
Maggid Mjengwa (pichani) sio jina geni.Bila shaka kabisa umewahi kumsikia,kumsoma na pengine hata kutembeleablog yake ambayo kimsingi ni kimbilio la yeyote yule anayependa kupata picha halisi ya maisha ya mtanzania wa kawaida hususani yule anayeishi kijijini kama ilivyo kwa babu na bibi yangu.Wasomaji,watembeleaji na wachangiaji wa blog yake wanapenda kumuita “Mwenyekiti”.
Yeye ni miongoni mwa waandishi wa makala zenye kuchoma kama sio kugusa hisia za wengi.Ukitaka kujua historia yake ya uandishi unaweza kuipata kwa kusoma mahojiano tuliyowahi kufanya naye siku za nyuma kwa kubonyeza hapa.
Maggid ni mpenzi wa michezo hususani wa soka.Ni mnazi wa Simba.Ni upenzi huo wa soka na michezo kwa ujumla ambao ulimfanya aanzishe gazeti lililoitwa “Gozi Spoti” ambalo lilidumu mitaani mpaka hivi karibuni alipoamua kulisitisha.
Jambo jema ni kwamba, kuondoka kwa “Gozi Spoti” kulifanyika kwa makusudi ili kulipisha gazeti jipya litakalojulikana kama Kwanza Jamii ambalo litaingia mitaani siku si nyingi chini ya usimamizi waIkolo Investment Ltd kampuni iliyo chini ya mwenyewe “Mwenyekiti”.Kwa hiyo tunaweza kabisa kuongeza cheo kimoja kwa “Mwenyekiti” na kumuita Mjasiriamali.
Kwanza Jamii ni jarida la uchambuzi wa masuala yanayohusu na kuigusa jamii.Haya ni pamoja na siasa,uchumi,elimu,michezo na utamaduni.Pia yatakuwemo masuala ya mazingira,jinsia na ukimwi . Ni jarida litakalokuwa linatoka kila siku ya Jumanne.
Tovuti ya www.bongocelebrity.com imepata nafasi ya kufanya mahojiano mafupi na ‘Mwenyekiti” kuhusiana na ujio wa jarida hili na pia kumdadisi kuhusu anachokiona kila atembeleapo vijiji na vijiji vya Tanzania.Anaona nini?Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo; (more…)
hivi huyu Mjengwa ni babu Kijana au Mzee? maana si simuelewi
ReplyDelete"While others try to reach the moon, we try to reach villages." J. K. Nyerere. Nafurahi sana kuona ndugu Mjengwa unatizima kauli hii kwa maneno na vitendo. Tu pamoja na kazi ya kuliletea taifa maendeleo bado ni kubwa.
ReplyDeleteajihadhari na waandishi makala wanaotumia majina ya bandia wameshavamia Raia mwema na Tanzania Daima.wakimaliza makala yao utaona wanaandika niandike.
ReplyDeleteNadhani mwenyekiti Mjengwa ni kijana na sio mzee!
ReplyDelete