yako niruhusu niweke jambo hiliili wadau waweze kulijadili kwaundani na Mchanganuo mzuri zaidi.Nikwamba mimi nilikuwepo ughaibuni kwa kipindi cha zaidi ya miakamiwili,Kwasasa nimerudi bongo kwa muda kuja kusalimia.
Jambo mojalililonifanya niweke mada hii hapa,ni mtazamo wa wenzangu niliowaachahuku nyumbani tz,Kwakuwa walitaraji nitakapo kuja nitakuja naMagari,fedha,navitu vingi vya thamani kwakuwa"tu nimetoka ulaya nasikuja na vitu hivyo.
Sasa kinachotokea nimekuwa napokea kashfambalimbali kama jana nikiwa maeneo fulani ya Magomeni Kagera Jamaa zanguwalianzisha mada isiyo rasmi kuhusu (WABEBA MABOX) na (WALA VUMBI) kwa maana ya watu wafanyao kazi zisizo rasmi wa Ughaibuni na Walewafanyaokazi zisizorasmi wa Tz.
Kwamba ninani zaidi.Binafsi hali halisi ya hukoughaibuni naijua na hali halisi niliyo ikuta hapa nyumbani ninayomkononi. Mimi kama mtoamada nimeona halihapa Tz Kwa wale wasio na kazirasmi Hapafai hata kidogo kwa kweli ndugu zangu mliopo huko jitahidinisana tena sana hali huku si njema kama mdhaniavyo au msikiavyo.
Maisha ni magumu sana. Hospitali hazina Madawa ya uhakika,Shule halikadhalikahazina madawati, waalimu wa siku hizi ni wa Vodafasta anasoma mwakammojajuukwa juu anatafutiwa shule,hizo shule huku zinazoitwa za Internationaljapo sielewi zinaitwa hivyo kwa vigezo vipi gharama zipo juu sana wadogozangu hawataweza kusoma ktk shule hizi,hizo za serikali ndiyo hizo mlizosikia waalimu wanakuja shule saa nne tena wamelewa wanafundisha nusu saahao wanaondoka wanasubiri kufundisha twishen,Mgao wa umeme huo waja.
Natamani muda wangu wa kurudi ughaibuni ukaribie mapema.
wadau natumaini mmenielewa cha msingi hapa nani zaidi kati ya
WABEBA MABOX na WALA VUMBI???
Asanteni,
mbeba box mwenzenu likizoni
(MUGISHA)
Hello Mdau;
ReplyDeleteNadhani tofauti ya mbeba box na mla vumbi ni akili yako tu. Kama ukiwa na akili timamu na malengo sahihi haijalishi unabeba box or unakula vumbi maisha yako yatakuwa swafi tu.
Mimi nilikuwa ughaibuni pia for my studies na nimewaona wabeba mabox wengi ambao kama wangethubutu kurudi kula vumbi huenda wangefanikiwa hadi sasa ukilinganisha na maisha wanayoishi kwani hata box lenyewe hawana hakika ya lini na wapi watabeba. Hasa nazungumzia wabeba box wenye elimu na ujuzi wao, yaani engineer mtu anaosha vyombo!!! nasema mtu kama huyu akija bongo anachance mzuri yakuwa succesful.
Kuhusu madawa,umeme, nk dogo nadhani kumbuka mkataa kwao ni mtumwa, ni vitu ambavyo kama ndivyo vinavyokuweka huko ujuwe haviji siku moja, taratibu bongo inakuwa. ukitembea na ukibuni chakufanya bongo utafanikiwa na usihofu.
G7
sasa unataka watu wachangie nini na wewe ushatoa mawazo yako, kwamba ndo watakubadilisha mawazo.usiwadanganye watu kuja huku na kama unaomba mida iishe urudi ni kwa sababu ulifika huko umechoka kama ulivyotoka huku.unafurahia kuwa mtumwa huku, sawa kila kitu serikali imeweka, lakini wewe unadhamana gani huku zaidi ya kuishi kama ombaomba.
ReplyDeletemaisha ya ulaya kwa waafrika wasio ana elimu kama wewe, sio mazuri hata kidogo, ukiacha kuonekana kama nyani, na zaidi ni mesheni tauni. mmeharibu hata mtazamo wa wengine ,kwani baada ya kubeba box mnauza bangi.
huyo mla vumbi bongo ni bora zaidi mara mia kuluko wewe usiyejua kesho iko vipi huku ulaya.
bora masikini kwao, kuliko tajiri mtumwa.
pole sana kwa elimu yako mbovu ,japo umeponda ya bongo, sioni umejifunza nini huku.
na wazungu hawatakupa nafasi ya kujifunza.
wamependeza,,asa uyo mwamunyange ana jicho linaitaaa mweeeee!!
ReplyDeletegwanda la wanajeshi sii mchezo,ila mmh!!hii kazi
Watanzania acheni thana potovu ya kwamba kila anayeishi ulaya atarudi Tanzania na magari na fedha za kuwanywesha bia, hayo mambo yalikua ya zamani watu walikua wanaenda ulaya na fedha za serikali wanalipwa perdim na marupurupu kibao, hao ndio walikua na hela ya kuchezea kununua magari na kuwanywesha bia. Bora wanaobeba maboksi wana uhakika wa matibabu mazuri na watoto wao wanasoma shule za kueleweka na ndio wanakuja kuchukua kazi hapo bongo kiulaini. Wala vumbi acheni kashfa wapendeni ndugu zenu hata kama wanabeba maboksi.
ReplyDeleteNi vigumu sana kujadili mada hii kwa hoja. Kila sehemu ina uzuri na ubaya wake na kila mtu ana vigezo vyake vya uzuri au ubaya. Umetaja changamoto tulizonazo nyumbani lakini kwa hao waliopo nyumbani unadhani suala la kulala masaa manne kwa siku baada ya kubeba maboksi siku nzima watalionaje? Vipi hali ya mashaka kwamba ukikosea hesabu za pesa kidogo umeuawa, hakuna cha jirani wala nani atakayekuokoa? Hospitali zetu sawa hazina dawa lakini vipi kwa mbeba maboksi asiye na bima ya afya? Hata daktari anaweza asimwone wakati anataka kufa. Mbeba maboksi ana uwezo wa kusomesha watoto kwenye shule bora za ughaibuni?
ReplyDeleteBinafsi nadhani kwa mtu ambaye mambo yake yamenyooka bongo mambo yake ni mazuri kuliko mtu ambaye mambo yake yamenyooka ughaibuni kwa sababu yuko nyumbani. Lakini ukiwa mbeba maboksi umepigika ughaibuni inawezekana kabisa bora mla vumbi nyumbani. Lakini kama nilivyosema mwanzo, sidhani kama maoni ya suala hili ni hoja. Ni hisia tu.
Acha dharau we bwa mdogo. hilo vumbi ndilo limekutoa sasa unaponda. Ubaya wenu mkitoka kidogo mkirudi mnaponda saaana. Ukikuta mtu anachakarika na vumbi mnamuona bwege. kwani kubeba box sifa si sawa tu na muendesha guta hapa town tofauti we uko ughaibuni yeye yuko nyumbani wote mtaji ni nguvu. hizo box kama zingekuwa hapa tungebeba tu. Maslahi ndugu. Kumbuka kila mkataa kwao ni mtumwa. Anyway econimic criss ndio hiyo sijui hizo box mtazibeba wapi? Nimeshangazwa na kusema kalikizo kaishe mapema uondoke kwani lazima kaishe si uondoke tu utuondolee kero. sasa huko unafanya nini kama huna tofauti na wala vumbi. mnatawaza wazungu huko mnachangachanga mnakuja kutishia huku. sie wala vumbi tunakula na nduguzetu kaja leo unampa 500 anasepa kesho mwingine anakula chakula sasa we anakula nani vyako? Acha dharau
ReplyDeleteget your life man, ushaona pande zote mbili, sasa chuja nafaka mwenyewe.
ReplyDeleteHali hiyo unayozungumza tangu uhuru ipo, hakuna elimu, afya, uongozi nk sasa kuna mtu mwenye akili timamu asilolijua hilo???
