Kali Ongala akifanya vitu vyake akiwa na timu yake ya GIF Sundsvall ya Sweden.
Pengine ndio mchezaji pekee mwenye asili ya Kitanzania aliyewahi kuchezea daraja la juu zaidi kuliko wote Tanzania. Akiwa mmiliki wa passport ya Kiingereza lakini katika profile yake anawakilishwa na bendera ya Tanzania.
Je TFF inamipango gani madhubuti kuhusiana na Wachezaji kama hawa ambao ukweli bado wanamapenzi na ndoto za kuchezea Taifa Stars?
Je serikali haioni umuhimu wa kuipitisha sera ya Dual Citizenship ambayo itawapa mwanya wachezaji kama hawa kurudi na kuiwakilisha nchi.
Wadau hii imekaaje?
Mdau Marekani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Hii kitu inamake sense ni wakati muafaka kw serikali yetu kufikiria kupitisha hili suala badala ya kusitasita sababu mwisho wa siku sisi ndio tutakaofaidika.Nchi za wenzetu walishaanza haya mamabo siku nyiingi.Tafadhali watanzania tuamke!!

    ReplyDelete
  2. Bwana Michuzi na Mdau wa Marekani

    Ni vizuri hii hoja imeletwa.

    Kwa kweli inavyookana ni kwamba kuna mitazamo mingi pale linapoulizwa hili swala la, nini maana ya Uraia wa nchi?

    Kuna wenye kufikiria kuwa sio uzalendo kuchukua Uraia wa nchi nyingine. Lakini, ukiangalia kwa makini, kwa nchi yetu, kwa bahati nzuri asilimia kubwa sana itakuwa inafanya hivyo kwa sababu za kiuchumi. Moyo na Uzalendo upo pale pale au hata zaidi, ila shughuli za Uchumi ndizo zinapelekea watu kuchukua Uraia wa nchi nyingine.

    Pagumu ni pale wanapokuambia kana Uraia wa nchi yako ndio uchukue wa nchi nyingine. Hii sana sana inakuja kutoka kwa nchi yetu kwa vile hawa wenye kukupa wa kwao, wengi wanakuacha wewe mwenyewe ujishughulishe na mambo yako ya kwenu, kama ukiacha au la, lwako. Sasa wapo wengi sana, bila shaka wote, ambao hawataki kuacha huo wa Tanzania. Wapo ambao inashindikana, again, kiuchumi inabadi wabadili na kuchukua nyingine na wakija nyumbani wanaficha za ugeni au hata kuzitumia, inategemea wanataka nini na wapo wapi.

    Wengi tunaongelea hili Swala tungependa sheria ikae wazi kutokana na wakati na iruhusu watoto wa Taifa hili wasipoteze hii nguvu kazi kwa sababu za kisheria za miaka ya 1960. Ule ubishi uliozuka wakati wa hii debate in 1960, ulikuwa wa Afrikanization, ambao upo karibu na yale ya Uzawa. Ukiangalia kwa makini, hizi ni sera za kuweza kugawa watu wa nchi. Sababu za kusema dual citizenship italeta pesa kwa nchi, kwa maoni yangu naona ni misplaced argument. Mine is simple, ni muhimu kwa kuwa hii ni nguvu kazi ya Tanzania, na Utanzania sio kutokana na wapi unaishi, bali uwe na mkazio kwa yale utakayotenda kama Mtanzania. Isiwe fungulia mbwa, lakini pia isiwaache watoto wa Tanzania kama akina Kali Ongala. Wapo wengi sana akina Kali Ongala.

    Tunavyojenga na kupigia debe tuwe na Utawala wa Sheria, basi pia tuwe na sheria zinazoenda na wakati na zinazofaa kwa manufaa ya nchi nzima, tena zenye kujenga Umoja.

    Kuna haja kubwa, tena kwa Utulivu kabisa, na kiungwana, kuandaa mijadala hii kwa Watanzania wote, waliopo online na offline, bila kuacha Wabunge wetu wote waliochaguliwa na future potentials, kuweza kulipitia hili swala kama issue, ili watu wote tuelewane. Linawezekana hilo. Siamini ndugu na wananchi wakielewa pande zote kwa undani, muafaka utakosena. I know, kwa sasa imekuwa cut and dry on both sides of the debate, na mwelekeo huu hauna manufaa kwa Taifa in a long run.

