Mheshimiwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipotembelea mjini London jana na kufanya Mkutano wa Viongozi wa Jumuiambalimbali za Watanzania nchini Uingereza. shoto ni balozi Mwanaidi Maajar na kulia ni mwenyekiti wa jumuiya ya watanzania waishio uingereza, abubakar faraji
akiwa na wanachama wa jumuiya
kila mtu alifurahi kumuona mh. waziri mkuu
akiwa na viongozi wa tawi la ccm london
akiwa na wanajumuiya





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Hivi mbona naona hao wanajuiya waliokwenda kuonana na waziri mkuu, ndio hao hao viongozi wa CCM, UK???Inakuaje hii?Alikwenda kuonana na wana-CCM au watanzania walioko pale?Au hao viongozi wa jumuiya ya watanzania kwa kuwa wengi wao ndio hao hao wa CCM huko UK basi hawakuona umuhimu wa kuwaita watu wengine ambao sio wana CCM, au wa upinzani kama wapo.

    Hizi siasa ktk jumuiya za watu wa ughaibuni zikomeshwe otherwise zitaongeza uhasama na chuki tu, kisa itikadi tofauti za vyama.

    MDAU-Marekani

    ReplyDelete
  2. Wewe mdau wa Marekani. Nakubaliana na wewe kwa upande mmoj kuwa wana CCM ndo walikuwa wengi hapo. Lakini hujajiuliza ni kwa nini watanania wengine hawakuja? Wana Jumuia wote walialikwa , mpaka wapemba, naomba uitajie ni Jumuia gani hapa Uingereza haikualikwa. Sasa ndugu yangu, si unajua Methali ya unaweza kumpeleka punda mpaka mtoni lakini huwezi kumlazimisha kunywa maji.
    Waziri Mkuu amekuja UK kuwasalimu Watanzania wote, sasa kama Wana CCM wana mwamko zaidi, unalalamika nini?? Haikuwa ni meeting ya wana CCM, lakini Wana CCM ndo wenye upeo wa juu na wamehamasika zaidi kuliko hao WANAOJIITA Watanzania wameshindwa kuja kumuona Waziri Mkuu wao kwa visingizio vya shift. Wakienda wengine mnatukana…Hebu amkeni, ndo mana hamfiki popote nyie, mtaishia kutukana kila siku.
    CCM Hoyee

    ReplyDelete
  3. mdau-marekani maneno yako msumari, sisi wengine hata hatukujuwa kama mheshimiwa atakuwa na nafasi ya kuwaona watanzania ingawa tunaishi karibu na wengi wa wana CCM waliopo kwenye hizo picha. Nadhani mkutano ulikuwa wa wana CCM waishio uk na sio watanzania waishio uk.

    ReplyDelete
  4. tawi la ccm london ni illegal..
    hamna mtu anaeruhusiwa kuendesha shughuli za kisiasa za nchi nyingine ndani ya uk, isipokuwa diplomats
    hilo tawi halijulikani na msajili wa vyama uk ni mambo ya kinenyeji underground. hizo ni siasa za msituni.
    hata mdc ya zimbabwe ambayo inapewa hela na uk ina mwakilishi na sio tawi...
    tz kulikua na tawi la anc likafungwa sa walivyopata uhuru

    ReplyDelete
  5. Watanzania hatukualikwa kuwa waziri mkuu ataongea na watanzania.mbona alipokuja JK tulitangaziwa na ukumbi ukawa mdogo?

    najua hawa ni opportunist toka REAding. wao wanaishi Reading halafu wanasema viongozi wa CCM lONDON kwa vile kuna ubalozi na airport wanaposhuka viongozi.

    cha ajabu wamejikusanya watu wa musoma na wachagga wa Reading wakafanya uchaguzi wa watu 20 wakasema wao ni viongozi wa Taifa wa ccm UK, hivyo sasa wana kwenda kwenye mikoa na matawi. Kama nyingi mnaijua CCM basi mngeanza na uchaguzi wa matawi,kata, wilaya,mikoa then Taifa.hiyo ndio katiba ya CCM NA taratibu za uchaguzi wake.