Unapozungumzia wabeba box unamaanisha wageni waliokuja Ughaibuni kipindi kifupi kilichopita kama wewe wa miaka miwili au sisi wakongwe wa ngwe kadhaa, binafsi naona fika kwamba waliopo huku ughaibuni na wanachezea nafasi waliyokuwa nayo ndio wa kuwashangaa, manaake umasikini wanaujua, na namba ya matatizo ya huko walipotoka wanaijua, bado tu hawako tayari kujikwamua kielimu na uchumi ili kuwasaidia ndugu zao waliobaki nyuma, watu wengi hawana dira ya kutosha na kuamua maamuzi ya maana, mfano kwenda shule na kujiendeleza kielimu na biashara, kazi kutumwa na wazungu kama watumwa wa karne ya 19, zamani tulikuwa tunakuja ulaya kwa mijeledi, sasa hivi tunaomba vibali, lakini bado ni vile vile tu, tukifika tunaendelea kuwa watumwa (wachache na sio wote), wengi wana uwezo wa kusoma kwa home student fees lakini wanazembea, wengi wananafasi za kusafiri nchi mbali mbali na kugundua nafasi tofauti za kujikwamua kiuchumi lakini hawafanyi hivyo.. hao ndio wa kuwashangaa na pengine kuwalaumu, kuhusu wanaofanya kazi zisizo rasmi na ni wageni katika nchi mbali mbali walizofika, sio tatizo kama wana focus na wanachofanya, namaanisha kama wanatumwa kidhalili kwa kipindi kifupi cha kutafuta elimu ili waweze kuinuka hapo baadae hakuna shaka, lakini kama Ndugu zangu hamna dira mtaishia viwandani na kazi za kudhalilika mpaka mnakufa, na swala zima lililowaleta ugaibunu kutafuta maisha bora litaishia kuwa ndoto, watu hawana hata SAVINGS ZA MAANA, ukitokea msiba ghafla watu wanatazamana kama mjusi kabanwa na mlango. na kila siku wanaenda kazini, lakini hela hazionekani, na hawagundui tu kwamba tatizo ni mishahara midogo wanayopata kwa kutokuwa na elimu ya kutosha, mfano hapa UK GP analipwa mshahara unaofika mpaka pound elf themanini kwa mwaka, barister analipwa pound tisini kwa saa, hela ambayo mbeba box anapata kwa masaa 16 ya kazi..., na bado tu watu hatuna changamoto ya kutokea mbio shule na kufika pale walipoika waAsia kama wahindi na wapakistani.. ITS TIME TO Wake UP GUYS NA KUGUNDUA NAFASI ZA DHAHABU TULIZONAZO.
Kuna watu wanalipiwa maelfu ya pesa kusomeshwa na wazazi wao,lakini wengine wana uwezo wa kusoma bure kwa vibali vya kuishi nchi hizi vinavyowaruhusu na bado wanazembea...
All the best ,na endelezeni redio mbao kwamba bongo Tambarare.... wakati umeme hakuna, hospitali hovyo, barabara mzozo, maji kitendawili, elimu mtego nk.
Utasikia ooh ntafanya biashara, ukimuuliza mtu business plan unayo anakutolea macho, anadhani biashara ni kuuza na kununua tu..!
NB: Wabongo wengi tunajidanganya kwamba sisi wakubwa kiumri kwahiyo shule sio jambo letu... natoa mfano mdogo tu, ukisoma degree ya aerospace engineering ambayo ni miaka mitatu tu, unamaliza na kulipwa mshahara wa zaidi ya pound elf 40 kwa mwaka, ambazo ni sawa na karibu milioni mia za kibongo....(sorry guys kama exchange rate imekaa vibaya) na ukifanya kazi kwa minimum wage au pund sita kwa saa unapata mshahara wa pound 13 kwa mwaka, mishahara yako ya miaka minne bila kulipa bili yoyote wala mahitaji ya maisha kwa miaka minne ndio huyu bwana aliyesoma uhandisi wa ndege anapata kwa mwaka, sasa tofauti ya kukaa darasani miaka nitatu inakusaidia nini wewe ambaye umepindwa kwa muda wote huo na bado huna kitu..???
Mdau UK.
Ku-compare wasio na kazi rasmi huko bongo na wasio na kazi rasmi huku abroad....ni kuwaonea hao wabongo, maana hata hao wenye kazi zao zinazoeleweka huko bongo wana maisha ya wasiwasi...mpiga box kama ana akili anaweza kutengeneza maisha mazuri tu huko nyumbani...maana pesa sio tatizo...nguvu yako tu!
ReplyDeleteMugisha rudi nyumbani Coventry !
ReplyDeletewacha mambo yako hayo ya kuuchuna Bongo !
Salam zake kaka Jeff
Mdau
BROTHER MICHUZI HII USITIE KAPUNI PLEASE!
ReplyDeleteMaisha ni kuhangaika, kujituma na kubahatisha. huwezi ukakaa tu kila lako likafanikiwa. sio lazima uishi nje ya tanzania au ndani ya tanzania ndio utafanikiwa kimaisha. Kufanikiwa na maisha hakuna definition moja, ila ni ya mtu binafsi. kila mmoja anaona kwa njia moja au nyengine kuwa amefanikiwa au hakufanikiwa. kuna anaeona kuwa na familia na nyumba au kibanda chake na kazi ya halali hana madeni ni mafanikio, pia wanaona kuwa bila ya magari, kujulikana, kunywa vilabuni, kuvaa pamba kali na kuwa na biashara kubwa kubwa ndio mafanikio. kuna wanaoona kuwa nilyoyataja hapo juu ni kuwa mafanikio na ni lazima wayapate hata kwa njia zisizo za halali na kuna wanaona kuwa ni mafanikio lakini sio lazima ufanye yasio ya halali ni kupitisha jitihada tu. Pia kuna ambao definition yao kubwa ya mafanikio ni kurudi nyumbani na kujionyesha kwa kila aina atakaa nje ya nchi mwkaa mzima anajituma usiku na mchana, kula na kulala ni kwa kubana matumizi ilimradi tu july atuwe bongo, na wapo ambao hadi hufika kuiba, sio katika maduka na mabenki bali hata kwa marafiki zao, na wengine nao hufika kuuza unga almuradi akienda bongo aonyeshe kuwa anapesa.
USIJALI WATU WANACHOSEMA, JALI MAISHA YAKO NA MALENGO YAKO. JARIBU KILA NJIA YA HALALI KUFIKIA MALENGO YAKO, USIVUNJIKE MOYO NA WALA USIJALI WANAOKUCHEKA. HAKUNA MJINGA MKUBWA KAMA YULE ANAEKAA TU ASIEFANYE JITIHADA YA KUJINUFAISHA MAISHA ILA KUKAA NA KUWACHEKA WANAOJITAHIDI KUTENGENEZA MAISHA YAO.
Ukibeba boxi una uwezo wa kulipa nyumba, simu, afya, na ka-gari ka kuzungukia. Pia una uwezo wa kujilipia japo part time school. Polisi si waonezi na hamna rushwa. Ukirudi bongo ni sawa na kuweka tone la maji kwenye bahari, hamna unachoongeza wala kupunguza, bongo itaendelea kuwa bongo.
ReplyDeleteWa-vumbi, unaweza hata kukosa mia ya dagaa. Hata daladala ya kupiga debe unaweza kuikosa.
Mbeba box anayesema bongo wanatesa aje basi? we unafikiri hawajui?
ReplyDeleteSasa msiwe na uchungu na ughaibu utafikiri ni nchi ya ukoo wenu, wahimizeni na watu wasiopata kazi nyumbani waje angalau wabebe box.
Box la majuu linalipa zaidi kuliko la bandarini au stendi ya basi.
ReplyDeleteLete box la mtoni.
ReplyDeleteJapo ni kazi ngumu, ukipata nafasi ya kutoka Bongo japo kwa muda toka - hasa kama kazi ufanyazo bongo si za kiprofeshono kivile.