    ReplyDelete
  3. Suala la uraia wa nchi mbili ni la muhmu sana ktk kipindi hiki cha dunia kijiji.Cha msingi watu tuangalie fursa za kuwa na uraia wa nchi mbili, nini faida na nin i hasara.

    Kwa maoni yangu, kuna faida nyingi kwa mtu binafsi na hata nchi. Kwa nchi, faida ni kwamba mtu anapokuwa na uraia wa nchi mbili anaweza kuwekeza Tanzania kama watanzania wengine kwa manufaa yake binafsi na Tanzania nayo ikafaidika.Pia ktk uingizaji wa magari, utumaji fedha nk nchi inafaidika pia.

    Kwa sheria ya sasa ambayo inazua uraia wa nchi mbili eti kwa kigezo ni kuondoa uzalendo, je kubinafsisha mashirika yote nako ni kuondoa uzalendo au?Maana haina tofauti na suala la uraia wa nchi mbili, kwa maoni yangu.Kama ni ukosaji wa uzalendo, basi tuachane na ubifsishaji, na pia tuondokane na kocha wa kigeni, kuanzia klabu...Simba, Yanga, Azam na Taifa Stars...kuwa na kocha wa kigeni ni uraia wa nchi mbili ni kitu kile kile.

    Matokeo ni kwamba mtu ambaye anachukua uraia wa nchi nyingine, Tanzania haifaidiki na kitu chochote kile zaidi ya hasara tu.Hivi chukua mfano siku Hasheem Thabit aamue kuchukua uraia wa Marekani na kuanza kukipiga NBA, Tanzania utafaidika na nini hasa??

    Kwa mimi binafsi kutokana na hali ya bongo ilivyo, nikisema nichukue uraia wa nchi kama Marekani au nchi yoyote ya ulaya, hata kama kuna uraia wa nchi mbili na Tanzania, huo siuhitaji.Maana ifike kipindi mtu uone faida za kuwa raia wa nchi fulani.Kama unakua raia wa nchi fulani hupati faida yoyote zaidi ya matatizo, maana yake nini sasa?

    Kuna watu wengi sana ughaibuni ambao wameshaukana uraia wa bongo, na wana nyadhifa zao muhimu...itabaki tu historia kuwa ana asili ya Tanzania na kuweka public holiday kama kenya kipindi cha Obama huku mtu akiwa hatambui hiyo Tanzania tena.

    Tubadilike, tutunge sheria kuendana na mazingira ya kisasa zaidi.

    MAKULILO Jr,

    ReplyDelete
  4. Sasa ninauhakika KARATASI limetoka na hoja umeikumbuka

    ReplyDelete
  5. Hakuna cha Uraia wa nchi mbili, chagua moja Kusuka au Kunyoa.

    ReplyDelete
  6. Shukrani kwenu wachangiaji wa hii mada shukrani mleta huu mjadala pia kwako Mkuu wa wilaya Tegeta njia ya kwenda Bagamoyo kwa mkuu wa nchi,kweli Tanzani inabidi tubadilike kisheria tumeona kwa wenzetu jinsi nchi zao wanavyofaidika
    Kwa mfano ukiwa ughaibuni uko hupo kimaisha lakini kule nyumbani Tanzania ndiko waliko wakina shangazi mjomba ukuwakumbuka leo lakini kesho utawakumbuka utawapa codi No swali na jibu lake nao watakwenda kuvuta mshiko WEAST UNION
    Pia utakavyo jituma lau utatafuta sehemu ya kwenda kupunzika kipindi cha likizo utakuwa na miladi endelevu utawekeza nyanja muhimu je yote hayo nchi haiajfaidika tuu,,
    Na hawa watu tunaoishi nao na kuzaa nao watahiji pia kuja kuwekeza au watoto watapenda aidha kuishi au kufanya kazi za kizalendo kwa hisani ya mifuko yao bado tuu hatujapiga hatua,,
    Jamani wabunge na Wizara husuka muende na alama za nyakati
    MPILI

    ReplyDelete
  7. Ni bora tumkose Kali asituchezee timu ya Taifa hatutaathirika sana kuliko wale walioshikilia uchumi wa nchi yetu ambao sio wazawa wa Tanzania lakini wana uraia wa Tanzania endapo watapata fursa ya kuwa na dual citizenship tumekwisha,manake watasomba mihela yote katika accounts zao za Tz na kupeleka kwenye nchi zao wanazozipenda zaidi.