    muda si mrefu tutamtumia JK,makamba na watendaji wa juu wa CCM makao makuu kuwa CCM London au UK ni kundi la wababaishaji.wanataka kutumia gea ya CCM kukimbia credit crunch UK.KWANI KAZI ZA CARE HAZILIPI TENA.

    watu hawa katiba ya CCM hawaijuI.tunapokuwa na shughuli hapa UK tunashirikiana watu toka pemba,unguja na Tanzania nzima na matangazo yanakuwa www.tzuk.com,tanzaniaone.co.uk au zenjidar.co.uk hakukuwa na TANGAZO la mkutano wa Pinda na watanzania.

    mzee michuzi ulikuwepo msafara wa JK alipokuwa na watanzania Church hill hotel uliona watu walivyojaa kuanzia wapemba,waunguja hadi wabara.

    jiulize wajumbe wa ccm wote ni watu wa musoma na kilimanjaro tu.hakuna mtu wa Zanzibar hata mmoja.huo si utaratibu wa ccm tunayoijua sisi.

    na kama wao wanaweza kubeza wapemba humu basi watumie muda wao kuwajibu kina mwanakijiji wa Chadema wanaoichafua ccm kwenye jamii forums kwni kule haina watetezi.
    wanamdanganya pinda akiondoka wao wako kwenye care hawana muda wa kuitangaza CCM, hatujawahi kuwaona hata siku moja wakipingana na wapemba wa CUF kwenye maandamano ya kuikashifu serikali.

    kingine uchaguzi wa 2005 wana cuf walichanga mamilioni ya pesa zaidi milioni 200 kwa waliopo UK kukiimarisha chama chao. jee wao wamempa ngapi waziri mkuu za kuimarisha chama Tanzania?

    ReplyDelete
  6. Ohh Tawi la CCM UK ni Illegal...Ohh Waziri Mkuu alikutana wa Wana-CCM peke yao...Ohh sisi wengine tunakaa jirani na Wana-CCM lakini hatukualikwa. Malalamiko, Malalamiko...kila kukicha..!!!

    E-mail ilisambazwa kwenye jumuiya zote za Watanzania UK, lakini walienda ndio hao hao!!!

    Hivyo hata kama Tangazo lingewekwa kwenye BBC 1, 2, ITV, Channel 4 na Channel 5 kwa mwezi mzima mfululizo; Watanzania kama nyie bado mngelalamika tu. Picha zote hizo mmeona viongozi wa CCM TU!!!!

    Kunyweni simu mjiue ndio tujue kweli kinawauma...ushamba wa hali ya juu mlionao...halafu eti na nyie mnasema "tunaishi Ulaya"..!!!!

    SIJUI MTAELIMIKA LINI??

    ReplyDelete
  7. CCM Juu.
    Hebu someni tena habari ya Ziara ya Waziri Mkuu. Alikutana na Viongozi wa jumuia mbalimbli, siyo Watanzania wote.
    Sasa kama Kiongozi wa zenji Dar hakuja, ana machungu yake labda alitaka Waziri Mkuu awe mpemba au ndugu yake.
    Kama Maalim hakufika basi nae anasumbuliwa na Credit crunch mpaka anashindwa kufika huko. Watu wenye mapenzi na nia ya maendeleo ndo siku zote wanasonga mbele. Hivi tangu CCM imefunguliwa, umefanya nini ambacho kimesaidia Watanzania wenzako au hata ndugu zako. Kazi kutukana wenzako na kukashifu. Uchaguzi wa CCM ni wa wazi sana, kila mtu mwanachama anahaki ya kugombea. Kama wamejazana Wachagga na Wamusoma ndioyo wanaonyesha moyo wa maendeleo, kama wewe mnyalukola hujali tulia kaa kwako, fanya kazi ikusaidie kukulisha.

