Leo asubuhi, nikiwa kwenye foleni maeneo ya jangwani, saa 1.20 asubuhi, gari la tatu kutoka gari langu kwa nyuma lilivamiwa na vibaka, wakafungua milango, ndani ya kama dakika 3 wakapora kila walichoweza kupora.
Ilikuwa ni kwenye foleni, jamaa wana visu, na kila mtu akawa anaangalia kama sinema hivi. HAKUNA MSAADA!
Watu kwenye daladala la karibu, wakawa wametulia kimyaaaaa. Na walio kwenye saloon cars wakawa wanafunga vizuri vioo ili wasiwe next target. Siku zote hizi WARNING nilikuwa sizipi uzito unaostahili, leo nimekubali. Naomba munielewe, Sizungumzii mtu kupora cheni au simu dirishani.
Jamaa wamefungua milango, na kunyang’anya kila walichokifikia.
Tafadhali sio tu ufunge vioo, lakini hakikisha milango imefungwa ( LOCKED) BONGO TAMBARAREEE!
Mdau OCTAVIAN ‘OC’
Octavian, lakini wewe ulifanya nini kusaidia?
ReplyDeleteItabidi sasa tuanze ku-drive na pistol mfukoni. Unamumwagisha mtu ubongo barabarani tu.
ReplyDeleteHapo ni bastola tu, fully loaded! halafu hao vibaka uchwara ndio watalijua jiji.....
ReplyDeleteJamani, zile difender zimeishia wapi, Tukubaliane kitu kimoja, mambo mengi yanayofanyika Tanzania yanasababisha madhaama sehemu nyingine, mfano, tukimuuliza Muheshimiwa IGP- Mwema, atasema hana askari na vitendea kazi, kang'ang'ania community policing weee mpaka basi, mabilioni yanayopotea kila siku kwenye, Radar, Richmond, Dowans, EPA na nyingine nyingi, zingetosha kabisa kumpa IGP uwezo wa kudhibiti hawa wahuni wachache. Hili tatizo halipo tu Jangwani jamani, lipo Salander Bridge pia, nimeshashuhudia mwenyewe mara mbili mtu akiporwa side mirrors na Handbag. Watanzania tushikamane kuishinikiza serikali kuthibiti hii hali.
ReplyDeleteMdau bora umelitoa hili wadau waweze kuchangia. Hili jambo lipo sana hapa Bongo sielewi ndio life style ya wabongo au vipi. Unaweza ukawa unaibiwa na hata kupigwa mchana peupeee lakini hakuna anayejitokeza kukusaidia hata kama kunawatu wanaopita karibu tena mwenye gari kama yupo karibu ndio anafunga vioo kabisaaa. Kwakweli wabongo tunakosa upendo kabisa kwa wenzetu.
ReplyDeleteNao vibaka siku hizi kutokana na tabia hiyo ya kuachwa wakimuibia mtu hakuna basi ndio wamezidisha hasa. Hayo maeneo ya hapo Magomeni ni kama kawa kwa kitendo hicho kwa wewe ndio mara ya kwanza kuona mimi nilishaona tena vitendo kama hivyo. Inakuwa kama watu wa Magomeni wanawajua vibaka hao na nijamaa zao.
Hii polisi jamii sijui itaimarika lini ikiwa sisi wenyewe tunaangalia tu hatushiriki kusaidia kupunguza hivi vitendo viovu vikiendelea. Hii inaonyesha wazi huko tunapoelekea tutakuja kuchinjana hivi njiani hakuna pia atakayesaidia.