    ReplyDelete
  8. Hicho kijitimu chake huyo jamaa yenu ni mdebwedo na tayari kimeshashuka daraja

    ReplyDelete
  9. Napenda kuwaunga mkono wadau wote....
    Umefika wa serikali yetu kwneda na wakati....Manayake siyo huyo tu anayecheza mpira nje...wapo vijana wengi huku ulaya wanavipaji vya kucheza mpira...na wakafanya makubwa
    Lakini kutoka kwa serikali kubana..kunakuwa hakuna maendeleo...
    Angalia wenzetu wa west africa walivyoendelea
    Kwa mfano timu ya senegal hiliyocheza world cup 2002
    Karibia wachezaji wote walikulia ufaransa na belgium lakini kwa kuwa walikuwa na urai wa nchi 2 waliweza kuwakilisha nchi yao pia
    Nadhani rais wetu ni mtu anayekwenda na wakati atalishigulikia swala hil

    ReplyDelete
  10. bahati mbaya ishu sio rahisi kama inavyofikirika.kwa inchi ka tz ambayo haijawa sawa kimfumo, inaogopa kupoteza mambo mengi,fikiria wezi ,au mafisadi wangekuwa na uraia wa nchi mbili ingekuwaje.nchi zote zilizokubali kitu hiyo ni zile ambazo zina mvuto, ambazo wananchi wa nchi myingine watakimbilia na mitaji au utaalamu ambao mwisho wa siku ni faida kwa nchi hiyo.
    kwa wabeba box sio habari nzuri lakini kwetu sie watunga sera ,habari ndiyo hiyo.

    ReplyDelete
  11. Ulaya Ukichukua Uraia Wao Wanakubali Ubaki Na Wa Kwaenu Ila Siku Kimbembe Uko Mitaa Ya Watu Unapata Matatizo Ukienda Embasy Ya Wazungu Wanakuambia Kaaombe Msaada Wa Embassy Ya Bongo Kwanza.Hapa Bwana Kila Mtu Abebe Salaba Lake Mwenyewe Kama Mtu Umeishi Bongo Nyundo 20 Inatosha Ikitokea Kuchukua Uraia Mwingine Chukua Umalizie Maisha Bongo Yenyewe Ishagawanywa Vipande vipande Na Wajanja

    ReplyDelete
  12. ACHA UJINGA MICHUZI HAIWEZEKANI KUFANYA MAAMUZI MAKUBWA KAMA HAYO KWASABABU NDOGO KAMA KUWAPATA AKINA K ONGARA, TUANGALIE MASUALA MAKUBWA NA IMPLICATIONS ZAKE.

    ReplyDelete
  13. Mtowa maoni kuhusu mada ya urai wa nchi mbili elewa kuwa nchi ni nani ambae yupo tayari kuingia na matatizo na TANZANIA wakati anashikilia pass za ulimwengu wa kwanza nchi hii itakutaka ufanye mabo wanayotaka wana siasa ukisema hutaki hapo ndio utaona madhila majungu na kila mbinu ili wakuangushe

    ReplyDelete
  14. Mimi nina uraia wa Tanzania na Kanada. Nimeupata kihalali lakini nashindwa kutumia uraia wangu wa Tanzania ili nisiombe viza kuja nyumbani. Nasafiri na pasi ya Kanada ili niweze kurudi Kanada.

    Haisaidii kabisa kunyima watu wasiwe na pasi mbili kwa sababu watu wengi wana pasi mbili, ili ikiwa halali basi itarahisisha kazi za kuomba visa.

    Mdau anaosema kwamba ukiwa na matatizo uraia wako wa ulaya husaidiwi kwa kuwa una wa Tanzania haelewi sheria za kimataifa. Mimi ni sasa sawa na raia aliyozaliwa Kanada. Watanisaidia katika shida yoyote kama raia wao. Na kama unajua mambo ya Kibongo wewe mwenyewe utaenda kwanza kwa wazungu kabla ya kupiga simu ubalozi wa bongo. Wengi wameandika hapa jinsi wanavyoteseka na service za ubalozi wetu urusi, na nchi nyingine.