Mwaka uloisha nimepiga kibarua hapa US & A nikakunja $ 40,000 na zaidi kidogo - PESA MFUKONI HIYO. Kabla ya makato ya kodi nilipata 50,000 na kidogo. Hizo si dola haba. Ni wachache nyumbani TZ wanaoweza kutengeneza namba hizo kihalali bila wizi wizi na mikato ya hapa na pale (kwa wafanyakazi)
Mgongo unaniuma mpaka natamani kuachana na box langu ila kwa sasa bado naliendeleza sababu limenijali so far
Kurudi nyumbani sooner or later ni muhimu
ReplyDeleteKwakweli mie huwa siwekagi cmment yangu humu but hii mada imenigusa sana, kwani hivi karibuni nilitaka kumrudisha mwanangu akasome bongo kwa muda then arudi tena USA, yani mama yangu akawa anmtafutia shule hiizo ambazo zinaone kana "classic" kwa mtazamo wa wa "Tz" yani gharama zao ziliniacha hoi, nikamwambia mama cha mwanangu atamalizi highschool huku, japo yeye alikuwa anaoni hizo gharama are ok! yani Feza girls-3,000,000Tsh, Babro girls- 3,500,000Tsh,Heven of peace 8,000$, International school of Tanganyika 14,700$-15,000$...etc. yani gharama za kumsomesha mtoto secondary huko bongo zinalingana na gharama za kusoma college huku USA.Lo bongo wizi mtu!
ReplyDeletehalafu kitu kingine ambacho kimetokea just last week, mtoto wa my best friend's sister, aliugua akiwa shule na ghfla akapoteza fahamu "akazimia"( hiyo shuele ipo maeneo ya Tegeta) eti hao masister badala ya kumkimbiza mtoto hospital, wenyewe wakampigia her uncle iliaje amchukuwe ampeleke hospital!!(wazazi wa mtoto hawaishi dar,)mmh?mtoto amabaye amepoteza fahamu?? yani uncle huyo mpaka alipofika hapo shule mtoto huyo alikuwa bado amezimia na walimu na wanafunzi kibao wamemzunguka, jamani yani hawa watu wabongo wanatreat maisha ya mtu kama kuku!!
Last in 2006 my sister alikuwa mjamzito, na anasumbuliwa na LBP, basi akaugua ghafla usiku, tukamkimbiza hospital ya Agakhani, eti yule nurse baada ya mgonjwa kutowa kipimo cha mkojo achukuwe apeleke kwenye maabara, akatuwambia sisi ( was mimi, mama, her husbund na shemeji yake) mmjoja wenu achukuwe apeleke kwenye maabara!! mh nikashangaa na kuanza kumuuliza huyo nurse, ukowapi usalama wa mgonjwa hapo?? je what abt confidentiality??...etc, but watu wabongo naona wamezowea wanaona hiyo nikwaida coz most of hospital wanafanya hivyo!!
Case nyingine mtoto wa mjomba wangu,binti mkubwa ambaye amebaliza form4, aliugua marelia last yr, then doctor ameend-up kumuover dose, mpaka ame "pooza miguu", kwakweli inaniuma sana, mie nimewaambimbia naenda huko this yr, na nitaakikisha huyo doctor anashtakiwa!
kwakweli bora niwe huku na beba mabox lakini napata basic needs kwa hali ya juu, kuliko bongo!kama mnakumbuka hile case ya Muhimbili kaka aliye fanyiwa surgery ya kichwa badala ya miguu!! wow bongo hapana to me!!
Sishangai Mugisha kwa nini umeishia kubeba box ulaya, maana hata kujieleza hujui! Sasa hii ni mada tujadili au ni maoni unatoa? Hivi unajuwa maana ya kutoa mada watu wajadili? Aaah nihisi kichwa chako kimejaa snow ya ulaya ni si ubongo unaoweza ku analyse mambo!Fanya urudi kwenye stress,giza lisilokwisha usiku mchana na baridi isiyopita, muda wote munaonekana nyuso tu kama Eskimos, rudi ukaoshe mavi mataahira wakizungu, ndo kazi inayokufaa tu,Bongo inawafaa wenye bongo tu, sio mbumbumbu kama wewe...!
ReplyDeleteKwanini utumbo utupwe na wenyewe twalia ndizi...!
Kwa kweli hali ni mbaya nyumbani kwetu hapa kwa wale tusio na shughuli maalum. huo ni ukweli ulio wazi. Pia kwa wabeba box hali ni mbaya sana kwa sasa hivi kutokana na shughuli nyingi za kiuchumi ulaya kua katika hali mbaya sana kwa sasa kutokana na GEC iliyoikumba Dunia kwa sasa. Hata wenye kazi lrasmi huko wanateterka kutokana na uchumi mbovu
ReplyDeleteYote kwa yote ukweli unabaki palepale kwamba nyumbani ni nyumbani. Nashindwa nikae upande gani katika hii mada kutokana na ukweli kwamba hali halisi katika bongo yetu bado ni mbaya sana. Mfumo wetu wa utawala ni mbovu mno uliopotoka na sera ya uwekezaji.
Mfano ukienda Kariakoo eti unakuta Mchina ana fremu anauza viatu kuanzia jumatatu hadi jumapili asubuhi hadi jioni tena analipa kodi ile ile sawa na mtanzania!
hiyo haitoshi Chalinze kuna wananchi wanamashamba kule na kunachama kinakopesha mtaji kwa ajili ya kulimia cha ajabu Tanzania kulivyo na "viongozi bora" kuna wachina wanakopeshwa fedha na chama hikikiki ili kulimia mashamba yao!
Kila unapokwenda unakuta hali ni ile ile kuanzia utalii hadi uagizaji magari ya mitumba unakuta kote wamekama wageni tu huku serikali ikiahidi maisha bors kwa watu wake ,kivipi wakati haitoi upendeleo kwa wananchi wake katiak kazi zisizohitaji utaalamu wa kutisha.
kwa hiyo mdau si ajabu kuona hali hiyo mbaya ndio serikali yetu inavyotawala
imegeuza ile sera ya mwalimu kwamba "siasa ni uchumi" na kua "uchumu ni siasa" kwamba kama huna uchumi mfukoni we si mwanasiasa!
Mdau Sijui kitu
Mweshimiwa ni bora urudi zako huku mapema !!! maisha ni kokote siku hizi angalau nibebe mabox na niweze kusaidia familia nyumbani.. hao wa hapo nyumbani hata kujisaidia wenyewe ni shida!!!hata kama wana kazi nzuri kama ulivyodai!!
ReplyDeletemimi umenishangaza sana kunipa habari hizi kwani wifi yangu huwa ananiambia kua bongo tambalale. mala ulaya na bongo ni sawa tu lami mpaka uchochoroni mara eti hakuna mgao wala nini hiyo ilikuwa zamani. umenichanganya sana ila kama hiyo ndiyo habari uliyotoa ni kweli box ni juu zaidi pia naziombea zibarikiwe.
ReplyDeletemimi nafanya kazi ya kubeba box hapa ughaibuni tatengemewa na ukoo wote huko bongo, na nina ndugu wengi huko bongo wanafanya kazi kubwa sana hawana msaada kwa ndugu yeyote ni wachoyo mpaka mwisho watu wa afrika wasijiringanishe na watuwa ughaibuni kwani afrika ni Dunia ya tatu na ughaibuni ni Dunia ya kwanza naona wanatamani wawe wao .