    Tuachie sisi Wana CCm tujipendekeze, na siku zote mtu wa mbele ndo anafanikiwa, wewe kaa nyuma usibiri kuja kuvutwa…
    Kidumu Chama Tawala.

    ReplyDelete
  8. stupid!!

    umoja ni nguvu utengano ni udhaifu

    box zimewachosha naona mnataka sasa kuwehuka!!

    ReplyDelete
  9. mheshimiwa anajua hao aliosimama nao wote njaa kali tu. wamechanja kwasana sasa wameshindwa. wameamuakujiunga na ccm mimi ninge kuwa huyo uncle nisingeweka sura yangu na pinda aibu tupu hata mmoja wamaana hayupo.kweli credit crunch .mrudi kwenu.

    ReplyDelete
  10. Nashukuru kwa majibu ya jazba ya hao wanaojiita CCM LONDON huku wao wakiishi Reading.

    nakuuliza swali chaguzi cha chama huwa zinaanza chini au juu?kumbe hata utaratibu wa uchaguzi wa chama chako huujui?halafu mnasema sisi washamba?

    kwanza kabisa sio sifa ya wanaccm kutukana watu kama mnavyojibu hapa susan na owena,huwezi kuwabeza Zenjdar kwani balozi kaja kutuunganisha sio kutugawa kama mnavyotaka nyinyi kufanya.

    hivi karibuni Massauni kachaguliwa kuwa mwenyekiti wa Taifa wa umoja wa vijana wa chama,jee uchaguzi ulianza juu au chini? ulianza kwa matawi,wilaya, mikoa na then taifa.
    kama nyinyi mmeshindwa kujua taratibu za chama za uchaguzi nani washamba?

    AU NYINYI MNA KATIBA NYINGINE SIO YA CCM,AU MUULIZE MTANZANIA YEYOTE AU RAIA WA NCHI YEYOTE ANAJUA UCHAGUZI HUANZIA CHINI NA WALE WAJUMBE WA CHINI HUENDA KUCHAGUA VIONGOZI WAJUU, HAIHITAJI HILI KWENDA SHULE AU KUWA ULAYA,

    wewe Susan ulipotaka kugombea uenyekiti TA na utaratibu wa ubalozi uliweka wazi mwenyekiti lazima awe na mgombea mwenza toka bara au kisiwani.

    mbona ulimtafuta Mpemba awe running mate wako?leo hii unawakashifu wapemba kwa lipi walilokufanyia?
    na kama mngetaka mchanganyiko uwepo kwenye ccm ungekuwepo.huo sio msingi alioweka mzee wetu mwalimu Nyerere na mzee wetu Karume.


    wakati chama kinazinduliwa -Wembley london iliwekwa wazi kuwa makao makuu au shughuli za chama zitafanyika London LEO mmezipeleka READING wakati sio makubaliano ya mwanzo ya chama,

    inajulikana nyote hamkuwepo.

    alikuwepo MZEE MPOPO na baba Balozi,Yahya Kiomone,Said John HAWA Ndio waasisi wa chama UK. na ilikubalika kuwa Makao makuu yawe East Ham KWENYE base ya watanzania.

    HATA MZEE MALECELA ALIKWENDA EAST HAM -LONDON KWENYE MAKAO MAKUU HALISI YA CCM UK,kuna watu toka Reading walikuja kushudia hilo na picha ziko www.tzuk.com

    lakini nyinyi mmekimbizia READING.

    watanzania duniani hasa tulio nje tuna utaratibu wa kutangaza mikutano yetu kwenye website na blog hasa mkuu michuzi anatusaidia tunajibanza kwake tukiwa na habari zatu anatuhabarisha bureeee bila sumni.