Kwa maoni yangu naona pia vibaka wamejiamini sana kutokana na wakimwibia mtu hakuna anayeingilia kumkamata pia hata wanapokamatwa wakienda polisi wanafungwa tu hauzidi mwaka wanatoka msamaha wa Rais ukipita. Hii imepelekea kufanya uporaji kuwa ndio ajira yao. (Mimi nitaiba nikikamatwa poa nitafungwa kwanza gerezani nitakuwa napata chakula cha bure kutofautisha na uraiani na pia muda si mrefu nitatoka kwa msamaa wa Rais au nikikamatwa nitatoa chochote nitaachiwa)
Pia Kinondoni yani msamaa wa Rais ulipopita yani vibaka wote unawaona uraiani bora maeneo ya studio sio mabaya sana lakini maeneo ya manyanya na Mkwajuni ukipita tu katika mitaa mida ya asubuhi basi wewe ujue utabananishwa na vibaka wakupore vitu vyote.
Nilinyanganywa simu mchana kweupee, nilipita mtaa mmoja nitokee Kinondoni Stereo nikakutana na kibaka ikawa tunapambana nikijiamini kwani niliona watu kwa mbali kidogo wananiona kuwa watanisaidia huku napiga kelele lakini hakuna aliyekuja zaidi ya kunishangaa hadi kibaka akaning’ata na kuchukua simu.
NAOMBA WATANZANIA TUBADILIKE..NCHI YETU NI NCHI YENYE AMANI..TUPENDANE, TUSHIRIKIANE, UKIONA MWENZAKO ANAPATA TATIZO KAMA HILO BASI ASIJITOKEZE MMOJA KUMSAIDIA TUJITOKEZE KWA WINGI TUMSAIDIE NDIVYO TUTAKAVYO TOKOMEZA MAOVU HAYA...TUITUNZE AMANI YETU YA NCHI SASAHIVI TUNAPOELEKEA PABAYA...MWENZIO AKIFANYIWA KITU KIBAYA JIHISI KAMA NI WEWE AU NDUGU YAKO KWANI IPO SIKU YATAKUFIKA NA WEWE..
Mdau H
du sasa bongo kunatisha naogopa hata kurudi kama mambo yamefikia hivo ndugu zetu huko watapona ndo mana mdogo wangu anataka kununua bunduki nikamkataza ya nini bongo kumbe ni muhimu kuwa nayo kwa mambo kama haya nchi inaenda kubaya
ReplyDeleteHii michuzi ni kweli au kamba kali tu kwa bongo yetu hii mambo kama hayo wapi na wapi kwanza sio tamaduni zetu au ulikuwa unaota donto ya mchana kaka
ReplyDeletetuache utani bwana serikali inaweza kushughulikia hili
ReplyDeletetunaomba serikali ifannye kazi yake
Ahsante kwa kutuhabarisha. Naelewa usingeweza kufanya chochote maana wao walikuwa na silaha na wewe huna. Pia ungetoka wangekuvamia na wewe.
ReplyDeleteCha msingi tukumbuke ku lock milango ya magari yetu
Nimekusoma OC .inabidi wanausalama wa yaangilie sana haya maeneo ya Jangwani ,Salender bridge pia maeneo ya Daraja la Ubungo yamekuwa na matukio mengi sana ya uharifu.
ReplyDeleteAfande Kova changamoto hiyo
Nimekusoma OC .inabidi wanausalama wa yaangilie sana haya maeneo ya Jangwani ,Salender bridge pia maeneo ya Daraja la Ubungo yamekuwa na matukio mengi sana ya uharifu.
ReplyDeleteAfande Kova changamoto hiyo
mbona na wewe hukusaidia kitu?
ReplyDeleteHii mimi inanishangaza, walikuwepo watu kwenye daladala, na maeneo mengine wameona, halafu wote wameuchuna, kwakuogopa visu na mapanga, hamjui munawapa vichwa hawa watu. Ilibidi watu wajitose, kwasababu na wao walikuwa wanawapima, kwa kujua wengi ni waoga.
ReplyDeleteTusidanganyike, kama hatutajitolea wenyewe tusitegemee polisi watakuwepo kila mahali. Inabidi kujitolea muhanga ili kuinusuru hii hali. Hayeni wachekeeni, kwani leo kwa yule kesho kwako.