    Kwa kifupi, hata kama serikali itapinga au wadau wengine hapa watapinga, wananchi wengi wa Bongo wana pasi mbili hasa wanaokaa nje. Na watazidi kuomba pasi ya nchi za kitajiri kutokana na kazi na urahisi wa kusafiri na kusaidiwa katika shida yoyote. Na kama serikali itawatia ndani watu kama mimi wenye pasi mbili basi utaona haraka haraka tutaukana uraia wa Tanzania. Si lazima uwe msomi kuchagua uraia wa nchi ya kitajiri kama tutabanwa au kutishwa na serikali. Sasa hivi tunaingia nyumbani kilaini na pasi zetu, sijaulizwa hata siku moja kwa nini inaonyesha kuwa nimezaliwa Tanzania au kama nina pasi ya Tanzania, tangu ubalozini kwetu mpaka uwanja wa ndege serikali haiulizi maswali yoyote, ili mradi unalipa viza fee yao.

    ReplyDelete
  15. so unataka wachezaji mpira peke yao ndio waruhusiwe kuwa na uraia wa nchi mbili? kwa nini wengine wasiruhusiwe? nchi chungu nzima zinaruhusu na nashangazwa sana na kasumba walokuwa nazo wale waliokuwa hawataki hili litokee tanzania.

    ReplyDelete
  16. Tatizo kubwa ninaliliona ni ndugu zetu wahindi ambao wana uraia wa Uingereza, India na ni raia wa Tanzania.Je serikali yetu imedhibiti vipi hawa ndugu?Ndo kwa maana hakuna mhindi anayetaka kujenga Tanzania wahindi wengi wamenunua majumba Canada, Marekani,Uingereza hasa Machester ni East Africa ya pili uwe mwangalifu usimtete mtu kwa kiswahili.Vijana wetu ambao wamebahatika kuishi nje hata kama wanabeba mabox kama wanavyojiita bado wakipatiwa nafasi wanaweza kuwekeza nyumbani hapa,lakini watu wachache walio na fikra zile za miaka ya 1947 bado hawajaona umuhimu wa kufanya hivyo.Mbona mnawakaanga watoto wetu hali wahindi wakifaidi uraia wa nchi zaidi ya moja kwa kificho na hakuna anaye hoji?.watanzania tuamke sasa tuanzenkuona mbali tuachane na utaratibu wa zamani ambapo kila kitu tuliachia watu kadha wawazee/wafikiri kwa niaba yetu,

    ReplyDelete
  17. Kaka Michuzi,
    Hii naweza kuiita mbegu inayofaa kupandwa katika mustakabali mwema wa kulitakia mema taifa letu katika nyanja hii ya michezo

    Haya ndiyo mawazo tunayotaka, kama kuchangia timu kunahitajika na mawazo yetu wachangiaji yasibezwe.

    Asanteni sana wadau kwa kuibua hili.

    ReplyDelete
  18. Uraia wa nchi mbili ni jambo zuri lakini kwa kuangalia mikataba tunayoiingia nina wasiwasi hatutatunga sheria ya uraia wa nchi mbili itakayosaidia nchi. Hiyo sheria inaweza kuwa nafasi nzuri kwa wasioitakia mema Tz kuja kukomba na kuanza mbele kwa kuchagua gia wanayotumia. Wanaweza kujiita Watanzania au wawekezaji. Bora wabaki na gia moja tu.