ReplyDeleteJibu ni moja tu
ReplyDeleteMind Your Own Business (MYOB)
Asikudanganye mtu bora mbeba boksi mara 100,kwani na mimi nilitoka bongo si chini ya wiki 2 zilizopita,alie nacho anacho na kama hunacho si nchi ya kukaa kabisa maana mtu unakata tamaa ya maisha na unaishia kutapeli. Matatizo chungu nzima ingawa watu wa bongo starehe wanazipenda mno.Na wakikujua kuwa umetoka nje basi kila mtu atakuelezea matatizo yake.Juu ya hivyo nyumbani ni kuzuri
ReplyDeleteJamani mbona kitu kiko wazi hapo,mbeba boxi wa ulaya ni bora mara elfu moja ya Mla vumbi wa Bongo, anayebishana na hilo ni mjinga na hakubali kama yeye ni mjinga na hajijui kama ni mjinga.Wangapi wako ulaya wanabeba boxi na wanawasaidia wazee wao na ndugu zao huko bongo?ni nani mla vumbi huko bongo anayeweza kuwasaidia wazee wake kama anavyosaidia mbeba boxi? Huo ni wivu tu wanatuonea gere.Tunajua wabeba boxi wengi sana waliowapelekea na kuwasaidia ndugu zao fedha na mali nyingi tu ili waendeshe biashara huko bongo na walichofanya ni ku-fuck up kila kitu, jamin au hamjui hilo???? Achana nao hao, wewe mbeba boxi wa ulaya una uwezo mpaka wa kwenda bongo na kurudi, muulize huyo mla vumbi wa bongo kama anweza kwenda hapo kenya tu,mavi yake!! Huo ni wivu tu achana nao hao, wanakusema halafu hapo hapo wanakuja kukuomba pesa, au uongo???
ReplyDeleteehe we mbeba box sasa mbona umeishia mada yako katikati mbona huku ulaya hujasimulia cha moto tunachokipata,wewe inaelekea hukusoma na ulivyokuwa huku hukutumia muda kuwaelimisha ndugu zako juu ya huku nahisi ulikuwa unatuma picha ukiwarubuni kuwa umekucha,anyway cha nsingi maisha ni popote,sababu hata huku ulaya shule wewe usifikirie mtoto akiongea kiingereza kaelimika mimi nipo uingereza nimegundua shule nyingi pia licha ya kuwa na vifaa watoto ndio wanaenda kujifunza mambo ya ajabu hadi ugay,ubaguzi unakera sehemu za kazi,na uzembe hospital somehow upo,so usikae ukadanganya watu,eti ulaya kuzuri labda ulaya ya zamani sahivi utachekwa ndugu,bongo ni shida lakini ukiplan maisha na kujituma ni kuzuri kama heaven.na sasa hivi nilivyoona bongo kila kitu kinawezekana ni plan yako tu,subiri urudi ulaya uoshe wazungu mpaka upate fangasi.
ReplyDeleteKuna watu wamepiga box,wamejisomesha, na wameweza kusaidia familia zao. Hapo huwezi kulinganisha na vibarua TZ. Nyumbani kweli matatizo yapo,kulaumu haisaidii,wala kukubaliana na hayo matatizo sio suluhisho. Tuweke siasa kando. Kila mtu awajibike anapoweza, iwe upo Europe, USA, au TZ. Only the strong will survive.
ReplyDeleteNdugu Mugisha mi naona umechanganya mada.
ReplyDeleteMada siku zote ni "Mbeba box wa Ulaya/Marekani na msomi aliyeajiriwa Bongo nani zaidi?"
Ila mbeba box wa Ulaya/Marekani na mla vumbi wa Bongo that has never been an issue... hapo ni wazi kuwa mla vumbi wa Bongo yuko twaaban.
mimi nilikuwa nafanya kazi bandarini karibu miaka 10 huko bongo, pesa niliyo kuwa huisha kabla ya mwezi, na sikuwa mtu wa starehe, baada ya kuja hapa ulaya nina miaka kama 13 hivi nimejenga nyumba moja pia nimenunua shamba kama hekta 300 pesa niliyo tumia sijatapeli au ruswa pia mara nyingi nasaidia ndugu na jamaa. Upande wangu sidharau mtu yeyeto ila inanisikitisha sana kuona mtu anafanya kazi nzito sana na malipo yake hayalingani na kazi, hili ni tatizo tulilo nalo huko nyumbani hatuoneani huruma. Sioni kwanini watu mlio nyumbani au mlio ulaya kuweka malumbano kwani maisha kila mtu anauchaguzi wake.
ReplyDeleteMICHUZI LET ME DROP MY POINTS HERE...!
ReplyDeleteHAKUNA JIPYA HAPA MIMI NILIVYO MALIZA SHULE PALE ST. ANTONY MBAGALA NILIKUWA GINIUS NIKAENDA MUZUMBE UNIVERSITY NIKAWA KICHWA KILA MTU DARASANI ALIKUWA ANA COPY MATERIAL YANGU. THEN I WENT TO CANADA FOR FURTHER STUDIES I LIVED THERE LIKE ANY MBEBA BOX I MEAN WORK IN A STORE AND PAY FOR MY SCHOOL. MANY PEOPLE DON`T KNOW HOW SMART I AM BECAUSE I LIKE TO WRITE IN MY MOTHER TONGUE. OKAY LETS COME TO A POINT. YOU CAN NOT COMPARE LETS SAY CANADA AND BONGO SIMPLY BECAUSE IN CANADA WE WERE PAID HOURLY FOR A STUPID JOB. HOW MANY ENGINEER LETS SAY CAN MAKE 2000 DOLLARS IN TWO WEEKS? ALSO WE DON`T HAVE MANY PLANTS TO FACILITATE ALL THESE ENGINEERS.I BELIEVE MANY OF THE ENGINEER CAN OBTAIN JOBS OVER THERE AND DO WONDERS RATHER THAN COMING HOME. THE ONLY THING WHICH MAKE US WABONGO LOOK BETTER THAN THEM BACK HOME TO SAY THE LEAST IS UFISADI! WE STEAL A LOT OF MONEY FROM OUR POOR COUNTRY.JUST LOOK MY CASE MY SALARY SINCE I CAME BACK FROM CANADA IS 450 US DOLLARS A MONTH. BUT THAT IS NOT ENOUGH TO CARRY ALL THE BILLS AND MAKE SURE MY KIDS AND EXTENDED FAMILY SURVIVE I AM AN ACCOUNTANT BY PROFFESSIONAL BUT YOU FIND OUT THAT SOMEONE WHO CARRY BOX IN CANADA AND AMERICA MAKE SUCH MONEY IN A WEEK WITHOUT OVERTIME!THIS ARGUMENT IS SILLY I WISH I WOULD HAVE GOT VISA AND GO BACK TO CANADA OR ELSE WHERE, LIFE HERE WITH PEOPLE LIKE LIUMBA,YONA, MULAMBA AND MANY YOU NAME THEM MAKE MY LIFE AND MANY LIKE MICHUZI VERY HARD. TO HAVE A GOOD JOB WEARING NECKTIE IS NOTHING IF YOU CAN`T EVEN PAY RENT, NO ELECTRICITY, NO WATER, NO MEDICINE NO PEACE, NO JUSTICE, PEOPLE ARE DYING EVERY DAY WITH NO REASON. I TOO WOULD LIKE TO GO OVERSEAS AND CARRY BOXES SO THAT I CAN HELP MYSELF AND MY EXTENDED FAMILIES WHO HAVE DINIED JUSTICE AND HOPE BY PEOPLE LIKE LIUMBA. FOR THOSE WHO THINK I CAN NOT TALK POINT PLEASE GIVE ME A BREAK I TELL YOU MASHAKA MUZUMBE INAWENYEWE IAM PROUD EDUCATED PERSON BUT LIFE HERE IN YOUR COUNTRY DOESN`T CARE ABOUT PEOPLE LIKE ME. AFRICA IS RICH BUT POOR IN MIND AND HEART. THANK YOU EVERY BODY. MUZUMBE ALUMN PETER NALITOLELA
kwa wale mnaoishi maisha ya mashindano ndo mko bize kuchangia ila mimi naona kila mtu na maisha yake! everybody mind your business
ReplyDeletemimi mwenyewe na masterz hapa tanzania toka mwaka juzi nilipata kazi nzuri kampuni flani nimefanya miaka 2 wakaniloga nikawa nikienda kazini asubuhi nakuta simba ofisini narudi mbio nikitoka nje nawaambia watu wanasema nimechnganyikiwa akiingia mtu mwingine hamuoni huyo simba. Basi nikaamua kutafuta kazi nyingine ndio naifanya mpaka leo lakini kwa ukweli mshahara sio wa halali kabisa ni mdogo sana na majungu mengi juu na ndugu bado wanalilia misaaada kila dakika ulaya kuzuri kama umejipanga! nyumbani ni nyumbani
ReplyDeleteMugisha,
ReplyDeletehayo ndio matatizo ya kukaa ughaibuni huku mnajirusha pasipo kukumbuka kwamba msahau kwao ni mtumwa,na nyumbani ni nyumbani tu.Wenzetu mlikuwa mnaendekeza ma-party kila wikiendi,matumizi makubwa kujirusha kwa sana kumbe nyumbani hamjafanya maandalizi yoyote.Kibaya zaidi wakati mnafanya vurugu za namna hiyo huku ugaibuni,makaratasi yako ovyo.Ndio maana ukipigwa bomba na kurudi bongo mikono mitupu watu wanaishia kukucheka.