M3
Hii ni dalili ya baadhi ya wananchi (na hasa wananchi wa chini kabisa kimapato) kukata tamaa na kufikia hali ya kusema, "liwalo na liwe". Hii inatokana na Upumbavu, Ujinga, na Uzembe wa Serikali na watendaji wake (pamoja na Rais) kutumia mida wote wa uongozi wao katika kujinufaisha wao na familia zao binafsi bila ya kujali nchi na wananchi wake.
ReplyDeleteSitetei wezi, na ningependa sana kama hawa vibaka wangeelekeza uharamia huu kwa watendaji wa serikali, na familia zao.
wewe unaetaka kumumwagisha mtu ubongo naomba nikuulize swali ulishamwaga wangapi??
ReplyDeleteangalia utaishia kunyongwa na ufisadi wenu..
mnataka wenzenu wafe na njaa?? na ufisadi wenu
hii ni trela bado picha kamili mtaiona
hakuna msaada wa story ukitaka kutoa msaada wape hela hiyo ni njaa tu inawasumbuwa ni ndugu zetu wanahitaji kuishi na kuishi ni kula sasa mnataka wao wafe na njaa.
ReplyDeletewaende na nyumbani kwa mkapa watapata hela ya kula mwaka mzima.
je ungelikuwa wewe unanjaa na nyumbani kwenu mzazi wako yuko hosp na hakuna hela ya matibabu je ungefanyanini???
ReplyDeleteau utamwacha ndugu yako afe na njaa kwa ajili ya mafisadi au utawakaba ili umtibie mzazi wako???
mimi naona hawanakosa ni kosa la selikali ya mafisadi kuifisadi nchi na kuleta ungumu wa maisha kwa walio wengi.
bora mtu ufe kwa kutafuta ridhiki kuliko kufa na njaa poa tu tumieni hizo bastora zenu kama mnaona kuuwa watu ni ufahari wenu mafisadi
ReplyDeleteila azabu zenu za kuibia walala hoi zinaongezeka.
Hayo yaliwahi kunikuta mwaka 2001 pale kwenye taa za barabarani za Ubungo. Walifanikiwa kunikomba kila kitu nilichokuwa nacho garini na kunijeruhi kwenye bega la upande wa kulia.
ReplyDeleteKwa bahati nzuri mmoja alikamatwa nanatumikia kifungo chake cha miaka 30
Wadau, anachosema huyu Mdau mwenzetu ni kweeeeeeli kabisa. Wiki iliyopita wameninyang'anya hereni zangu ivi ivi hapo hapo jangwani maeneo ya Kwa Macheni!! Ilikuwa ni saa moja dakika ishirini na tatu (07:23am) nikiwa kwe foleni. Watu walikuwa wameshangaa na kunipa pole tu. Vijana wako Smart huwezi amini wala kudhania. Nawahimiza watu wote mlock milango ya magari yenu na kufunga vioo. Na kwa wale watembea kwa miguu umezuka wizi wa waendesha pikipiki kukwapua pochi za kina dada na kutokomea nazo. Hilo lilitokea mwishonimwa mwezi wa pili maeneo ya Ubungo. Jeshi letu la polisi tunaomba litusaidie kucheki katka maeneo tajwa ili kutunusruru maana itafika mahali sasa wataanza kuchinja watu wakienda Kulijenga Taifa!!!! Sharly
ReplyDeletehi wadau
ReplyDeletethis is just the beginning
ngoja watu waanze kupungwa makazini kutokana na hili lirecession linalokuja
watoto wanamaliza mashule ajiri haba
sekta binafsi nazo zitajibu mapigo kwa kutokuajiri
bidhaa haziuziki labda za china!
nakwambia ni kasheshe tupu
askari wa doria wapo siku hizi?
Mdau
Ni juzi tu niliona katika blog moja ya http://ajali-traumaclass.blogspot.com imetolewa tahadhari baada ya dada mmmoja kuvamiwa hapo jangwani majira ya saa3. Ninachojiuliza mimi ni kwamba, nikiwakama mtumiaji wa njia hiyo kilasiku, huwa naona askari wanapatrol katika eneo hilo. Je, wanakuwa wapi au ndo vibaka wanawa-time?Inatia hofu hofu sana. Je, ukimfyatua na bastola mtu kama huyo inasimama vipi?