    ReplyDelete
  19. Hii inaonyesha kwa jinsi gani TFF na Serikali kwa ujumla wasivyotilia mkazo jambo hili. Tunazidi kufunga kila siku na fedha za serikali zinazidi kupotea na Nguvu mali tunazo.Kwanini? Tukisema tuanze kuwakusanya hawa wachezaji wetu wilioko nje ambao wana situation kama ya Kalimangonga basi tunaweza kuwa Taifa Stars nzima kutoka nje. Mkumbuke swala sio kuchezea MAN U au Liver, swala ni kucheza nje. Mchezaji wa nje hata kama anachezea timu ya daraja la nne ni wa nje tu huwezi kumfananisha na Haruna Moshi. Tutakaa tunapigizana kelele weee na Maximooo weee lakini sote tunajua kwa taifa Stars ya ndani tu hatuwezi kufika kokote. Mimi ningependa kutoa wazo Iiundwe Taifa Stars ya wachezaji kutoka nje bila kujali anacheza wapi na daraja lipi na Hii ya sasa ambayo imesheheni wanyumbani then iindaliwe mechi tuone nani atafungwa hapo TFF na Watanzania wote wataanza kuthamini umuhimu wa hawa vijana ambao tunawapoteza kila siku. Tumeshapolwa Leornado na Msumbiji na akaja akatuliza hapo hapo nyumbani sasa mtashangaa Kali, Njohole, Mnyamulu wakija na Harambee Stars wakatuliza hapo hapo nyumbani?? MWAKALEBELA NA TENGA tunajua ni wapitiaji wakubwa sana wa blog hii na tunajua maoni haya mnayaona sasa mnasubiri mpigiwe zumari ili muanze kuwathamini vijana hawa?? Kuna kijana ametoka Arusha na sasa anakipiga Readings Fc hapo UK na hata alishapata kutokea katika vyombo vya habari hapo UK siku aliyomkaba Tienry Henry timu yake ilikpokutana na Alsernal hata siku moja hatujasikia ameitwa hata kwenye mazoezi ya Stars. Sikieni labda hamjui msitegemee mtu achezee Chelsea ndio muanze kumuita Stars. Njia moja ya kuwa promote Wachezaji wa nje ni kuwaita wakiwa katika vijivilabu vyao vidogo, kwa kufanya hivyo mnawajengea heshima hapo vilabuni kwao na kufanya iwe rahisi kwao kuuzwa katika madaraja ya juu. Hivyo ndivyo mtakavyo promote hawa vijana wakiwa nje!

    ReplyDelete
  20. Watanzania tuna kauginjwa ka kuthamini vya nje na kudharau vya kwetu. Ndio tunavipaji vingi nje lakini tunavikana. Wakichukua Uraia wa nje basi mnaanza kuosha vinywa ooh sio Mzalendo! Hivi mi niulize; "Uzalendo ni hali ya Mwananchi kuipenda nchi yake tuu au Hata Nchi Kuthamini wananchi wake"?
    Leo tunaona mlivyowaokota hao Vancouvar White Caps na kuwadhamini na kila siku tunapiga kelele wee Kuhusu Tanzanite Fc timu inayomilikiwa na watanzania na inavijana wenye vipaji. Hivi haiwaingii akilini kwamba kama mkiwaaalika hawa Tanzanite Fc kuna manufaa zaidi ya hao wachezea barafu. Kwanza hata uwanja robo hakujaza sasa biashara inakuwaje hapo. Mimi nina amini mkiwaaalika hao vijana wa kitanzania basi sidhani kama kutakuwa na nafasi ya kuweka mguu. Kwa wale ambao hamjawaona hao vijana jamani wanakipiga!!Tuweni wakweli sasa! Wakati umefika!

    ReplyDelete
  21. mimi naona uraia ni IDENTITY thats your lebel, can anything, anyone calim to be a chritian at the same time a hindu? Lazima awe neutral na anataka kuwa na faida zote mbili na kukimbia hasara zote mbili. How can you be really commited to something if you can run away from it?
    I wouldnt!
    Uraia uwe wa nchi moja, unless wauambie sababu nzuri za kutosha, kutufanya tubadili definition ya uraia.
    Sio sababu za kutaka mchezaji, au investor, kwani hao individuals have their prices, if we need them bad enough we can buy them into Tanzania.
    Wasitupe wekaness zilizopo kushabikia duo citizenship, hoping kwamba itasolve hizo weakneses. Si kweli, it is much cheaper kupleka timu nzima shule aliosoma huyo sijui nani, wakajifunze, wakiwa raia wa tanzania na kuja kuikuza timu yetu kuliko kuwa na wachezaji ambao hawaipendi Tanzania KIHIVYO.

    ReplyDelete
  22. Bwana misupu na mdau mleta mada, dual citizenship kwa nchi masikini kama sisi ni 'dili' kwa raia wetu walio kwenye diaspora na ni hatari kwa usalama wa Taifa.

    Wakati wengi watatumia fursa kama hii kuchuma kwa ajili ya nyumbani, kuna wengine WACHACHE ILA WENYE MIKONO MIREFU SANA NA UBINAFSI, a.ka. mafisadi watatumia njia/fursa hii kuhamishia rasilimali na itakuwa ngumu sana kuwafuatilia hawa.

    Yote kwa yote, dual citizenship ni 'dili' hasa kwenye libeneke la diaspora. Kwa hili naunga mkono hoja!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...