    wakija The Commedy michuzi anatuhabarisha,

    wakija Jahazi Modern ANATUAMBIA WATAKUWA WAPI KIINGILIO BEI GANI,

    HATA VIONGOZI WAKIJA TUNAPATA TAARIFA KWA MICHUZI BLOG, JEE MKUTANO HUU WA PINDA NA WATANZANIA ULIWEKWA MICHUZI?

    mbona baada ya kukutana nae mmeleta picha zenu humu HARAKA HARAKA kwa michuzi,KWANINI MSITUMIANE EMAIL KAMA MNAVYODAI MIALIKO ILITOLEWA KWA EMAIL?KWANZA MTANZANIA GANI MWENYE EMAIL ZA WATANZANIA WOTE? KWANINI ASITUMIE NJIA RAHISI YA KUTUMA KWA MICHUZI HALAFU SISI TUNAPATA HABARI KUPITIA KWA MICHUZI? NJIA RAHISI NA YA BURE KABISA.

    Balozi tunaomba ukae na hawa wasiojua hata itikadi ya chama wanakuja na majibu ya kuleta ubaguzi kwa kauli zao za kipuuzi dhidi ya watanzania wenzetu kwa kutumia jina zuri la CCM kuwa wasitumie kauli chafu kama hizi kutugombanisha,AU KUTOCHONGANISHA NA CHAMA.

    MAMA BALOZI umefanya kazi kubwa kutuunganisha watanzania leo kazi yako nzuri wataiharibu hawa wasio kijua chama.

    Swali kwa wana ccm Reading a.k.a London.kama kweli mnakijua chama Salum Tambalizeni alikuwa nani kwenye chama?Thabit Kombo ali play role gani kwenye chama?

    BIBI TITI MOHAMED alikifanyia nini chama? ikiwa katiba na taratibu cha ccm hamzijui maswali haya kwenu ni mtihani wa Cambridge.

    tusidanganyane mnatumia CCM kama njia ya kurudi nyumbani kupata ajira baada ya CREDIT CRUNCH (RECESSION) KUSHIKA KASI.

    CCM IKO KUWAUNGANISHA WATANZANIA SIO KUWAGAWA KWA UMUSOMA NA UKILIMANJARO.

    MNADAI KUWA WA MUSOMA NA WACHAGGA NDIO WANAKIPENDA CHAMA MBONA TANZANIA MIKOA YA MUSOMA NA KILIMANJARO NDIO INAOONGOZA KWA UPINZANI?

    TIZAMA LINDI,SINDIGA,PWANI,SONGEA,IRINGA,DODOMA HUKO CCM IMESHIKA HATAMU KWA KUWA NA WANACHAMA WANAOJITOLEA KWENYE CHAMA CHAO NA WANA MAPENZI YA DHATI HATA DIWANI TU WA UPINZANI HAYUPO KAMA MNAKIPENDA CHAMA NENDENI MIKOANI KWENU MUWAONDOE WAPINZANI.

    NYIE MNAFUATA MASLAHI TU.

    JEE MMECHANGIA KIASI GANI HADI SASA KWA MAKAO MAKUU YA CHAMA?

    ZAIDI MMEPELEKA PROPOSAL YA KUTAKA MPEWE DOLA ELFU THEMANINI TOKA MAKAO MAKUU YA CHAMA WAKATI KULE NDIO KUNA MATATIZO ZAIDI NA NYINYI MKO ULAYA MNAVYODAI ,

    YAANI NYINYI MKO ULAYA MNAOMBA DUNIA YA TATU?

    JEE MATAWI YA CCM NAMTUMBO,MASASI,KILWA MASOKO MMEWAHI KUSIKIA YANAOMBA PESA MAKAO MAKUU?