ReplyDeleteSAFI SANA.
ReplyDeleteHao jamaa mi nawafagilia sana, maana ni kielelezo kizuri cha hali tuliyiofika najua naweza kueleweka vibaya lakini aliye na macho haambiwi tazama. Hata MUNGIKI waliianza hivi leo wanakaribia kuwa insurgence
Watanzania wengi ni wagumu sana kuwasaidia wenzao wanapopatwa na matatizo. hivi ni kweli uwingi ule wa magari katika foleni na daladala zote hizo watu wanashindwa kuwa na umoja na kushuka na kukabiliana na majambazi ama wahuni? si pati jibu. hivi kama watu wangeshuka katika madaladala kama matatu hao vibaka wengeweza kufanya unyama huo?
ReplyDeleteTuache uoga wa kihindi wa kujifungia ndani.
waacheni jamaa nao wajilipe washaburuzwa sana na mafisadi hao
ReplyDeletehayo mambo ni kweli kabisa na yanatokea maeneo ya jangwani wakati wa foleni. wiki iliyopita pia dada wawili wafanyakazi wa muhimbili(nurses)waliporwa kwa staili hiyo hiyo. hakuna aliyewasaidia, kwa kuwa vibaka walikuwa na mapanga na visu. walichukua simu, pochi na kila walichoweza kubeba, asubuhi kweupeee
ReplyDeletehayo mambo ni kweli kabisa na yanatokea maeneo ya jangwani wakati wa foleni. wiki iliyopita pia dada wawili wafanyakazi wa muhimbili(nurses)waliporwa kwa staili hiyo hiyo. hakuna aliyewasaidia, kwa kuwa vibaka walikuwa na mapanga na visu. walichukua simu, pochi na kila walichoweza kubeba, asubuhi kweupeee
ReplyDeleteNadhani ndo kilichobakia, kuwa na bastola, nadhani serikali ilegeze masharti ya watu kununua silaha, itaongeza discipline.
ReplyDeleteDuh e bwanaeeeee...Kova atakuwa anayo habari hii na lazima kutakuwa na askari wa doria walipangwa eneo hili!! Mara kibao huwa inatokea pale Jangwani nyakati za foleni haswa asubuhi!Huwa wanafuatilia kilichomo na aina ya abiria waliomo kuanzia magomeni! wakishaona kwamba milango haitawapa shida kufunguka na abiria si mapande ya watu/mabaunsa basi wanali-mark hilo gari na ku-set ambush pale chini Darajani, sehemu ambayo wao kukimbia bila kufukuzwa na umati wa watu wenye hasira inakuwa rahisi!Sasa sijui tufanyeje?maanake pale hakuna ujanja na ni lazima mtu uende kazini saa hizo...KOVA SAIDIA BANA!!
ReplyDeletemkiwa kwenye magari yenu msitegemee msaada kutoka kwenye daladala kwani saiz kuna chuki kati ya watumiaji wa daladala na wenye magari.tunapoelekea sio pazuri jamani!
ReplyDeleteWANACHOFIKIRIA ABIRIA WALIOBANA KWENYE DALADALA NI KUWA"ENDAPONITASHUKA KUSAIDIA BASI NI WAZI KABISA KUWA SITOIPATA TENA NAFASI YA KUKAA KWENYE KITI HADI POSTA MPYA PALE NITAKOPORUDI KWENYE DALADALA"WATANZANIA TULIANZISHA KAMTINDO KAZURI KABISA KA KUSAIDIANA NA HATA KUCHOMANA MOTO,ILA SASA NAONA ULE UPENDO UMEANZA KUPOTEA NA WATU TUNETAWALIWA NA HAKA KANENO"fisadi" AMBAPO KILA ALIYEJITAHIDI KIDOGO KUWA NA KAGARI AU MAISHA YA KULA MATATATU KWA SIKU BASI NI FISADI;HEBU JAMANI TURUDIE ZILE ZAMA ZA KUSHIRIKIANA KAMA ZAMANI ITAPENDEZA!