Tekla anakusalimu,tunahangaika nae hapa Coventry
huyu jamaa ni anatuambia kuwa maisha ya mtu maskini ulaya ni bora kuliko ya mtu maskini bongo. watu wengi wenye kubeba mabox ulaya ambao wanatoka bongo mara nyingi wanakua na elimu zao nzuri lakini hawakujua kupata kazi nzuri ulaya au north america kama elimu yako ni ya bongo ni vigumu sana. majority ya foreigners huwa wanaishia kufanya kazi kama za ABC (AMERICA BUTTOCKS CLEANING) au BBC (BRITISH BUTTOCKS CLEANING) kwenye nursing homes au wanabeba mabox. hii si afadhali ubaki bongo ukajitafutie shughuli nyingine kuliko kuishia kujidhalilisha. wengine wanasema eti wanapata dollars nyingi lakini kumbuka maisha ya huko ni ghali sana. kitu kingine huko saa zote unadharauliwa wakati bongo unatembea ukiwa unaweka kichwa chako juu. weather ya huko hata usiseme wakati wote ni baridi na watu wanatoka wakati wanakwenda kazini. hii ndio maana wanasema kuwa madaktari wa akili wanaona patients wengi sana wakati wa winter. kabla ujasema maisha ya ulaya ni bora fikiria utakapo zeeka utawachwa ndani peke yako. usisahau kama unakaa kwenye nyumba ni lazima uondoe snow iliyofunika driveway yako. haya yote hayakupati ukiwa bongo. hapa bongo kuna watu wanaishi maisha bora kuliko huko ulaya. tofauti ni kwamba middle class ya bongo ni ndogo lakini we are improving. japokua ninaishi nje ya nchi yetu na nina kazi nzuri BONGO IS ALWAYS THE BEST PLACE FOR ME.
ReplyDeleteKwa mtazamo wangu bora kubeba box ulaya/USA kuliko maisha ya bongo. Maana mshahara wa mtu aliyosoma masters huko bongo hauwezi kulingana na mbeba box wa Ulaya/USA. Kama mtu utatumia bajeti yako vizuri ya mshahara wako wa kubeba box unaweza fanya mambo mazuri huko bongo kuliko mtu aliyokaa kwenye ofisi bongo na kupepewa na kiyoyozi. Mie naona bora mbeba box ulaya kuliko mla vumbi wa bongo.
ReplyDeleteNILISHASEMA, NASEMA TENA NA NITAENDELEA KUSEMA SIKU ZOTE, WATANZANIA WALIOKO NJE(WABEBA BOKSI)WANA UNAFUU KIMAISHA ASILIMIA 99.99, HII NI FACT AMBAYO HATA MBISHANE MPAKA KUKU wAOTE MENO BADO ITAENDELEA KUWA KWELI. MBEBA BOKSI AKILIPWA BAADA YA WIKI MBILI NI SAWA NA MLA VUMBI AKILIPWA BAADA YA MIEZI MIWILI, SASA MNALINGANISHA KITU GANI? BONGO WANA MAGARI NYUMBA ETC LAKINI KULIA KILA SIKU, KUANZIA TIBA, SHULE,UMEME,MAJI, USALAMA ETC. HIVYO BASI USHAURI WANGU NI KUWA VIJANA BONGO MKIPATA NAFASI YA KUONDOKA HUKO ONDOKENI, NCHI IMESHATEKWA NA MAFISADI, HAWAWAJALI WANAKULA JASHO LENU HALAFU BADO MNAWASAGIA WABEBA BOKSI, MBEBA BOKSI ANALIPA TAX NA ANAKULA MATUNDA YAKE, BONGO HII HAIPO, NDIO BONGO NI KWETU LAKINI IMEFIKIA MAHALI KILA MTU AJINAFASI KIVYAKE, UNAENDA PALE AMBAPO UNAWEZA KUNEEMEA, HUWEZI KULINGANISHA MBEBA BOKSI NA MLA VUMBI, MLA VUMBI HANA HOPE HATA KIDOGO, MBEBA BOKSI ANA HOPE YA ELIMU NA AFYA BORA ANGALAU MAISHA YAKE YANA UNAFUU ESPECIALLY KWA WATOTO WAO, DAWA BONGO FEKI KUTOKA INDIA, CHINA ETC, ZIMESHAEXPIRE SASA MNAENDELEA KUJADILI KITU GANI. KUJA TUTAKUJA KUSALIMIA NA KUSAIDIA NDUGU, LAKINI KILA MTU AANGALIE USALAMA WAKE. DEFINITION YA SUCCESS KWA MLA VUMBI NI KUWA NA GARI NA NYUMBA, LAKINI PETROLI BEI YAKE MNAIWEZA? NAULI ZA DALADALA ZENYEWE SHIDA SASA MNALINGANISHA KITU GANI HAPA JAMANI? HAYA ENDELEENI MAANA NINAMENGI NAOGOPA KUMALIZA NAFASI KWA AJILI YA WENGINE.
ReplyDelete-mdau Toronto-
Anoni wa March 05,2009 2:07, hata kama Mada ingekuwa Mbeba boksi vs Msomi aliyeajiriwa bongo, bado mbeba boksi angekuwa juu kwa vigezo vile vile,uchumi, matibabu, elimu etc, kwani hujasoma hizo comments hapo juu. Mtoto wa mbeba boksi ambaye anasoma shule ya kawaida viwango vyake bado haviwezi kulinganishwa hata na hizo wanazoita international school bongo, mshahara wa huyo msomi wa mwisho wa mwezi ni sawa na mshahara wa mbeba boksi wa wiki moja,tena hapa nazungumzia wabeba boksi ambao hawana elimu, wale wenye degree zao kama nursing,education,technology etc ndio huwaguswi kabisa. Nurse huku analipwa 26-35dollars per hour, huyo msomi wa bongo analipwa hivyo? kwa hiyo bado mada imeelemewa na wabeba boksi upende usipende. Matibabu ya mbeba boksi ni ya kuaminika, msomi bongo anataka kwenda na yeye nje kutafuta hayo hayo matibabu sasa huoni unajicontradict mwenyewe! bodo wala vumbi wana safari ndefu, unless waache roho zao za wivu na waombe wenzao wabeba boksi wawasaidie walau kuja huku. Ni hayo tu.
ReplyDeleteMpenda boksi US.
we anonymoush wa March 04 2009,11:34 kutokana na maelezo yako inaonekana wewe ni wale wazembe waliokuja ulaya wakajibwatika tu, hutaki kujiendeleza(kwasababu huna mapepa),umechelewa kimaisha sasa unatapatapa na kusema eti elimu huku zinafundisha mambo mengi ya ajabu pia, hayo mambo yapo kila mahali na yanakuwa promoted na media, lakini hakuna mzazi huku atakaye fumbia macho issue kama hizo, labda nyie huko kwenu uswahilini UK, lakini huku Canada mjomba hayo hayapo, ukitaka kusafisha wazee matako umetaka mwenyewe, watu wanaenda shule na wanafanya kazi nzuri tu, huna haja ya kwenda kusoma degree, hapa courses hata ndogo ndogo zinalipa kishenzi, by the way nchi ambayo haijaathirika kiuchumi katika kumi bora Canada ni number 1, sasa usipotoshe watu na uswahili wenu wa huko UK, eti bongo ukiplan vizuri utafaidi, hata huku ukiplan vizuri utafaidi tena kishenzi. Kama umelosti usiwajaze wenzio ujinga wewe!!