    ZAIDI VIJANA WANAJITOLEA KWA HALI NA MALI KUHAKIKISHA CHAMA KINASHIKA HATAMU NA WAPINZANI HAWACHUKUWI KITU MAENEO HAYO,.KUMBE NDIO MAANA MMEJAZANA KWENYE CHAMA UK KWA KUSUBIRI DOLA ELFU THEMANINI?HII NAYO NI EPA NYINGINE.TUTAMSHTUWA MAKAMBA,MSEKWA, NA MWENYEKITI TAIFA.

    DOLA ELFU THEMANINI KWA LIPI?WAKATI MAHOSPITAL ZETU HAZINA MADAWA NA ZINAHITAJI MICHANGO YETU.JIFUNZENI KWA WAGANDA NA WAKENYA WANATAFUTA NJE NA KUPELEKA KWAO KWA MASLHAI YA JAMII PITIENI MICHUZI MUONE WANAVYOFANYA VITU MAREKANI SIO NYINYI MNATAKA MLETEWE.

    ReplyDelete
  11. NDIO MAANA WACHAGGA NA WAKURYA WAMEZAJAZA CCM LONDON KUMBE KUNA MSHIKO.AMA KWELI UKIONA KUNA MCHAGGA UJUE NYUMA YAKE KUNA EPA.

    ReplyDelete
  12. Kiongozi wa ZenjiDar ni Saleh Jabir yeye ni mtoto wa Ilala,baba yake alikuwa kiongozi wa Yanga Jabir Katundu.

    sio mpemba wala muunguja.huyu ndio muasisi wa muziki wa bongo fleva akiwa na marehemu black moses.nyimbo zake za mwanzo ni Ice ice baby,Ukimwi etc. ni mtoto wa mjini kweli kweli.msimuingize na upemba au useif sharifu Hamadi.

    Kweli vyama hivi ughaibuni vimeanza kutugawa na kutupiana maneno ya kashfa.naona hisia za ukabila zimeanza kuchukua mkondo wake.

    ReplyDelete
  13. CCM Idumu

    ReplyDelete
  14. huyo anon wa march 4 1:51 ndio hao hao kumbe kimemuuma eeeh, ye ndio hana elimu. eti mwenye elimu anabeba box, wamekaa ofisini , nyie msiokuwa na elimu ndimnaosha wazee huko, bibi zenu mbona amuwaoshi, rudini nyumbani basi muonyeshe elimu yenu ulaya yataka elimu njoo bongo uone,eti mnywe sumu kunywa wewe unaetaka umaarufu alafu ndio sisi. pumbavu zako.

    ReplyDelete
  15. Kama wewe unaona ni Dr Slaa wa UK basi jitokeze hadharani uanze kukashifu hao watu. Mbona Mikutanoni unakuja unashindwa kuyasema haya wewe halafu unajifanya anonymous?
    Njoo udili na sisi wanachama kwanza kabla ya kwenda mbali huko kukashifu Viongozi. kama ulikosa kura sasa unalalamika nini, si demokrasia hiyo?
    Cha kufanya kaka endelea kupiga shift,mambo ya kutukana watu hapa bila sababu haina maana.

    Kuhusu mambo ya East London, hao walikuwa ni Viongozi wa muda na walikuwa wanaishi huko. Sasa kama uongozi wao uliisha si vitu vinabadilika? Au unataka bado tuwe na matendo ya enzi za nyerere?
    Sitaki nikuaibishe humu ndani lakini kabla hujaanza kuongea mambo yasiyo na maana hebu tulia na kadi yako ya CCM na uchambue kama ni chama unachokitaka au unataka CUF siyo unashikilia vyote. Sisi huku nyuma tunakuangalia tu.