ReplyDelete'Hii sasa ni kamba ngumu, uchumi tunao tunaukalia'- maneno ya Xplastaz.
ReplyDeleteMaana yake ajira hakuna, walionacho wanazidi kupora, soma magazeti ya siku hizi 'mabilionea' ndio wanaanza kufikishwa mahakamani.
Njia za kupunguza uhalifu sio raia kubeba bastola au kumwaga polisi. Maana hizo bastola pia zitaibiwa ili kupora simu za mikononi, briefcase au mikoba.
Jibu ni serikali kupanga mikakati endelevu ya kupanua wigo wa kuwezesha raia wenyewe kama vijana kupata ajira, kufanya kilimo cha kisasa au mikopo na mafunzo ya kuendesha biashara.
Ikiwa masuala hayo niliyosema hapo juu haitafanyiwa kazi, basi tutegemee kuona uhalifu wa kutumia mabavu/nguvu ukiongezeka kwa kasi kulingana na kasi ya wizi wa 'kalamu' unaofanywa na 'mabilionea.
Hao waliokuwa kwenye daladala waliona shida kutoka kusaidia kwa sababu sasa hivi sio kila mwenye gari ni jirani mwema. Kuna mafisadi humo humo.
ReplyDeleteKatika hali hiyo msaada utautoaje? hata kama una bastola maana ukikosea na kumpata mtu mwingine utaozea jela, hakuna mtu yuko tayari kupambana na kundi lenye visu na mapanga kwa kuwa wao kwa kawaida huwa wamelewa bangi au unga kwa hiyo hata wakiona pistol wataendelea kuvamia. Hapa ni polisi kufanya kazi yao tu kwa kuwa wao wanaogopwa.
ReplyDeletehivi kwanini watu wanaendelea kuishi hapo Jangwani!?
ReplyDeletesi mnatafuta matatizo lakini wenyewe!?
recession hii hiyo, ohooo..
Anyway, sijui kwanini hamuwachomi!?
I Luv You Bongo, Japo Sijafika?
= = =
Buffalo,
New York
Hivi kweli tumeshindwa hata kuzuia vibaka....
ReplyDeleteMimi sikubaliani na kwamba recesssion ndo inasababisha haya majanga.
Hawa vibaka wanajua kwamba serikali yao siku zote iko likizo siku zote kwahiyo wanafanya wanavyotaka..
Mimi nina jamaa yangu alivamiwa nyumbani kwakwe Mbezi saa nne usiku.Akapiga simu polisi mara nyingi tu..wakipokea wanasema hawana usafiri kwahiyo hawawezi kusaidia.
Tell me, how u gonna feel when you are facing death and law enforcement are telling you..just die man we ain't coming over....this is BS
Kuna wimbo 'Tusibweteke' ktk Youtube. Kwa kuwa sasa mtoto bongo anazaliwa na madeni na aliyekopa siyo anayelipa......
ReplyDeleteHili suala ni 'systemic problem' (mfumo-mzima) siyo la Kamanda Kova wala Polisi. Hapa ni mfumo mzima wa nchi iliyokosa mkakati wa kuwawezesha wale walio watoto wa wakulima/wafugaji/wavuvi/wafanyakazi masikini na ndio maana uhalifu wa kupata hela ya 'kuganga njaa' utaendelea kuongezeka kwa sana.
mimi sishauri wafanywe chochote kumpiga mtu bastola kwa ajili amekuibia simu sio haki, huku uk ukiiba unaambiwa stop stop kama kuna polisi karibu wanakutoa mbio.