ReplyDeleteShida ya wabongo,wala vumbi, wanaletewa hela na wabeba boksi halafu wanaziponda hovyo, si wazazi mpaka wake kwa waume, halafu mnataka kumlinganisha mbeba boksi na mla vumbi, mbeba boksi anatuma hela nyumbani, msomi wa bongo hata kusaidia tu nyumbani shida, anamtafuta jamaa yake ambae ni mbeba boksi amsaidie, ujinga mtupu!!
ReplyDeleteI am sorry to say this but the guy who wrote that peace is total ignorant. Unajua haya ndio matatizo ya watu walikwenda UK wakaona kama wamepatia maisha.
ReplyDeleteNimekaa Ulaya for over a dacade now, lakini hata siku mmoja sijawai kufananisha Ulaya na Tanzania. How in the world unafananisha nchi zilizoanzishwa mwaka 1700 na nchi ya 1961? That is total insane.... Ohhh sijui hospital mbaya, sasa nani akafanye mabadiliko wakati wewe mwenyewe una akili ya kitumwa?
I am so sick and tired of this slave mentality. Please spare your time for something productive. Shwain.
Mchumi wa Texas
Ndugu zangu, nyumbani ni nyumbani tu. Kwa wale wasio na kazi rasmi warudishwa hapa kwa kesi za madawa ya kulevya na wengine maiti zao zinakaa zaidi ya mwezi ndio zifike bongo, tena misiba mingine inatokea kwenye mazingira ya kutatanisha. Hata kwa wasomi hali zinatofautiana. Hakuna general rule namsapoti anayesema mind your own business, lakini pia angalieni dini, wengi huko mmejisahau, Sadaka ina samani kubwa nyumbani kuliko nje, au hamtoi hata sadaka? Je zaka? sitaki kusengenya ningetaja majina ya watu wenye umri mkubwa nje kiasi kwamba huku nyumbani wameanza kusahaulika. kama kuna mafanikio kwanini hamwatembelei jamaa zenu? kuna aibu umezipata mnaficha au ni wachoyo? jiulize nafsi yako sasa hivi Je nikifa huku ughaibuni nina savings ya kutosha kupeleka huu mwili bongo? achani kunyonyana, tafuta kwa akili hakipatikani timua urudi,mtu hafukuzwi nyumbani na wabongo ni wakarimu, si unajua.
ReplyDeleteMI NAONA KILA MTU AFUATILIE MAMBO YAKE HUU WOTE HAPA NI UPUUZI TU KAMA MI NI JAMBAZI NA MAKE MONEY KIVYANGU KAMA WE NI MWALIMU KIVYAKO TUHESHIMIANE TU
ReplyDeletewatu wamekua wakitukana wabeba ma-boxi wa uk, us na kwingineko...
ReplyDeleteKAZI AMBAZO ZINAFANA NA BOX TZ NI
TBL, DAHACO(SWISS PORT), BANDARINI, COCA COLA, UCHAPAJI WA MAGAZETI, WAFANYAKAZI WA HOTELI ZOTE, RECEPTIONIST WOTE, VIWANDANI WOTE CASHIER...
ASILIMIA 95 YA KAZI TZ NI ZA KUBEBA BOX
MTU ANYEBEBA BOX NI UN-SKILLED WORKER, KAZI NYINGI TZ SIO SKILLED JOB.
WA TZ MNAWEZA MKAWA MNAJITUKANA WENYEWE
Kwa kweli wadau wanaosema kila mtu ana sababu zake tofauti za kutaka kukaa nje, kurudi nyumbani au kutotaka kwenda nje kuishi wamesema vema.
ReplyDeleteBinafsi, niko nje miaka kumi sasa. Nimeondoka Tanzania sio kwa sababu nilikuwa na matatizo ya kifedha. Nimetoka katika familia yenye uwezo. Ni uwezo uliotokana na kuchapa kazi sio kuibia umma. Nilisoma International school miaka 10 mpaka IB2 (Form Six), nikaenda Marekani kusoma miaka saba (B.A and MBA) na hata siku mmoja sijafikiria kukaa Marekani kwa kuwa maisha ya nyumbani yalikuwa sio ya shida kabisa.
Nimeondoka Tanzania kwa kuwa serikali inawakandamiza wafanyabiashara. Nikaamua kuuza biashara yangu na kuwaachisha kazi Watanzania 170 kwa kuwa kila siku TRA, askari, ofisa ya afya na kadhalika wanataka hongo. Ukitoka nje huwa unaona jinsi tulivyo nyuma na wenzetu. Serikali ilikuwa ishukuru wasomi tumerudi hata kama hakuna umeme, maji safi wala tiba bora. Lakini kila siku ilikuwa ni kero. Kama sio TRA basi jambazi anakusubiri getini. Sijataka kuishi kama walivyoishi wazazi wangu, niliona jinsi ilivyowaharibia afya yao kwa mawazo kila siku, mara mbili walishapokonywa biashara yao na Nyerere na Sokoine bila sababu yoyote zaidi ya kutajirika kwa kuchapa kazi kuliko majirani zao.
Kwa kifupi nimeondoka sio kwa kuwa nilikuwa na shida ya fedha bali nataka kuishi bila ya kero. Lakini rafiki zangu wamerudi Tanzania na wanapenda kuishi huko na biashara zao. Mimi quality ya maisha ni bora kuliko fedha. Sasa, badala ya kuingiza elfu ishirini dola kwa mwezi, naingiza elfu nne, lakini maish yangu ni bora zaidi. Nitaishi maisha marefu kutokana na matibabu bora na haki yangu kama binadamu kulindwa. Hii ni sababu yangu binafsi, na kama nilivyosema, wenzangu wamerudi na wanastarehe huko. Kila mtu aangalie mwenyewe wapi kuzuri katika kuendeleza maisha yake.
da nyie wote naona mnapoteza muda hapa tu ukweli ni kwamba ulaya kabambe. mimi niko hapa uk kwa muda wa miaka 11 sasa nimefika kama student nimesomeshwa mpaka ni kamliza,na wakati huohuo nilikuwa na fanya kazi kwenye viwanda enzi zile mshahara kama unafanya kwenye factory za wabagradesh akijua we mwanafunzi anakupa £3 kwa saa. sasa imagine nikipiga masaa yangu kumi kila siku baada ya college naondoka na £180 hata na zaidi kwa wiki.ninaongelea miaka ya tisini ndio mshahara wenyewe sasa imagine, nika maliza shule kwa ulaini kabisa visa ikaisha,ikabini ni minye hapahapa kimya. Nikapata kazi kwa wazee na maannisha kazi ya care( nursing home). huko kazi nyororo kabisa sio kila care wazee hajiwezi mshahara £9 kwa saa weekend double, hapo siende college wala nini nakazi enzi hizo zilikuwa za kumwaga ,sasa huko kulikuwa na kitu kinaitwa sleep in, yani wewe unalala tu asubuhi ukiamka £25 mshahara plus kazi ulioifanya during the day. mpo. haya maisha yaka change miaka 2002 kukawa na madeal ya kujiripua haya nika jiwasha (mkimbizi)Uukijilipua unapewa kwa kujistili na fedha wa pewa pia plus pesa unayo pata kwa vijibibi.baada ya mambo kuwa shwari nikapata kibali cha kuishi moja kwa moja, sababu visa iliisha nilikuwa siwezi kwenda bongo sasa nina stay nikapata travel document hapo ndio wale walavumbi waliokuwana sema arudi yule ndio kesha endekeza mabox hata ndugu zake hawajali walinyamaza maana kwa nilishuka na pesa tosha ya kuwapa hata walioko vijijini, jenga nyumba chap chap yakwangu mpaka wazazi wangu enzi hizo ujenzi ulikuwa lahisi sana viwanja nilinunua kama sina akili nzuri sasa walavumbi hao hao wakaingi na staili mpya this time nabeba unga.Pesa zote hizo katowa wapi, wamesha saahau nilikuwa na beba mabox basi mimi hatakuaga si kuaga mbio nikarudi kuendeleza mabox sasa ikafika wakati ina bidi niombe uraia nikapata na passport ya uk so this time nina familia na nyumba ni nayo na kazi nzuri ya social worker na bongo naenda nitakavyo uk nina huwakika wa maisha watoto wakoshule bomba na wala silipi mama wazazi nyumbani wana hakika na maisha yao kama sio kwangu kwawajukuu. ninachosubiri sasa ni pension yangu ndio nirudi bong0 milionea,sasa muda huo watasema jamaa aishiwi huyo.sasa mimibinafsi naona ulaya tambarare kama utakuwa mvumilivu napia mbeba mabox akiumwa uzeeni anarudi uk kwa matibabu sababu ni raia sasa mlavumbi hiyo ndio faida ya kubeba mabox nyie kaeni tu mle vumbi mkisubiri mwisho wa mwezi mkale kitimoto.