    ReplyDelete
  16. Hivi nyinyi mnajiita ccm halafu mnamkashfu hadi Nyerere?Enzi za Mwalimu hadi the Comedy wanazitukuza KAZI za Mwalimu Nyerere kwenye vipindi vyao.

    nyinyi makada mnamkashfu hadi muasisi wa chama? kweli mko serious au ndio hiyo Epa ya CCM UK ndio mmeifuata?

    hoja ya msingi ametoa mchangiaji wa juu kuwa chaguzi huanza chini na kwenda ngazi ya Taifa nyinyi mlifanya hivyo?tunaomba jibu la swali hili kwanza.

    mlichofanya ni ubinafsi kujivika majoho ya uongozi kwanza halafu kwenda mitaani kufanya chaguzi za matawi mkihofia kukosa nafasi za uongozi.ningekuwa kwa pinda ningemwambia hawa ni matapeli wa mjini wasikupotezee muda.

    changamoto nyingine mmepewa nendeni mkawajibu chadema kupitia tovuti yao ya jamiiforums huko CCM inashambuliwa kila dakika na nyinyi mlio na uwezo wa kutumia computer na mnajitia wasomi wajibuni kina mwanakijijikama ni wanaume.

    hivi sasa anatoa jarida la cheche kila jumanne kuitukana serikali ya CCM,kwanini msitumie fursa hii kuwakabili Chadema?kabla ya kumtisha huyo mwana ccm mwenzenu mnayemfananisha na DR.Slaa?

    naomba mtajeni humu, yaani badala ya kugombana na CUF,Chadema mnataka kugombana na mwanaCCM mwenzenu?mnaleta mambo ya Ole sendeka na Mallya?

    kwa maandishi ya hawa wanaojibu kwa niaba ya ccm humu inaonekana kuna kazi,kwani hawajui nini wanafanya.

    pia mstafute ugomvi na CUF wao ndio wameshika nchi hii ya uingereza kila kona, sio wanafiki kama nyinyi wakiambiwa kuchangia chama chao wanachangia, kina Mwanakijiji wanakesha jamii forums kujitolea kwa chama chao.nyie mnataka mpewe muda wa kumjibu mwanakijiji hamna.

    kweli kabisa watu wa mikoa ya musoma na Kilimanjaro ni opportunist kwani mara watakuwa wana NCCR mara TLP mara chadema, ni mikoa hiyo tu ndio watu wake sio waaminifu kwa CCM-MANDUMILAKUWILI.

    ombi tumieni muda huu kuijua katiba,kanuni na taratibu za CCM.
    someni kitabu cha mzee kawawa muone busara zake sio nyinyi.

    ReplyDelete
  17. CCM LONDON KUNA MSINA NORTHAMPTON HAYO NDIO MAMBO YA KUYAENDEA MBIO.ONESHENI UZALENDO WENU HUKO ITASAIDIA SANA KUTUPA MOYO SISI WENGINE AMBAO TUNAWASHABIKIA.

    ReplyDelete
  18. Mdau wa juu alikusudia kuwa Northampton kuna msiba wa kijana Elyas anatakiwa apate michango ili taratibu za mazishi zitimie,tuutumie kuwa wamoja na tujitolee kwa nguvu zote tusitengane kwa itikadi za CCM UK.tumeanza vyama yameingia mambo ya ukabila na sasa utakuja udini. tujiepushe na haya ndugu zangu WaTanzania.

    ReplyDelete
  19. Badala ya kutumia nguvu nyingi kuwatukana wana CCM, tumieni nguvu nyingi kuangalia ni jinsi gtani mtalikomboa Taifa letu. Maneno matupu hayavunji mfupa. Kama kweli CCM ingekuwa mbaya hivyo isingekuwepo mpaka sasa. Sasa ndugu zanguni, henu tungalie ni jinsi gani tunaweza kuleta maendeleo kwa vitendo kuliko kukaa chini na kupoteza muda kwenye mablog. Usiku ucha. Tuangalie ni jinsi gani tunaanza na mabadiliko, watu watatusikiliza zaidi tukifanya kazi kwa vitendo kuliko kumsubiri mtu akufanyie halafu unatukana..

    Hebu amkeni basi tufanye kazi ili tuwe na sababu za maana..

