

Wakati ijumaa hii ikipamba moto kwa burudani kibao hapa jijini Dar, Wazee wa Ngwasuma "The Dream Team" FM Academia wao watakuwepo ndani ya ukumbi wa VATICAN CITY HOTEL - SINZA, show hii inafuatia baada ya maombi ya wapenzi wa Ngwasuma kuomba bendi hiyo kupiga tena baada ya kuwakonga mioyo washabiki hao wiki kadhaa zilizopita.
Katika show hiyo pia kutakuwa na suprise visit ya mkongwe wa muziki wa siku nyingi Kanda Bongoman ambaye atapita tu kusalimia akielekea katika show yake huko msasani club.
FM Academia imejiandaa kupiga nyimbo mpya sita ambazo bado hazija sikika popote na wapenzi wa Ngwasuma leo ijumaa 20/03/2009 watapata nafasi hiyo ya kipekee.
Hii ni katika pasha moto ya safari yao ya Uingereza mwezi ujao ambapo watasherehekea Pasaka pake Reading tarehe 12 aprili, 2009 na kabla ya siku hiyo tarehe 11 aprili, 2009 watakuwa birmingham.
HIZO NYIMBO MPYA ZA NGWASUMA MIE NIMEZISIKIA KWENYE KAMBI YAO YA MAZOEZI. KAMA NYIE HAMJAZISIKIA, POLENI KWANI NI ZA KUKATA KWA SOKA BUTU. HAHAHAHAH TEHEHETEHEEHEHEE
ReplyDeleteKanda Bongo man kasafiri na visa gani?? This is another no show!! Trust me
ReplyDeleteNatumaini hatatuachia familia zilizopeana talaka kama ilivyokuwa miaka ile kule nchi ya jirani.
ReplyDelete