ReplyDeleteMheshimiwa Michuzi, naomba nichangie maoni yangu kuhusu suala hili la Wabeba mabox na Wala vumbi.
ReplyDeleteNashukuru umetoa maoni yako kuhusu wala vumbi na wabeba mabox. Cha msingi ni akili ya mtu kutengeneza maisha yake. Kupata pesa kila mmoja anaweza. Kutumia pesa kila mmoja hahitaji kujifunza. Ila moja ni kwa lugha ya wenyewe "how to manage your money" ndo shida ya wengi.
Nikiwa mmoja wapo niliye na mang'amuzi ya kuishi Tanzania na nchi za ughaibuni, baada ya kuhitimu na kuwa na uzoefu mkubwa wa fani yangu toka ughaibuni, nikaamua niajiriwe bongo, mshahara niliopangiwa kwa mwezi ni sawa na pato ninalotengeneza ughaibuni kwa siku mbili. Kwa vile sikutupa jongoo na mti wake, nikaona bora nirudi ughaibuni kwani mabox yaweza nisaidia hata kupata kipanya (Hiace) iwe ndo mchango wangu kwa walavumbi wanaohaha kukimbiza dadada hata kuingilia madirishani kama kule Mbagala, Gongolamboto n.k.
Cha msingi wengi tunakasumba huko nyumbani tz. Walioendelea wanatafuta kazi inayompatia tija nzuri na wala si kazi tu kwa vile itanifanya nionekane Officer wakati pato lenyewe nazidiwa na mkokota mkokoteni ambaye anaweza kwa siku kusaka 15,000 kwa siku wakati huko ofisini unaambulia chini ya 5,000 kwa siku.
Huyo mbeba mabox unayemsema huko FEDEX, UPS nk. kwa saa analipwa $12 - $15, na ndiye anayekuletea vipanya unavyokimbiza kudandia kupitia dirishani.
Jamani kwetu ndo kuzuri ila tu huku tupo na akili ya kutafuta cha kutuenzi na kusaidia kuinua uchumi wa nchi yetu. Tuwe watu wenye mtazamo mpana na wa mbali, yaani kiona mbali.
Jamaa kwa saa anaishi ughaibuni na anakuja huko nyumbani kwa likizo eti afike na magari na vikorombwezo vingi inajenga dhana gani?
Ninunue gari ya kwenda nayo bongo nitakayotumia wiki moja au tatu za likizo yangu. hiyo ni kwaajili ya kwenda kutesa bongo au nini?
Kila la kheri Watanzania. Naipenda nchi yangu na watu wake.
Tuungane tuheshimiane ili tujenge nchi yetu kwa ustaarabu na hapo wengi wetu tutastaarabika kama walivyo staarabika tuwaonao kama wametutangulia kimaendeleo
Na Shotipangu Njelemela
NILIKUWA ULAYAKIKAZI KWA MIAKA NANE. MSHAHARA WANGU ULIKUWA DOLA 3,000 KWA MWEZI.
ReplyDeleteMATUMIZI YALIKUWA HIVI
NYUMBA DOLA 800
BASI DOLA 150
KULA 300
UMEME 100
KUFUA 100
MENGINEYO 300
KWA HIYO DOLA 1700 ZINATUMIKA NABAKIWA NA DOLA 1,300 KAMA AKIBA, HUKU SIJAVAA SIJANUNUA MAHITAJI MENGINE, WACHA PESA ZA KUWATUMIA WAZAZI WANGU.
NIMERUDI HAPA TANZANIA MWAKAJANA NIMEPATA KAZI YA SHILINGI MILIONI 2 NAISHI KAMA MFALME. ULAYA HAKUAFAI. MAISHA NI JINSI UNAVYOYACHUKULIA KWANI KUWNA WATANZANIA WALIOPO NJE NA WAPO HOHEHAHE. KUNA WABONGO WALIOPO HAPAHAPA,WANAISHI PARADISE. LIFE IS WHAT YOU MAKE IT
PETER NALITOLELA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEE
ReplyDeleteHATA KAMA WAKIKUPONDA MIE NAKUFAGILIAA....
WEWE NI KM MASHAKA,INAELEKEA MMENONA SANA...MNANG'AAAAAA..NDIO MAANA MASENENE IN ENLISH MABALALEZZZZZZZZZZZ WANAWAFATENI..!!
ILA UACHE KUMFATA MASHAKA!!!!!!UNAWEZA KUPATA MAUSPOON BILA KUTUMIA JINA LA MASHAKA!..ALAA!!!!KAMA HAPO JUU UMEONGEA VIZUUUUUUUUURI...UKAMALIZIA KWA KUTAJA JINA LA MASHAKA! EBOHH???HUJIAMINI AU???..YAANI MPK USIKIKE NI LAZIMA KUMKANYAGIA MASHAKA????...NDUGU BADILIKA!!!
(kigulunyembe)
Maniga wa kibongo kelele nyingi nauli si unayo Nigga? Wee rudi kiwanja pia Karibu huku Marekani ucheki zali.Mzee Mugi endeleza kujituma na kuwa ukienda Bongo mara kwa mara kuna siku utaibuka na deal na wanaokucheka kokote kule unakohangaika na maisha yako watafunga midomo yao..kulaleki. Mi nakwambaia utaona mwenyewe weka bidii na sala Mungu si Athumani.
ReplyDeleteUsiibe. Usiue. Usiseme Uongo. Achana na wezi wa EPA. Achana na majungu. Time is money.
Life is what YOU Make it. Life is anywhere. Sums it all.
watanzania mlioko nje ya nchi fanyeni kazi zenu kwa bidii, pelekeni pesa zenu nyumbani ili mjitayarishe kwa maisha ya baadae. kumbukeni maisha ya ujana ni mafupi na maisha ya uzee ulaya yanatisha. make sure utakapo staafu una nyumba nzuri. gari na pesa za kuishi vizuri bongo na ukiwa mgonjwa una pesa za kutibiwa nje ya nchi. fanya nyumbani kuwe kama florida kule wazee wa canada na usa wanakwenda kuishi wakati wakizeeka. uzuri wa bongo utaweza kupata watu wa kukusaidia ndani ya nyumba. mimi wazazi wangu ni madaktari huku north amerika. walisoma wakati amerika ilikua inaruhusu madaktari kutoka nje kuja kuendeleza masomo yao huku. kila wakati wazee wangu wanazungumza kuwa hawataki kustaafu huku. hii si kwasababu ya pesa lakini wanaona quality ya maisha east africa ni bora kuliko hapa.
