Hi Michuzi,
J'pili nilikwenda kumwabudu Mungu wangu kwenye moja ya makanisa hapa Maryland, nje kidogo ya Washington DC na kukuta kwaya bombaaa ya 'Watoto' yatimakutoka Uganda ikitumbuiza, kama njia mojawapo ya ku- raise funds kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kijiji cha watoto yatima huko Uganda.
Watoto wapatao 1,700 tayari wanaishi katika nyumba hizo, ambapo kila watoto 8 huishi na mlezi wa kulipwa ambaye anawatunza kama mama wa familia ya watoto wasiozidi 8.
Lengo ni kuhakikisha kwamba watoto yatima wanalelewa katika nyumba za kawaida badala ya vituo vya watoto kama ilivyo TZ na nchi nyingine nyingi.
Mdau Lilly


yeah!! thats very good idea, nadhani TZ nasi tungeiga mfano!!
ReplyDeleteKituo kama hicho tunacho hapa kwetu Tanzania na kinaitwa SOS (maarufu kama kwa mama Anna Mkapa)kina nyumba zaidi ya 22 na kila nyumba ina watoto 8 - 10 wanalelewa na mama mmoja mmoja, watoto ni wasafi na wanalelewa vizuri sana,kituo hicho kina nursery school na watoto wote ni lazima wasome.
ReplyDeleteRudini nyumbani muone, sio tanzania ile mliyoiacha na mkataa kwao mtumwa.
Nakubaliana na annon wa kwanza,Pia Tz kuna utaratibu mwingine umeanzishwa long time na NGO's ambapo hawajengi centre ya watoto yatima bali wanawawezesha/empower walezi wa hao watoto ili waweze kuwalea vizuri majumbani kuliko kukaa kituoni ambapo wanamiss family life experience na inawaathiri kisaikolojia.
ReplyDeleteNGO zinatoa ada, gharama za chakula na matibabu kwa kiasi, lakini mtoto analelewa ndan ya familia hata kama ni babu, bibi lakini hawakai kituoni.
sorry I mean nakubaliana na mama T si Annon wa 1
ReplyDeleteAnon 2 si kila anayeishi nje ya Tanzania ni kwamba ameikana nchi yake.Watu wa namna hiyo hutawakuta wanasoma habari za Tanzania online kwani hawana interest.
ReplyDeleteKuna sababu nyingi za watu kuwa nje ya nchi na kwani hata hapo kwetu tunao wageni kibao...Mwisho nashukuru kusikia angalau kuna kituo cha namna hiyo Tanzania,ila tungependa watoto wote yatima wapate nafasi kama hiyo..Kwani hakuna lisilowezekana
Nauli ya kusafirisha hao watoto kwenda USA ingetosha kujenga hiyo nyumba!
ReplyDeleteMama T sio kila mtu humu bloguni yupo nje ya nchi. Naweza nikawa Mwanza/Bukoba au hata hapo morogoro lakini nisikijue au wala kukisiki hicho kituo. Hivyo badala ya kushambulia watu na kusema warudi nyumbani wakati wala hujui walipo nadhani ungeishia tuu kwenye paragraph ya kwanza ambayo imesheheni maelezo kamili kwa wasomaji waliopo nje na ndani ya tanzania.
ReplyDeleteKuwa nje ya nchi isiwe tabu, watu hawakatai kwao ni shida tuu zinawafanya wanajaribu kutafuta maisha hapa na pale....
Kama kuna vituo hivyo tanzania ni vizuri sana...na kama unavisifia hivyo. Manake kuna kimoja kiko pale moshi - shanti town watoto wanabakana wenyewe kwa wenyewe, lugha ya matusi ndio kwao na hawatunzwi vizuri..yaani wapo wapo tuu. I hope kitakuwa kimebadilika sasa au kimefungwa
ReplyDeletehao watoto wa uganda wataperform hapa UK - west midlands mwezi huu
ivi why umu ndani watu wanalumbana sana na kukaa nje au bongo??
ReplyDeletemnaboa sana sana
kokote ni maisha na kila mtu ana yake,kua mahali fulani si umaarufu au laana!!duniani wote tunapita...
grow up folks!!
watoto yatima ni wetu sote,tuwatunze kwa lolote uchonacho
i like it ni nzuri sana watoto wanajitahidi kweli wanmafipaji mbali mbali hawa watoto! kuhusu swala la nje au ndani ni ujinga wa baathi ya watanzania wanaopenda kushindana maisha! kuwa nje au ndani ya nchi ni uamuzi wa mtu na mipango yake ya maisha kwahiyo haikuhusu! mama T ungekuwa na busara zaidi unge mind biashara zako achana na watu na maisha yao
ReplyDelete