    ReplyDelete
  20. hakuna mtu anayeitukana ccm ila wajinga wachache wanaojiita ccm London ndio wanakuja na kauli za kudharau watu na kutaka kuwatenga kuwa hawa ni wapemba au laa.

    hoja zote za msingi wameshindwa kujibu kama kudai kuwa kulikuwa na taarifa za mkutano wa waziri mkuu wakati wao wenyewe wakiwa na mikutano yao,wana tangaza hapa hapa kwa michuzi.

    maendeleo hayawezi kuja bila kuwa na nia thabiti ya kuwaunganisha na kuacha kuwabeza wengine.

    changamoto kwa ccm London mmesaidia nini msiba wa huyo kijana? au kwa vile hatoki musoma/machame ndio hamshiri?

    ReplyDelete
  21. hakuna anayesema CCM mbaya,ni nzuri imetufanyia mengi chuo kikuu Dodoma n.k
    ila tutawaumbua wote wanaotumia mgongo wa ccm kupenyeza itikadi mbaya za ukabila au ubara na uzanzibar.

    tutakesha kwenye blog kuwaumbua na kuwataja.kama hawa wabaabishaji wa CCM READING ambao kazi yao kukashfu watu mara hawajasoma,mara wanaonewa wivu au wawaite watu washamba n.k,

    swali nani kasoma kwenye ccm Reading?susan Lyimo(mzee) kama angesoma asingefanya Care.au owena? wangekuwa wasomi wasingeshindwa kujua taratibu za chama za uchagzui, wala wasingekuwa na majibu ya kibongo fleva eti wenye wivu wajinyonge.

    mara wawaite wenzao washamba n.k.

    sisi wenye mapenzi ya dhati na CCM yetu tulipokuja ughaibuni tayari tulikuja na kadi zetu za uanachama nyinyi mliokiona chama hakina kitu mlipokuwa bongo, na mlipofika hapa baada ya kuona CREDIT CRUNCH imeingia ndio mkakumbuka uchochoro wa chama cha mapinduzi ili kuweka sawa maisha yenu.

    sisi tumekulia kwenye chipukizi.kati yenu hakuna hata mmoja anaweza kuimba wimbo wa nambari one ccm kwa kichwa au alipitia chipukizi.
    mzee kawawa katiba ya chama anayo kichwani tu.

    ReplyDelete
  22. SUSAN MZEE NAOMBA UNITUMIE KADI ZA CCM 56, ADDRESS YANGU NI DUKES HOUSE, MANCHESTER, M60 2NS. CCM OOYEE!! KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!! NB. HIVI UKIWA NI MWANACHAMA WA CCM, JE UNAKUWA SI MTANZANIA? INAVYOONEKANA MAONI YA WATU WENGI AMBAO NI CHADEMA, CUF, ZAWA+ZENJYDAR(A.K.A - CUF), AMA VYAMA VINGINE VYA UPINZANI WAO NI WATANZANIA HALISI. WATANZANIA UGHAIBUNI BADO TUNA SAFARI NDEFU, NILIFIKIRI UBAGUZI UPO KWA WAZUNGU NA WEUSI TU, KUMBE HATA SISI WATANZANIA TUNABAGUANA, TUKIKUTANA MITAANI TUNA UNAFIKI NA CHUKI BINAFSI

    ReplyDelete
  23. ZAWA NA ZENJIDAR SIO CUF,MATUSI MMEANZA NYINYI CCM,UNAMWAMBIA AKULETEE KADI HUMU HUNA SIMU YAKE AU EMAIL YAKE? HUO NI UBABAISHAJI HATA ADDRESS YENYEWE HAIKO KAMILI NI MAONI YENU WENYEWE CCM READING KUJIFAGILIA HUMU.MATAPELI WA KISIASA WAKUBWA. MANCHESTER KUNA WATU 56 WANAWEZA KUWA CCM?LONDON KUNA WANACHAMA 20 ITAKUWA NA MANCHESTER?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...