ReplyDeleteWEWE ANON WA 4:31 NIMEONA MAELEZO YAKO INGAWA YANATIA SHAKA SANA.OKAY KAMA ULIKUWA UNABAKIWA NA $1300.00 AMBAZO NI SAWA NA SHILINGI MILLIONI 1.7 BAADA YA KUTOA NAULI,CHAKULA NA KILA KITU UNACHOFANYA HUKU ULAYA/MAREKANI.NA UKALINGANISHA NA TANZANIA KUWA UNAPATA MILLIONI 2.0 ILA KWA TANZANIA MBONA HUKUTAJA GHARAMA ZA CHAKULA,KUFUA,GHARAMA ZA NYUMBA NA USAFIRI? NINA IMANI UKITOA HIZO GHARAMA ZA KUISHI HUKO TANZANIA AMBAZO BADO NI KUBWA UTABAKIWA NA LAKI NANE AU TISA TU.JAMANI TUSEME UKWELI HIZO KAZI ZA KULIPWA MILLIONI MBILI HUKO TANZANIA ZIPO WAPI? MBONA KUNA NDUGU WENGI WAMEMALIZA MASTERS HAPA USA NA ENGLAND MPAKA LEO WANATAFUTA KAZI NA KUNA WENGINE PAMOJA NA KUWA NA MASTERS ANALIPWA 1.1 MILLIONI KWA MWEZI.KWA USHAURI WANGU LOLOTE LINAWEZEKANA POPOTE,KUNA WAKO NYUMBANI NI VIZURI WAKAWEPO HUKO NA KUNA WENGINE WAKO HAPA USA NA EUROPE NA WAMESHAWEKA MIZIZI NI VIZURI KILA MTU AKAENDELEA KIVYAKE VYAKE MSIWAKATISHE TAMAA WATU.HAYA MAMBO NI YA KIBINAFSI KUAMUA KUKAA UGHAIBUNI AU NYUMBANI LA MSINGI KILA MTU ANAVYOJISIKIA NA ANA FURAHA NA MAISHA YAKE.HIVYO SIKUONA UMUHIMU SANA WA KUWEKA HII DEBATE KWA SABABU INAINGILIA PERSONAL LIFE YA MTU YAANI KUMWAMULIA MTU WHICH IS WHICH AND WHAT IS WHAT.NINGEONA KAMA BUSARA ZAIDI KAMA TUNGEJADILI MAMBO MUHIMU ZAIDI YA HILI KAMA VILE SAKATA LA RADA,TUI-PRESSURE SERIKALI KUWAKAMATA WALA RUSHWA KAMA VIJISENTI,JINSI YA KUTOKOMEZA RUSHWA,KUJADILI JINSI YA KUNYANYUA UCHUMI,EDUCATION NA MENGINEYO MENGI AMBAYO YANATOKEA KATIKA MAISHA YA WATANZANIA KILA SIKU.
ReplyDeleteKweli life ni kokote, na jinsi mtu unavochukulia life. Kuna watu wako tayari kulala njaa kuliko kusimangiwa chakula. Ni sawa na mwingine kubeba box huku ana elimu ya kutosha wakati angewezarudi bongo apate kazi ya kawaida na aishi kawaida.
ReplyDeleteWhat I hate about ughaibuni, unless unaishi, Florida au Miami, west ni bariiiidiiiii. Halafu duh, life ni balaa.
Binafsi niko huku since 2005 ila I cant wait muda wangu uishe nirudi bongo. najua nitalipwa kawaida, ila nikikaa kwenye basi hakuna anaekumbatia pochi yake, always summer na, kuna uwezekano wa kupanda cheo. I am sure nikiwa dar nitafikia dreams zangu.
By the way, hivi nani atakaeifanya bongo bomba kama sio sisi??
Poleni saaaaana...bora mimi niliyesoma na nina elimu yangu safi naenjey maisha hapa bongo kwa kupata kazi serikalini....NAWASHUKURU SANA BABA na MAMA yangu...bebeni mabox na kuleni vumbi kwa shida zenu...POLENI SANA
ReplyDeleteNYIE MNAKAO JIVUNIA KUBEBA MABOX NA KUPATA $5000 TUNZENI HIZO PESA ZENU KWA KUNUNUA NYUMBA BONGO. MSIPOFANYA HIVYO JUENI MKIFIKIA MIAKA 40-50 HIZO KAZI HAZITAKUWEKO KWA WATU KAMA NYIE. ANGALIENI WENZENU WA KENYA NA UGANDA WANAVYO WEKEZA KWAO. WATU KAMA WAINDI NA WACHINES WALIPENDA SANA KWEO NDIO WAKAFIKA WALIPO. HIZO NUKLIA TECHNOLOGY ZAO ZILILETWA NA WATU WAO WALIOKUWA WANAISHI WEST. KWASABABU HII MSIKAE HAPO MNADHARAU NCHI ZENU. FIKIRIENI MTASAIDIAJE NCHI YENU. SIO VIBAYA KWENDA NJE YA NCHI KUTAFUTA MAISHA LAKINI KUMBUKENI NYUMBANI.
ReplyDeletekufua dola 100
ReplyDeleteje mashine ya kufulia itakua bei gani??
nguo ana nunua kila mwisho wa mwezi.
uwezi ukafananisha dunia ya kwanza na ya tatu.
mbona hiyo milioni mbili hajaipigia mahesabu...
sassa hivi anawapa hela wazazi wake
ughaibuni babu siyo wabongo tu bali mnaigeria, muiran , watu wote duniani wanakimbilia US au UK, there must be something good there!
ReplyDeleteSisi acha tule vumbi tu hapa...jamaa wakishuka tupeanaga taarifa kama hatuna akiri nzuri.. pia wamewiva kwa afya..wala siamini kama wanabebaga maboksi.
UNACHEZA WEWE MICHUZI ANAKULA VUMBI UNAWEZA KUJIFANANISHA NAE,EMBU ACHA KELELE WEWE.
ReplyDeleteUnaweza kujiajiri mwenyewe hata ughaibuni. Unaweza kuajiri watu wengine na wazungu hata ughaibuni.Kazi za kuvuja jasho zipo na kazi za kutumia akili zipo. Watu ni wavivu kufanya mitihani inayotakiwa ili wapande ngazi. Degree peke yake hazitoshi hata ukiwa nazo nne. Lazima ujue networking with people and how to express yourself. Resume nzuri,confidence, work experience nzuri na shule nzuri vinalipa sana ni ujanja wako na bahati zako. Follow your heart/talents.
ReplyDeleteAnything is possible. Hardowk and constancy in purpose is important. Show your competence and be able to prove yourself.
Msifikirie sana kazi za kuajiriwa ajiriwa na wazungu, fikirieni kuwaajiri wao na pia kuwashinda wao. Umoja ni nguvu. Kama wee ni Engineer fikiria kuwa na kiwanda badala ya kuridhika mno na $120,000kwa mwaka. Kama wee ni laywer au accountant fikiria kuwa na ofisi yako na wateja wako. Chochote kinawezekana kokote unapoishi. Ukombozi huanza kifikra na matendo.
Hii inaonyesha ni jinsi gani wala vumbi walivyochanganyikiwa kiasi kwamba wanashindwa hata kujielewa,kaka yangu ni mbeba box wa siku nyingi na ameweza kutusaidia karibu familia nzima na yeye mwenyewe kujenga nyumba ya nguvu sio kibanda, na kaka mwingine yupo bongo na kazi ya maana anashindwa hata kununua uwanja, na sio kama hapendi ila anashindwa kutokana na hali halisi na kwa kuwa yeye si mwizi ni mlokole ndio kabisa.
ReplyDeleteHili jambo haliitaji elimu ya hali ya juu kuweza kulinyambua ila tunaliona gumu sababu wengi tunalinyambua kwa mitazamo binafsi kuliko mtazamo wa jumla na ndio maana watanzania tulio wengi tutabaki kuwa masikini, ikiwa unashindwa kujua vipimo vya maendeleo ni jinsi gani utaweza kuendelea, wala vumbi wangapi ambao wanaweza kumudu kodi ya nyumba, usafiri, matibabu ada kwa watoto na wao wenyewe, milo mitatu bila rushwa, magendo au wizi?
ReplyDelete