ReplyDeletelakini ukifisadi chamoto utakiona.
kwa hiyo wakupigwa bastola ni hao mafisadi wanaowaibia kila siku na sasa hivi wameanza kuwarithisha watoto wao uwizi wanaiba kuanzia milioni tshs mpaka $£.
azabu lazima iendane na kosa, sio mtu anapora elfu 50 anauliwa, mtu anaiba mabilioni anatembea, hizo bilioni ndio zingeweza kuajiri askari wengi huyo wa elfu hamsini asingeweza kusogea
michuzi usiibane hii kama kawaida yako
mdau uk
Bwana michuzi mimi naona tunadanganyana kwenye blog yako kwasababu, sababu zinazomfanya aliyoko kwenye daladala asimsaidie aliyeko kwenye gari ndogo wakati anakabwa,ni zile zile zinazomfanya mtanzania yoyote iwe uturuki au mexico asimsaidie mtanzania mwenzake awapo matatizoni.Nikianza na sababu ya msingi yaani woga, naweza kusema huu ni ugonjwa wa mtanzania ambao ndo wa kwanza kisha ni ukimwi kabla ya ugonjwa wa umbeya.(jamani WASHINGTON DC kuna umbea!!!!)Nakupa mfano kuhusu ugonjwa wa woga.Angalia watoa maoni tu kwenye blog yako wengi wanajiita anonymous kwasababu ya woga.Kama unachokisema ni point na waweza kukidifendi kwanini usiseme wewe ni Ngema? au ni umbea? sikubaliani na mtoa hoja kwamba solution ni kununua pistal,maana nchi zilizochukuwa solution hiyo sasa hivi wanalia ikiwa marekani ndo ya kwanza. Hii itafanya walewale akina mka....mka......nani yule jamaa aliye uza nchi?samahani michuzi nimemsahau jina jamaa mmoja mwenye tumbo kama furushi la bamia.Labda tuwe na kikao cha siri maana hata humu kwenye blog, vibaka huwa wanachangia tena sana.Hujasikia vibaka wengine wakidai eti tuwaache maana hawana chakula? unakubali hiyo kaka michu? kwani babu zetu waliiba? pale wakati simu za mikononi hazijaingia? ni kutaka starehe tu. Na nawaonya vibaka wote mkidhubutu kwenda mbagala rangitatu nitatuma tume yangu yakuwachunguza kisha nitaachia vibaka wa kibondemaji wawashughulikie ninyi na wenzenu.
ReplyDeleteHii taharifa wapatie hawa jamaa wa ccm nchini marekani katika mtandao wao www.ccmmarekani.blogspot.com hili wakubwa waione kilaisi
ReplyDeleteOctavian mbona vijana hawakurudi na kitu cha maana? ile ngoma haikuwa ya pedeshee next time we chuna kama ulivyouchuna leo!! baadae unaweza ukapata mambo Maeda sinza! hivyo ndio Migo Migo tunavyoish!!
ReplyDeleteWenu
Dingi la Kinoma
SERIKALI YA WASELA IMELALA KILAMTU ANAFANYA ANAVYOTAKA.KUIBA SERIKALINI,MAOFISINI NA HATA KWENYE IDARA ZA KUKUSANAYA MAPATO YA SERIKALI NA HAKUNA ANAYESEMA KITU.
ReplyDeleteHIVI NAMBA YA SIMU YA DHARURA KUPIGA POLISI NI NGAPI? BADO ILE ILE 999 NA INAFANYA KAZI KWELI? KIKWETE NA MACHEKI WENZAKE KAZI IPO.
KU-LOCK DOOR HAITASAIDIA KITU,ITAFIKIA ATUA VIBAKA WATAFUNJA HADI VIOO VYA MAGARI KUWAFIKIA WALENGWA!
ReplyDeleteWhat we need from our police force in for them to use technology to solve problems. Surely they could install surveillance cameras at these hotspots. I don't think it will cost that much! And then deal with the culprits accordingly
ReplyDeletewewe anonymous wa March 07, 2009 2:58 AM uliyependekeza tahari hii wapewewe jamaa wa ccm nchini marekani mimi nimwetumia lakini bado hawajaibandika www.ccmmarekani.blogspot.com
ReplyDeleteNimetembelea mtadao wao mpaka sasa hawajapost.